Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mojhamed Shein, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi alipowasili Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume akirejea ziarani Nchini Comoro alipokuwa katika ziara ya siku nne ya Kiserekani. kulia Mama Mwanamwema Shein, wakati walipowasili Zanzibar leo mchana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na Mama Mwanamwema Shein, wakisalimiana na Wazee waliofika uwanja wa ndege kumpokea akitokea Nchini Comoro kwa ziara ya Kiserekali ya siku nne.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Makamanda wa Ulinzi na Usalama waliofika kumpokea leo mchana akitokea Nchini Comoro.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar wakiwa katika ukumbi wa VIP,kabla ya kuzungumza na waandishi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Zanzibar akitokea ziarani Comoro, Katika mazungumzo hayo amezungumzia mafanikio ya ushirikiano baina ya Comoro na Zanzibar katika nyanja za Utalii na Biashara kati ya Zanzibar na Comoro
Waandishi wa habari wakifuatilia mazungumzo ya Rais Shein alipokuwa akieleza mafanikio ya ziara yake Comoro.