Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitoa taarifa rasmi
ya Serikali kuhusu upotoshaji wa baadhi ya vifungu vya sheria unaendelea
kufanywa na baadhi ya viongozi wa Kisiasa juu ya uhalali wa kuendelea
kuwepo madarakani Rais wa Zanzibar. Taarifa hiyo aliitoa katika kituo cha matangazo ya Shirika la Habari Zanzibar {ZBC-TV } Karume House Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Press Release:-
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar imewahakikishia Wananchi wa Zanzibar na
Tanzania kwa ujumla kwamba Rais aliyepo madarakani hivi sasa ataendelea
kushika madaraka ya Urais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi mpaka pale utaratibu wa Kikatiba na Kisheria wa kumpata Rais
utakapokamilika.
Kauli
hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi wakati akitoa Taarifa ya Serikali akisisitiza Taarifa ya awali ya
Serikali iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar kuhusiana na kauli za kupotosha zinazotolewa na baadhi ya
Viongozi wa vyama vya Kisiasa kuhusu uhalali wa kuendelea kuwepo kwa
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliyopo madarakani
pamoja na Serikali yake.
Balozi
Seif aliwaomba Wananchi wazipuuze kauli za upotoshaji zinazotolewa
zikiashira zaidi uvunjifu wa amani na kuwataka waendee kuwa watulivu na
kudumisha amani iliyopo Nchini.
Alisema
Kifungu cha 28 Mbili {a} cha Katiba ambacho kimekuwa kikitumika katika
kutoa tafrisi potofu kwa Wananchi kwamba Rais aliyopo madarakani
atamaliza muda wake wa miaka mitano kuanzia Tarehe ambayo alipokula
kiapo cha uaminifu na kiapo cha kuwa Rais.
Balozi
Seif alieleza kwamba ni dhahiri kwamba dhamira ya kifungu hicho cha
Katiba ilikuwa kuweka bayana kuwa kama uchaguzi Mkuu utafanyika na
msindi wa kiti chja Urais atatangazwa rasmi na Tumen ys Uchaguzi, hivyo
muda wake wa kuendelea Mtu kuwa Rais ungemalizika kwa kufuatana na
masharti ya Kifungu hicho.
Alifafanua
kwa kuwa Tume ya Uchaguzi haikumtangaza mshindi wa kiti cha nafasi ya
Urais ni dhahiri masharti ya kifungu hicho hayataweza kusimama na hivyo
masharti ya Kifungu cha 28 {1} {a} cha Katiba kitakuwa na nguvu za
Kikatiba kumpa uwezo wa Rais aliyopo madarakani kuendelea na madaraka ya
Urais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Alisema
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi anapatikana kwa
mujibu wa masharti ya Kifungu cha 27 cha Katiba ambacho Rais
anachaguliwa kufuatana na Katiba Hiyo na kwa mujibu wa Sheria yoyote
itakayotungwa na Baraza la Wawakilishi hukusu Uchaguzi wa Rais na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Balozi
Seif alifahamisha kuwa ili Rais wa Zanzibar apatikane kwa mujibu wa
Katiba na sheria ya Uchaguzi nambari 11 ya Mwaka 1984, Tume ya Uchaguzi
ya Zanzibar inapaswa kuendesha uchaguzi na hatimae kumtangaza mshindi wa
nafasi ya Urais ambae atashika madaraka hayo pale ambapo atakuwa
ameapishwa rasmi kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Katiba ya Zanzibar.
Alisema
Kifungu cha 28 {1} {a} cha Katiba kinaweka utaratibu kuhusu muda wa
kuendelea kuwa kuwa Rais, na kwamba kwa kufuatana na kifungu hicho, mtu
aliyechaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi ataendelea na dhamana hiyo mpaka pale ambapo Rais anayefuata
ale kiapo cha kuwa Rais.
Alieleza
kwamba kwa msingi huo wa Kikatiba ni vyema Wananchi wakafahamu na
kuelewa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Braza la Mapinduzi
ataendelea kuwepo madarakani mkapa pale Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar
itakapomtangaza mshindi wa kiti cha Urais na Rais Mteule atashika
madaraka hayo baada ya kuapishwa rasmi kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha
Katiba.