Thursday, 18 December 2014

Uwanja wa Gombani Ukiwa katika Ujenzi wa Njia ya Kukimbilia


Afisa Mdhamini wa Wizara ya Habari, Utamaduni,Utalii na Michezo Pemba Ndg Ali Nassor, akitowa maelezo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Wawakilishi ya Habari, Mifugona Utalii Mhe.Mbarouk Juma Mlinde akiwa na Kamati yake wakitembelea uwanja wa Gombani Pemba,uwanja wa gombani ukiwa katika matayarisho ya kuwekwa Tatan .
Wajumbe wa Kamati ya Baraza la Wawakilishi ya Mifugo,Habari na Utalii wakimsikiliza Afisa Mdhamini wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Ndg Ali Nossor hayuko pichani wakati walipofika kuangalia maendeleo ya Uwanja wa Gombani Pemba 
 Mhe Mohammed Raza akiuliza swali baada ya kupata maelezo ya Uwanja wa Michezo wa Gombani Pemba, wakati wa ziara yao kisiwani Pemba. 
Waheshimiwa Wawakilishi wakimsikiliza Mhandisi wa ujenzi huo wa uwekaji wa Tatan katika uwanja wa Gombani akitowa maelezo ya ujenzi huo kwa Kamati hiyo ilipofika kuangalia maendeleo ya uwanja huo.



Buldoza la Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Pemba , likichawanya Kifusi katika barabara ya kukimbilia kwa ajili ya kuweka TATAN.