Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi

Mwanafunzi Isra Hilal Mwadini akifuatiwa na mwenzake Tamima Abass Sheha wakipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wakati wa hafla ya Maulidi ya Jumuiya ya Chuo cha Samael Academy.Kulia ya Balozi Seif ni Rais wa Sameil Academy Sheikh Nassir Bin Said.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizindua rasmi Bara bara ya pili ya Amani hadi Mtoni baada ya kukamilika awamu ya mwisho ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Akiwa na Balozi mdogo wa India nchini Tanzania wakiangalia maonyesho yaliofanya na Msanii kutoka India, Bi Navi Madhav hapo Ngome Kongwe

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Dk. Khalid S. Mohamed

akizungumza na Wadau wa Maendeleo wa Mfuko wa TASAF, walipofika Ofisini kwake kuzungumzia maendeleo ya Mfuko wa TASAF III,na kutembelea Mradi wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini (PSSN) katika Jimbo la Muyuni Wilaya ya Kusini Unguja katika Kijiji cha Muyuni B

Wazir wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakifurahia jambo wakati wa semina ya siku moja kuhusu matokeo makubwa na ya haraka katika kuleta mageuzi ya kiuchumi na kuleta maendeleo nchini iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein

Tuesday, 28 October 2014

Balozi Seif Azungumza na Balozi Mteule wa Tanzania Nchini Rwanda Ofisini kwake Vuga.

Balozi Mteule wa Tanzania Nchini Rwanda Balozi Said Ali Siwa akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake Barala la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Balozi Mteule wa Tanzania Nchini Rwanda Bwana Said Ali Siwa aliyefika Ofini kwake Baraza la Wawakilishi kujitambulisha rasmi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo(Picha na OMPR.)

Na Othman Khamis OMPR.
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Rwanda zina wajibu wa kuendelea kushirikiana pamoja katika kudumisha udugu na ujirani mwema kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya mataifa hayo mawili wanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akizungumza na Balozi Mteule wa Tanzania Nchini Rwanda Balozi Said Ali Siwa aliyekuja kuaga rasmi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.

Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar iliyopo katika jengo la Baraza la Wawakilishi liliopo Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Balozi Seif Alisema Rwanda na Tanzania zimekuwa na mafungamano ya karibu kwa muda mrefu hasa ule wakati wa Mataifa hayo yakipigania kupata uhuru kutoka kwa wakoloni.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimuomba Balozi Said Ali Siwa kuhakikisha kwamba  anasimamia vyema uhusiano huo ambao unaonekana kupata majaribu wakati Rwanda ilipokuwa na sintofahamu wa vurugu za Kisiasa zilizosababisha vite vya Kikabila Nchini humo.

Alisema  Tanzania ililazimika kipindi hicho kupokea wakimbizi wa Rwanda ambao walihitaji kupata hifadhi kutokana na vurugu hizo zilizoleta maafa makubwa Nchini Rwanda.

Hata hivyo Balozi Seif alimtahadharisha Balozi Said kuwa tayari kupambana na changamoto atazokabliana nazo wakati wa utekelezaji wa majukumu yake ya Kidiplomasia Nchini Rwanda.

Balozi Seif aliipongeza Serikali ya Rwanda  kwa jitihada ilizochukuwa za kurejesha hali ya utulivu miongoni mwa wananchi wake .

Mapema Balozi Mteule wa Tanzania Nchini Rwanda Bwana Said Ali Siwa alisema uteuzi alioupata ni fursa kubwa na ni muhimu kwake katika muelekeo wa kutekeleza jukumu alilokabidhiwa na Taifa.

Balozi Said alimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwamba atakuwa tayari kuchota fikra na mawazo ya waliomtangulia ili kuona kazi yake ya Kidiplomasia inakwenda katika matarajio yaliyokusudiwa.

Alisema muda wote hatosita kuchota uzoefu alionao Balozi Seif kwa lengo la kutekeleza vyema na makini majukumu aliyopangiwa.

Monday, 27 October 2014

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Bwana Egon Kochanke ofisini kwake vuga Mjini Zanzibar.  Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.






















Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Bwana Egon Kochanke akibadilisha mawazo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  katika jitihada za kuimarisha ushirikiano kati ya Ujerumani na Zanzibar.  Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.



Balozi  wa Ujerumani Nchini Tanzania Bwana Egon Kochanke alisema amani na usalama ndio njia pekee na ya msingi itakayoyavusha salama Mataifa  mbali mbali ya Bara la Afrika katika kuimarisha uchumi na usawi wao.
Bwana  Egon alieleza hayo wakati akijitambulisha rasmi alipokuwa na  mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake  Vuga Mjini Zanzibar.
Balozi Egon Kochanke alisema mataifa mengi ya Bara la Afrika yamekosa fursa ya kuendelea na harakati za kujiletea maendeleo kwa kukumbwa na wimbi la vurugu na vita.
Alizitolea mfano Nchi za Somalia, Sudani ya Kusini pamoja na Nigeria ambazo zimekosa utulivu wa kisiasa kutokana na kukumbwa na vitendo vya uvunjifu wa amani likiwemo suala la Ugaidi linaloonekana kuitishia amani ya Dunia.
Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania alipongeza  na kuridhika na mazingira mazuri ya Rasilmali na uwekezaji yaliyomo ndani ya Visiwa vya Zanzibar jambo ambalo alisema atatumia nafasi yake ya Kidoplomasia Kuitangaza kwa Makampuni na mashirika ya Uwekezaji vitega uchumi ya Nchini kwake.
“ Nitachukuwa juhudi kama Balozi kujaribu kuyashawishi Makampuni na Mashirika ya Kijerumani kulitumia Soko la Zanzibar katika kuendeleza miradi yao kiuchumi na kibiashara “. Alisema Balozi huyo wa Ujerumani Nchini Tanzania.
Balozi Egon alifahamisha kwamba Zanzibar inaeleweka vyema Nchini Ujerumani kutokana na uzalishaji wake wa vyakula na bidhaa za Viungo ambavyo hupendwa na kuwa na watumiaji wengi duniani.
Katika kuunga mkono juhudi za Zanzibar katika kujinasua kiuchumi pamoja na kuimarisha soko la Ajira Balozi Egon alifahamisha kwamba Serikali ya Ujerumani itaandaa mipango maalum wa kutoa mafunzo ya kazi za amali kwa vijana wa Kizanzibari.
Alisema mpango huo utakaoendeshwa Nchini Ujerumani  utajengewa mazingira ya kwenda sambamba na kuwaalika wataalamu wa sekta mbali mbali Zanzibar kupata fursa ya kutangaza mazingira na  vivutio vya uwekezaji  vya Visiwa vya Zanzibar kwa taasisi na makampuni ya Nchi hiyo.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  aliiomba Ujerumani kuendelea kuiunga mkono Zanzibar na Tanzania kwa ujumla katika harakati zake za kuimarisha uchumi na maendeleo ya ustawi wa Jamii.
Balozi Seif alisema Serikali hivi sasa inaendelea kuimarish miundo mbinu katika sekta mbali mbali za kiuchumi ikilenga zaidi uimarishaji wa kilimo ambacho huchukua zaidi ya asilimia 80%  ya wananchi wote Nchini Tanzania.
Alisema ili kufanikisha sekta hiyo zana za kisasa kama Matrekta yatahitajika katika kuwawezesha wakulima wengi hasa vijijini kuongeza uzalishaji utaozingatia taaluma ya kisasa kwa lengo la kuondokana na kilimo cha asili chenye mapato madogo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kupitia Balozi huyo wa Ujerumani Nchini Tanzania aliwaomba  wawekezaji, mashirika na Taasisi za Ujerumani kujenga viwanda mbali mbali vitakavyookoa mazao ya kilimo mashambani.
Alisema Zanzibar ni kituo kikubwa cha biashara ndani ya ukanda wa  Bara la Afrika ambacho wawekezaji hao wanaweza kukitumia jambo ambalo pia watapunguza wimbi la ukosefu wa ajira kwa vijana wengi wanaomaliza masomo yao.





Sunday, 26 October 2014

Balozi Seif Azindua Safari za Ndege ya FlyDubai kutoka Dubai hadi Zanzibar.


Wasanii wa DMCA, wakitowa burudani wakati wa Uzinduzi wa Safari ya Ndege ya Shirika la Ndege la Fly Dubai iliozinduliwa na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibare Balozi Seif Ali Iddi iliofanyika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.
Ndege ya Shirika la FlyDubai ikiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume tayari kwa Uzinduzi wake uliofanywa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,Itaaza safari zake moja kwa moja kutoka Dubai hadi Zanzibar na ina uwezo kuchukua Abiria 240.  

Wafanyakazi wa FlyDubai wakiwa tayari kuipokea ndege yao ikitokea Dubai wakiwa na maua kwa ajili ya uzinduzi huo. uliofanyika Zanzibar. 



Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi,akiwa na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Flydubai Bwana Sudhir Sreedhara aliyevaa miwani wakiangalia burdani ya ngoma ya Msewe Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar mara baada ya ndege ya Kampuni hiyo kutua kuanzai safari zake kati ya Dubai na Zanzibar.
Abiria wa Kwanza wa ndege ya Fly Dubai wakishuka katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar wakati ndege hiyo ilipotuwa kwa mara ya kwanza Zanzibar kwa ajili ya kuzindua Safari zake Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akizindua Safari za Ndege za Kampuni ya FlyDubai itakayo toa huduma za moja kwa moja kutoka Dubai hadi Zanzibar, inayotarajiwa kuaza hivi sasa kwa safari zake hizo, Balozi Seif akizungumza katika hafla hiyo iliofanyika katika viwanja vya ndege vya Zanzibar. 

                Waheshimiwa wakifuatilia hala ya Uzinduzi wa Ndege ya Fly Dubai.

Naibu Waziri wa Wizara ya Miundombinu na Mawasaliano Zanzibar Mhe. Issa Gavu, akizungumza wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika viwanja vya ndege vya kimataifa vya Abeid Amani Karume Zanzibar.

Makamu wa Rais wa Kampuni ya Flydubai Bwana Sudhir Sreedhara, akiwahutubia wananchi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Safari za ndege za Shirika kla ndege la FlyDubai, zilizofanyika katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu nsa Mawasiliano Zanzibar Dk. Juma Akili, akizungumza wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa safari za ndege ya FlyDubai. Zanzibar. 

Viongozi wa Serekali wakihudhuria katika hafla ya Uzinduzi wa Ndege ya Shirika la Ndege la Fyl Dubai uliofanyika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani KarumeZanzibar. iliozinduliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.


Baadhi ya wageni waalikwa katika sherehe za hafla ya Uzinduzi wa Safari ya Ndege ya Fly Dubai  iliofanyika katika uwanja wa ndege Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Flydubai Bwana Sudhir Sreedhara akimkabidhi zawadi ya Jahazi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, watika hafla ya uzinduzi wa safari za ndege za Kampuni ya FlyDubai,kati ya Dubai na Zanzibar.kulia kwa Balozi Seif ni Naibu Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Mh. Issa Haji Ussi Gavu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akimkabidhi zawadi ya Mlango wa Zanzibar Makamu wa Rais wa Kampuni ya FlyDubai Bwana,Sudhir Sreedhara wakati wa hafla ya uzinduzi wa safari za ndege za Kampuni ya FlyDubai, zilizofanyika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Serikali na wea Kampuni ya FlyDubai, kutoka kushoto Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Pandu Ameir Kificho, Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai.Mhe.Omar.Mjenga, Makamu wa Rais wa Flydubai Bwana Sudhir Sreedhara, Balozi Seif Ali Iddi, Naibu Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Mhe. Issa Haji Gavu, Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Dk.. Juma Malik Akili na ni Mratibu wa Kampuni ya Kimataifa ya usafiri wa anga ya Flydubai Bwana Riyaz Jamal.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,akimuonesha jengo jipya la abiria katika uwanja huo,Makamu wa Rais wa Flydubai Bwana Sudhir Sreedhara wakati wa hafla ya uzinduzi wa ndege hiyo uliofanyika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar. Mratibu wa Kampuni ya Kimataifa ya usafiri wa Anga ya Flydubai Bwana Riyaz Jamal.
Balozi Seif akimpongeza Makamu wa Rais wa Flydubai Bwana Sudhir Sreedhara kwa auwamuzi wa kampuni yake kutoa huduma za usafiri wa ndege kati ya Dubai na Zanzibar.Kati kati ni Mratibu wa Kampuni ya Kimataifa ya usafiri wa Anga ya Flydubai Bwana Riyaz Jamal.na kushoto Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai Balozi Omar Mjenga.
Makamu wa Rais wa Flydubai Bwana Sudhir Sreedhara akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar wakati wa kumalizika kwa hafla ya uzinduzi wa safari ya ndege ya kampuni ya FlyDubai itakayoaza safari zake moja kwa moja kutoka Dubai hadi Zanzibar kwa bei rahasi kwa wateja wake kupata fursa kusafiri na ndege zao kwa bei nafuu na huduma bora.kulia ni Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai Balozi Omar Mjenga.

Mahafali ya 21 ya Chuo cha Taaluma ya Sayansi ya Afya Zanzibar

.

Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Taaluma za Afya Zanzibar Dkt. Abdalla Ismail Kanduru akitoa tamko la kuwatunuku stashahada wahitimu wa Chuo hicho katika Mahafali ya 21 yalifanyika Mbweni.
 Wahitimu wa Chuo cha Taaluma za Afya  Zanzibar wakila kiapo cha utiifu mbele ya mgeni rasmi Balozi Seif Ali Iddi katika mahafali ya 21 yaliyofanyika chuoni Mbweni.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na wahitimu wa Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya Zanzibar katika Mahafali ya 21 yaliyofanyika Chuoni Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Wa kwanza (kulia) ni Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman na wa kwanza (kushoto) Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho Dkt. Abdalla Ismail Kanduru

Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimtunuku  zawadi Mhitimu Leila Ali kwa kuwa miongoni mwa wanafunzi  waliofanya vizuri zaidi katika mahafali ya Chuo cha Taaluma za Afya Mbweni Zanzibar.
Wahitimu wa fani mbali mbali wa Chuo hicho wakimsikiliza mgeni rasmi (hayupo pichani) baada ya kuwatunuku stashahada katika mahafali ya 21.
Wageni waalikwa walioshiriki mahafali ya 21 ya Chuo cha Taaluma za Afya Zanzibar wakifuatilia maadhimisho  hayo yaliyofanyika Chuoni, Mbweni.

Sunday, 5 October 2014

Balozi Seif Akutana na Muwekezaji kutoka Marekani na Balozi wa Heshima wa Tanzania U S A.

 Balozi wa Heshima wa Tanzania Nchini Marekani ambae pia ni Murugenzi wa Kampuni ya Ms Shimoja Dr. Robert Shumake akimtambulisha Makamu wa Rais wa Kampuni ya maendeleo ya ujkenzi ya Detroit Nchini Marekani Bw. Andrew G. McLemore kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi walipokutana kwa mazungumzo VIP ya Uwanja wa ndege wa Pemba.Aliyepo kushoto na Balozi Seif ni Afisa Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani Mh. Suleiman Saleh.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na Balozi wa Heshima wa Tanzania Nchini Marekani ambae pia ni Murugenzi wa Kampuni ya Ms Shimoja Dr. Robert Shumake kwenye uwanja wa ndege wa Pemba.(Picha na Hassan Issa OMPR)


Na.AOthman Khamis Ame
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi  Seif Ali Iddi alikuwa na mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Ms Shimoja kutoka Jimbo la Michigan Nchini Marekani Dr. Robert Shumake.
Mazungumzo hayo yamefanyika katika chumba cha watu mashuhuri { VIP } kilichopo kwenye uwanja wa ndege wa Pemba ambapo Balozi Seif aliwasili akitokea Mjini Dodoma baada ya kumalizika kwa Bunge Maalum la Katiba.
Katika mazungumzo yao Mkurugenzi Mkuu huyo wa Kampuni ya Ms Shimoja Dr. Robert Shumake ambaye amepata heshima ya kuwa Balozi wa Heshima wa Tanzania Nchini Marekani alielezea kuridhika na mazingira mazuri ya uwekezaji kisiwani Pemba.
Dr. Shumake alisema Uongozi wa Kampuni yake utaangalia maeneo ambayo inaweza kuwekeza vitega uchumi kama alivyomuahidi Balozi Seif wakati wa ziara yake katika Jimbo la Seattle Nchini Marekani mwaka jana.

“ Muda wangu mfupi niliopata kutembelea maeneo tofauti ya Tanzania ikiwemo Zanzibar umenipa faraja na shauku ya kuangalia fursa zilizopo za uwekezaji na namna  uongozi wa Kampuni yangu utakavyochangamkia fursa hiyo “. Alisema Dr. Robert Shumake.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliuhakikishia Uongozi wa Kampuni hiyo ya Ms. Shimoja kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko tayari kuupa msaada wakati unaohitaji kuwekeza hapa Zanzibar.
Balozi Seif alimueleza Dr. Shumake kwamba Zanzibar tayari imetoa fursa kwa wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza miradi na vitega uchumi vyao ili kusaidia kunyanyua pato la taifa sambamba na kuongeza soko la ajira.
Alisema yapo maeneo na sekta ambazo Kampuni ya Ms Shimoja inaweza kuyatumia kuwekeza akiyataja kuwa ni patoja na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Pemba, Bandari ya Wete, Sekta ya utalii pamoja na nyumba za mkopo nafuu.
Alifahamisha kwamba miradi ya nyumba za mikopo nafuu kwa kiasi kikubwa inaweza kuwasaidia zaidi vijana wenye ajira mpya  ili wajenge hatma bora ya maisha yao ya baadaye.
Dr. Robert Shumake Mkurugenzi wa Kampuni ya Ms. Shimoja ambae pia ni Balozi wa Heshima wa Tanzania Nchini Marekani alikuwepo Nchini Tanzania kutia saini mkataba wa uanzishwaji wa treni iendapo kwa mwendo wa kasi kati yake na Wizara ya Uchukuzi ya Tanzania.
Treni hiyo itakapokamilika itakuwa ikitoa huduma ya usafiri kati ya Dar es salaamu na pugu kwa kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
4/10/2014.