Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi

Mwanafunzi Isra Hilal Mwadini akifuatiwa na mwenzake Tamima Abass Sheha wakipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wakati wa hafla ya Maulidi ya Jumuiya ya Chuo cha Samael Academy.Kulia ya Balozi Seif ni Rais wa Sameil Academy Sheikh Nassir Bin Said.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizindua rasmi Bara bara ya pili ya Amani hadi Mtoni baada ya kukamilika awamu ya mwisho ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Akiwa na Balozi mdogo wa India nchini Tanzania wakiangalia maonyesho yaliofanya na Msanii kutoka India, Bi Navi Madhav hapo Ngome Kongwe

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Dk. Khalid S. Mohamed

akizungumza na Wadau wa Maendeleo wa Mfuko wa TASAF, walipofika Ofisini kwake kuzungumzia maendeleo ya Mfuko wa TASAF III,na kutembelea Mradi wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini (PSSN) katika Jimbo la Muyuni Wilaya ya Kusini Unguja katika Kijiji cha Muyuni B

Wazir wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakifurahia jambo wakati wa semina ya siku moja kuhusu matokeo makubwa na ya haraka katika kuleta mageuzi ya kiuchumi na kuleta maendeleo nchini iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein

Tuesday, 30 December 2014

Balozi Seif awatakia kheri ya mwaka mpya wazee hapa Nchini


 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Sheikh Mkuu wa Msikiti wa Asili wa Ijumaa Micheweni Mjini  Sheikh Haji Khatib Haji.
 Balozi Seif akitoa Mkono wa Pole kwa Watoto na Wajukuu wa Muasisi wa Afro Shirazy Party Marehemu Bibi Ashura Abeid hapo Nyumbani kwa Tibirinzi Chake chake Pemba.
 Balozi Seif akibadilishana mawazo na Mzee Khamis Mkadara Khamis wakati alipokwenda kumkagua na kumtakia kheir ya Mwaka Mpya wa 2015.
 Mzee Bakari Khamis Kombo wa Kijiji cha  Micheweni akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefika kumjulia hali na kumtakia kheri ya mwaka mpya wa 2015

  Balozi Seif akimsalimia mzee  Khamis Othman Kapona wa Kijiji cha Chekea Mtambwe alipokwenda kumtembelea na kujua hali yake pamoja na kumpa kheri ya mwaka mpya
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimtakia kheri ya mwaka mpya wa 2015  Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Jimbo la Micheweni Mzee Kombo Fundi Kombo wakati alipomtembelea na kujua hali yake.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

Monday, 29 December 2014

Balozi Seif akagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Konde - Wete



GARI ya Kampuni ya Mecco ikimwaga lami katika mashine maalumu ya kuchawanyia lami hiyo, katika barabara ya Konde-Wete kama wanavyoonekana wafanyakazi wa kampuni hiyo wakiwa kazini.


GARI maalumu ya kutandazia lami ya kampuni ya Mecco, ikiwa kkazini katika barabara ya Konde-Wete, kama inavyoonekana kazi hiyo ikiwa inaendelea kwa kasili, ili kukamilika kwa barabara hiyo.



GARI maalumu ya kuweka sawa lami kutoka katika kampuni ya Mecco ikiweka lami hiyo, katika barabara ya Konde-Wete kama ilivyokutwa na mpiga picha.



MAKAMO wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Balozi Seif Ali Iddi akipata maelekezo ya hali ya uwekaji wa lami katika barabara ya Konde- Wete, kutokana kwa msimamizi wa Ujenzi wa Kampuni hiyo Abdulkadir Mohammed Bujet, wakati alipotembelea na kuangalia hali ya barabara hiyo inavyokwenda.

Na Othman Khamis Ame, OMPR
Harakati za ujenzi wa Bara bara ya Wete hadi konde ikiwa miongoni mwa mradi wa Bara bara tatu Kisiwani Pemba zinaendelea baada ya maridhiano baina ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  na mjenzi wa mradi huo Kampuni ya Mwananchi Contracting Company Engineering { MECCO }.
Ujenzi wa Bara bara hizo wa awamu ya kwanza wenye urefu wa Kilomita zaidi ya 30 ulioanza rasmi Tarehe 15 Mei mwaka 2009 umekuwa ukisua sua kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo uchelewaji wa feha kutoka kwa mfadhili wa mradi huo Benki ya Maendeleo ya Kiislamu { BADEA.
Maridhiano hayo yalifiikiwa kutokana na Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar kutembelea mradi huo mapema mwezi huu na kufikiwa maazimio ya yaliyoagiza juhudi zifanywe ili madai ya mjenzi wa bara bara hizo yashughulikiwe kwa upande mwengine wa Serikali.
Maazimio hayo 
pia
 yalielekezwa na kumuomba mjenzi aendelee na kazi kulingana na uwezo wake alionao wakati Serikali Kuu inaendelea kushughulikia malipo ya madai yake mbali mbali.
Akitoa maelezo kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefanya ziara ya kukagua maendeleo hya ujenzi wa bara bara kutoka Wete hadi Konde  Afisa Mdhamini wa Miundo mbinu na Mawasiliano Pemba Nd.Hamad Ahmed Baucha alisema Uongozi wa usimamizi wa kazi hiyo umeishukuru Kamati hiyo ya Baraza la Wawakilishi kwa uamuzi wake wa kuingilia kati suala hilo.
Nd. Baucha alisema hatua hiyo mbali ya kunusuru hasara nyengine lakini pia imetia moyo na chachu kwa wananchi  pamoja na wawekezaji kufanya shughuli zao kwa uhakika baada ya kukamilika kwa miundo mbinu ya mawasiliano ya bara bara.
Alisema kazi ya uwekaji lami kwenye bara bara hiyo ya Wete hado Konde ilianza mnamo Tarehe 19 mwezi huu na kuendelea kwa kasi ikileta matumaini ya kuwa kazi hiyo inaweza kukamilika kwa wakati uliopangwa.
Mwakilishi wa Kampuni ya Mwananchi Contracting Company Engineering               { MECCO } Bwana  Abdullkadir Mohammed Bujet alimuhakikisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  wahandisi wa kazi hiyo watajitahidi kutekeleza mradi huo katika kiwango bora kinachokubalika.
Bwana Bujet alisema ujenzi huo wa lami hivi sasa unafanyika kwa masafa ya mita mia tato kwa siku kiwango kinacholeta faraja kwa kukamilika kazi hiyo katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Januari mwakani.
Alifahamisha kwamba hivi sasa tayari kilo mita 14.2 za bara bara hiyo itokayo Wete hadi Konde imeshawekewa lami zikibakia kilo mita 12 tu kukamilisha awamu hiyo.
Mradi huo wa awamu ya kwanza wa ujenzi wa kilo mita 30 unahusisha kufumua bara bara, kujenga tuta la bara bara,ujenzi wa madaraja mdogo madogo { pipe culvert } pamoja na madaraja saba sehemu mbali mbali ya bara bara zote mbili za Wete Gando na Wete Konde.
Kuchelewa kukamilika kwa wakati mradi huo wa bara bara tatu za Pemba uliokuwa wa gharama  ya shilingi Bilioni 23,389,551,848.75 umesabisha kuongezeka na kufikia gharama ya shilingi Bilioni 30,176,874,854/- hadi utakapokamilika.
Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akikamilisha ziara yake ya siku tatu Kisiwani Pemba kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo aliutembelea msikiti mkongwe kabisa ndani ya Ukanda wa Afrika Mashriki uliopo Micheweni Mjini Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Akisalimiana na uongozi wa Kamati ya msikiti huo pamoja na baadhi ya waazi wake  Balozi Seif aliwakumbusha waumini wa Dini ya Kiislamu kuendelea kushikamana kama maamrisho ya dini yao yanavyoelekeza.
Alisema Dini ya kiislamu imekuwa ikisisitiza suala la amani jambo ambalo likifuatwa na kutekelezwa ipasavyo husaidia kuwapa utulivu pamoja na wananchi kufanya ibada za shughuli zao kama kawaida.
Aliwaasa kuwa na hadhari ya kuchanganya dini na siasa kama baadhi ya watu nhasa wanasiasa kujaribu kushawishi watu kufanya hivyo matokeo yake ni kuanzisha cheche za uhasama na wasi wasi katika jamii.
Msikiti wa Ijumaa wa Micheweni Mjini unakisiwa kujengwa tokea karne ya 14 kipindi ambacho kilikuwa na harakati za kueneza kwa Dini ya Kiislamu katika mwambao wa Afrika Mashariki.

Balozi Seif: CCM bado madhubuti na inazidi kuimarika


 Mlezi wa CCM Mkoa wa Magharibi Balozi Seif akipandisha Bendera ya CCM Mbele ya Tawi la CCM Mombasa kwa Mchina kabla ya kuweka jiwe la msingi la Twi hilo
  Balozi Seif  ambae 
pia
 ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM akiweka jiwe la msingi la Tawi la CCM Mombasa kwa Mchina.

 Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Tawi la CCM  Mombasa  kwa Mchina Nd. Ahmada Yahya Abdulwakil akitoa ufafanuzi wa ujenzi mbele ya Mlezi wa CCM Mkoa wa Magharibi Balozi Seif mara baada ya kuweka jiwe la Msingi la Tawi hilo.

 Mlezi wa CCM Mkoa wa Maghribi Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika Picha ya pamoja na uongozi mzima wa Tawi la CCM Mmobasa kwa Mchina, Wilaya ya Dimani na Mkoa wa Magharibi mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la Tawi hilo.
Wanachama wapya 79 wa CCM na Jumuiya zake wa Tawi la CCM Mombasa kwa Mchina wakila liapo mara baada ya kukabidhiwa kadi na Mlezi wa CCM Mkoa wa Magharibi Balozi Seif Ali Iddi.

Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
 
Na Othman Khamis Ame, OMPR
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi alisema wimbi la vijana wa vyama vya upinzani kuamua kuvihama vyama hivyo na kujiunga na CCM ni dalili za umadhubuti  wa chama hicho unaoonekana kuimarika kila wakati.
 
Alisema chama cha Mapinduzi chenye sera  na ilani imara inayokiwezesha kushinda kila baada ya miaka mitano tokea kuanza kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa Tanzania ndio kimbilio la watu wote wenye busara ya kutaka kujiunga na ulingo wa siasa.
 
Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Mlezi wa Mkoa wa Magharibi Kichama alisema hayo mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Tawi la Chama cha Mapinduzi Mombasa kwa Mchina Wilaya ya Dimani Mkoa wa Magharibi.
 
Alisema makundi ya wafuasi wa vyama vya upinzani wanaoamuwa wenyewe kuvihama vyama vyao na kujiunga na Chama cha Mapinduzi ni muelekeo wa ishara kwa CCM kuendelea kuongoza dola katika uchaguzi  Mkuu ujao wa mwaka 2015.
 


Hata hivyo Balozi Seif aliwatahadharisha Viongozi na Wanachama wa CCM wasikae na kubweteka na mawazo ya kushinda uchaguzi bila ya sera na mikakati ya kujipanga vyema kwa ajili ya ushindi huo.
 
Aliwaomba wana CCM popote pale walipo nchini Tanzania kuendelea kushikamana na kuacha majungu, fitna na makundi ili  ushindi uwe rahisi zaidi ya chaguzi zote zilizopita za mfumo wa vyama vingi hapa Nchini.
 
Balozi Seif aliupongeza Uongozi, wanachama na  wapenzi wa chama hicho waliojitolewa kwa nguvu zao na kuhakikisha kwamba ujenzi wa Tawi la Mombasa kwa Mchina unasimama imara.
 
Alisema licha ya kuungwa mkono na wapenzi na watu tofauti katika ujenzi wa Tawi hilo lakini nguvu za ukamilishaji wa tawi hilo zitaendelea kubakia mikononi mwa Viongozi pamoja na Wanachama wenyewe wa Tawi hilo.
 
Aliutaka uongozi wa Mkoa wa  Magharibi kuwa na tahadhari ya uvamizi wa makaazi unaofanywa na baadhi ya watu kwa lengo maalum la kuongeza nguvu za  kuimarisha vyama vya kisiasa katika kujiandaa kwa uchaguzi Mkuu ujao.
 
Balozi Seif akiwa pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar   aliwakumbusha masheha na Wakuu wa Wilaya  nchini kuendelea kufuata sheria za nchi ipasavyo ili kila mwenye haki yake anapata fursa  bila ya vikwazo,ubaguzi wala itikadi za kisiasa.
 
Alisema tabia ya baadhi ya watu zaidi wana siasa kushindikiza masheha kutoa vibali  kwa wafuasi au vijana wao kwa kutaka kupatiwa vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi wakati muda wa ukaazi wa vijana hao haujatimia ni kuvunja sheria za nchi.
 
“ Suala hili la kutishwa masheha na kulaumiwa Wakuu wa Wilaya nililikemea nilipokuwa katika ziara yangu wiki hii Kisiwani Pemba. Na hapa nalirejea tena kwa kuwakumbusha masheha na wakuu hao wa Wilaya kufanya kazi zao kwa kujiamini “. Alisema Balozi Seif.
 
Aliwataka na kuwaasa vijana kujiepusha na ushawishi huo wa wana siasa wa kutaka kuwalazimisha kufanya mambo yaliyo kinyume na sheria na utaratibu wa Nchi.
 
Katika kuunga mkono ujenzi wa Tawi hilo la Mombasa Kwa mchina Mlezi huyo wa Mkoa wa Magharibi Kichama Balozi Seif aliahidi kukamilisha ukumbi wa Tawi hilo kwa kutoa mchango wa Jipsam, taa ,mafeni yote ukumbini hapo pamoja na kusaidia  Seti moja ya Jezi kwa Timu kati ya timu 16 zilizomo ndani ya Tawi hilo .
 
Mapema akitoa Taarifa fupi ya ujenzi wa Tawi hilo Mwenyekiti wa Ujenzi ambae pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM  Nd. Ahmada Yahya Abdulwakil  alisema ujenzi huo ulioanza rasmi Tarehe 28 Septemba 2013 umekuja kufuatia wanachama hao kukosa ofisi ya kufanyia kazi  zao za Kisiasa.
 
Nd. Ahmada alisema tawi hilo lenye ofisi zote zinazohitajika zikiwemo za jumuiya za chama litakuwa na huduma za kisasa zinazokwenda na wakati  pamoja na ukumbi wa Mikutano ambao utakodishwa kwa shughuli za kijamii ili kuliongezea mapato Tawi hilo.
 
Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Ujenzi wa Tawi la CCM Mombasa kwa Mchina aliwashukuru viongozi na wapenzi wote wa chama hicho waliojitolea kuunga nguvu katika ujenzi wa Tawi hilo lenye hadhi ya chama chenyewe.
 
Katika hafla hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi la Tawi la CCM Mombasa Kwa Mchina Balozi Seif alikabidhi kadi kwa wanachama wapya  79 wa chama cha Mapinduzi pamoja na Jumuia zake wa Tawi hilo.
 
Ujenzi wa  Tawi la Chama cha Mapinduzi Mombasa kwa Mchina  hadi sasa umeshagharimu zaidi ya shilingi Milioni 45,100,000/- .
 

Balozi Seif aendelea na ziara kisiwani Pemba


 
KATIBU mkuu Wizara ya Kilimo na Mali asili Zanzibar, Mhe:Afani Othman Maalim akimfahamisha jambo Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Balozi Seif Ali Iddi, wakati alipotembelea shamba la mboga mboga la kikundi cha Wengi Wape Uwandani Vitongoji Chake Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA)

 
MAKAMO wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Balozi Seif Ali Iddi, akimuuliza jambo Katibu Mkuu wizara ya Kilimo na Maliasili Zanzibar Mhe:Afani Othman Maalim, wakati alipotembelea shamba la mboga mboga la kikundi cha Wengi Wape cha Uwandani Vitongoji Chake Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA)

 
MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Mhe:Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mhe:Jabu Khamis Mbwana, wakati alipowasili katika Tawi la CCM Jiheshimu Mnarani Kigomasha.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

 
MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe:Balozi Seif Ali Iddi, akikunjuwa kitamba kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi, Tawi la CCM tuheshimiane Mnarani Makangale Wilaya ya MIcheweni Kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA)

 
KATIBU wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba, Abrahman Makame akimpatia malezo ya Ujenzi wa Maskani ya Profesa Jakaya Kikwete huko Chekea Mtambwe Wilaya ya Wete Mkoa wa kaskazini Pemba. (Picha na Abdi Suleiman, PEMBA)

 
MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe:Balozi Seif Ali Iddi, akimuangalia Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Raiza wa Zanzibar Mhe:Mohamed Aboud, aliyekaa kitako katika maskani ya Mhe:Profesa Jakaya Kikwete. (Picha na Abdi Suleiman, PEMBA)

 
MJUMBE wa kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe:Balozi Seif Ali Iddi, katikati akiwa amekaa kitako katika Maskani ya Mhe:Profisa Jakaya kikwete, kushoto ni waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Mhe:Mohammed Aboud Mohammed na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mhe:Omar Othman Khamis. (Picha na Abdi Suleiman, PEMBA)

 
MJUMBE wa kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe:Balozi Seif Ali Iddi, katikati akiwa amelala katika Maskani ya Mhe:Profisa Jakaya kikwete, baada ya kuitembelea kuikagua maskani hiyoo huko Chekea Mtambwe Mkoa wa Kaskazini Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA)

 
MJUMBE wa kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe:Balozi Seif Ali Iddi, akipokea zawadi ya ndizi aina ya mkono Mmoja, kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Wete Kombo Hamad Yussuf katikaki.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA)

MJUMBE wa kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe:Balozi Seif Ali Iddi, akimkabidhi katiba zilizopendekezwa na Bunge la Katiba, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Wete Kombo Hamad Yussuf, ambazo Aprili mwakani wananchi wataipigiakura.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA)

Sunday, 21 December 2014

Balozi Seif amwakilisha Dk Shein alipofungua tamasha la sita la Kiislamu


 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein akilifungua Tamasha la Sita la Kiislamu Zanzibar  hapo jumba la Wananchi Forodhani Mjini Zanzibar.

 Balozi Seif akimkabidhi cheti maalum Balozi wa Palestina Nchini Tanzania Bwana Nassib Abu Jesh kwa ushiriki wa Ubalozi huo kwenye kuunga mkono TYamasha la Kiislamu Zanzibar.
Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na msanii maaruru aliyepata sifa kipindi kifupi kutokana na Qasida yake ya Nadu Ustadh Juma Zubeir baada ya kumkabidhi cheti maalum kutokana na ubunifu wake uliosaidia Tamaduni ya kiislamu.

Kulia yao ni Mwenyekiti wa Tamasha la Kiislamu Zanzibnar Ustadh Jabir Haidar Jabir.

Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
 
Na Othman Khamis Ame, OMPR
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Al-Hajj Dr. Ali Mohamed Shein ametoa wito kwa jamii kupitia Tamasha la Kiislamu kuendelea kuelimishana na kukumbushana umuhimu wa kuendeleza amani na kuepuka mifarakano baina ya waislamu wenyewe na hata wale wanaoamini Dini nyengine hapa nchini.
 
Alisema Walimu na Masheikh  nao wasichoke kuukumbusha umma faida ya kuwepo kwa amani ya nchi kwa vile bado yapo matukio yanayothibitisha na kuashiria uwepo wa baadhi ya watu walioghafilika.
 
Al Hajj Dr. Ali Mohamed Shein alieleza hayo wakati wa hafla ya ufunguzi wa Tamasha la sita la Kiislamu katika Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo katika Kasri ya Kifalme Jumba la Wananchi Forodhani Mjini Zanzibar.
 
Alisema ni jambo la kusikitisha kuona kwamba baadhi ya waislamu wanaendeleza mifarakano na migogoro katika nyumba za ibada vitendo vinavyoashiria uvunjaji wa sheria vinavyopelekea  uharibifu wa mali, kuumizwa watu wasio na hatia na wakati mwengine kusababisha upotevu wa maisha ya watu.

 
Rais wa Zanzibar alifahamisha kwamba matukio hayo maovu ni kinyume na mafundisho ya dini yenyewe sambamba na kukiukwa kwa haki za Binadaamu ambapo kwa ujumla wake  Mwenyezi Muungu amekuwa akiwaasa waja wake kuacha kumwaga damu kusiko na hatia.
 
Alieleza kwamba wakati umefika kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu na wananchi wote nchini kujifunza athari za kutoweka kwa hali ya amani wakishuhudia kutokea katika nchi mbali mbali Duniani.
 
“ Matokeo ya hali kama hii ya kusikitisha kama tunavyoshuhudia katika baadhi ya Mataifa ya Kiislamu kama vile Syria, Afghanistan na Iraq na hali wanayokabiliana nayo wananchi wa Palestina “. Alisema Dr. Sheni.
 
Rais wa Zanzibar alisisitiza kwamba ni wazi kuwa athari za matokeo ya kutoweka kwa hali ya amani huwafika watu wote lakini waathirika wakuu zaidi katika janga hilo ni watoto, wanawake,watu wenye ulemavu, wagonjwa pamoja na wazee wasioweza kujihami.
 
Al – Hajj Dr. Ali Mohamed Shein alitoa wito kwa Tamasha hilo la Kiislamu kuwa chachu ya kuelimishana na kukumbushana  katika kukabiliana na vitendo vya udhalilishwaji wa wanawake na watoto  ambavyo vinaonekana kuendelea kulitia doa Taifa.
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi lielezea faraja yake kutokana na wazo lililoibua kuanzishwa kwa Tamasha la Kiislamu hapa Zanzibar ambalo limekuwa chem chem ya elimu na maarifa ya Kiislamu.
 
Alisema Tamasha hilo lina fursa pana ya kuibua vipaji katika umahiri wa kusoma na kuhifadhi Quran Tukufu, usomaji wa Maulidi, Qasida, mashairi na Kiarabu na Kiswahili pamoja na uigizaji.
 
Dr. Shein alisema kwamba michezo mbali mbali  iliyosuniwa na Kiongozi wa Dini ya Kiislamu Mtume Muhammad { SAW } ni miongoni  mwa mambo na masuala ya msingi yanayosaidia kurithisha watoto Utamaduni ya Kiislamu.
 
Aliwaomba wasimamizi wa Tamasha hilo la Kiislamu kuzidi kuliimarisha kwa kubuni shughuli mbali mbali zinazohusiana na utamaduni wa Kiislamu ili kuongeza maarifa na taaluma inayopatikana kupitia Tamasha hilo.
 
Alieleza kwamba ipo haja ya kulitanga zaidi Tamasha hilo kwa kutumia fursa mbali mbali zilizopo kwa lengo la kuliongezea umaarufu pamoja na kuongeza idadi ya wageni wanaofika Nchini wakiwemo Wazanzibari wanaoishi mataifa mbali mbali Duniani.
 
Mapema Mwenyekiti wa Tamasha la Kiislamu Zanzibar { Zenj Empire Islamic Festival} Ustaadh Jabir Haidar Jabir alisema tamasha hilo lililoanzishwa Tarehe 13/12/2009 limelenga kuimarisha utamaduni wa Kiislamu nchini.
 
Ustadh Jabir alisema wiki ya Tamasha hilo  hutoa fursa kwa waumini wa Dini ya Kiislamu hasa wanafunzi  wa vyuo na madrasa kujumuika pamoja kwenye usomaji Qasida, harakati za Kiislamu kama michezo na mafunzlo ya dini jambo ambalo hutoa mwanga na mafundisho kwa washiriki hao kuelewa mila na tamaduni zao.
 
Alisema Juhudi zinazochukuiliwa na Uongozi wa Tamasha hilo ni kusaidia kuratibu mafungamano yanayojumuisha watu wa dini na madhehebu tofauti kuishi pamoja na upendo na kushirikiana.
 
Tamasha la Kiislamu Zanzibar lililoasisiwa na kuanzishwa karibu miaka sita iliyopita limekuwa na utaratibu wa kushirikisha 
pia
 michezo mbali mbali  iliyosuniwa na Mtume Muhammad { SAW } kama vile michezo ya riadha, kuogelea, Qasida, Maulidi ya Homu na usomaji wa Quran.
 
Wiki ya Tamasha la Kiislamu Zanzibar { Zenj Empire Islamic Festival } iliyoanza Tarehe 17 Disemba inamalizia Tarehe 21 Disemba ambapo watu wa rika mbali mbali wakiwemo Mabalozi na Maafisa wao wa Nchi za Nje waliopo Nchini Tanzania na watalii  wamepata fursa ya kushiriki tamasha hilo.

Viettel Global Investment JSC kutoka Taiwan yataka kutoa huduma vijijini


 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Ofisa wa Kampuni ya Mitandao ta Teknolojia ya Mawasiliano ya Vietnam Tawi la Dar es salaam Bibi Le Duy Duong Ofisini kwake Vuga.Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi naTeknolojia ya SMT Profesa Makame Mnyaa Mbarawa na Mkurugenzi Mkuu wa Viettel Tanzania Bwana Nguyen Thanh Quang.

 Balozi Seif akizunguimza na Ujumbe wa  Kampuni ya Mitandao ta Teknolojia ya Mawasiliano ya Vietnam Tawi la Dar es salaam ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkuu wa Viettel Tanzania Bwana Nguyen Thanh Quang mara baada ya mazunguimzo yao.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Uongozi wa Bodi Mpya ya Mpango wa kurasimisha rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania { MKURABITA } ofisini kwake Vuga.

Kushoto ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mh. John Chiligati ambae 
pia
ni Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki Mkoani Singida.

Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

Uongozi wa Kampuni ya Uwekezaji wa  Mtandao wa Mawasiliano ya Teknolojia ya kisasa  ya Vietnam { Viettel Global Investment JSC. } umeonyesha nia ya kutaka kutoa huduma za mawasiliano kwa njia ya mtandao wa Kisasa katika maeneo ya Vijiji hapa Zanzibar.

Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo Tawi la Tanzania Bwana Nguyen Thanh Quang akiuongoza ujumbe wa Viongozi watatu wa Kampuni hiyo alieleza hayo wakati akibadilishana mawazo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Bwana Nguyen alisema kwamba Kampuni hiyo kwa kiasi kikubwa inaelewa umuhimu wa kizazi kipya  kupatiwa elimu bora inayokwenda na wakati wa sasa wa Teknolojia ya mawasiliano ili kiwe na uwezo kamili wa kukabiliana na maisha yao ya baadaye.

Alisema hatua ya kutiliana saini mkataba na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya ujenzi wa Vituo vya huduma za mawasiliano ya mtandao katika maeneo ya vijiji visivyo na huduma hizo ni  miongoni mwa malengo ya Kampuni hiyo.

Mkurugenzi huyo wa Kampuni ya Viettel Tanzania Limited alimueleza Balozi Seif kwamba Taasisi hiyo iko tayari kutoa huduma kama hizo kwa upande wa Zanzibar endapo watapata fursa ya kufanya hivyo katika mamlaka inayohusika.


Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Moh’d Aboud Moh’d aliutaka Uongozi wa Kampuni hiyo kufanya utafiti wa kitaalamu katika kuangalia namna gani huduma zao za mawasiliano wanaweza kuzisambaza vijijini.

Waziri Aboud alisema katika kufanikisha azma hiyo aliutaka Uongozi wa Kampuni hiyo kufanya mawasiliano  na wataalamu wa masuala ya teknolojia na mawasiliano hapa Zanzibar ili kuwa na  mwanzo mzuri kwa Kampuni hiyo kuweza kutekeleza azma yake njema kwa mustakabala wa Jamii.

Mapema Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Profesa Makame Mnyaa Mbarawa  alisema uwepo wa Kampuni hiyo Nchini Tanzania umekuja kufuatia ziara ya Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda Nchini Vietnam ambapo alitoa fursa kwa makampuni mbali mbali ya uwekezaji vitega uchumi kutumia fursa za Tanzania kuwekeza Nchini Tanzania.

Profesa Mbarawa alisema Kampuni hiyo tayari imeanza kuwekeza katika mradi wa mawasiliano Vijijini ambapo miongoni mwa makubaliano yake na Serikali imepanga kujenga vituo 4,000 vya mawasiliano kwenye maeneo ya vijiji vyenye ufinyu wa mawasiliano Nchini Tanzania.

 Alisema mradi huo utakwenda sambamba na ujenzi wa mkongo wa mawasiliano ambapo Kampuni hiyo pia itatoa huduma za mitandao ya mawasiliano katika Hospitali za Wilaya, Ofisi za Halmashauri pamoja na ofisi za Polisi na Shule za Wilaya.

Akitoa shukrani zake kwa  Uongozi wa Kampuni hiyo ya Viettel Tanzania Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  alisema bado mpaka sasa yapo baadhi ya maeneo vijijini yanakosa huduma za mawasiliano ya mitandao pamoja na simu.

Balozi Seif aliueleza Uongozi wa Kampuni hiyo ya Viettel Tanzania kwamba  zipo taasisi za mitandao kwa kushirikiana na wataalamu waliojaribu kufanya utafiti wa kuenea kwa huduma hizo za mawasiliano  na kugundua hitilafu hiyo.

Kampuni ya  Viettel Global Investment JSC  tayari imeshawekeza katika Mataifa ya Cambodia, Laos, Hait,. Msumbiji,Timor ya Mashariki,Peru, Cameroun Burundi na Tanzania katika masuala ya Teknolojia, Mawasilino pamoja na Teknolojia ya Habari.

Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alikutana na Uongozi wa Bodi Mpya ya Mpango wa kurasimisha rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania { MKURABITA } iliyofika Zanzibar kujitambulisha rasmi baada ya kuteuliwa kushika dhamana hiyo.

Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mheshimiwa John Chiligati ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki Mkoani Singida alisema utafiti uliofanywa na Bodi hiyo kujua rasilmali ya Taifa umegundua kwamba  asilimia 90% ya shughuli za Watanzania pamoja na asilimia 86% ya mali zao zimejificha zikifanywa nje ya utaratibu wa kisheria.

Mh. Chiligati alisema wataalamu wanapofanya majumuisho ya pato la Taifa inawawia vigumu kutokana na vyombo vya fedha kukosa uhusiano na sehemu hizo mbili.

Mwenyekiti huyo wa bodi ya Mkurabita alifahamisha kwamba mfumo wa urasilimishaji umelenga kutambuliwa kwa rasilimali za Taifa katika vyombo vinavyohusika  pamoja na kuunganishwa na mtaji.

Ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Ofisi ya msajili wa ardhi kwa kuanza kupima ardhi ambayo ndio rasilmali kuu ya Taifa jambo ambalo alieleza kwamba limepokewa vyema na wananchi walio wengi.

Naye Mtendaji Mkuu wa Mkurabita Bibi Serapia Mgeni alisema kwamba Maafisa wa Biashara wana wajibu wa kuelimisha na kuelekeza wafanyabiashara ndogo ndogo badala ya kuendelea na mpango wa kukamata wale wasio na vibali vya biashara.

Bibi Serapia alifahamisha kwamba Mpango wa kurasimisha rasilimali na biashara za wanyonge Tanzania { MKURABITA } umelenga kuzijengea uwezo Taasisi zilizojikubalisha kusaidia jamii katika masuala ya kuimarisha uchumi wa Taifa.

Akitoa nasaha zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliipongeza Bodi hiyo ya Mkurabita kwa kusimamia utekelezaji wa uimarishaji wa uchumi katika maeneo mbali mbali hapa nchini.

Balozi Seif alisema Uongozi wa Mkurabita una wajibu wa kuelimisha wananchi waelewe malengo ya chombo hicho yaliyojikita zaidi katika kusimamia uchumi wa taifa hasa kupitia wafanyabiashara wadogo wadogo.

Hata hivyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alikemea tabia ya baadhi ya watendaji wa taasisi na mashirika ya umma kuendeleza urasimu ambao umekuwa ukipigiwa kelele za kudhoofisha maendeleo ya Taifa.

Balozi Seif aliuahidi uongozi huo wa Bodi ya Mkurabita kwamba Serikali Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaangalia upya suala la usajili wa biashara ndogo ndogo wa Zanzibar ulingane na ule wa Tanzania Bara ili kutoa nafuu kwa wahusika.

Friday, 19 December 2014

Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohammed Aboud akizindua Utekelezaji wa Miradi ya kutoa Ajira ya muda unasimamiwa na TASAF awamu ya III wa mpango wa Kunusuru Kaya Masikni katika Kijiji cha Kijini Matemwe Wilaya ya Kaskazini A Unguja.



 Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Moh'd Aboud Moh'd akipanda mti wa Mkwaju ikiwa ni ishara na kumbukumbu ya uzinduzi wa  Miradi ya Ajira kwa muda kwa kaya masikini inayosimamia na TASAF awamu ya III katika kijijini cha Kijini Matemwe. Picha na  Maryam Abdi (OMPR).
  Mratibu  wa TASAF  Unguja Bbi Fatma Moh'd Juma akimpa maelezo mafupi Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais kuhusu Uzinduzi wa Utekelezaji wa miradi ya ajira kwa muda kwa walengwa wa mpango wa Kunusuru Kaya Masikini  katika kijiji cha Kijini Matemwe. Picha na Maryam Abdi (OMPR.)

 Baadhi ya Wananchi waliohudhuria katika mkutano wa Uzinduzi wa Miradi wa ajira kwa muda. Picha na Maryam Abdi (OMPR.)
  Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Nd. Issa Ibrahim Mahmoud akizungumza na wananchi kuhusu TASAF awamu ya III una lengo la kuongeza kipato katika kaya masikini. Picha na Maryam Abdi (OMPR)
Mhe. Waziri wa Nchi na baadhi ya  Viongozi wa Serikali waliohudhuria katika Uzinduzi wa Miradi ya Ajira muda wakiomba dua, katika Kijiji cha Kijini Matemwe. Picha na Maryam Abdi (OMPR)

 Mkurugenzi Mtendaji Ndg. ladislaus Mwamanga akitoa maelezo mafupi kuhusu Tasaf awamu ya III na ajira za muda kwa walengwa waliokuwepo katika mpango. Picha na Maryam Abdi Hassan OMPR.
































Thursday, 18 December 2014

Kamati ya Sensa Taifa yakutana


Kikao cha 14 cha Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 kilikutana chini ya Mwenyekiti wake Waziri Mkuu wa SMT Mh. Mizengo Pinda akiwa sambamba na Mwenyekiti Mwenza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Kikao hicho kilichoshirikisha wajumbe wa pande zote mbili za Muungano wakiwemo mawaziri na watendaji waandamizi wa taasisi za serikali kimefanyika katika Ukumbi wa Waziri Mkuu uliopo Ikulu Jijini Dar es salaam.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
 
Na Othman Khamis, OMPR
Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 imekutana katika Kikao chake cha Kawaida cha 14 chini ya mwenyekiti wake Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda.
Kikao hicho kilichoshirikisha 
pia
 Mwenyekiti Mwenza wa Kamati hiyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Wajumbe wa Pande zote mbili za Muungano ambao ni baadhi ya Mawaziri na watendaji wa Taasisi za Umma kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dar es salaam.
Akiwasilisha utekelezaji wa agizo la Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2012 la kikao cha 13 Kamishna wa Sensa Tanzania Hajat Amina Mrisho alisema kazi za usambazaji  wa chapisho la tatu la Taarifa za msingi la Kidemografia, Kijamii na Kiuchumi unaendelea kusambazwa kwa watumiaji.
Hajat Amina alisema kwamba utaratiubu wa kusambaza taarifa hizo katika ngazi ya Mkoa imeanza katika Mkoa wa Pwani Tanzania Bara ambako warsha iliyohusisha Viongozi na watendaji katika ngazi ya Mkoa na Wilaya imeshafanyika mwezi Oktoba mwaka 2014.

Kamishna wa Sensa huyo Tanzania alifahamisha kwamba warsha kama hizo zinatarajiwa kuendelea katika Mikoa mengine hapa Nchini mara uwezeshaji utakapokamilika.
Kigusia suala la uhakiki wa mipaka ambayo inastahiki kufanyika kwa uangalifu mkubwa utakaoshirikisha wadau wote wa mikapa Hajat Amina alisema kazi hiyo imepangwa kufanyika nchi nzima kulingana na uwezo wa Kifedha.
Alisema hadi sasa shughuli hiyo hadi sasa imeweza kufanyika katika Wilaya za Gairo na Chemba,Bagamoyo na hivi sasa inaendelea Wilkaya ya Kiteto kwa Tanzania Bara na Wete Visiwani Zanzibar.
Akiwasilisha Taarifa za uhakiki wa mipaka katika Wilaya ya Kiteto Afisa Takwimu wa Taifa Bwana Enest Bugambi alisema ipo changamoto nyingi zinazowakwaza wananchi hasa lile suala la kuhama hama kwa wafugaji na wakulima na kuingia ktaika maeneo ha hifadhi ya misitu.
Bwana Enest alisema uimarishaji wa usalama wa umiliki wa ardhi kwa maeneo ya kilimo na mifugo ndilo jambo la msingi litakalopunguza au kuondoa kabisa migogoro ya mipaka pamoja na umiliki wa ardhi.
Mtaalamu huyo wa Takwimu alifahamisha kwamba timu ya wataalamu wake tayari imesha hakiki vijiji vipatavyo 36 wakibakisha vijiji kumi  ndani ya Wilaya ya Kiteto katika mpango mzima wa matumizi ya chapisha la Sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2012.
Wakichangia katika Kikao hicho cha 14 cha Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 baadhi ya Wajumbe wa Kamati hiyo walisema bado suala la migogoro ya wafugaji na wakulima litaendelea kuwepo kwa vile taratibu za umiliki wa ardhi haujawa makini.
Walishauri kutumiwa kwa wataalamu wa taasisi zinazosimamia maendeleo ya jamii ili kutoa taaluma kwa umma katika maeneo mbali mbali hasa zile sehemu za migogoro ili kupunguza matokeo ya ya balaa yakiwemo yale ya mauaji.
Walisema viongozi wa kidini na kisiasa ni vyema wakashirikishwa katika kusaidia migoogoro pale inapotokea katika maeneo wanayoishi.
Akitoa nasaha zake mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda aliipongeza Timu ya wataalamu wanaosimamia uhakiki wa mipaka kwa kazi kuibwa waliyoifanya katika kipindi kifupi.
Mh. Pinda alisema kitendo cha wataalamu hao kushirikisha watendaji wa taasisi husika katika zoezi hilo imeleta uelewa na kupunguza joto la migogoro ya mipaka ambalo lilikuwa likionekana kuelekea kubaya.
“Ni mwanzo mzuri uliofanywa na wataalamu wetu unatoa mwanga mzuri wa muelekeo wa kupunguza migogoro ya mipaka ya ardhi na kustawisha jamii “. Alisema Mh. Pinda.
Mwenyekiti huyo wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 aliiomba kamati hiyo ya uhakiki wa mipaka kuandaa taarifa yao katika mfumo wa kisasa wa teknolojia utakaowawezesha maafisa wa Sensa na ustawi wa jamii kuzitumia vizuri katika kutoa elimu kwa umma.