Wednesday, 30 July 2014

Mwenge wa Uhuru wawasili Zanzibar


 Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Getrudi Mpaka akitoa salam za Mkoa huo kabla ya kuukabidhi Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Mjini Magharibi leo july 30.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadiki akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi Khamis, makabidhiano hayo yamefanyika uwanja wa ndege mkongwe Kiembesamaki leo. (Picha na Makame Mshenga- Maelezo Zanzibar).
 Vijana wa Chipukizi wakiimba nyimbo ya Mwenge.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Ikulu na Utawala Bora Dkt. Mwinyihaji Makame akishika mwenge wa Uhuru ulipowasili Zanzibar.
 
Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Hamza Ibrahim kutoka Mjini Magharibi na maaskari wakiukimbiza Mwenge.

 Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi Khamis akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Magharibi Hasan Mussa Takrima kwa ajili ya kuukimbiza katika Wilaya yake
Mkuu wa Wilaya ya Magharibi Hasan Mussa Takrima akikimbiza Mwenge wa Uhuru mara baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini tayari kuanza ziara yake