Mwenyekiti wa Mamlaka ya kukuza Biashara Tanzania (TANTRADE) Bi. Thabetha Mwambenja akiteta jambo na Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko wa Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui katika ufunguzi wa maonyesho ya Biashara ya Edi el Fitri yanayofanyika Uwanja wa Maisara Mjini Zanzibar.
Sehemu ya waalikwa waliofika katika maonyesho ya Biashara ya Edi El Fitri yanayoandaliwa kwa pamoja kati ya TANTRADE na Wizara ya Biashara ya Zanzibar kila mwaka wakimsikiliza mgeni Rasmi katika ufunguzi wa maonyesho hayo.
Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko wa Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui akikata utepe kufungua maonyesho ya Biashara ya Ed El Fitri katika viwanja vya Maisara, wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa TANTRADE Bi. Sabetha Mwambenja na kati kati ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE Bi. Anna Bulondo.
Waziri wa Biashara Viwana na Masoko Nassor Ahmed Mazrui akiangalia bidhaa za wajasiriamali kwenye maonyesho ya Biashara ya Edi El Fitri katika kiwanja cha Maisara.
Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko wa Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui katika picha ya pomoja na viongozi mbali mbali.