Monday, 21 July 2014

Uzinduzi wa mikopo ya wastaafu

 VIONGOZI wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) wakimsikiliza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar , Mhe. Balozi Seif Ali Idd(hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Mikopo ya Wastaafu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kwa kushirikiana na TPB, uzinduzi huo ulifanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View iliyopo Kilimani mjini Zanzibar.(Picha na Haroub Hussein).
 WAFANYAKAZI wa Benki Posta Tanzania (TPB) wakiwa katika uzinduzi wa Mikopo ya Wastaafu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kupitia Benki hiyo uliozinduliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar , Mhe. Balozi Seif Ali Idd katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani.(Picha na Haroub Hussein).

 OFISA Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Ndg. Sabasaba Moshingi akitoa maelezo ya benki hiyo wakati wa uzinduzi wa Mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kwa kushirikiana na Benki hiyo uliofanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View.(Picha na Haroub Hussein).

 WAALIKWA mbali mbali wakiwa katika uzinduzi wa Mikopo kwa Wastaafu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kwa kushirikiana na Benki ya Posta Tanzania (TPB), uzinduzi huo ulifanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani.(Picha na Haroub Hussein).

 KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF), Ndg. Khamis Filifili Thani akitoa maelezo ya mfuko huo katika uzinduzi wa Mikopo kwa wastaafu wa ZSSF kwa kushirikiana na Benki ya Posta Tanzania (TPB) uliofanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View.(Picha na Haroub Hussein).
 WAZIRI wa Fedha Zanzibar, Mhe. Omar Yussuf Mzee akizungumza katika uzinduzi wa Mikopo kwa Wastaafu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanizbar (ZSSF) uliofanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View iliopo Kilimani mjini Zanzibar.(Picha na Haroub Hussein).
 MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Idd akizindua mfuko wa Mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kwa kushirikiana na Benki ya Posta Tanzania (TPB) uliofanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View iliopo Kilimani mjini Zanzibar.(Picha na Haroub Hussein).
MKUU wa Mkoa wa Mjini Magharib , Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis akitoa shukrani katika uzinduzi wa Mikopo kwa Wastaafu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kwa mashirikiano na Benki ya Posta Tanzania (TPB) uliofanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View iliopo Kilimani mjini Zanzibar.(Picha na Haroub Hussein).