Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi

Mwanafunzi Isra Hilal Mwadini akifuatiwa na mwenzake Tamima Abass Sheha wakipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wakati wa hafla ya Maulidi ya Jumuiya ya Chuo cha Samael Academy.Kulia ya Balozi Seif ni Rais wa Sameil Academy Sheikh Nassir Bin Said.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizindua rasmi Bara bara ya pili ya Amani hadi Mtoni baada ya kukamilika awamu ya mwisho ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Akiwa na Balozi mdogo wa India nchini Tanzania wakiangalia maonyesho yaliofanya na Msanii kutoka India, Bi Navi Madhav hapo Ngome Kongwe

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Dk. Khalid S. Mohamed

akizungumza na Wadau wa Maendeleo wa Mfuko wa TASAF, walipofika Ofisini kwake kuzungumzia maendeleo ya Mfuko wa TASAF III,na kutembelea Mradi wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini (PSSN) katika Jimbo la Muyuni Wilaya ya Kusini Unguja katika Kijiji cha Muyuni B

Wazir wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakifurahia jambo wakati wa semina ya siku moja kuhusu matokeo makubwa na ya haraka katika kuleta mageuzi ya kiuchumi na kuleta maendeleo nchini iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein

Tuesday, 3 November 2015

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitoa Taarifa ya Serikali akisisitiza Taarifa ya awali ya Serikali iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitoa taarifa rasmi ya Serikali kuhusu upotoshaji wa baadhi ya vifungu vya sheria unaendelea kufanywa na baadhi ya viongozi wa Kisiasa  juu ya uhalali wa kuendelea kuwepo madarakani Rais wa Zanzibar.  Taarifa hiyo aliitoa katika kituo cha matangazo ya Shirika la Habari Zanzibar {ZBC-TV } Karume House Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
























 Press Release:-

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imewahakikishia Wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kwamba Rais aliyepo madarakani hivi sasa ataendelea kushika madaraka ya Urais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi mpaka pale utaratibu wa Kikatiba na Kisheria wa kumpata Rais utakapokamilika.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akitoa Taarifa ya Serikali akisisitiza Taarifa ya awali ya Serikali iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuhusiana na kauli za kupotosha zinazotolewa na baadhi ya Viongozi wa vyama vya Kisiasa kuhusu uhalali wa kuendelea kuwepo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliyopo madarakani pamoja na Serikali yake.
Balozi Seif aliwaomba Wananchi wazipuuze kauli za upotoshaji zinazotolewa zikiashira zaidi uvunjifu wa amani na kuwataka waendee kuwa watulivu na kudumisha amani iliyopo Nchini.
Alisema Kifungu cha 28 Mbili {a} cha Katiba ambacho kimekuwa kikitumika katika kutoa tafrisi potofu kwa Wananchi  kwamba Rais aliyopo madarakani atamaliza muda wake wa miaka mitano kuanzia Tarehe ambayo alipokula kiapo cha uaminifu na kiapo cha kuwa Rais.
Balozi Seif alieleza kwamba ni dhahiri kwamba dhamira ya kifungu hicho cha Katiba ilikuwa kuweka bayana kuwa kama uchaguzi Mkuu utafanyika na msindi wa kiti chja Urais atatangazwa rasmi na Tumen ys Uchaguzi, hivyo muda wake wa kuendelea Mtu kuwa Rais ungemalizika kwa kufuatana na masharti ya Kifungu hicho.
Alifafanua kwa kuwa Tume ya Uchaguzi haikumtangaza mshindi wa kiti cha nafasi ya Urais ni dhahiri masharti ya kifungu hicho hayataweza kusimama na hivyo masharti ya Kifungu cha 28 {1} {a} cha Katiba kitakuwa na nguvu za Kikatiba kumpa uwezo wa Rais aliyopo madarakani kuendelea na madaraka ya Urais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Alisema Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi anapatikana  kwa mujibu wa masharti ya Kifungu cha 27 cha Katiba ambacho Rais anachaguliwa kufuatana na Katiba Hiyo na kwa mujibu wa Sheria yoyote itakayotungwa na Baraza la Wawakilishi hukusu Uchaguzi wa Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Balozi Seif alifahamisha kuwa ili Rais wa Zanzibar apatikane kwa mujibu wa Katiba na sheria ya Uchaguzi nambari 11 ya Mwaka 1984, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar inapaswa kuendesha uchaguzi na hatimae kumtangaza mshindi wa nafasi ya Urais ambae atashika madaraka hayo pale ambapo atakuwa ameapishwa rasmi kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Katiba ya Zanzibar.
Alisema Kifungu cha 28 {1} {a} cha Katiba kinaweka utaratibu kuhusu muda wa kuendelea kuwa kuwa Rais, na kwamba kwa kufuatana na kifungu hicho, mtu aliyechaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ataendelea na dhamana hiyo mpaka pale ambapo Rais anayefuata ale kiapo cha kuwa Rais.
Alieleza kwamba kwa msingi huo wa Kikatiba ni vyema Wananchi wakafahamu na kuelewa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Braza la Mapinduzi ataendelea kuwepo madarakani mkapa pale Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar itakapomtangaza mshindi wa kiti cha Urais na Rais Mteule atashika madaraka hayo baada ya kuapishwa rasmi kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Katiba.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Viongozi wa Dini mbali mbali Nchini aliokutana nao Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar














Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya pamoja na Vongozi wa Dini mbali mbali Nchi mara baada ya kufanya mazungumzo nao Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.  Kushoto ya Balozi Seif ni Kiongozi wa Timu ya Waislamu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Kabi na Kulia ya Balozi ni Kiongozi wa Wakristo Askofu Augustino Mweleli Shao.  Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.

  Press Release:-

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakamilisha taratibu zilizobakia na tayari inajiandaa kuwachukulia hatua za Kisheria watu wote waliohusika kuharibu kwa makusudi zoezi zima la Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar uliofanyika Tarehe 25 Mwezi Oktoba mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akizungumza na Viongozi wa Dini mbali mbali Nchini aliokutana nao Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kutafakari na kutafuta mbinu za kuendelea kujaribu kudumisha amani ya Nchi iliyotetereka  na kuleta mtafaruku katika kipindi hicho cha Uchaguzi.
Balozi Seif alisema ina uthibitisho kamili wa vielelezo vya ushahidi wa udanganyifu kwa maeneo yote ya Zanzibar hasa katika Majimbo ya Uchaguzi ya Kisiwa cha Pemba.
Alisema Afisa  wa Tume ya Uchaguzi au Mtu yoyote aliyehusika na udanganyifu huo aelewe kwamba mkondo  wa sheria utamkumba kwa vile vitendo walivyofanya wameisababishia hasara kubwa Serikali pamoja wa washirika wa maendeleo walioamua kusaidia uchaguzi huo.
Balozi Seif alibainisha kwamba  wakati wahusika hao wanapandishwa katika vyombo vya kisheria kujibu shutuma zinazowakabili Serikali kwa upande wake  itaweka hadharani uthibitisho kamili wa vielelezo vya ushahidi wa udanganyifu huo ili Wananchi wapate fursa ya kuelewa dhambi hiyo mbaya waliyofanyiwa na watu wachache kwa tamaa binafsi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwahakikishia Viongozi hao wa Dini kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejipanga vizuri kupitia vyombo vyake vya ulinzi kwa kupiga Doria maeneo yote katika kuona amani ya nchi inaendelea kudumu.
Aliwapongeza Viongozi hao wa Dini kwa jitihada zao wanazochukuwa za kutumia busara zao kwa kukutana na Viongozi  wa pande mbali mbali za Kisiasa wakilenga kusaidia kutuliza mumkari na machungu ya waumini wao ambao takriban wote ni  wafuasi wa vyama vya Kisiasa vilivyopo hapa Nchini.
Alivilaumu baadhi ya vyombo vya Habari hasa vile vya Nchi za Magharibi jinsi vilivyoonyesha wazi Taarifa zao nyingi  wanazotowa za zoezi zima la uchaguzi Mkuu wa Zanzibar zikionyesha  kuegemea upande mmoja tu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alielezea masikitiko yake juu ya wangalizi wa Kimataifa walioamua kufuatilia uchaguzi Mkuu wa Zanzibar kwamba hawakwenda Kisiwani Pemba muda wote wa zoezi la kupiga kura kufuatilia changamoto zilizojitokeza katika majimbo ya Pemba.
" Nimesikitishwa na waangalizi wa Kimataifa waliokuwepo Zanzibar kwa karibu mwezi mmoja kufuatilia kampeni na uchaguzi wake wameshindwa kwenda Pemba wakati wa zoezi la kupiga kura na kuonekana  zaidi katika majimbo ya Kisiwa cha Unguja.
Balozi Seif aliishauri Idara ya Habari Maelezo kuendelea kufuatilia Taarifa zinazotolewa na vyombo mbali mbali vya Habari ndani na nje ya Nchini na kukemea au kutoa Taarifa dhidi ya uchochezi unaotolewa na vyombo hivyo.
Nao Viongozi hao wa Dini mbali mbali Nchini wameishukuru na kuipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na ile ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hatua iliyochukuwa katika kusimamia amani ya Nchi.
Wananchi wa Zanzibar  wamerejea katika harakati zao za kawaida  za kimaisha  baada ya kutokea hitilafu tofauti ndani ya zoezi zima la upigaji kura kwenye  uchaguzi Mkuu wa Tarehe 25 Mwezi uliopita na kupelekea kuibuka kwa mtafaruku uliotikisa  amani ya Taifa.