Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi

Mwanafunzi Isra Hilal Mwadini akifuatiwa na mwenzake Tamima Abass Sheha wakipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wakati wa hafla ya Maulidi ya Jumuiya ya Chuo cha Samael Academy.Kulia ya Balozi Seif ni Rais wa Sameil Academy Sheikh Nassir Bin Said.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizindua rasmi Bara bara ya pili ya Amani hadi Mtoni baada ya kukamilika awamu ya mwisho ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Akiwa na Balozi mdogo wa India nchini Tanzania wakiangalia maonyesho yaliofanya na Msanii kutoka India, Bi Navi Madhav hapo Ngome Kongwe

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Dk. Khalid S. Mohamed

akizungumza na Wadau wa Maendeleo wa Mfuko wa TASAF, walipofika Ofisini kwake kuzungumzia maendeleo ya Mfuko wa TASAF III,na kutembelea Mradi wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini (PSSN) katika Jimbo la Muyuni Wilaya ya Kusini Unguja katika Kijiji cha Muyuni B

Wazir wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakifurahia jambo wakati wa semina ya siku moja kuhusu matokeo makubwa na ya haraka katika kuleta mageuzi ya kiuchumi na kuleta maendeleo nchini iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein

Tuesday, 23 September 2014

Dk Shein Ahudhuria Sherehe za Miaka 50 ya Elimu Bila Malipo Viwanja vya Amaan

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono wanafunzi waliopita mbele ya jukwaa la viongozi katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Zanzibar wakati wa sherehe za kilele cha miaka 50 ya Elimu bila Malipo zilizofanyika leo.
 Wanafunzi wa Skuli ya wanawake ya Al- Ihsaan ya Magogoni Jitmai wakipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akipokea maandamano ya wanafunzi wa skuli mbali mbali za Unguja na Pemba katika sherehe za miaka 50 ya Elimu bila malipo zilizofanyika kitaifa katika uwanja wa Amaan Studium leo
Wanafunzi wa Chuo cha Ufundi JKU wakipita mbele  ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akipokea maandamano ya wanafunzi wa skuli mbali mbali za Unguja na Pemba katika sherehe za miaka 50 ya Elimu bila malipo zilizofanyika kitaifa katika uwanja wa Amaan Studium leo
Wanafunzi wenye ulemavu  tofauti wakipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kwa maandano wakati wa sherehe za  miaka 50 ya Elimu bila Malipo zilizofanyika katika uwanja wa amaan Studium

Walimu na Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Taifa SUZA wakipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  wakati wa  maandamo ya kusherehekea kilele cha miaka 50 ya Elimu bila malipo ilizofanyika katika uwanja wa amaan Studium
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Walimu na Wanafunzi katika Sherehe za Miaka 50 ya Elimu bila malipo zilizofanyika kitaifa katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja leo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi kombe Msaidizi Afisa Elimu Mkoa wa Kaskazini Unguja Maulid Nafasi Juma wakati wa  Sherehe za Miaka 50 ya Elimu bila malipo zilizofanyika kitaifa katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja leo
Baadhi ya wanafunzi wa Skuli mbli mbli za Sekondari wakiwa katika jukwaa wakati wa sherehe za Miaka 50 ya Elimu bila malipo zilizofanyika kitaifa katika Uwanja wa Amaan Studium 
Baadhi ya Viongozi waliohudhuria katika sherehe za miaka 50 ya Elimu bila Malipo zilizofanyika katika uwanja wa Amaan Studium na mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
Baadhi ya walimu wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  wakati alipokuwa akizungumza na Walimu, Wazee,Wanafunzi katika  sherehe za kilele cha miaka 50 ya Elimu bila Malipo zilizofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Zanzibar(Picha na Ramadhan Othman Ikulu)





Thursday, 18 September 2014

Dk.Shein awasili Zanzibar akitokea ziarani Nchini Comoro.


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mojhamed Shein, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi alipowasili Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume akirejea ziarani Nchini Comoro alipokuwa katika ziara ya siku nne ya Kiserekani. kulia Mama Mwanamwema Shein, wakati walipowasili Zanzibar leo mchana.  
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na Mama Mwanamwema Shein, wakisalimiana na Wazee waliofika uwanja wa ndege kumpokea akitokea Nchini Comoro kwa ziara ya Kiserekali ya siku nne. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Makamanda wa Ulinzi na Usalama waliofika kumpokea leo mchana akitokea Nchini Comoro. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar wakiwa katika ukumbi wa VIP,kabla ya kuzungumza na waandishi. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Zanzibar akitokea ziarani Comoro, Katika mazungumzo hayo amezungumzia mafanikio ya ushirikiano baina ya Comoro na Zanzibar katika nyanja za Utalii na Biashara kati ya Zanzibar na Comoro
Waandishi wa habari wakifuatilia mazungumzo ya Rais Shein alipokuwa akieleza mafanikio ya ziara yake Comoro.

Wednesday, 17 September 2014

Balozi Seif aiagiza Wizara ya Miundu mbinu na Mawasiliano kuifanyia matengenezo makubwa barabara ya Donge Mtambile - Muwanda


 Baadhi ya Wananchi wa Vijiji vya  Donge Mchangani na Donge Muwanda wakiwa katika Mkutano wa kueleza kero zinazowakabili walizoziwasilisha kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo katika Ukumbi wa Skuli ya Sekondaro ya Muwanda Wilaya ya Kaskazini “ B “.
 Baadhi ya Wananchi wa Vijiji vya  Donge Mchangani na Donge Muwanda wakiwa katika Mkutano wa kueleza kero zinazowakabili walizoziwasilisha kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo katika Ukumbi wa Skuli ya Sekondaro ya Muwanda Wilaya ya Kaskazini “ B “.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wananchi wa Donge Munda na Donge Mchangani mara baada ya kupokea changamoto zinazowakabili Wananchi hao
Bibi Halima Haji Omar akimueleza Balozi Seif changamoto zinazowakabili wana Saccos wa Donge Muwanda na Mchangani ya ukosefu wa mashine ya kusukumia maji kwa ajili ya uzalishaji wa mazao yao tatizo ambalo Balozi Seif aliwaahidi kulitatua kwa kuwapatia Mashine  hiyo.

Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

Na Othman Khamis Ame , OMPR
 
Wizara ya Miundo Mbinu na Mawasiliano Zanzibar imeagizwa kuchukuwa tatua za dharura za kuifanyia matengenezo makubwa Bara bara ya Donge Mtambile hadi Muwanda pwani ili kuwapunguzia usumbufu wa muda mrefu wanaoupata Wananchi wa eneo hilo hasa wakati wa mvua.
 
Agizo hilo limetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akizungumza na Wananchi wa Donge Mchangani na Muwanda katika Mkutano wa kupokea kero za Wananchi hao uliofanyika katika Ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Muwanda.
 
Balozi Seif alisema nia ya Serikali Kuu ni kuhakikisha kwamba maeneo yote Mijini na Vijijini yanatengenezewa   miundo mbinu mizuri ya bara bara na Mawasiliano ili kuyajengea mazingira murwa  na uwezo wa uzalishaji maeneo hayo.
 
Alisema vijiji vya Donge Muwanda na Mchangani vimebarikiwa kuwa na ardhi ya rutba inayozalisha vyakula vingi vya mizizi, mboga mboga  na nafaka hivyo juhudi za Serikali zitahitajika kufanywa ili kuwajengea mfumo mzuri wa bara bara wakulima wa maeneo hayo kupelekea mazao yao kwenye masoko.

 
Alieleza kwamba Wizara ya Miundo mbinu na Mawasiliano italazimika kutekeleza kazi hiyo kwa hatua ya awali ya uwekaji Kifusi ili kupunguza mashimo wakati nguvu za muda mrefu zitawekwa katika kuiwekeza lami na kudumu kwa kipindi kirefu zaidi.
“ Nia ya Serikali Kuu wakati wote ni kuona inatengeneza bara bara zote kuu na hata zile zenye kuelekea kwenye maeneo ya  uzalishaji wa mazao ya kilimo na biashara “. Alisema Balozi Seif.
Aliwapongeza Wananchi wa Vijiji hivyo viwili kwa ustahamilivu wao wa muda mrefu waliouonyesha kutokana na ukosefu wa miundo mbinu ya bara bara na kuwashukuru kwa kazi kubwa wanaoendelea kuichukuwa katika kuimarisha mazao ya kilimo.
 
Akigusia suala la uharibifu wa mazingira unaoonekana kuikumba mno Wilaya ya Kaskazini “B “ Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliwaomba wananchi wa Wilaya hiyo kuwa mstari wa mbele katika kukabiliana pamoja na kudhibiti uchafuzi wa mazingira.
 
Balozi Seif alisema kasi ya uchimbaji wa mchanga ndani ya Wilaya ya Kaskazini “ B” hivi sasa inatisha jambo ambalo itafikia wakati wakulima ndani ya Wilaya hiyo kukosa maeneo ya kilimo yenye rutba.
 
Alifahamisha kwamba kutokana na kasi hiyo anatarajia kuiagiza Idara ya Misitu na mali zisizorejesheka Zanzibar kupunguza kasi ya utoaji wa vibali vya uchimbaji mchanga katika Wilaya ya Kaskazini “ B “.
 
Balozi Seif aliongeza kwamba kasi ya uchimbaji mchanga hivi sasa inahatarisha hata miundo mbinu ya umeme inayopelekea baadhi ya nguzo za waya mkubwa wa huduma hiyo kuwa hatarini kuanguka.
 
“ Uchimbaji wa mchanga kwa jinsi ulivyoshamiri  hivi sasa kwa kisingizio cha mchanga wa Kakaskazini “ B “ ni mzuri na bora kwa  ufyatuaji matofali kuliko pengine popote pale hapa Zanzibar unahatarisha hata nguzo kubwa za miundo mbinu ya umeme kuanguka “. Alitahadharisha Balozi Seif.
 
Kuhusu Katiba Mpya ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema mchakato huo hivi sasa unaendelea  vyema katika Mbunge Maalum la Katiba mjini Dodoma na matarajio makubwa ni kukamilika ifikapo Oktoba 4 Mwaka huu.
 
Balozi Seif aliwanasihi Wananchi watakapopelekewa Katiba Mpya waiunge mkono kwa kuipigia kura kwa vile mfumo wa muundo wa Katiba uliopendekezwa na Wabunge walio wengi ndani ya Bunge hilo ndio wenye muelekeo wa kulinda Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania iliyopo kwa karibu miaka 50 sasa.
 
Alisema nje ya muundo huo uliopendekezwa na wengi kwa hali halisi ya siasa ya Tanzania inavyotaka kupelekwa na baadhi ya wanasiasa ni kutaka kuhatarisha Muungano uliopo sasa.
 
Mapema akisoma Risala ya Wananchi hao wa Vijiji vya Donge Muwanda na Donge Mchangani Bwana Ahmed Abdulla alielezea changa moto zinazowakabili Wananchi hao katika harakati zao za kila siku.
 
Bwana Ahmed alizitaja changa moto hizo kuwa ni ubovu wa Bara bara yao, ukosefu wa huduma za Maji safi na salama, Deni la Kituo cha Ualimu, pamoja na ukosefu wa zana za kilimo na Trekta.
 
Katika Mkutano huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliahidi kulilipa Deni la Kituo hicho cha Ualimu la Shilingi Laki 9000,000 /-, kusaidia Kompyuta, mashine ya Foto Kopi pamoja na kuomba kupatia gharama za ujenzi wa vyoo vya Kituo hicho.
Pia Balozi Seif akaahidi kuvipatia mashine ya kusukumia maji kwa ajili ya uzalishaji wa mazao ya kilimo wana vikundi vya ushirika vya Vijiji vya Donge Mchangani na Donge Muwanda ikienda sambamba na  kufuatilia tatizo la Maji safi na salama kupitia Mamlaka ya Maji Zanzibar { ZAWA }.
 

Tuesday, 16 September 2014

Dk Shein akutana na Rais wa Comoro Dr Ikililou Dhoinine kwa mazungumzo


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mawaziri mbali mbali  wakati alipowasili katika   Ikulu ya Comoro kwa mazungumzo na Rais wa Nchi hiyo Dr. Ikililou Dhoinine jana akiwa katika ziara ya kiserikali,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa katika mazungumzo na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Comoro Dr.Ikililou Dhoinine Ikulu Mjini Comoro jana,Dk.Shein yupo Comoro kwa ziara ya kiserikali akiwa na ujumbe aliofuatana nao. [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Comoro Dr.Ikililou Dhoinine (katikati) wakiwa katika mazungumzo ya pamoja na ujumbe wa Rais na Viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Comoro   Ikulu Mjini Comoro jana katika  ziara ya kiserikali akiwa na ujumbe aliofuatana nao. [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Comoro Dr.Ikililou Dhoinine baada ya  mazungumzo Ikulu Mjini Comoro jana,akiwa katika  ziara ya kiserikali  na ujumbe aliofuatana nao. [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

 Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akiwa na Mke wa Rais wa Jamuri ya Muungano wa Comoro Mama Dhoinine wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Comoro Dr.Ikililou Dhoinine katika viwanja vya Ikulu ya Comoro jana. [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiteta na  mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Comoro Dr.Ikililou Dhoinine Ikulu Mjini Comoro jana, wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa ujumbe Serikali ya Mapinduzi ukiwa katika ziara Nchini Comoro. [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Rais wa Jamuri ya Muungano wa Comoro Dr.Ikililou Dhoinine wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa ujumbe Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika ziara ya kiserikali nchini Comoro. [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

Sunday, 14 September 2014

Wadau wa Maendeleo wa Mfuko wa TASAF Watembelea Wananchi walioko katika Mpango wa Kaya Masikini Kijiji cha Muyuni B Zanzibar.

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Tanzania Ndg. Ladislaus Mwamanga, akitowa maelezo na kuufahamisha Ujumbe wa Wadau kutoka Benki ya Dunia wanaochangia  Mfuko wa Tasaf awamu ya Tatu, kuhusiana na Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (PSSN) ulipofika kuonana na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Dk.Khalid  S. Mohamed, Ofisini kwake Vuga Zanzibasr.
Wadau wa Maendeleo wa Mfuko wa Benki ya Dunia wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Dk. Khalid S. Mohamed, akitowa maelezo ya mafanikio ya Mfuko wa Tasaf katika Jamii ilivyotowa matunda katika sekta mbalimbali wakati wa kutathimini mafanikio yake Tasaf III.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Dk. Khalid S. Mohamed, akizungumza  na Wadau wa Maendeleo wa Mfuko wa TASAF, walipofika Ofisini kwake kuzungumzia  maendeleo ya Mfuko wa TASAF III, na kutembelea  Mradi wa Mpango wa Kunusuru  Kaya masikini (PSSN) katika  Jimbo la Muyuni Wilaya ya Kusini Unguja katika Kijiji cha Muyuni B
Wadau wa Maendeleo wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Dk. Khalid S. Mohamed, akizungumza na ujumbe huo uliofika  Ofisini kwake Vuga, kutoka kushoto Ndg. Manuel A.Salazar, (Lead Social Protection Specialist Eastern and Southern Africa) Bi Ida Manjolo,Afisa Benki ya Dunia Dar-es-Salaam, Bi Usha Mishra (Chief Social Policy Anylsis and Development).wakifuatilia mazungumzo hayo katika ukumbi wa mkutano Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Vuga Zanzibar,
Ujumbe wa Wadau wa Maendeleo wakiwasili katika viwanja vya Skuli ya Muyuni B kuonana na Wanakaya wa kijiji hicho kupata maelezo ya mafanikio ya Mradi wa Mpando wa kunusuru Kaya Masikini (PSSN) Jumla ya Kaya 74 zinanufaika na mpango huo wa kunusuru kaya masikini Zanzibar. kwa kijiji cha Muyuni B.
Mkurugenzi wa  Mratibu wa Shughuli za Serikali Zanzibar Ndg. Issa Ibrahim, akitowa maelezo kwa Ujumbe wa Wadau wa Maendeleo wa Benki ya Dunia walipofika katika Kijiji cha Muyuni B Unguja kuonana na Wananchi wa Kaya 74 zinazonufaika na Mpando wa Kunusuru Kaya Masikini unaosimamiwa na TASAF awamu ya III,
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ndg, Ladislaus Mwamanga, akizungumza na kuwatambulisha Wadau wa Maendeleo wa Benki ya Dunia wanaochangia Mfuko wa Tasaf, akizungumza na Wananchi hao wakati wa ziara hiyo ya kutathimini mafanikio ya Mpango huo wa Kunusuru Kaya Masikini katika Kijiji cha Muyuni B Unguja.

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dk. Idris Muslim Hijja akizungumza wakati wa hafla ya kutembelea Kijiji cha Muyuni B, Ujumbe wa Wadau wa Maendeleo wa Benki ya Dunia kuangalia na kutathimini mafanikio ya Tasaf III, katika Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini, katika wananchi wa Kijiji hicho na kusikiliza maoni yao juu ya mpango huo.
Wadau wa Maendeleo wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kusini, Unguja Mhe. Dk. Idris Muslim Hijja akizungumza wakati wa hafla hiyo, kutoka kulia Mwakilishi wa Benki ya Dunia Ndg. Muderis  Abdulahi Mohammed, Afisa wa Benki ya Dunia Dar-se-Salaam Bi Ida Monjolo, Afisa wa Benki ya Dunia Kusini na Kaskazini ya Afrika, Ndg.Manuel A.Salazar na Mwakilishi wa Unicef Bi Usha Mishra.  
Mwanakaya wa Kijijin cha Muyuni B akisoma risala kwa Wananchi wa Kijiji cha Muyuni B, kutokana na mafanikio ya mgao wa Fedha kwa ajili ya Mpango wa Kunusuru Kaya  Masikini (PSSN) unaosimamiwa na Tasaf III, Jumla Kaya 74 zimenufaika na mpango huo na tayari wameshagawiwa shilingi milioni karibu kumi na moja na kupata mafanikio kwa walengwa na mpango huo, na kuongezeka watoto kwenda skuli na wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano kuhudhuria kliniki. 
Maofisa wa Mfuko wa TASAF Tanzania wakifuatilia hafla hiyo na Wanakaya wa Kijiji cha Muyuni B kutoa maelezo ya mafanikio kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini.hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya skuli ya muyuni B, Wilaya ya Kusinu Unguja.
Wananchi wa Kaya 74 zinazofaidika na Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kijiji cha Muyuni B, wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ndg. Ladislaus Mwamanga, akizungumza katika hafla hiyo kwa wananchi wa kijiji cha muyuni.
Mwakilishi wa Benki ya Dunia katika Afrika Ndg. Manuel A Salazar, akiuliza katika mkutano huo na Wananchi wa Kaya 74 zinazofaidika na Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kijiji cha  Muyuni B, jinsi wanavyofaidika na mpango huo, tokea walivyopata mgao huo.
Mwakilishi wa Benki ya Dunia Ndg.Muderis  Abdulahi Mohammed,akizungumza katika mkutano huo na Wananchi wa kijiji cha Muyunio B, wakati walipofika kuangalia na kujuwa mafanikio waliyoyapata. 
Mkurugenzi Miradi wa TASAF Ndg. Amadeus Kamagenge, akitowa maelezo kwa  wananchi wa kijiji cha Muyuni B. kuja kwa Ujumbe wa Benki ya Dunia kutaka kujua mafanikio na matatizo ya Mradi wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini(PSSN) kutoka kwao. walengwa na mpango huo.  
Sheha wa Shehia ya Muyuni B, Mhe. Ali Haji Mume, akizungumza katika mkutano huo na Wadau wa Maendeleo wa Benki ya Dunia katika mkutano wa kutathimini mafanikio ya mpango wa kunusuru kaya masikini, uliofanyika katika viwanja vya skuli ya msingi muyuni B,