Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiweka saini
kitabu cha maombolezo katika Ofisi ya Ubalozi mdogo wa India uliopo Migomani
nje kidogo ya Mji wa Zanzibar kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa India Profesa
Abdul Kalam Azad kilichotokea Tarehe 27 Julai 2015. Picha na Hassan Issa –
OMPR
Balozi Seif akimfariji Balozi Mdogo wa India aliyepo Zanzibar Bwana
Setandar Kumar mara baada ya kuweka saini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo
cha Rais wa 11 wa India Profes Abdul Kalam Azad. Picha na Hassan Issa –
OMPR
Press
Release:-
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi leo ameweka saini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Rais mstaafu wa
India Bwana Avul Pakir
Jainulabdeen Abdul Kalam kilichotokea Tarehe 27 July 2015 huko shillong Meghalaya Nchini India.
Balozi Seif Ali Iddi ameweka saini kitabu hicho cha
Maombolezo hapo katika Ofisi ya Ubalozi Mdogo waJamuhuri ya India uliopo Mtaa wa Migombani nje kidogo ya
Mji wa Zanzibar.
Bwana Avul Pakir Jainulabdeen Abdul Kalam alishika
madaraka ya kuiongoza India tarehe 25 July mwaka 2002 hadi
Tarehe 25 July mwaka 2007 akiwa Rais wa 11 wa Taifa hilo kubwa Barani Asia.
Marehemu
Abdul Kalam Azad amezaliwa mnamo Tarehe
15 October mwaka 1931 ndani ya ukoo maskini akiwa Mtoto wa Nne
miongoni mwa Watoto wa Mzee Avul Pakir
Jainulabdeen katika Kabila la Tamil.
Kiongozi
huyo
wa 11 wa Jamuhuri ya India wakati wa Utoto wake alilazimika kufanya
kazi ya kusambaza magazeti mitaani wakati akiwa na umri mdogo kabisa
akijaribu
kusaidia familia yake ya kimaskini kuongeza kipato ili kupunguza ukali
wa
maisha uliokuwa ukiikabili familia hiyo.
Bwana
Abdul Kalam alipata elimu ya msingi katika Skuli ya Ramanathanpuram Schwarts
Matriculation akiwa miongoni mwa wanafunzi bora na mwenye juhudi katika masomo
yake na kupelekea kuwa mahiri katika masomo ya Hesabu.
Alijiunga
na
msomo ya sekondari katika chuo cha Saint Joseph na baadaye kujiunga na
chuo Kikuu cha Madras kwa masomo ya sayansi na hatimae kufaulu vyema
somo la Physics
Mwkaka 1854.
Mwaka 1955 Marehemu Abdul Kalam
alijiunga na mafunzo ya Uhandisi wa shughuli za anga katika Chuo Kikuu cha
Teknolojia cha Madras akiwana ndoto
siku moja kuwa askari wa Anga ndoto iliyofifia baadaye baada ya msongo
wa mawazo.
Alifanikiwa kupata shahada ya
Udaktari na kuwa muhadhiri katika vyuo mbali mbali Vikuu Nchini India kabla ya kujiunga
katika ulingo wa Kisiasa katika chama cha National Democratic Alliance { NDA }.
Tarehe 10 Juni Mwaka 2002 Chama
cha NDA ambacho kilikuwa na nguvu wakati huo kilimteua Bwana Abdul Kalam
kugombea nafasi ya Urais dhidi ya vyama vya Samajwadi Party na National
Congress Party ambapo baadaye Chama cha Samajwadi Party kikatangaza kumuunga
Mkono Bwana Kalam.
“ Nimehemewa! Kila pahala
kwenye vyombo vya Habari na mitandao ya Kijamii nimetakiwa
nitoe ujumbe. Nikafikiria ujumbe gani nitatoa wakati huu kwa wananchi wa India ?
”. Yalikuwa ni maneno ya Bwana Abdul
Kalam baada ya kuteuliwa na Chama chake
kugombea nafasi hiyo ya Urais wa India mwaka 2002.
Bwana Abdul Kalam Azad aliyefikisha umri wa Miaka 83 alikuwa akipenda sana kukutana
na watoto wa Skuli za Maandalizi kubadilishana mawazo wakati wa uhai wake hata kipindi alipokuwa na maradaka ya Urais.
Mwenyezi Muungu ailaze roho ya Marehemu Profesa Abdul Kalam Azad
aliyekuwa Muumini wa Dini ya Kiislamu Mahali Pepa Peponi. Amin.