Sunday, 16 November 2014

Balozi Seif Akizungumza na Ujumbe wa Makampuni ya Uwekezaji China. Wakati wa Ziara yake katika mjini wa Hainan China

Makamu wa Rais wa Kiwanda cha Dawa za Binaadamu cha Shuangcheng Bwana Jianlin Yuan akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na Ujumbe wake wakati walipotembelea kiwanda hicho wakiwa katika ziara ya Kiserikali Katika Jimbo la Kisiwa cha Hainan.
Ujumbe wa Zanzibar Ukiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ukifanya azungumzo na Ujumbe wa Makampuni ya uwekezaji vitega uchumi katika Jimbo la Hainan ukiongozwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Nyumba na Maendeleo ya Miji na Vijiji ya Hainan.
 Balozi Seif na Ujumbe wake wakiwa katika kikao cha pamoja cha ushirikiano kati ya Zanzibar na Uongozi wa Manispaa ya Mji wa  Haikou ukiongozwa na Meya wa Mji Huo Mstahiki NI Qiang.
Mwenyekiti wa Kiwanda cha kusindika bidhaa za nazi pamoja na matunda  kiliopo Haikuu Bwana Huang Chunguang akimfahamisha Balozi Seif na Ujumbe juhudi zinazochukuliwa na Kiwanda hicho katika kulitumia vyema zao la nazi.Kushoto ya Balozi Seif ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi na Kulia yake ni Waziri wa Ardhi Mh. Ramadhan Abdulla Shaaban na Waziri wa Habari Mh. Sai Ali Mbarouk.(Picha na Hassan Issa OMPR  China)




Makampuni na Taasisi mbali mbali za uwekezaji wa miradi ya Kiuchumi na maendeleo katika Jimbo la Kisiwa cha Hainan yameombwa kuzitumia taaluma zao kwa kufanya utafiti utakaoyawezesha Makampuni hayo kutumia fursa za uwekezaji zilizopo ndani ya Visiwa vya Zanzibar. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitoa ombi hilo wakati akizungumza na Viongozi wa Taasisi  an makampuni hayo katika mikutano tofauti akiwa katika ziara ya Kiserikali kwenye Kisiwa rafiki cha Jimbo la Hainan Nchini Jamuhuri ya Watu wa China.

Balozi Seif alisema wakati Zanzibar inaendelea kufungua milango ya uwekezaji katika kuimarisha uchumi wake  fursa ziko wazi kwa wawekezaji wa Jamuhuri ya Watu wa China hasa Kisiwa cha Hainankuitumia nafasi. Alisema ipo miradi mbali mbali inayoweza kuanzishwa na Kampuni za China hapa Zanzibarf kwa lengo la kutoa huduma ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki pamoja na Nchi wa Kusini mwa Afrika { SADC }.

Balozi Seif aliitaja baadhi ya miradi inayoweza kuwekezwa na Makampuni hayo kuwa ni pamoja na Viwanda vidogo vidogo vya Dawa, za Binaadamu, Vyakula vya Matunda, usindikaji wa Samaki pamoja na vifaa vya Kilimo ambavyo 
pia
 vinaweza
 kusaidia kupunguza tatizo la ajira.

Aliwaeleza Viongozi wa Taasisi hizo kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibarf { ZIPA } iko tayari na huru kushirikiana na taasisi zote zitakazojitokeza kuonyesha nia ya kutaka kuwekeza Zanzibar.


 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliipongeza Jamuhuri ya Watu wa China kwa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika harakati zake za Maendeleo jambo ambalo ni ushahidi unaothibitisha uhusiano wa muda mrefu kati ya China na Zanzibar na Tanzania kwa jumla.

Naye Kiongozi wa Makampuni na Taasisi hizo za Kisiwa cha Jimbo la Hainan Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Nyumba na Maendeleo ya Miji na Vijiji Bwana Du Haiying alisema Taasisi zao zimeanzishwa kwa lengo la kustawisha Uchumi na ustawi wa Jamii.

Bwana Du Haiying alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwamba Makampuni mengi ya Jamuhuri ya Watu wa China hivi sasa yanaendelea kuunga mkono sera za China katika kuimarisha uhusiano na Mataifa mbali mbali ya Bara la Afrika.

Bwana Du alifahamisha kwamba ziara za mara kwa mara za Viongozi wa juuwa Serikali ya China wakiongozwa na Rais wa Bwana Xi Jinping katika nchi tifauti za Afrika zinania ya kuunga mkono maendeleo ya Bara la Afrika.

Mapema Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh.Said Ali Mbarouk alisema Zanzibar kupitia Kamisheni yake ya Utalii hivi sasa iko katika juhudi za kujitangaza kiutalii kwa kufungua ofisi katika Mji mbali mbali Duniani.Mh. Mbarouk alisema juhudi hizo zimelenga kuongeza idadi ya wageni na watalii wanaoingia Zanzibar ambao wengi kati yao hutokea nchi za Ulaya, Marekani , Nchi za Scandnavia na baadhi ya nchi za Afrika.


Waziri Mbarouk aliwataja baadhi  ya watalii wanaoingia Zanzibar wengi kati yao wanatoka Italy, Ujerumani, Uingereza, Nchi za Scandinavia, Afrika Kusini, Marekani, Uholanzi na nchi chache za Bara la Afrika.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo alisema China ni nchi ya mwisho watalalii wake wanaofanya ziara za Matembezi Zanzibar kiwango ambacho hakilingani na idadi ya watalii wa Nchi hiyo wanaofikia Milioni Moja kwa Mwaka.
Akitoa ufafanuzi kwa viongozi hao wa Mashirika na Taasisi mbali mbali za uwekezaji za Kisiwa cha Jimbo la Hainan Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji Vitegha Uchumi Zanzibar { ZIPA } Nd. Salum Nasso Khamis alisema Muwekezaji anaruhusika kuwekeza mradi wake mara baada ya kukamilisha taratibu  za Mamlaka zinazohusika.


Nd. Salum alisema hatua ya mwanzo anayotakiwa muwekezaji kuifanya ni pamoja na kuandika maombi ya mradi anaotaka kuutekeleza pamoja na vielelezo vyote vitakavyompa urahisi wa kukubalika maombi yake bila ya usumbufu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Ujumbe wake amemaliza ziara yeka Katika Kisiwa cha Jimbo la Hainan kwa kutembelea eneo huru la uwekezaji vitega uchumi pamoja na Kwanda cha kusindika samaki Mjini Haikou.


Ujumbe huo pia ulipata fura sa kuangalia Bandari mpya ya Kisasa ya Sanya inayohudumia meli kubwa  za utalii, abiria ,mizigo pamoja na kukagua ujenzi wa nyumba za wafanyakazi na makazi ya wananachi zinazouzwa kwa mkopo nafuu.
Halikadhalika  ziara ya ujumbe huo wa Zanzibar pia ilifika na kuangalia uzalishaji katika kiwanda cha Dawa cha Hainan pamoja na Kiwanda cha uzalishaji wa biadhaa mbali mbali za nazi na baadhi ya matunda yanayootehswa kwenye kisiwa hicho.


Kesho Balozi Seif anatarajiwa kwenda katika Mji wa shenzhen kuendelea na ziara yake kwa kutembelea Makao Makuu ya Kampuni ya Huawei inayoshughulikia masuala ya Teknolojia ya Kisasa { ICT } kabla ya kumaliza ziara yake Mjini Beijing.