Sunday, 14 September 2014

Wadau wa Maendeleo wa Mfuko wa TASAF Watembelea Wananchi walioko katika Mpango wa Kaya Masikini Kijiji cha Muyuni B Zanzibar.

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Tanzania Ndg. Ladislaus Mwamanga, akitowa maelezo na kuufahamisha Ujumbe wa Wadau kutoka Benki ya Dunia wanaochangia  Mfuko wa Tasaf awamu ya Tatu, kuhusiana na Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (PSSN) ulipofika kuonana na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Dk.Khalid  S. Mohamed, Ofisini kwake Vuga Zanzibasr.
Wadau wa Maendeleo wa Mfuko wa Benki ya Dunia wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Dk. Khalid S. Mohamed, akitowa maelezo ya mafanikio ya Mfuko wa Tasaf katika Jamii ilivyotowa matunda katika sekta mbalimbali wakati wa kutathimini mafanikio yake Tasaf III.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Dk. Khalid S. Mohamed, akizungumza  na Wadau wa Maendeleo wa Mfuko wa TASAF, walipofika Ofisini kwake kuzungumzia  maendeleo ya Mfuko wa TASAF III, na kutembelea  Mradi wa Mpango wa Kunusuru  Kaya masikini (PSSN) katika  Jimbo la Muyuni Wilaya ya Kusini Unguja katika Kijiji cha Muyuni B
Wadau wa Maendeleo wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Dk. Khalid S. Mohamed, akizungumza na ujumbe huo uliofika  Ofisini kwake Vuga, kutoka kushoto Ndg. Manuel A.Salazar, (Lead Social Protection Specialist Eastern and Southern Africa) Bi Ida Manjolo,Afisa Benki ya Dunia Dar-es-Salaam, Bi Usha Mishra (Chief Social Policy Anylsis and Development).wakifuatilia mazungumzo hayo katika ukumbi wa mkutano Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Vuga Zanzibar,
Ujumbe wa Wadau wa Maendeleo wakiwasili katika viwanja vya Skuli ya Muyuni B kuonana na Wanakaya wa kijiji hicho kupata maelezo ya mafanikio ya Mradi wa Mpando wa kunusuru Kaya Masikini (PSSN) Jumla ya Kaya 74 zinanufaika na mpango huo wa kunusuru kaya masikini Zanzibar. kwa kijiji cha Muyuni B.
Mkurugenzi wa  Mratibu wa Shughuli za Serikali Zanzibar Ndg. Issa Ibrahim, akitowa maelezo kwa Ujumbe wa Wadau wa Maendeleo wa Benki ya Dunia walipofika katika Kijiji cha Muyuni B Unguja kuonana na Wananchi wa Kaya 74 zinazonufaika na Mpando wa Kunusuru Kaya Masikini unaosimamiwa na TASAF awamu ya III,
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ndg, Ladislaus Mwamanga, akizungumza na kuwatambulisha Wadau wa Maendeleo wa Benki ya Dunia wanaochangia Mfuko wa Tasaf, akizungumza na Wananchi hao wakati wa ziara hiyo ya kutathimini mafanikio ya Mpango huo wa Kunusuru Kaya Masikini katika Kijiji cha Muyuni B Unguja.

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dk. Idris Muslim Hijja akizungumza wakati wa hafla ya kutembelea Kijiji cha Muyuni B, Ujumbe wa Wadau wa Maendeleo wa Benki ya Dunia kuangalia na kutathimini mafanikio ya Tasaf III, katika Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini, katika wananchi wa Kijiji hicho na kusikiliza maoni yao juu ya mpango huo.
Wadau wa Maendeleo wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kusini, Unguja Mhe. Dk. Idris Muslim Hijja akizungumza wakati wa hafla hiyo, kutoka kulia Mwakilishi wa Benki ya Dunia Ndg. Muderis  Abdulahi Mohammed, Afisa wa Benki ya Dunia Dar-se-Salaam Bi Ida Monjolo, Afisa wa Benki ya Dunia Kusini na Kaskazini ya Afrika, Ndg.Manuel A.Salazar na Mwakilishi wa Unicef Bi Usha Mishra.  
Mwanakaya wa Kijijin cha Muyuni B akisoma risala kwa Wananchi wa Kijiji cha Muyuni B, kutokana na mafanikio ya mgao wa Fedha kwa ajili ya Mpango wa Kunusuru Kaya  Masikini (PSSN) unaosimamiwa na Tasaf III, Jumla Kaya 74 zimenufaika na mpango huo na tayari wameshagawiwa shilingi milioni karibu kumi na moja na kupata mafanikio kwa walengwa na mpango huo, na kuongezeka watoto kwenda skuli na wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano kuhudhuria kliniki. 
Maofisa wa Mfuko wa TASAF Tanzania wakifuatilia hafla hiyo na Wanakaya wa Kijiji cha Muyuni B kutoa maelezo ya mafanikio kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini.hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya skuli ya muyuni B, Wilaya ya Kusinu Unguja.
Wananchi wa Kaya 74 zinazofaidika na Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kijiji cha Muyuni B, wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ndg. Ladislaus Mwamanga, akizungumza katika hafla hiyo kwa wananchi wa kijiji cha muyuni.
Mwakilishi wa Benki ya Dunia katika Afrika Ndg. Manuel A Salazar, akiuliza katika mkutano huo na Wananchi wa Kaya 74 zinazofaidika na Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kijiji cha  Muyuni B, jinsi wanavyofaidika na mpango huo, tokea walivyopata mgao huo.
Mwakilishi wa Benki ya Dunia Ndg.Muderis  Abdulahi Mohammed,akizungumza katika mkutano huo na Wananchi wa kijiji cha Muyunio B, wakati walipofika kuangalia na kujuwa mafanikio waliyoyapata. 
Mkurugenzi Miradi wa TASAF Ndg. Amadeus Kamagenge, akitowa maelezo kwa  wananchi wa kijiji cha Muyuni B. kuja kwa Ujumbe wa Benki ya Dunia kutaka kujua mafanikio na matatizo ya Mradi wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini(PSSN) kutoka kwao. walengwa na mpango huo.  
Sheha wa Shehia ya Muyuni B, Mhe. Ali Haji Mume, akizungumza katika mkutano huo na Wadau wa Maendeleo wa Benki ya Dunia katika mkutano wa kutathimini mafanikio ya mpango wa kunusuru kaya masikini, uliofanyika katika viwanja vya skuli ya msingi muyuni B,