Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi

Mwanafunzi Isra Hilal Mwadini akifuatiwa na mwenzake Tamima Abass Sheha wakipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wakati wa hafla ya Maulidi ya Jumuiya ya Chuo cha Samael Academy.Kulia ya Balozi Seif ni Rais wa Sameil Academy Sheikh Nassir Bin Said.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizindua rasmi Bara bara ya pili ya Amani hadi Mtoni baada ya kukamilika awamu ya mwisho ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Akiwa na Balozi mdogo wa India nchini Tanzania wakiangalia maonyesho yaliofanya na Msanii kutoka India, Bi Navi Madhav hapo Ngome Kongwe

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Dk. Khalid S. Mohamed

akizungumza na Wadau wa Maendeleo wa Mfuko wa TASAF, walipofika Ofisini kwake kuzungumzia maendeleo ya Mfuko wa TASAF III,na kutembelea Mradi wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini (PSSN) katika Jimbo la Muyuni Wilaya ya Kusini Unguja katika Kijiji cha Muyuni B

Wazir wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakifurahia jambo wakati wa semina ya siku moja kuhusu matokeo makubwa na ya haraka katika kuleta mageuzi ya kiuchumi na kuleta maendeleo nchini iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein

Monday, 10 August 2015

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa pamoja na Uongozi wa Wizara ya Elimu akitembelea majengo ya Kituo cha Mafunzo ya Amali

Haiba ya eneo la mbele la Kituo cha Mafunzo ya Aamali kiliopo Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja ambacho hufundisha vijana waliomaliza masomo yao ya Kidatu cha Nne katika fani mbali mbali za ujasiri amali. Picha na Hassan Issa – OMPR Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa pamoja na Uongozi wa Wizara ya Elimu akitembelea majengo ya Kituo cha Mafunzo ya...

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wafanyabiashara pamoja na wataalamu wa ushauri wa Uhandisi kutoka Nchini Misri waliopo Tanzania

Makamu  Mwenyekiti wa Taasisi ya Ushauri wa Uhandisi katika miundombinu ya ujenzi, usarifu wa Miji, Majengo ya Kisasa pamoja na Vituo vya Kimataifa vya Biashara { ECG } ya Nchini Misri Mhandisi Amri Alouba  akimuonyesha  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar michoro  iliyotengenezwa na Wataalamu wa ECG ya jinsi linavyoweza kujengwa eneo la Darajani na...

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiweka saini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Rais mstaafu wa India Bwana Avul Pakir Jainulabdeen Abdul Kalam

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiweka saini kitabu cha maombolezo katika Ofisi ya Ubalozi mdogo wa India uliopo Migomani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa India Profesa Abdul Kalam Azad kilichotokea Tarehe 27 Julai 2015. Picha na Hassan Issa – OMPR Balozi Seif akimfariji Balozi Mdogo wa India aliyepo...

Thursday, 6 August 2015

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitekeleza Ahadi ya Serikali aliyoitoa Dole na Ndunduke

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikabidhi Hati  ya umiliki wa eneo la Kilimo kwa Bwana Yuweni Kibwana Nzukwi  Mmoja miongoni mwa wakulima wa Vijiji vya Dole, Ndunduke na Kijichi  baada ya upatikanaji wa ufumbuzi wa mgogoro wa maeneo hayo. Picha na Hassan Issa - OMPR Mkulima Ana Nyaka Buluju wa Dole    akikabidhiwa...

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifanya ziara fupi ya kukaguwa maendeleo ya ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya Wilaya ya Kusini

Moja kati ya majengo ya Skuli mpya ya Wilaya ya Kusini inayojengwa katika eneo la Kibuteni ambao ujenzi wake una suasua kutokana na Mkandarasi kuchelewa kupata fedha za kuendesha mradi huo. Picha na Hassan Issa – OMPR Mkuu wa ujenzi wa Kampuni ya United Builders Mhandisi Hamza Najum akimpatia maelezo Balozi Seif Ali Iddi aliyefika kukagua ujenzi wa Skuli ya Sekondari...