Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi

Mwanafunzi Isra Hilal Mwadini akifuatiwa na mwenzake Tamima Abass Sheha wakipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wakati wa hafla ya Maulidi ya Jumuiya ya Chuo cha Samael Academy.Kulia ya Balozi Seif ni Rais wa Sameil Academy Sheikh Nassir Bin Said.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizindua rasmi Bara bara ya pili ya Amani hadi Mtoni baada ya kukamilika awamu ya mwisho ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Akiwa na Balozi mdogo wa India nchini Tanzania wakiangalia maonyesho yaliofanya na Msanii kutoka India, Bi Navi Madhav hapo Ngome Kongwe

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Dk. Khalid S. Mohamed

akizungumza na Wadau wa Maendeleo wa Mfuko wa TASAF, walipofika Ofisini kwake kuzungumzia maendeleo ya Mfuko wa TASAF III,na kutembelea Mradi wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini (PSSN) katika Jimbo la Muyuni Wilaya ya Kusini Unguja katika Kijiji cha Muyuni B

Wazir wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakifurahia jambo wakati wa semina ya siku moja kuhusu matokeo makubwa na ya haraka katika kuleta mageuzi ya kiuchumi na kuleta maendeleo nchini iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein

Sunday, 16 November 2014

Balozi Seif Akizungumza na Ujumbe wa Makampuni ya Uwekezaji China. Wakati wa Ziara yake katika mjini wa Hainan China

Makamu wa Rais wa Kiwanda cha Dawa za Binaadamu cha Shuangcheng Bwana Jianlin Yuan akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na Ujumbe wake wakati walipotembelea kiwanda hicho wakiwa katika ziara ya Kiserikali Katika Jimbo la Kisiwa cha Hainan.
Ujumbe wa Zanzibar Ukiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ukifanya azungumzo na Ujumbe wa Makampuni ya uwekezaji vitega uchumi katika Jimbo la Hainan ukiongozwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Nyumba na Maendeleo ya Miji na Vijiji ya Hainan.
 Balozi Seif na Ujumbe wake wakiwa katika kikao cha pamoja cha ushirikiano kati ya Zanzibar na Uongozi wa Manispaa ya Mji wa  Haikou ukiongozwa na Meya wa Mji Huo Mstahiki NI Qiang.
Mwenyekiti wa Kiwanda cha kusindika bidhaa za nazi pamoja na matunda  kiliopo Haikuu Bwana Huang Chunguang akimfahamisha Balozi Seif na Ujumbe juhudi zinazochukuliwa na Kiwanda hicho katika kulitumia vyema zao la nazi.Kushoto ya Balozi Seif ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi na Kulia yake ni Waziri wa Ardhi Mh. Ramadhan Abdulla Shaaban na Waziri wa Habari Mh. Sai Ali Mbarouk.(Picha na Hassan Issa OMPR  China)




Makampuni na Taasisi mbali mbali za uwekezaji wa miradi ya Kiuchumi na maendeleo katika Jimbo la Kisiwa cha Hainan yameombwa kuzitumia taaluma zao kwa kufanya utafiti utakaoyawezesha Makampuni hayo kutumia fursa za uwekezaji zilizopo ndani ya Visiwa vya Zanzibar. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitoa ombi hilo wakati akizungumza na Viongozi wa Taasisi  an makampuni hayo katika mikutano tofauti akiwa katika ziara ya Kiserikali kwenye Kisiwa rafiki cha Jimbo la Hainan Nchini Jamuhuri ya Watu wa China.

Balozi Seif alisema wakati Zanzibar inaendelea kufungua milango ya uwekezaji katika kuimarisha uchumi wake  fursa ziko wazi kwa wawekezaji wa Jamuhuri ya Watu wa China hasa Kisiwa cha Hainankuitumia nafasi. Alisema ipo miradi mbali mbali inayoweza kuanzishwa na Kampuni za China hapa Zanzibarf kwa lengo la kutoa huduma ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki pamoja na Nchi wa Kusini mwa Afrika { SADC }.

Balozi Seif aliitaja baadhi ya miradi inayoweza kuwekezwa na Makampuni hayo kuwa ni pamoja na Viwanda vidogo vidogo vya Dawa, za Binaadamu, Vyakula vya Matunda, usindikaji wa Samaki pamoja na vifaa vya Kilimo ambavyo 
pia
 vinaweza
 kusaidia kupunguza tatizo la ajira.

Aliwaeleza Viongozi wa Taasisi hizo kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibarf { ZIPA } iko tayari na huru kushirikiana na taasisi zote zitakazojitokeza kuonyesha nia ya kutaka kuwekeza Zanzibar.


 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliipongeza Jamuhuri ya Watu wa China kwa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika harakati zake za Maendeleo jambo ambalo ni ushahidi unaothibitisha uhusiano wa muda mrefu kati ya China na Zanzibar na Tanzania kwa jumla.

Naye Kiongozi wa Makampuni na Taasisi hizo za Kisiwa cha Jimbo la Hainan Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Nyumba na Maendeleo ya Miji na Vijiji Bwana Du Haiying alisema Taasisi zao zimeanzishwa kwa lengo la kustawisha Uchumi na ustawi wa Jamii.

Bwana Du Haiying alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwamba Makampuni mengi ya Jamuhuri ya Watu wa China hivi sasa yanaendelea kuunga mkono sera za China katika kuimarisha uhusiano na Mataifa mbali mbali ya Bara la Afrika.

Bwana Du alifahamisha kwamba ziara za mara kwa mara za Viongozi wa juuwa Serikali ya China wakiongozwa na Rais wa Bwana Xi Jinping katika nchi tifauti za Afrika zinania ya kuunga mkono maendeleo ya Bara la Afrika.

Mapema Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh.Said Ali Mbarouk alisema Zanzibar kupitia Kamisheni yake ya Utalii hivi sasa iko katika juhudi za kujitangaza kiutalii kwa kufungua ofisi katika Mji mbali mbali Duniani.Mh. Mbarouk alisema juhudi hizo zimelenga kuongeza idadi ya wageni na watalii wanaoingia Zanzibar ambao wengi kati yao hutokea nchi za Ulaya, Marekani , Nchi za Scandnavia na baadhi ya nchi za Afrika.


Waziri Mbarouk aliwataja baadhi  ya watalii wanaoingia Zanzibar wengi kati yao wanatoka Italy, Ujerumani, Uingereza, Nchi za Scandinavia, Afrika Kusini, Marekani, Uholanzi na nchi chache za Bara la Afrika.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo alisema China ni nchi ya mwisho watalalii wake wanaofanya ziara za Matembezi Zanzibar kiwango ambacho hakilingani na idadi ya watalii wa Nchi hiyo wanaofikia Milioni Moja kwa Mwaka.
Akitoa ufafanuzi kwa viongozi hao wa Mashirika na Taasisi mbali mbali za uwekezaji za Kisiwa cha Jimbo la Hainan Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji Vitegha Uchumi Zanzibar { ZIPA } Nd. Salum Nasso Khamis alisema Muwekezaji anaruhusika kuwekeza mradi wake mara baada ya kukamilisha taratibu  za Mamlaka zinazohusika.


Nd. Salum alisema hatua ya mwanzo anayotakiwa muwekezaji kuifanya ni pamoja na kuandika maombi ya mradi anaotaka kuutekeleza pamoja na vielelezo vyote vitakavyompa urahisi wa kukubalika maombi yake bila ya usumbufu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Ujumbe wake amemaliza ziara yeka Katika Kisiwa cha Jimbo la Hainan kwa kutembelea eneo huru la uwekezaji vitega uchumi pamoja na Kwanda cha kusindika samaki Mjini Haikou.


Ujumbe huo pia ulipata fura sa kuangalia Bandari mpya ya Kisasa ya Sanya inayohudumia meli kubwa  za utalii, abiria ,mizigo pamoja na kukagua ujenzi wa nyumba za wafanyakazi na makazi ya wananachi zinazouzwa kwa mkopo nafuu.
Halikadhalika  ziara ya ujumbe huo wa Zanzibar pia ilifika na kuangalia uzalishaji katika kiwanda cha Dawa cha Hainan pamoja na Kiwanda cha uzalishaji wa biadhaa mbali mbali za nazi na baadhi ya matunda yanayootehswa kwenye kisiwa hicho.


Kesho Balozi Seif anatarajiwa kwenda katika Mji wa shenzhen kuendelea na ziara yake kwa kutembelea Makao Makuu ya Kampuni ya Huawei inayoshughulikia masuala ya Teknolojia ya Kisasa { ICT } kabla ya kumaliza ziara yake Mjini Beijing.

Thursday, 13 November 2014

Makamu wa Rais Balozi Seif Aza ziara kutembelea Sekta ya Uchumi China


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na ujumbe wake wakifuatana na mwenyeji wao Mkuu wa Kijiji cha Uwekezaji wa Mji wa Chengmai Bwana Yang Si Tao wakielekea ukumbi wa mkutano kwa mazungumzo.
Kulia ya Balozi Seif ni Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA Nd. Salum Nassor Khamis, Mkurugenzi Mambo ya Nje Zanzibar Balozi Silima Kombo haji.
Mkuu wa Kijiji cha Maeneo huru ya uwekezaji katika Mji wa Chengmai aliyevaa shati jeupe Bwana Yang Si Tao akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Balozi Seif aliyepo kushoto yake wakati ujumbe wa Zanzibar ulipoangalia maeneo hayo ukiwa katika  ziara ya siku 10 Jimboni Hainan
Ujumbe wa Zanzibar ukiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na Ule mwenjeji wa
Hainan ukiongozwa na Gavana wa Jimbo hilo Bwana Jian Dingzhi ukiendelea na mazungumzo yao ya uhusiano hapo katika Hoteli ya Le Meriden Mjini Haikou.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akimkabidhi zawadi wa Kasha lililojaa vyakula vya viungo { spices } Gavana wa Jimbo la Hainan Bwana Jian, Dingzhi mara baada ya kumaliza mkutano wao rasmi wa
ushirikiano.

Gavana wa Jimbo la Kisiwa cha Hainan Bwana Jian Dingzhi akibadilishana mawazo na Mgeni wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.(Picha na Hassan Issa, OMPR China)  


Uongozi wa Kisiwa cha Jimbo la Hainan Nchini Jamuhuri ya Watu wa China iko tayari wataalamu na awekezaji wake kufungua milango ya uwekezaji katika Visiwa vya Zanzibar katika miradi ya Kilimo, Utalii na Mazao ya Baharini kwa lengo la kusaidi maendeleo ya Zanzibar.



Gavana wa Jimbo la Hainan Bwana Jian Dingzhi alitoa kauli hiyo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  na ujumbe wake ambao umenza ziara rasmi ya Kiserikali ya Siku Kumi katika Jimbo hilo hapo Hoteli ya Le Meriden Mji Mkuu wa Kisiwa hicho wa Haikou.



Bwana Jiang Dinmgzhi alimueleza Balozi Seif kwamba Jimbo hilo ambalo ni Kisiwa kiliopo ncha ya Kusini mwa China limekuwa na utajiri mkubwa wa wataalamu wa Sekta hizo ambao unaweza kusaidia maendeleo na uchumi wa Zanzibar.



 Alisema Uongozi wakeutaandaa utaratibu na mipango ya kusaidia kutoa taaluma ya kisasa kwa wavuvi na  wakulima wa Zanzibar ili wapate fursa ya kuzalisha kitaalamu miradi yao hali itakayowaongezea kipato na kupunguza umaskini.



 Gavana Jian Dingzhi halifahamisha kwamba hatua hiyo italenga kuimarisha zaidi uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya Zanzibar na Hainan Visiwa vinavyolingana na kufanana kimazingira.



Alielezea faraja yake kuona kwamba Kizazi kipya cha jamii ya Wananchi wa Jamuhuri ya Watu wa China kimekuwa kikijifunza uhusiano wa kidugu unaoendelea kuimarika baina ya pande hizo mbili.



Gavana huyo wa Jimbo la Hainan aliwashauri na kuwaomba wafanyabiashara wa Zanzibar kulitumia soko la Hainan hasa lile la mazao ya Baharini katika kuendeleza biashara zao.



Alisema Hainan imekuwa mzalishaji mkubwa wa mazao ya Baharini yanayokadiriwa kufikia Tani 50,000 ndani ha mwaka huu wa 2014.



Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Sekta za Kilimo, Utalii na Mazao ya Baharini zimekuwa zikitoa mchango  kuongeza mapato ya Taifa.



 Balozi Seif alimueleza Gavana Jian Dingzhi kwamba ziara ya Ujumbe wake ndani ya Jimbo la Hainan itatoa fursa ya kujifunza  maendeleo yaliyopatikana ambayo yameliwezesha Jimbo hilo kupata ufanisi mpana.



Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliushauri Uongozi wa shirika la Ndege la Hainan kuanzisha safari za moja kwa moja za usafiri wa anga kati ya Visiwa hivyo kwa lengo la kupanua wigo wa biashara hasa utalii.



Alisema uamuzi huo endapo utafikiwa unaweza kutoa nafasi kwa wawekezaji wa Hainan kuhamasika na hatiame kuamua kuwekeza miradi yao ya kiuchumi katika Visiwa vya Zanzibar.



“ Ziara yangu hii pamoja na mambo mengine ya ushirikiano na uhusiano kati ya Zanzibar na Hainan lakini 
pia
imelenga
 kushawishi wafanyabiashara na wawekezaji wa Hainan kuwekeza vitega uchumi vyao Zanzibar “.Alisema Balozi Seif.



Mapema asubuhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na Ujumbe wake walitembelea meneo huru ya uwekezaji pamoja na kuangalia uzalishaji katika kiwanda cha usindikaji Samaki kwenye mji wa Kisiwa cha Haina, Haikou.



Akizungumza na wawakilishi wa Kiwanda hicho na ule wa Maeneo huru ya uwekezaji wakiongozwa na Meya wa Mji waChengmai Bwana Zhaomin Ji , Balozi Seif aliwapongeza Wananchi wa Hainan kwa hatua kubwa waliyofikia katika kuimarisha maendeleo yao.



Balozi Seif maendeleo hayo yanatoa nafasi kwa Zanzibar kujifunza  kupitia ziara za mara kwa mara za viongozi
na watendaji wake.
Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeanzisha maeneo huru ya uwekezaji pamoja na mfumo wa Bandari huru ya kiuchumi ili kuimarisha maendeleo yake lakini bado miundombinu katika maeneo hayo yangali duni.



Naye Msaidizi wa Meya wa Mji wa Chengmai ambae pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Kamati ya Chama ya Mji huo Bwana Sitao Yang alisema Hainan ni miongoni mwa Majimbo yenye rasilmali kubwa ya kiuchumi ikitanguliwa na Taiwan.



Alisema uchumi wa Jimbo la Hainan umekuwa na kufikia uwekezaji wa Yuan Bilioni 20 mwaka huu kutokana na kuimarika kwa miundo mbinu yake inayotoa fursa katika uwekezaji wa sekta ya Utalii.



Bwana Sitao alimuhakikishia Balozi Seif kwamba juhudi zitaongezwa katika kuona uhusiano wa kidugu naendelea kuimarika kati ya Zanzibar na Hainan kwa kuweka ubia katika miradi ya kiuchumi na maendeleo.
Wakati wa Jioni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Ujumbe wake walijumuika pamoja na wajumbe wa Mkutano wa Tano wa Ushirikiano kati ya China na Afrika kwenye chakula cha jionikilichoandaliwa na Gavana wa Hainan Bwana Jian Dingzhi hapo kwenye Hoteli ya Le Meriden Mjini Haoku.

Wednesday, 5 November 2014

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mhe:Mohamed Aboud Mohamed Ziarani Pemba

MKUU wa Skuli ya Alkhamis Cump Vitongoji inayomilikiwa na JWTZ Pemba,Meja Essau Lusila, akimfahamisha jambo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mhe:Mohamed Aboud Mohamed, wakati alipofanya ziara ya kutembelea majengo ya skuli hiyo, huko Vitongoji Wawi Chake Chake
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mhe:Mohamed Aboudn Mohamed, katikati akitembelea ujenzi wa Skuli ya Alkhamis Camp,kulia Mwakilishi wa Jimbo la Wawi Mhe.Saleh Nassor Juma, na Mkuu wa Skuli hiyo ya Alkhamis Cump Meja Essau Lusila na Viongozi wa Serekali wakiwa katika ziara hiyo ya Waziri Aboud..

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mhe:Mohamed Aboud Mohamed, akizungumza na wanafunzi na walimu wa skuli ya Alkhamis Cump Vitongoji, mara baada ya kukagua skuli hiyo kulia ni Mkuu wa Wilaya
ya Chake Chake Mhe:Hanuna Ibrahim Massoud




MHANDISI Mkaazi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Pemba Khamis Massoud, akitoa ufafanuzi juu ya madai ya wananchi wa shehia ya Vitongoji, Uwandani na Kibokoni ambao nyumba zao zitabolewa kwa ajili
ya kupisha ujenzi wa barabara kutoka Ole hadi Kengeja.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

Tuesday, 4 November 2014

Mwanachama wa Diaspora Dk. Mehta afungua Hospitali Mahonda Nje ya Mji wa Zanzibar.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akisalimiana na Mwenyekiti wa Kiwanda cha Sukari Mahonda Bwa. Mahesh Patel, alipowasilin katika viwanja vya hospital hiyo mahonda kwa uaji ya uzinduzi wake. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akisalimiana naDk. Ameesh G Mehta, mmiliki wa hospital hiyo, alipowasilin katika viwanja vya hospital hiyo mahonda kwa ajili ya uzinduzi wake. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi, Seif Ali Iddi, akikata utepe kuashiria kuzindua jengo la Hospital ya Jamii Mahonda ilioazishwa na Mwanadiasfora Dk Ameesh G Mehta, kulia na kusho Mwenyekiti wa Kiwanda cha Sukari Mahonda Bwa. Mahesh Patel, wakishuhudia uzinduzi huo uliofanyika wa hospitali hiyo.  

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa hospital hiyo kushoto Dk Ameesh Mehta na kulia kwa Balozi Seif Mwenyekiti wa Kiwanda cha Sukari Mahonda Bwa, Mahesh Patel na Viccky Patel Afisa wa Kiwanda cha Sukari Mahonda. ANZIBAR 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akimsikiliza Dk Mehta, akielezea moja ya vifaa katika hospitali hiyo baada ya kutembelea baadhi ya vyumba vya matibabu katika hospitali hiyo.baada ya kuifungua huko mahonda Zanzibar. 
Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi, akipata maelezo ya vifaa vya uchunguzi wa maradhi katika chumba cha kuchunguza wagonjwa watakaofika katika hospital hiyo kupata huduma kutoka Dk Mehta akionesha vifaa hivyo.





Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd., akiwahutubia Wananchi wa Mahonda wakati wa uzinduzi wa hospitali ilioazishwa na Mwanachama wa Diasfora kuwekeza katika Kijiji hicho kwa kutowa huduma ya Afya kwa Jamii, uzinduzi huo umefanyika mahonda jirani na kiwanda cha sukari mahonda Zanzibar. 

Dk. Ameesh G Mehta, akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa hospital yake katika kijiji cha mahonda Zanzibar na kueleza huduma zitakazotolewa katika hospital hiyo kwa Wananchi wa mahonda na vitongoji vyake wanapofika kupata huduma za afya kwa gharama nafuu,

Mwenyekiti wa Kiwanda cha Shanta Sugar Factory & Export Trading Group Ndg. Mahesh Patel , akizunmgumza katika uzinduzi huo wa hospitali ya Kijamii iliozishwa na Mwanadiasfora wa Zanzibar Dk Ameesh G Mahta anayemiliki hospitali ya Dk. Mehta's Hospital ilioko Vuga Zanzibar na kiwanda cha Sukari Mahonda kwa kutowa huduma ya Afya kwa Jamii katika kijiji cha Mahonda na Mkoa wa Kaskazini Unguja. 
 Baadhi ya waalikwa katika hafla ya ufunguzi wa hospitali ya Dk Mehta's, huko mahonda Zanzibar.
     Baadhi ya waalikwa katika hafla ya ufunguzi wa hospitali ya Dk Mehta's, huko mahonda Zanzibar.
Wazee wa Kijiji cha mahonda wakifuatilia hafla hiyo ya uzinduzi wa hospitali ya Jamii iliojengwa na Mwanachama wa Diasfora wa Zanzibar Dk Ameesh .G. Mehta's, nje kidogo ya mji wa Zanzibar. 
Wageni waalikwa wakifuatilia hafla ya ufunguzi wa hospital ya Dk. Mehta's Hospital Mahonda Zanzibar.
Wananchi wa Mahonda wakimsikiliza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwahutubia Wananchi wa Mahonda na Wafanyakazi wa kiwanda cha Sukari wakati wa hafla ya ufunguzi wa Hospitali ya Kisasa katika kijiji cha mahonda Zanzibar.
Chumba cha kulaza wagonjwa na mapumziko katika hospitali hiyo kwa wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kwa kupa matibabu ya afya zao.
Sehemu ya chumba cha kuhudumia wagonjwa kwa matibabu zaidi ya uchunguzi katika hospitali hiyo huko mahonda na kutowa huduma kwa Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja. 
                 Chumba cha kuhudumiwa wagonjwa katika hospitali hiyo ikiwa na vifaa vyake kamili.

Shekh wa Kijiji cha Mahonda akisoma dua baada ya uzinduzi wa hospital hiyo ilikarabatiwa na Mwanadiasfora Dk Ameesh G Mahta's na kiwanda cha Sukari Mahonda. kutowa nafasi kwa wananchi wa mahonda kupata huduma ya afya karibu yao.
DK Ameesh G Mahta, akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa hospitali ya Jamii iliofunguliwa na Dk. Mehta's Hospital huko Mahonda Zanzibar nje kidogo ya mji wa Zanzibar Mkoa wa Kaskazini Unguja Wilaya ya Kaskazini A. Dk. Ameesh Mehta ni mmoja wa Wazanzibar Wanaoishi nje ya Nchi akiwa ni mwanachama wa Diasfora waliojitokeza kuwekeza nyumbani katika sekta ya Afya Zanzibar.