Monday, 21 July 2014

Balozi Seif Ziarani Nungwi




 Katibu wa CCM Tawi la Nungwi Nd. Adibu Ali Sheha akitoa Taarifa fupi ya Maskani ya CCM ya Amani na Utulivu ya Kijiji hicho ambayo itajengwa kwa mchanga wa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Zanzibar Dr. Ali Mohd Sheni kwa kushirikiana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi.

 Baadhi ya wanamaskani ya amani na Utulivu ya Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja wakisikilizika Majumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif hayupo pichani aliyefika kwenye maskani hiyo kutekeleza ahadi waliyotoa na Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohd Sheni.
Mjumbe Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wanamaskani  ya Amani na Utulivu Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.

 Balozi Seif akimkabidhi fedha Taslim Shilingi Milioni 4,000,000/-  Mwanachama wa Maskani ya Amani na Utulivu ya Nungwi Bibi Leila Kheir Haji kwa ajili ya ujenzi wa maskani yao ikiwa ni utekelezaji wa ahadi waliyoitoa na Rais wa Zanzibar.

 Baadhi ya Akina Mama wa Kijiji cha Mvuleni Kidoti wakitoka ndani ya pango kujipatia huduma za maji safi wakishuhudiwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Balozi Seif aliyetembelea kijiji hicho.

 Akina Mama wa Mvuleni wakijiandaa kupandisha mlima mkubwa kuelekea kijijini kwao baada ya kuisaka huduma hiyo kwenye pango liliopo ng’ambo ya Kijiji hicho.


Balozi Seif akikagua Msikiti wa Ijumaa wa Kijiji cha Mvuleni ambao unahitajika kunyanyuliwa ili kutoa hufrsa nzuri kwa waumini wa dini ya Kiislamu kufanya ibadaza yao kwa utulivu.



Balozi Seif akimkabidhi Seti ya Jezi Kijana Zamir Simai Haji kwa ajili ya Timu ya Vijana wa CCM wa Kijiji cha Mvbuleni kiliopo Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.