Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi

Mwanafunzi Isra Hilal Mwadini akifuatiwa na mwenzake Tamima Abass Sheha wakipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wakati wa hafla ya Maulidi ya Jumuiya ya Chuo cha Samael Academy.Kulia ya Balozi Seif ni Rais wa Sameil Academy Sheikh Nassir Bin Said.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizindua rasmi Bara bara ya pili ya Amani hadi Mtoni baada ya kukamilika awamu ya mwisho ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Akiwa na Balozi mdogo wa India nchini Tanzania wakiangalia maonyesho yaliofanya na Msanii kutoka India, Bi Navi Madhav hapo Ngome Kongwe

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Dk. Khalid S. Mohamed

akizungumza na Wadau wa Maendeleo wa Mfuko wa TASAF, walipofika Ofisini kwake kuzungumzia maendeleo ya Mfuko wa TASAF III,na kutembelea Mradi wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini (PSSN) katika Jimbo la Muyuni Wilaya ya Kusini Unguja katika Kijiji cha Muyuni B

Wazir wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakifurahia jambo wakati wa semina ya siku moja kuhusu matokeo makubwa na ya haraka katika kuleta mageuzi ya kiuchumi na kuleta maendeleo nchini iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein

Sunday, 10 August 2014

Mama Asha: Vijana waungwe mkono kwenye harakati zao za kijamii


Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kitope Mama Asha Suleiman Iddi akimkabidhi Vifaa vya Michezo Nahodha wa Timu ya Soka ya Jimbo la Donge Ussi Ali-Haji Bakar Juma ambayo imepiga kambi ikijiandaa na mashindano ya Kombe la Majimbo Taifa yaliyoanza rasmi Tarehe 6 mwezi huu.

Mwenyekiti wa Kambi ya mazoezi ya Timu za Soka za Majimbo la Donge na Kitope Mwinyi Mahfoudh Muhsin akipokea vifaa na vyakula kutoka kwa Mama Asha Suleiman Iddi kwa ajili ya wachezaji wa Timu za Majimbo ya Donge na Kitope waliopiga kambi kwenye Ofisi ya CCM Jimbo la Kitope hapo Kinduni.
Baadhi ya wachezaji wa Timu za Soka za Majimbo ya Kitope na Donge waliopiga kambi kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Majimbo Taifa wakimsikiliza Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kitope Mama Asha Suleiman Iddi hayupo pichani wkati wa uzinduzi wa kambi hiyo hapo Ofisi ys CCM Jimbo la Kitope iliyopo Kinduni.

Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ

Na Othman Khamis Ame, OMPR
Viongozi wa ngazi mbali mbali Nchini wanapaswa muda wao mwingi kuutumia katika kuendelea kuwaunga mkono Vijana kwenye harakati zao za kijamii ili wapate muongozo sahihi utakaowapa njia ya kufanikiwa vyema katika malengo wanayojipangia ya hapo baadae.
Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kitope Mama Asha Suleiman Iddi alitoa kauli hiyo wakati akizindua rasmi Kambi ya Timu za Soka za Majimbo ya Donge na Kitope zinazojiandaa kwa mashindano ya Kombe la Majimbo Taifa yaliyoanza rasmi Tarehe 6 Mwezi huu.
Hafla hiyo fupi iliyofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM Jimbo la Kitope iliyopo Kinduni Wilaya ya Kaskazini “B “ ilishuhudiwa pia Mama Asha akikabidhi Vifaa vya  michezo kama Jezi Seti mbili kwa kila Timu, Mipira,Track Suits kwa ajili ya Viongozi wao pamoja na vyakula mbali mbali vyote vikigharimu zaidi ya shilingi Milioni Tano Nukta Tatu { 5,300,000/- }.


Mama Asha alisema ukaribu wa wazazi kwa watoto na Vijana  wao ndio jambo la msingi litakalotoa fursa nzuri kwa Watoto hao kuwa na maadili na utamaduni sahihi unaokubalika katika Jamii.
Mke huyo wa Mbunge wa Jimbo la Kitope alisema wachezaji hao wa  Timu zote mbili za Majimbo ya  Kitope na Donge wanapaswa kucheza kwa bidii na nidhamu ili kuleta ushindi ndani ya Wilaya yao ya Kaskazini “ B “.
Mama Asha aliwataka wachezaji hao wajiepushe mbali na vitendo vya udanganyifu vinavyotumiwa na baadhi ya watu hasa wanasiasa vya kuwashawishi vijana kujiingiza katika vitendo viovu.
Alisema Watu na Viongozi hao matapeli hutumia muda wao mwingi kuwavurugia vijana mwenendo wao na baadae huwasababishia hata kukosa muda wa kuendeleza michezo yao ambayo kwa hivi sasa imeonyesha mwanga wa kutoa ajira.
Katika kuwahamasisha wachezao hao wa Timu zote mbili za Majimbo ya Donge na Kitope Mke huyo wa Mbunge wa Jimbo la Kitope alisema kwamba endapo wachezaji hao wataleta ushindi ndani ya Wilaya yao ya Kaskazini “ B “ amehidi kutoa shilingi Milioni Moja na Nusu kwa Timu itakayopeleka kikombe cha ushindi wa mashindano hayo ya Kombe la Majimbo Taifa na shilingi Laki mbili na Nusu kwa Kila Mchezaji.
Akitos shukrani kwa niaba ya wachezaji wa timu zote Mbili za Majimbo hayo ya Donge na Kitope mwakilishi wa wachezaji hao Omar Ali Khamis alimuhakikishia Mama Asha kwamba vifaa vyote hivyo walivyopatiwa watavitumia kama inavyotarajiwa.
Omar Ali Khamis alisema wachezaji hao wana kila sababu ya kufanya vyema katika mashindano hayo ya kombe la Majimbo Taifa na kuahidi kwamba Timu hizo zitaingia mbili bora na kuweka rikodi nzuri ya Wilaya na Majimbo hayo.
Mapema Mbunge wa Jimbo la Donge ambae pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa Mh. Sadifa Juma Khamis alisema bahati iliyoje kwa Wananchi wa Jimbo la Kitope kupata Mbunge anayejali shida na changamoto zinazowakabili Wananchi wake hasa wanamichezo wa Jimbo hilo.
Mh. Sadifa ambae aliahidi kuwapatia Seti ya TV na King’amuzi chake Wanakambi hao ili kujua kinachojiri Duniani hasa katika ulimwengu wa Soka aliwataka Wananchi hao kuendelea kumpa fursa ya kuongoza Jimbo lao la Kitope Mbunge wao Balozi Seif Ali Iddi katika kipindi kijacho ili akamilishe malengo aliyojiwekea.
Mbunge huyo wa Jimbo la Donge aliwaasa Wananchi na Viongozi wa Majimbo hayo pamoja  na Wilaya nzima kujenga utamaduni wa kuwaandaa viongozi wa baadae ili kuwa na uhakika wa safu ya Uongozi ndani ya Majimbo na Wilaya hiyo.

Monday, 4 August 2014

Kikao cha kamati ya Uongozi cha Bunge la Katiba chafanyika leo



Mwenyekiti wa Bunge Maalum Mhe. Samuel Sita akiongoza kikao cha Kamati ya Uongozi cha Bunge hilo kilichokaa leo kupanga ratiba ya Bunge hilo linaloanza Jumanne, 5 Agosti 2014 baada ya kuarishwa tarehe 25 Aprili 2014

Sunday, 3 August 2014

Dk Shein azindua Maonyesho ya kilimo ya nane nane mkoani Lindi


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa Maonesho ya kilimo ya nane nane kitaifa mwaka huu   katika viwanja vya Ngongo Mkoani  Lindi leo.[Picha na Ramadhan Othman Lindi.]
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali wakati alipowasili katika  Viwanja vya Ngongo yanapofanyika maonesho ya Kilimo ya nane nane kitaifa Mkoani Lindi. [Picha na Ramadhan Othman Lindi.]
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo katika banda la Benki kuu ya Tanzania BOT katika maonesho ya kilimo  ya nane nane kitaifa Mkoani Lindi katika viwanja vya Ngongo. [Picha na Ramadhan Othman Lindi.]
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo katika banda la sekta ya Afya katika maonesho ya kilimo ya nane nane kitaifa yanayofaanyika Mkoani Lindi katika viwanja vya Ngongo. [Picha na Ramadhan Othman Lindi.]

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Dk.Geoffrey Mkamito Mtafiti wa Mazao ya Mizizi, katika banda la Bodi ya Korosho katika maonesho ya kilimo ya nane nane kitaifa yanayofaanyika Mkoani Lindi katika viwanja vya Ngongo. [Picha na Ramadhan Othman Lindi.]
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Meneja Biashara na Masoko Numwagile A.Mwaijumba wa Shirika la Nyumbu kuhusu mashine ya utengenezaji wa matofali ya udongo   katika maonesho ya kilimo ya nane nane kitaifa yanayofaanyika Mkoani Lindi katika viwanja vya Ngongo. [Picha na Ramadhan Othman Lindi.]
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na wananchi wa manispaa ya Lindi Mjini na Vitongoji vyake baada ya kuzindua rasmi maonesho ya kilimo  ya nane nane kitaifa katika viwanja vya Ngongo leo Mkoani Lindi. [Picha na Ramadhan Othman Lindi.]

Wananchi watahadharishwa kuwa na macho na baadhi ya wanasiasa wasiotaka maendeleo

 Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seiof Ali Iddi akibadilishana mawazo na Uongozi wa Kamati ya Skuli ya Sekondari ya Fujoni mara baada ya kukaguwa majengo ya Maabara na Maktaba na kukabidhi mbao kwa ajili ya uwezekaji majengo hayo.
 Balozi Seif akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari ya Fujoni kulia yake Maalim Mabrouk Ishaq Daima Mbao pamoja na mitwiko yake kwa ajili ya uwezekaji majengo mapya ya Maktaba na Maabara ya Skuli hiyo.
 Balozi Seif akikabidhi Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Fujoni Maalim Mabrouk Ishaq Daima fedha za fundi wa uwezekaji wa mapaa ya majengo ya Maabara na Maktaba ya Skuli hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif akizungumza na Uongozi wa Kamati ya Skuli ya Sekondari ya Fujoni ndani ya Ofisi ya Mwalimu Mkuu mara baada ya kukabidhi vifaa kwa ajili ya uwezekaji wa majengo ya Maabara na Maktaba ya Skuli hiyo.

Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
 
Wananchi wameendelea kutahadharishwa kuwa macho na tabia ya baadhi ya wanasiasa wenye hulka ya kushawishi jamii kutoshiriki harakati za maendeleo na ustawi wa jamii kwenye maeneo yao kwa sababu tu ya itikadi ya kisiasa.
 
Tahadhari hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi wakati akikabidhi vifaa mbali mbali vya uwezekaji wa majengo ya Maabara na Maktaba ya Skuli ya Sekondari ya Fujoni iliyomo ndani ya Jimbo la Kitope Wilaya ya Kaskazini “ B”.
 
Balozi Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema ipo miradi mingi ya maendeleo ya wananchi katika maeneo tofauti mengine ikipata usaidizi wa ufadhili wa wawekezaji waliomo katika maeneo hayo, lakini cha kushangaza ni kuona baadhi ya wanasiasa walafi hushawishi wananchi hao wasijihusishe kushiriki katika miradi hiyo.
 
“ Upo mradi wa uwekezaji wa Kitalii uliomo ndani ya jimbo langu ambao uongozi wake umeonyesha nia safi ya kutaka kusaidia maendeleo ya wananchi wanaouzunguuka mradi huo. Lakini cha kusikitisha ni kuona baadhi ya wanachi wake wamesusia kwa sababu tu za ushawishi wa Kisiasa uliochochewa kwa makusudi “. Alisema Mbunge huyo wa Jimbo la Kitope.


Balozi Seif aliushukuru na kuupongeza Uongozi  mzima wa Kamati ya Skuli ya sekondari ya Fujoni kwa umahiri wake wa kuwajengea hatma njema ya kielimu watoto wao.
 
Alisema juhudi hizo ndizo zilizozaa matunda bora ya kielimu kwa kutoa fursa kubwa kwa wanafunzi wa skuli hiyo kuendelea na masomo yao ya kidato cha tano na sita baada ya kufaulu katika kiwango kinachokubalika Kitaifa.
 
“ Pongezi Maalum zimfikie mwalimu Mkuu wa Skuli yetu ya Fujoni  kwa kazi kubwa ya kusimamia maamuzi ya Kamati ya Uongozi wa skuli. Napata faraja kuona umoja wenu ndio onaofanikisha malengo mliojipangia “ Alifafanua Balozi Seif.
 
Akiwathibitishia Wananchi wa Jimbo la Kitope kuendelea kuliongoza Jimbo hilo endapo watampa ridhaa tena katika uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2015 Balozi Seif alisema yeye pamoja na Viongozi wenzake watahakikisha wanaongeza nguvu zao za kiuwezeshaji katika miradi mbali mbali wanayoianzisha wananchi hao.
 
Alisema kazi ya Uongozi ni kuhakikisha inaendelea kuwajengea  mazingira  makubwa zaidi wananchi wake hasa wanafunzi wa skuli zilizomo kwenye Jimbo hilo ili wawe na uwezo wa kuingia vyuo vikuu na kufikia daraja la utaalamu utakaokuja wasaidia wazazi na jamii inayowazunguuka hapo baadaye.
 
Mapema Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kitope Mama Asha Suleiman Iddi alisema maendeleo ya kielimu yaliyopatikana ndani ya skuli ya Fujoni wapo wapo baadhi ya watu waharidhiki nayo kutokana na choyo cha roho walichokuwa nacho.
 
Mama Asha alieleza kwamba maendeleo hayo ambayo ni ya kupigiwa mfano yanastahiki kuigwa na vijiji vyengine vyenye malengo ya kujipatia maendeleo yanayotokana na nguvu zao wenyewe.
 
Mama Asha lielezea masikitiko yake na kulaani kitendo  kilichofanywa na baadhi ya watu kumsingiziwa kwamba aliahidi kujenga madrasa moja iliyomo ndani ya Kijiji cha Fujoni jambo ambalo niuzushi unaotaka kumuharibia kisiasa.
Alieleza kwamba tabia aliyojijengea ndani ya jamii ni kwamba anapo ahidi jambo tayari ameshajiandaa na kamwe hachukui muda mrefu kuitekeleza ahadi hiyo akielewa kwamba asipotekeleza tayari ameshabeba dhima kwa mwenyezi mungu.
 
Akitoa shukrani kwa niaba ya Uongozi  wa Kamati ya Skuli Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari ya Fujon i Mwalimu Mbrouk Ishaq Daima alimuhakikishia Mbunge huyo wa Jimbo la Kitope kwamba Kamati hiyo itakuwa tayari wakati wote kutekeleza malengo yanayopangwa katika skuli hiyo.
 
Mwalimu Mabrouk Ishaq alimpongeza Mbunge huyo kwa jitihada zake anazochukuwa katika kuona maendeleo ya elimu ya skuli hiyo pamoja na Jimbo zima yanafikiwa.
 
 

African Coast ya Upenja yaomba radhi kwa Balozi Seif


 Mzee wa Timu ya African Coast Ali Soud akipokea mchango wa Mbunge wa Kitope Balozi Seif kwa ajili ya kulipa deni ya kambi ya timu hiyo pamoja na ada ya timu, kadi za wachezaji pamoja na Mrajisi wa michezo.
Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi Kepteni ya Timu ya Soka ya African Coast ya Upenja Ali Hassan Mipira,seti ya Jezi pamoja na Fulana za mazoezi kwa ajili ya wachezaji wa timu hiyo iliyomo ndani ya Jimbo lake.

Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ
 
Uongozi na wachezaji wa Timu ya Soka ya African Coast ya Kijiji cha Upenja umemuomba radhi Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi kufuatia uamuzi wa Timu hiyo kuruhusu kufanyika kwa Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Upinzani uliozaa kashfa na matusi dhidi ya mbunge huyo.
 
Wachezaji hao waliomba radhi hiyo Mbele ya Mbunge huyo hapo katika Ukumbi wa Tawi la CCM la Kijiji cha Upenja kilichomo ndani ya Jimbo la Kitope Wilaya ya Kaskazini “B “ mkutano uliohudhuriwa pia na Wazee na baadhi ya viongozi waasisi wa CCM wa Kijiji hicho.
 
Akiwasilisha salamu hizo za kuomba radhi Msemaji wa Timu hiyo ya Soka ya African Coast Juma Mshamba alisema wachezaji na Viongozi wa clabu hiyo walifikia uamuzi wa  kukutana na Uongozi wa Wazee wa Tawi hilo kwa lengo la kuomba radhi baada ya tukio hilo la mvua za matusi dhidi ya Viongozi wao.
 
Juma Mshamba alisema pamoja na nia safi ya Viongozi na Wachezaji hao ya kuruhusu Mkutano huo, lakini pia zilitumika mbinu za hadhaa kwa Viongozi wa upinzani kuahidi kuwapatia fedha za kuendesha klabu yao pamoja na kuwatengenezea uwanja wao mambo ambayo hakuna hata moja hadi sasa lililotekelezwa na chama hicho cha upinzani.
 
Juma Mshamba lifahamisha kwamba Viongozi na wachezaji hao wamemuahidi na kumuhakikishia Mbunge wao kwamba kitendo hicho kilichofanyika cha kuruhusu mikutano unayozaa kashfa kwa Viongozi katu wamethibitisha kwamba   hakitarejewa tena katika maisha yao.


“ Mheshimiwa tunakubali na kuthibitisha kwamba tumeteleza katika maamuzi yetu ya ghafla na tunomba tueleweke kuwa mtoto anaponyea kiganja chake mzazi hachukui maamuzi ya kukikata bali hukisafisha kiganja hicho “. Alifafanua Juma Mshamba kwa niaba ya Viongozi na wachezaji wenzake.
 
Akizungumza na Wazee, Viongozi na wachezaji hao wa African Coast Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi alisema tayari ameshawasamehe tokea wakati wa mshindano ya Jimbo la Kitope ya Kombe la ZAWEDA ambapo timu hiyo iliidhinishwa kushiriki kwenye mashindano hayo.
 
Alisema uwamuzi huo umechukuliwa na kamati ya mashindano hayo ikielewa wazi kwamba ushawishi wa viongozi wa upinzani ndio sababu iliyopelekea wanamichezo hao kuteleza.
 
Balozi Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaasa wanamichezo hao kujiepusha na vitendo vyote vinavyoashiriadalili za  uvunjifu wa amani katika maeneo yao.
 
Balozi Seif alieleza kwamba  ipo mifano ya wazi katika nchi mbali mbali Duniani inayoonyesha kuchezewa  kwa amani na hivi sasa Mataifa hayo yametumbukia katika fadhaa na balaa jambo ambalo hata Vijana  wa mataifa hayo wanashindwa kuendeleza michezo na burudani zao.
 
Alifahamisha kwamba amani inapotoweza popote pale jamii huchukuwa muda mrefu kuirejesha katika hali yake ya kawaida huku ikiacha makovu na simanzi miongoni mwa watu waliotetereka.
 
Mbunge huyo wa Jimbo la Kitope aliwapongeza Vijana hao wa Kijiji cha Upenja kwa msimamo wao waliouonyesha wa kuendelea kukiunga mkono chama Tawala cha Mapinduzi.
 
Balozi Seif aliwataka wanamichezo hao kuzidisha juhudi katika harakati zao za kimichezo ili kujijengea msingi mzuri wa kupata ajira ndani ya sekta hiyo ambayo kwa hivi sasa inaonekana kuchukuwa eneo kubwa la ajira Duniani.
 
“ Mnapaswa kuendeleza michezo mkizingatia suala la nidhamu kama nilivyosisitiza kwenye fainali ya mashindano yetu ya Jimbo kombe la ZAWEDA  na Uongozi wa Jimbo utakuwa tayari kuchukuwa jitihada za  kusaidia changamoto zenu “. Alisema Balozi Seif.
 
Katika kuunga mkono jitihada zao za kuimarisha michezo Mbunge huyo wa Jimbo la Kitope aliwahakikishia wanamichezo hao kwamba zile changa moto zinazowakabili likiwemo marekebisho wa uwanja wao yatafanyiwa kazi na Uongozi wa Jimbo hilo.
 
Naye Mke wa Mbunge huyo wa Kitope Mama Asha Suleiman Iddi aliwatanabahisha wanamichezo hao kuwa mbali na udanyanyifu wa baadhi ya watu wanaowatumia wanamichezo katika kushiriki  kufanya maovu mitaani.
 
Mama Asha alisema maovu hayo huibuliwa ndani ya makundi ya vijana na wanamichezo kwa kutumiwa mwamvuli wa dini ingawa dini hizo misingi yake mikubwa ni kuimarisha amani na mshikamano miongoni mwa waumini wake.
 
Katika mkutano huo wa kuomba radhi  Balozi Seif aliichangia Timu hiyo ya Soka ya African Coast ya Upenja Seti ya Jezi, Fulana za Mazoezi, Mipira, fedha taslimu shilingi Laki 625,000/- kwa ajili ya kulipa ada za sajili, Deni la kambi wakati wakiwa katika mashindano ya ligi ya Wilaya, kadi za wachezaji pamoja na fedha za mrajisi wa michezo.
 

Friday, 1 August 2014

KIKAO CHA KUJENGA UELEWA JUU YA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA TASAF AWAMU YA TATU WA KUNUSURU KAYA MASIKINI KWA KAMATI YA UONGOZI NA KAMATI YA USIMAMIZI

 Baadhi ya wanakamati ya Uongozi na Kamati ya Usimamizi wakipata maelezo mafupi kuhusu TASAF Awamu ya III ni mpamgo wa kunusuru kaya masikini. Picha Maryam |Abdi OMPR.

 Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Mhe. Abdalla Mwinyi ni mwenyekiti wa Kamati hizo akipata maelezo mafupi kutoka kwa Afisa Mratibu Unguja. Picha na Maryam Abdi  OMPR.
Wajumbe wa Kamati ya Uongozi wakipata uwelewa zaidi  kuhusu TASAF Awamu III ni mpango wa Kunusuru Kaya Masikini. Picha na Maryam Abdi OMPR.