Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi

Mwanafunzi Isra Hilal Mwadini akifuatiwa na mwenzake Tamima Abass Sheha wakipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wakati wa hafla ya Maulidi ya Jumuiya ya Chuo cha Samael Academy.Kulia ya Balozi Seif ni Rais wa Sameil Academy Sheikh Nassir Bin Said.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizindua rasmi Bara bara ya pili ya Amani hadi Mtoni baada ya kukamilika awamu ya mwisho ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Akiwa na Balozi mdogo wa India nchini Tanzania wakiangalia maonyesho yaliofanya na Msanii kutoka India, Bi Navi Madhav hapo Ngome Kongwe

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Dk. Khalid S. Mohamed

akizungumza na Wadau wa Maendeleo wa Mfuko wa TASAF, walipofika Ofisini kwake kuzungumzia maendeleo ya Mfuko wa TASAF III,na kutembelea Mradi wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini (PSSN) katika Jimbo la Muyuni Wilaya ya Kusini Unguja katika Kijiji cha Muyuni B

Wazir wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakifurahia jambo wakati wa semina ya siku moja kuhusu matokeo makubwa na ya haraka katika kuleta mageuzi ya kiuchumi na kuleta maendeleo nchini iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein

Tuesday, 3 November 2015

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitoa Taarifa ya Serikali akisisitiza Taarifa ya awali ya Serikali iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitoa taarifa rasmi ya Serikali kuhusu upotoshaji wa baadhi ya vifungu vya sheria unaendelea kufanywa na baadhi ya viongozi wa Kisiasa  juu ya uhalali wa kuendelea kuwepo madarakani Rais wa Zanzibar.  Taarifa hiyo aliitoa katika kituo cha matangazo ya Shirika la Habari Zanzibar {ZBC-TV } Karume House Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
























 Press Release:-

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imewahakikishia Wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kwamba Rais aliyepo madarakani hivi sasa ataendelea kushika madaraka ya Urais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi mpaka pale utaratibu wa Kikatiba na Kisheria wa kumpata Rais utakapokamilika.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akitoa Taarifa ya Serikali akisisitiza Taarifa ya awali ya Serikali iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuhusiana na kauli za kupotosha zinazotolewa na baadhi ya Viongozi wa vyama vya Kisiasa kuhusu uhalali wa kuendelea kuwepo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliyopo madarakani pamoja na Serikali yake.
Balozi Seif aliwaomba Wananchi wazipuuze kauli za upotoshaji zinazotolewa zikiashira zaidi uvunjifu wa amani na kuwataka waendee kuwa watulivu na kudumisha amani iliyopo Nchini.
Alisema Kifungu cha 28 Mbili {a} cha Katiba ambacho kimekuwa kikitumika katika kutoa tafrisi potofu kwa Wananchi  kwamba Rais aliyopo madarakani atamaliza muda wake wa miaka mitano kuanzia Tarehe ambayo alipokula kiapo cha uaminifu na kiapo cha kuwa Rais.
Balozi Seif alieleza kwamba ni dhahiri kwamba dhamira ya kifungu hicho cha Katiba ilikuwa kuweka bayana kuwa kama uchaguzi Mkuu utafanyika na msindi wa kiti chja Urais atatangazwa rasmi na Tumen ys Uchaguzi, hivyo muda wake wa kuendelea Mtu kuwa Rais ungemalizika kwa kufuatana na masharti ya Kifungu hicho.
Alifafanua kwa kuwa Tume ya Uchaguzi haikumtangaza mshindi wa kiti cha nafasi ya Urais ni dhahiri masharti ya kifungu hicho hayataweza kusimama na hivyo masharti ya Kifungu cha 28 {1} {a} cha Katiba kitakuwa na nguvu za Kikatiba kumpa uwezo wa Rais aliyopo madarakani kuendelea na madaraka ya Urais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Alisema Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi anapatikana  kwa mujibu wa masharti ya Kifungu cha 27 cha Katiba ambacho Rais anachaguliwa kufuatana na Katiba Hiyo na kwa mujibu wa Sheria yoyote itakayotungwa na Baraza la Wawakilishi hukusu Uchaguzi wa Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Balozi Seif alifahamisha kuwa ili Rais wa Zanzibar apatikane kwa mujibu wa Katiba na sheria ya Uchaguzi nambari 11 ya Mwaka 1984, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar inapaswa kuendesha uchaguzi na hatimae kumtangaza mshindi wa nafasi ya Urais ambae atashika madaraka hayo pale ambapo atakuwa ameapishwa rasmi kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Katiba ya Zanzibar.
Alisema Kifungu cha 28 {1} {a} cha Katiba kinaweka utaratibu kuhusu muda wa kuendelea kuwa kuwa Rais, na kwamba kwa kufuatana na kifungu hicho, mtu aliyechaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ataendelea na dhamana hiyo mpaka pale ambapo Rais anayefuata ale kiapo cha kuwa Rais.
Alieleza kwamba kwa msingi huo wa Kikatiba ni vyema Wananchi wakafahamu na kuelewa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Braza la Mapinduzi ataendelea kuwepo madarakani mkapa pale Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar itakapomtangaza mshindi wa kiti cha Urais na Rais Mteule atashika madaraka hayo baada ya kuapishwa rasmi kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Katiba.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Viongozi wa Dini mbali mbali Nchini aliokutana nao Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar














Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya pamoja na Vongozi wa Dini mbali mbali Nchi mara baada ya kufanya mazungumzo nao Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.  Kushoto ya Balozi Seif ni Kiongozi wa Timu ya Waislamu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Kabi na Kulia ya Balozi ni Kiongozi wa Wakristo Askofu Augustino Mweleli Shao.  Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.

  Press Release:-

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakamilisha taratibu zilizobakia na tayari inajiandaa kuwachukulia hatua za Kisheria watu wote waliohusika kuharibu kwa makusudi zoezi zima la Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar uliofanyika Tarehe 25 Mwezi Oktoba mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akizungumza na Viongozi wa Dini mbali mbali Nchini aliokutana nao Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kutafakari na kutafuta mbinu za kuendelea kujaribu kudumisha amani ya Nchi iliyotetereka  na kuleta mtafaruku katika kipindi hicho cha Uchaguzi.
Balozi Seif alisema ina uthibitisho kamili wa vielelezo vya ushahidi wa udanganyifu kwa maeneo yote ya Zanzibar hasa katika Majimbo ya Uchaguzi ya Kisiwa cha Pemba.
Alisema Afisa  wa Tume ya Uchaguzi au Mtu yoyote aliyehusika na udanganyifu huo aelewe kwamba mkondo  wa sheria utamkumba kwa vile vitendo walivyofanya wameisababishia hasara kubwa Serikali pamoja wa washirika wa maendeleo walioamua kusaidia uchaguzi huo.
Balozi Seif alibainisha kwamba  wakati wahusika hao wanapandishwa katika vyombo vya kisheria kujibu shutuma zinazowakabili Serikali kwa upande wake  itaweka hadharani uthibitisho kamili wa vielelezo vya ushahidi wa udanganyifu huo ili Wananchi wapate fursa ya kuelewa dhambi hiyo mbaya waliyofanyiwa na watu wachache kwa tamaa binafsi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwahakikishia Viongozi hao wa Dini kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejipanga vizuri kupitia vyombo vyake vya ulinzi kwa kupiga Doria maeneo yote katika kuona amani ya nchi inaendelea kudumu.
Aliwapongeza Viongozi hao wa Dini kwa jitihada zao wanazochukuwa za kutumia busara zao kwa kukutana na Viongozi  wa pande mbali mbali za Kisiasa wakilenga kusaidia kutuliza mumkari na machungu ya waumini wao ambao takriban wote ni  wafuasi wa vyama vya Kisiasa vilivyopo hapa Nchini.
Alivilaumu baadhi ya vyombo vya Habari hasa vile vya Nchi za Magharibi jinsi vilivyoonyesha wazi Taarifa zao nyingi  wanazotowa za zoezi zima la uchaguzi Mkuu wa Zanzibar zikionyesha  kuegemea upande mmoja tu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alielezea masikitiko yake juu ya wangalizi wa Kimataifa walioamua kufuatilia uchaguzi Mkuu wa Zanzibar kwamba hawakwenda Kisiwani Pemba muda wote wa zoezi la kupiga kura kufuatilia changamoto zilizojitokeza katika majimbo ya Pemba.
" Nimesikitishwa na waangalizi wa Kimataifa waliokuwepo Zanzibar kwa karibu mwezi mmoja kufuatilia kampeni na uchaguzi wake wameshindwa kwenda Pemba wakati wa zoezi la kupiga kura na kuonekana  zaidi katika majimbo ya Kisiwa cha Unguja.
Balozi Seif aliishauri Idara ya Habari Maelezo kuendelea kufuatilia Taarifa zinazotolewa na vyombo mbali mbali vya Habari ndani na nje ya Nchini na kukemea au kutoa Taarifa dhidi ya uchochezi unaotolewa na vyombo hivyo.
Nao Viongozi hao wa Dini mbali mbali Nchini wameishukuru na kuipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na ile ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hatua iliyochukuwa katika kusimamia amani ya Nchi.
Wananchi wa Zanzibar  wamerejea katika harakati zao za kawaida  za kimaisha  baada ya kutokea hitilafu tofauti ndani ya zoezi zima la upigaji kura kwenye  uchaguzi Mkuu wa Tarehe 25 Mwezi uliopita na kupelekea kuibuka kwa mtafaruku uliotikisa  amani ya Taifa.

Monday, 10 August 2015

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa pamoja na Uongozi wa Wizara ya Elimu akitembelea majengo ya Kituo cha Mafunzo ya Amali

Haiba ya eneo la mbele la Kituo cha Mafunzo ya Aamali kiliopo Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja ambacho hufundisha vijana waliomaliza masomo yao ya Kidatu cha Nne katika fani mbali mbali za ujasiri amali. Picha na Hassan Issa – OMPR
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa pamoja na Uongozi wa Wizara ya Elimu akitembelea majengo ya Kituo cha Mafunzo ya Amali kilichopata vifaa vipya  vya kufundishia vilivyotolewa msaada na Serikali ya Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran. Picha na Hassan Issa – OMPR
Mkuu wa Kituo cha Mafunzo ya Amali Mkokotoni Maalim Mkubwa Khamis Ibrahim wa mwanzo kutoka kushoto akimtembeza Balozi Seif aliyepo kati kati kwenye maeneo tofauti ya Kituo hicho baada ya kupata vifaa vipya vya kufundishia. Picha na Hassan Issa – OMPR
Mkuu wa Kituo cha Amali Mkokotoni Maalim Mkubwa akimpatia maelezo Balozi Seif jinsi chuo hicho kitakavyokuwa na uwezo wa kutengeneza vyombo vya moto kwa mfumo wa kisasa wa Kompyuta. Picha na Hassan Issa – OMPR
Balozi Seif akionekana kufarajika  baada ya kuonamashine za kisasa za kutengenezea thamani za ofisini na majumbani zilizomo ndani ya Kituo cha Amali Mkokotoni. Picha na Hassan Issa – OMPR





















Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwapongeza walimu wa Kituo cha Amali Mkokotoni kwa kazi kubwa ya kuwafinyanga vijana katika mazingira ya muelekeo wa kuweza kijitegemea wenyewe badala ya kusibiri ajira za Serikali. Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mheshimiwa Ali Juma Shamuhuna.
Picha na Hassan Issa – OMPR

   Press Release:-
Ile dhamira ya Serikali ya Mapin duzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali  Zanzibar ya kuanzisha  mafunzo ya Amali ili kuwapa fursa ya uhakika Vijana kupambana na changamoto zinazowakabili za ajira Nchini imeanza kuonyesha  muelekeo wa matumaini.
Muelekeo huo wa matumaini unafuatia Kituo cha Mafunzo ya Amali kiliopo Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja kupokea Vifaa  mbali mbali vya kisasa vya masomo vilivyotolewa msaada ya Serikali ya Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran.
Vifaa hivyo vikiwemo vile vya Ufundi wa Magari, Fanicha cha Maofisini, Mafriji,  Televisheni na Matrekta vinakadiriwa kugharimu  Dola  Laki Tano { 500,000 } za Kimarekani sawa na zaidi ya shilingi Bilioni Moja za Kitanzania.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipata fursa ya kufanya ziara fupi kuangalia vifaa hivyo ambavyo baadhi yake tayari vimeshaanza kutumiwa na Wanafunzi wa Kituo hicho.
Mkuu wa Kituo cha Mafunzo ya Amali Mkokotoni Maalim Mkubwa Khamis Ibrahim alimueleza Balozi Seif kwamba Uongozi wa Kituo hicho kwa Kushirikiana na Wizara ya Elimu unafanya juhudi za kuwapata wataalamu waliobobea watakaosaidia kutoa mafunzo kwa walimu wa Kituo hicho waweze kudumu kuvitumia kwa kuwafundisha Wanafunzi wao.
Maalim Mkubwa alisema vipo vifaa vya kutengenezea vyombo vya moto vinavyotumia mfumo wa Kisasa wa Komyuta ambavyo watumiaji wake watalazimika kupata taaluma ya kina.
Akitoa Taarifa kamili ya Kituo hicho baada ya ziara hiyo Maalim Mkubwa Khamis Ibrahim alisema lengo la kuanzishwa Kituo hicho karibu miaka mitatu iliyopita ni kuwapatia mafunzo ya Amali Vijana baada ya kukosa kuendelea na mafunzo yao ya Sekondari.
Alisema Kituo hicho hivi sasa kinafundisha Fani 11 zinazomjengea uwezo wa kujiajiri mwenyewe Mwanafunzi baada ya kumaliza mafunzo yake ya miaka Mitatu akizitaja baadhi ya fani hizo kuwa ni pamoja na Ufundi Magari, Uashi, Uchongaji, Friji,umeme, bomba, uchoraji pamoja na Mapishi.
Maalim Mkubwa alifahamisha kwamba  wakati Kituo kiko mbioni kufunga vifaa vya mawasiliano ili kwenda katika mfumo wa kisasa mkakati mkubwa wa miaka Mitano umeandaliwa katika kuwawezesha wanafunzi wanaomaliza mafunzo yao kufanya Mtihani wa Veta ili kuwajengea uwezo wa elimu wanayoipata ikubalike Kitaifa.
Alifahamisha kwamba mkakati huo umeshasaidia Vijana kadhaa  waliopitia Kituo hicho ambao kwa sasa idadi yao imefikia 180 na wengi kati yao wameshaajiriwa katika Taasisi mbali mbali za Umma na hata zile binafsi za ndani ya nje ya Nchi.
Akizungumzia mtazamo wa baadae wa Kituo hicho cha Mafunzo ya Amali Mkokotoni Mkuu wa Kituo hicho Maalim Mkubwa alisema kwamba mpango unaandaliwa wa kuwapatia mafunzo Kituoni hapo wanafunzi wanaomaliza Kidato cha Pili.
Alisema mkazo utawekwa wa kuwapatia mafunzo Vijana hao ya jinsi ya kuendesha Biashara chini ya Shirika la Kazi la Umoja wa Mataifa { ILO } kwa Vile Vijana hao  wapatao 6,000 wanaomaliza masomo kila mwaka hivi sasa hawaajiriki.
Akitoa shukrani zake kwa juhudi kubwa inayochukuliwa na walimu wa Kituo hicho katika kuwafinyanga wanafunzi hao Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema wakati umefika kwa kila mwana jamii kujifunza kazi yoyote ya amali itakayomuwezesha kuongeza mapato yake na kujikimu Kimaisha.
Alisema hatua hiyo kwa uande mwengine itasaidia pia kuipunguzia mzigo Serikali Kuu kwa kuagiza baadhi ya vifaa nje ya Nchini ambavyo kama jamii itajipanga vyema vinaweza kutengenezwa hapa hapa Nchini.
Makamu wa ili wa Rais wa Zanzibar alilipongeza wazo la busara la Uongozi wa Kituo hicho cha Mafunzo ya Amali la kuwaandalia mafunzo Wanafunzi wanaomaliza Kidato cha Pili.
Balozi Seif aliushauri Uongozi wa Kituo hicho kwa Kushirikiana na Wizara ya Elimu kwamba ni vyema wanafunzi wanaomaliza mafunzo yao kusaidiwa vifaa vitakavyowapa hamasa ya kuipenda kazi yao wakati watapoamua kujiajiri katika maeneo yao.
Alisema Serikali Kuu inaweza kusaidia kukiwezesha Kituo hicho  kununua vifaa  hivyo ikiwa kama zawadi kwa kufanikisha vyema mafunzo yao na kianzio kizuri cha mwanzo wa maisha yao.
Mapema Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mheshimiwa Ali Juma Shamuhuna alisema vifaa hivyo  ni ahadi iliyotolewa na Serikali ya Jamuhuri ya Kjiislamu ya Irani karibu Miaka mitatu iliyopita.
Waziri Shamuhuna alisema Kituo cha Mafunzo ya Amali Mkokotoni kilikuwa na upungufu wa vifaa vya mafunzo tokea kilipoanzishwa miaka Mitatu iliyopita  ambapo zile ndoto zilizokuwa zikiotwa na Walimu na Wanafunzi wa Kituo hicho sasa zimetimia.
Alisema  Walimu wa Kituo hicho sasa watakuwa na uwezo na shauku kubwa ya kusomesha kwa juhudi na maarifa baada ya kupata vifaa tofauti vitakavyokuwa chachu ya matumaini katika siku zijazo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wafanyabiashara pamoja na wataalamu wa ushauri wa Uhandisi kutoka Nchini Misri waliopo Tanzania

Makamu  Mwenyekiti wa Taasisi ya Ushauri wa Uhandisi katika miundombinu ya ujenzi, usarifu wa Miji, Majengo ya Kisasa pamoja na Vituo vya Kimataifa vya Biashara { ECG } ya Nchini Misri Mhandisi Amri Alouba  akimuonyesha  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar michoro  iliyotengenezwa na Wataalamu wa ECG ya jinsi linavyoweza kujengwa eneo la Darajani na kuwa katika mazingira ya Biashara  ya Kimataifa. Picha na Hassan Issa – OMPR
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wafanyabiashara pamoja na wataalamu wa ushauri wa Uhandisi kutoka Nchini Misri waliopo Tanzania kuangalia maeneo ambayo wanaweza kuwekeza miradi ya Kiuchumi. Picha na Hassan Issa – OMPR
Meneja wa Biashara wa  Kampuni ya Kimataifa ya AIKAN ya Nchini Misri Bwana  Mohammed Alef Sherief  wa kwanza kutoka kushoto akimfahamisha Balozi Seif hayupo pichani fursa zinazotolewa na Taasisi yake katika kuwajengea Vijana uwezo wa kufanya Biashara. Picha na Hassan Issa – OMPR
Balozi Seif katika Picha ya pamoja na Wafanyabiashara na wataalamu wa ushauri wa Uhandisi kutoka Nchini Misri mara baada ya kufanya mazungumzo nao Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Kushoto ya Balozi Seif ni Makamu  Mwenyekiti wa Taasisi ya Ushauri wa Uhandisi katika miundombinu ya ujenzi, usarifu wa Miji, Majengo ya Kisasa pamoja na Vituo vya Kimataifa vya Biashara { ECG } ya Nchini Misri Mhandisi Amri Alouba  na Balozi wa Tanzania Nchini Misri Balozi Mohammed Hamza. Kulia ya Balozi Seif ni Mtaalamu wa Taasisi ya Ushauri wa Uhandisi katika miundombinu ya ujenzi, usarifu wa Miji ya ECG Mhandisi Sherif Meurad pamoja na Meneja wa Biashara wa  Kampuni ya Kimataifa ya AIKAN ya Nchini Misri Bwana  Mohammed Alef Sherief. Picha na Hassan Issa – OMPR     
Balozi Mdogo wa Oman aliyepo Zanzibar Bwana Ali akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kabla ya kufanya mazungumzo yao ya Ushirikiano wa  kuimarisha uhusiano wa Kihistoria wa muda mrefu wa kidugu uliopo baina ya Oman na Zanzibar. Picha na Hassan Issa – OMPR
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na Balozi Mdogo wa Oman aliyepo Zanzibar Bwana Ali Abdullah Ofisini kwake Mtaa wa Vuga Mjini Zanzibar. Picha na Hassan Issa – OMPR
  
 Press Release:-
Taasisi ya Ushauri wa Uhandisi katika miundombinu ya ujenzi, usarifu wa Miji, Majengo ya Kisasa pamoja na Vituo vya Kimataifa vya Biashara { ECG } ya Nchini Misri imeamua kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika azma yake ya kusaidia Uchumi wa Zanzibar na ustawi wa Wananchi wake.
Kiongozi wa Ujumbe wa Wafanyabiashara wa Misri wanaotembelea Tanzania kuangalia maeneo wanayoweza kushirikiana na Serikali katika uwekezaji Mhandisi Amr Allouba alisema hayo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisi kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Mhandisi Amri Allouba ambae pia ni Makamu  Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya  uhandisi ya { ECG } alisema Wataalamu wa Taasisi hizo wako tayari kuelekeza nguvu zao ndani ya ukanda wa Afrika ya Mashariki, Zanzibar ikiwa miongoni mwake kutokana na mazingira mazuri ya rasilmali pamoja na uwekezaji.
Makamu Mwenyekiti huyo wa Taasisi ya Uhandisi ya ECG alisema Wataalamu wa Taasisi hiyo tayari wameshaandaa michoro ya jinsi linavyoweza kujengwa eneo la Darajani na kubadilishwa kuwa katika mazingira ya kisasa ya Biashara  ya Kimataifa.
Mhandisi Amr alifahamisha kwamba eneo hilo la Darajani upande wa iliyokuwa kituo cha Dala dala pamoja na Makontena linaweza kujengwa Vituo vya Biashara bila ya kuathiri mipango Miji iliyowekwa katika Mji Mkongwe wa Zanzibar ambao umo katika urithi wa Kimataifa.
Alieleza kwamba mradi huo endapo unaweza kukubalika na Serikali ujenzi wake  unaweza kuchukuwa miezi 12 hadi 18 baada ya kukamilika kwa michoro husika itayozingatia taratibu za Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia masuala ya  Sayansi, Elimu na Utamaduni { Unesco } linalohusika na hifadhi ya Mji Mkongwe wa Zanzibar.
Naye  Meneja wa Biashara wa  Kampuni ya Kimataifa ya AIKAN ya Nchini Misri Bwana  Mohammed Alef Sherief alimueleza Balozi Seif kwamba Taasisi yake imekuwa ikitoa mafunzo ya biashara ili kuwajengea uwezo vijana kujimudu kimaisha baaada kumaliza masomo yao.
Bwana Sherief alisema mpango huo unaohusisha wataalamu waliobobea katika fani ya Biashara  huandaliwa katika mazingira bora yanayotoa ushawishi kwa vijana kupenda kujiunga badala ya kubakia  kuzurura mitaani na hatimae kujiingiza katika vikundi viovu.
Akitoa Shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  aliupongeza Ujumbe huo wa Wafanyabiashara na wahandisi kutoka Nchini Misri kwa uwamuzi wake wa kutaka kusaidia taaluma katika sekta ya uwekezaji vitega uchumi hapa Zanzibar.
Balozi Seif alisema Zanzibar hivi sasa imo katika mipango ya kuimarisha uchumi wake kupitia sekta ya viwanda, uvuvi, vituo vya biashara pamoja na maeneo mengine jambo ambalo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itazingatia Michoro iliyotayarishwa na Wataalamu hao katika azma ya kufanikisha mipango yake.
Taasisi ya Ushauri wa Uhandisi katika miundombinu ya ujenzi, usarifu wa Miji, Majengo ya Kisasa pamoja na Vituo vya Kimataifa vya Biashara { ECG } ya Nchini Misri tayari imeshajenga Vituo Sita vya Kimataifa vya Kiabiashara katika Nchi za Qatar, Kuweit, Sudan, Kenya, Tanzania Bara na wenyeji Misri.
Mhandisi Amr Allouba amekuwa mshauri muelekezi aliyesimamia kujengwa kwa Kijiji cha Kisasa cha Kibiashara cha Kimataifa kikiopo katika vitongoji vya Mtaa wa Kadizani ndani ya Mji wa Cairo Nchini Misri.
Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikutana na Balozi Mdogo wa Oman aliyepo Zanzibar Bwana Ali Abdulla Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Katika mazungumzo yao Balozi Seif kupitia Balozi Mdogo huyo wa Oman aliishukuru Serikali ya Nchi hiyo kwa jitihada inazochukuwa katika kusaidia harakati za Maendeleo ya Wananchi wa Zanzibar.
Balozi Seif alisema kwamba Oman yenye uhusiano wa kidugu na kidamu na Zanzibar imekuwa mshirika mkubwa kwa Zanzibar hasa katika masuala ya kusaidia fursa za Elimu ya Juu kwa wanafunzi wa Visiwa vya Zanzibar.
Mapema Balozi Mdogo wa Oman aliyepo Zanzibar Bwana Ali Abdulla alimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Nchi yake itaendelea kuiunga mkono Zanzibar katika harakati zake za kuelekea kwenye maendeleo.
Balozi Ali Abdulla alisema uhusiano wa Kihistoria wa muda mrefu wa Wananchi wa Oman na Zanzibar unatokana na maingiliano ya kidamu yaliyopo  kwa karne nyingi zilizopita kati  ya watu wa pande hizo mbili.

 









Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiweka saini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Rais mstaafu wa India Bwana Avul Pakir Jainulabdeen Abdul Kalam

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiweka saini kitabu cha maombolezo katika Ofisi ya Ubalozi mdogo wa India uliopo Migomani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa India Profesa Abdul Kalam Azad kilichotokea Tarehe 27 Julai 2015. Picha na Hassan Issa – OMPR




















Balozi Seif akimfariji Balozi Mdogo wa India aliyepo Zanzibar Bwana Setandar Kumar mara baada ya kuweka saini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Rais wa 11 wa India Profes Abdul Kalam Azad. Picha na Hassan Issa – OMPR

 Press Release:-

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi leo ameweka saini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Rais mstaafu wa India  Bwana Avul Pakir Jainulabdeen Abdul Kalam kilichotokea Tarehe 27 July  2015 huko shillong  Meghalaya Nchini  India.
Balozi Seif Ali Iddi ameweka saini kitabu hicho cha Maombolezo hapo katika Ofisi ya Ubalozi Mdogo waJamuhuri ya  India uliopo Mtaa wa Migombani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Bwana Avul Pakir Jainulabdeen Abdul Kalam alishika madaraka ya kuiongoza India  tarehe 25 July  mwaka 2002 hadi Tarehe  25 July mwaka 2007 akiwa Rais wa  11 wa Taifa hilo kubwa Barani Asia.
Marehemu Abdul Kalam Azad  amezaliwa mnamo Tarehe 15 October  mwaka 1931  ndani ya ukoo maskini akiwa Mtoto wa Nne miongoni mwa Watoto wa Mzee Avul Pakir Jainulabdeen katika Kabila la Tamil.
Kiongozi huyo wa 11 wa Jamuhuri ya India wakati wa Utoto wake alilazimika kufanya kazi  ya kusambaza magazeti mitaani  wakati akiwa na umri mdogo kabisa akijaribu kusaidia familia yake ya kimaskini kuongeza kipato ili kupunguza ukali wa maisha uliokuwa ukiikabili familia hiyo.
Bwana Abdul Kalam alipata elimu ya msingi katika Skuli ya Ramanathanpuram Schwarts Matriculation akiwa miongoni mwa wanafunzi bora na mwenye juhudi katika masomo yake na kupelekea kuwa mahiri katika masomo ya Hesabu.
Alijiunga na msomo ya sekondari katika chuo cha Saint Joseph na baadaye kujiunga na  chuo Kikuu cha Madras  kwa masomo ya sayansi  na hatimae kufaulu vyema somo la Physics Mwkaka 1854.
Mwaka 1955 Marehemu Abdul Kalam alijiunga na mafunzo ya Uhandisi wa shughuli za anga katika Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Madras akiwana ndoto   siku moja kuwa askari wa Anga ndoto iliyofifia baadaye baada ya msongo wa mawazo.
Alifanikiwa kupata shahada ya Udaktari na kuwa muhadhiri katika vyuo mbali mbali Vikuu Nchini India kabla ya kujiunga katika ulingo wa Kisiasa katika chama cha National Democratic Alliance { NDA }.
Tarehe 10 Juni Mwaka 2002 Chama cha NDA ambacho kilikuwa na nguvu wakati huo kilimteua Bwana Abdul Kalam kugombea nafasi ya Urais dhidi ya vyama vya Samajwadi Party na National Congress Party ambapo baadaye Chama cha Samajwadi Party kikatangaza kumuunga Mkono Bwana Kalam.
“ Nimehemewa!  Kila pahala kwenye  vyombo vya  Habari na mitandao ya Kijamii nimetakiwa nitoe ujumbe. Nikafikiria ujumbe gani nitatoa wakati huu kwa wananchi wa India ? ”. Yalikuwa ni maneno ya Bwana  Abdul Kalam baada ya  kuteuliwa na Chama chake kugombea nafasi hiyo ya Urais wa India mwaka 2002.
Bwana Abdul Kalam Azad aliyefikisha  umri wa Miaka 83 alikuwa akipenda sana kukutana na watoto wa Skuli za Maandalizi kubadilishana mawazo wakati wa uhai wake hata  kipindi alipokuwa na maradaka ya Urais.
Mwenyezi Muungu ailaze roho ya Marehemu Profesa Abdul Kalam Azad aliyekuwa Muumini wa Dini ya Kiislamu Mahali Pepa Peponi. Amin.

Thursday, 6 August 2015

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitekeleza Ahadi ya Serikali aliyoitoa Dole na Ndunduke

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikabidhi Hati  ya umiliki wa eneo la Kilimo kwa Bwana Yuweni Kibwana Nzukwi  Mmoja miongoni mwa wakulima wa Vijiji vya Dole, Ndunduke na Kijichi  baada ya upatikanaji wa ufumbuzi wa mgogoro wa maeneo hayo. Picha na Hassan Issa - OMPR
Mkulima Ana Nyaka Buluju wa Dole    akikabidhiwa hati ya umiliki wa eneo la kilimo kutoka kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  hapo Skuli ya Wazazi Dole Wilaya ya Magharibi  “A “. Picha na Hassan Issa - OMPR





















Baadhi ya wakulima wa  Vijiji vya Dole, Ndunduke na Kijichi wakifuatilia zoezi la kukabidhiwa hati zao za umiliki wa maeneo ya kilimo kwenye Vijiji vyao lililafanywa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi. Picha na Hassan Issa - OMPR 
  
Press Release:-

Hatma ya Mgogoro wa maeneo ya Kilimo unaowahusisha Wakulima wa Vijiji vya Dole, Ndunduke, Kijichi na Nguruweni dhidi ya baadhi ya watu wanaovamia  maeneo hayo hivi sasa umeshafikia ukingoni baada ya kurindima kwa takriban miaka 12.
Mgogoro huo ulizuka kufuatia baadhi ya watu wenye uwezo wa kifedha pamoja na marafiki na familia za maafisa wa taasisi za Kilimo kuvamia maeneo hayo wakati wakielewa kwamba wakulima wa asili wa maeneo hayo walikuwa wakiyatumia kuendeleza shughuli zao za kilimo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitekeleza Ahadi ya Serikali aliyoitoa Tarehe 14 Disemba mwaka 2012 ya kuwamilikisha Wakulima hao alikabidhi Hati za umiliki huo kwa Wakulima 145 wa Dole, Ndunduke na Kijichi hapo katika maeneo ya skuli ya Wazazi Dole.
Wakulima hao 145 ni miongoni mwa wote Mia 222 wa Vijiji hivyo ambao walipata hati hizo baada ya kuyatumia maeneo hayo ya Serikali  yaliyokuwa chini ya Wizara ya Kilimo wanayolimwa kwa kipindi kirefu cha maisha yao.
Akizungumza na Wakulima na Wananchi wa Vijiji hivyo vya Dole, Ndunduke na Kijichi Balozi Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeamuwa kufanya hivyo ili kuwapa fursa ya umiliki wakulima hao waendeleze shughuli zao za Kilimo kwa utulivu zaidi.
Balozi Seif aliwatanabahisha wakulima hao  kuelewa kwamba maeneo waliyopewa ni kwa ajili ya kilimo kama walivyofanyiwa wenzao wa Kijiji cha Nguruweni .
 Alisema maeneo hayo tokea asili kutokana na mazingira yake yamekuwa ni vianzio vya maji, hivyo Serikali Kuu haitoruhusu kamwe watu wakaamua kubadilisha utaratibu na kuanza kujenga nyumba za kudumu za kuishi.
“ Wananchi wa Nguruweni bado bado wanafuata utaratibu waliopewa kama Hati zao zinavyoelekeza. Na Nyinyi wakulima wa Dole, Ndunduke pamoja na Kijichiinafaa muige mfano wa wenzenu wa Nguruweni “. Alisema Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwashukuru na kuwapongeza Wananchi na Wakulima wa Dole, Ndunduke, Nguruweni na Kijichi kwa ustahamilivu wao mkubwa waliouonyesha ambao umeipa faraja Serikali na kufikia hatua njema na ya mafanikio.
Balozi Seif aliwashauri Wakulima hao mbali ya kuendeleza shughuli za kilimo mchanganyiko lakini pia wana fursa ya kuimarisha miti ya mishoki shoki  kwa nia ya kuongeza  mapato yao na kujikimu kimaisha katika azma ya kupunguza umaskini.
Akitoa Taarifa fupi katika mkutano  huo wa makabidhiano ya hati ya umiliki wa maeneo ya kilimo, Mwenyekkiti wa Wakulima wa Dole, na Ndunduke Dr. Daudi Silas Mukaka alisema Serikali Kuu imeonyesha nia thabiti ya kuwajali Wananchi wake.
Dr. Mukaka alisema Wananchi pamoja na Wakulima wa Dole na Ndunduke wamefarajika sana kutokana na kazi kubwa iliyochukuliwa na Serikali  Kuu chini ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwa kushirikiana na baadhi ya Viongozi wa Taasisi za Kilimo na Ardhi katika kulipatia ufumbuzi wa kudumu suala hilo la mgogoro wa maeneo ya kilimo.
Alifahamisha kwamba mgogoro huo wa miaka 12 ulianza hatua za kuchukuliwa  ufumbuzi katika kikao cha Tarehe 14 Disemba Mwaka 2012 chini ya Mwenyekiti wa Kamati iliyoundwa Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Abdullah Mwinyi ambapo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alitoa ahadi ya kupatiwa ufumbuzi tatizo hilo.
Mapema Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mh. Abdullah Mwinyi  alisema licha ya Wananchi wa Vijiji hivyo kuonyesha ishara ya hasira lakini alifarajika kuona kwamba busara ilitawala katika kulishughulikia tatizo hilo.
Mheshimiwa Abdullah alisema Wananchi hao wanapaswa kuendelea kumpongeza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kutokana na Uongozi wake wa busara wa kuweka ahadi na akawa makini kuitekeleza.
“ Kiongozi mzuri ni yule anayeweka ahadi akaitekeleza. Balozi Seif anastahiki kupongezwa na kushukuriwa kwa suala hili ambalo sote tunaelewa lilivyokuwa na ugumu wake “. Alisema Mkuu huyo wa Mkoa wa Mjini Magharibi.
Migogoro ya ardhi katika maeneo mbali mbali ya Visiwa vya Zanzibar hivi sasa inaonekana kuchukuwa sura mpya ya kuanza kuchukuliwa hatua za ufumbuzi kutokana na uamuzi wake wa kusajili ardhi yote ya Zanzibar.