Katibu wa Kamati ya Bandari ya Nyanjale Kiomba Mvua Bwana Moh’d Ali akitia saini
makubaliano yaliyofikiwa baina ya Wanakijiji hicho na Uongozi wa Hoteli ya
Kimataifa ya Sea Cliff iliyopo Kama nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Wajumbe wawili wa Kamati ya Bandari ya Kiomba Mvua Bwana Othman Ashkina na Bibi Chiku Sheikh wakimwaga wino kwenye maridhiano waliyofikia na Hoteli ya Sea Cliff. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Meneja Mkuu wa Hoteli ya Sea Cliff Bwana Abre Esterhuizen akimwaga wino kwenye maridhiano hayo ya makubaliano na wana Kijiji cha Kiomba Mvua. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Menaja Utawala na Uendeshaji wa Hoteli ya Sea Cliff Bwana Abdulmalik Mussa Kushoto na Meneja wa Mchezo wa Golf wa Hoteli hiyo Bwana Heirz Papenfus wakijumuika kutia saini Mkataba huop wa maridhiano. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Balozi Seif akishuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Kanal
Mstaafu Juma Kassim Tindwa Kulia yake na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa huo kushoto
yake Nd. Haji Juma Haji chini ya usimamizi wa Mwanasheria wa Makamu wa Pili
aliyesimama Bibi Mwanaisha Shamte akitia saini kama shahidi kwenye mkataba wa
maridhiano hayo. Picha na Hassan Issa wa –
OMPR – ZNZ.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Wajumbe wawili wa Kamati ya Bandari ya Kiomba Mvua Bwana Othman Ashkina na Bibi Chiku Sheikh wakimwaga wino kwenye maridhiano waliyofikia na Hoteli ya Sea Cliff. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Meneja Mkuu wa Hoteli ya Sea Cliff Bwana Abre Esterhuizen akimwaga wino kwenye maridhiano hayo ya makubaliano na wana Kijiji cha Kiomba Mvua. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Menaja Utawala na Uendeshaji wa Hoteli ya Sea Cliff Bwana Abdulmalik Mussa Kushoto na Meneja wa Mchezo wa Golf wa Hoteli hiyo Bwana Heirz Papenfus wakijumuika kutia saini Mkataba huop wa maridhiano. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Press Release:
Hatma njema ya
Kikao Maalum kilichotayarishwa kwa ajili ya utiaji saini makubaliano baina ya
Muwekezaji wa Hoteli ya Kimataifa ya Sea Cliff iliyopo katika Kijiji cha Kama
na Wananchi wanayoizunguuka Hoteli hiyo imefikiwa.
Utiaji saini
makubaliano hayo ulikuwa ufanyike Tarehe 10 Mwezi Mei Mwaka huu lakini
ulishindikana baada ya uamuzi wa wajumbe wa upande wa Kamati ya Bandari ya
Nyanjale Kiomba Mvua kutokufika katika kikao hicho bila ya sababu zisizoeleweka.
Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa pamoja na baadhi ya Viongozi wa
Mkoa wa Kaskazini Unguja, Taasisi za Ardhi na Mazingira walishuhudia utiaji
saini huo ambapo upande wa Hoteli ya Sea Cliff uliwakilishwa na Meneja Mkuu wa
Hoteli hiyo Bwana Abre Esterhuizen,Meneja wa Mradi wa Mchezo wa Golf wa Hoteli
hiyo Bwana Heirz Papenfus pamoja na Meneja Utawala na Uendeshaji wa Hoteli
Bwana Abdullmalik Mussa.
Upande wa
wana kijiji cha Kiomba Mvua ukaongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bandari ya
eneo hilo Nd. Mbwana Amour Khamis, Katibu wa Kamati hiyo Nd. Moh’d Ali Ameir
pamoja na wajumbe wawili Bibi Chiku Sheikh Nd. Othman Ashkina.
Hafla hiyo
ya utiaji saini Mkataba huo wa makubaliano ilifanyika katika ukumbi wa Hoteli
hiyo ya Kimataifa ya Sea Cliff iliyopo Kama kilomita chache kaskazini ya Mji wa Zanzibar.
Mgogoro
baina ya Muwekezaji huyo na Wananchi wa Vijiji jirani ambao ulihusu zaidi eneo la Bandari ya
Madagaa pamoja na bara bara iendayo eneo hilo ulifikia makubaliano kufuatia
vikao mbali mbali vilivyokuwa vikiendelea katika kutafuta maridhiano ya pande
zote mbili.
Vikao vya
pamoja kati ya Uongozi wa Hoteli ya Sea Cliff na Viongozi wa Kamati Nne za Vijiji
vya Kiomba mvua vilikuwa vikifanyika kwa pamoja kupitia muongozo ulitolewa na
Kamati ya Baraza la Wawakilishi kuhusu maridhiano ya pande hizo husika.
Mazingira
halisi ya mgogoro wa Kiomba mvua na Muwekezaji wa Sea Cliff umefikia hatua
nzuri ya maridhiano lakini kilichokuwa kikionekana wakati wa kufikia hatma yake
ya mwisho ni baadhi ya watu kuanza kuhusisha mgogoro huo na masuala ya Kisiasa.
Akizungumza
kwenye Kikao hicho Mwakilishi wa Mradi wa Hoteli ya Sea Cliff Bwana Yassir De
Costa ameishukuru na kuipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa jitihada
zake inazochukuwa katika kuunga mkono Taasisi za uwekezaji vitega uchumi hapa
nchini.
De Costa
alisema katika muelekeo wa kusaidia maendeleo ya wananchi wa vijiji vya jirani,
Mradi wa Hoteli ya Sea Cliff umeamua kusaidia utunzaji wa mazingira ya Mikoko, kuwapatia
Gari ya usafiri, kujenga mabanda ya wavuvi na vyoo vyake pamoja na ujenzi wa
bara bara.
Alisema
huduma hizo zitakwenda sambamba na wananchi hao kupatiwa Eka moja na nusu kwa
ajili ya uanikaji wa dagaa, fedha taslim shilingi Milioni 11 zitakazohudumia
bidhaa zao kuhamia eneo jipya pamoja na shilingi milionji 16 kwa ajili ya
kuendeleza kamati hiyo.
Alieleza
kwamba wakaazi wote wanaozunguuka mradi huo watakuwa na fursa ya kupatiwa
huduma za Afya katika Kituo cha Afya cha Hoteli hiyo ambapo utaratibu
utaandaliwa kwa mgonjwa atakayezidiwa maradhi kwa kupelekwa Hospitali ya Rufaa
ya Mnazi Mmoja.
Akitoa
nasaha zake mara baada ya zoezi hilo la utiaji saini makubaliano hayo Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliwapongeza wananchi wa kiomba
mvua kwa uamuzi wao huo na kuwataka waendelee kushirikiana na wawekezaji ili
kusaidia kuimarisha uchumi wa taifa kupitia sekta ya uwekezaji.
Balozi Seif
ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Kitope linalounda eneo hilo alisema Viongozi
Wakuu wa Serikali wamekuwa wakisafiri nchi tofauti kujaribu kubembeleza
wawekezaji wan chi hizo kuja kuwekeza
miradi yao nchini ili kusaidia kunyanyua uchumi wa Taifa.
Hata hivyo
Balozi Seif alionyesha masikitiko yake kutokana na kitendo cha kutiwa saini
makubaliano hayo kuchelewa kwa karibu mwaka mzima kutokana na sababu za tatizo
hilo kuingizwa siasa jambo ambalo linavuruga maendeleo ya jamii.
“ Mara
nyingi nimekuwa nikialikwa kuzindua miradi ya wananchi katika Mkoa wa Kusini
Unguja inayogharamiwa na wawekezaji. Hivyo ni vyema kwa wanakijiji cha Kiomba
mvua na vijiji vyengine nchini wakaiga
mfano huo wa wenzao wa Mkoa wa Kusini “. Alisema Balozi Seif.
Aliwaomba
wananchi hao kuhakikisha kwamba yanapojitokeza matatizo baina yao na Taasisi au
Makampuni yanayowekeza katika maeneo yao kwenda katika ngazi zinazohusika
badala ya kukimbilia kupatuka kwenye vyombo vya Habari.
Mapema Mkuu
wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Meja Mstaafu Juma Kassim Tindwa alisema Taifa bado
linaendelea kukabiliwa na tatizo la umaskini ambapo muhimili wa kusaidia mapato
ya Nchi kwa sasa ni kukaribisha Makampuni na Taasisi katika sekta ya uwekezaji.
Kanal
Mstaafu Tindwa alifahamisha kwamba Sekta ya uwekezaji hasa katika miradi ya Utalii Nchini hivi sasa
imekuwa ikisaidia kwa kiwango kikubwa miraji ya Kiuchumi,kijamii kwa asilimia pana
zaidi.
Mkuu huyo wa
Mkoa wa Kaskazini Unguja aliiagiza Kamati ya Ulinzi na usalama ya Mkoa huo
kuhakikisha kwamba inadhibiti na kuchukuwa hatua za kisheria kwa mtu au kikundi
chochote kinachojaribu kuvuruga miradi ya uwekezaji na maendeleo ya wananchi katika Mkoa huo.
Mhe. Tindwa
alikemea tabia ya baadhi ya watu
walioamua kuiba tangi la kuhifadhia maji na baadhi ya milango kwenye soko
lililojengwa na Hoteli ya Sea Cliff kwa ajili ya wananchi na wavuvi hao wa Kijji cha Kiomba Mvua.
Akitoa
shukrani kwa niaba ya wananchi na wavuvi wenzake wa Kijiji cha Kiomba Mvua
Katibu wa Kamati ya Bandari ya Kijiji hicho Bwana Mbwana Moh’d Ali Ameir
alisema wananchi hao watakuwa tayari kushirikiana na uongozi wa mradi huo ili
malengo yaliyokusudiwa yafikiwe.
Katibu Moh’d
akiomba radhi kutokana na matokeo yaliyojitokeza kwenye mgogoro huo alisema
moja kati ya jukumu walilokubali kulibeba wana kjijiji hao ni kuhakikisha suala la mazingira ya eneo hilo linalindwa na
kuwa katika hali ya kuridhisha.
Mgogoro
baina ya muwekezaji wa Hoteli ya Sea Cliff na wanakijiji wanaoizunguuka Hoteli
hiyo ulikuwa ukivukuta katika suala la matumizi ya bandari, eneo la kuanikia
madagaa pamoja na bara bara mambo ambayo muwekezaji huyo ameyakubali kuyatekeleza kwa mujibu wa makubaliano
yaliyofikiwa.