Kamanda Mkuu wa Brigedia Nyuki Zanzibar Bwigedia Jenerali Cyrill Ivor Mhaiki akibadilishana mawazo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefika uwanja wa Ndege wa Zanzibar kuangalia matayarisho ya mwisho ya ujio wa Rais wa Msumbiji hapa Zanzibar. Picha na Hassan Issa OMPR – ZNZ.
Kushoto ya Balozi Seif ni Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar Balozi Silima Kombo, Mshauri wa Rais wa Zanzibar katika masuala ya Kiuchumi na Uhusiano wa Kimataifa Balozi Moh’d Ramia, Kamanda wa Brigedia Nyuki Zanzibar Brigedia Jenerali Cyrill Ivor Mhaiki na Mjumbe wa Kamati ya Sherehe na maadhimisho ya Kitaifa kutoka JWTZ Kanali Shaaban Lissu. Picha na Hassan Issa OMPR – ZNZ.
Balozi Seif akikiendesha Kikao cha Kamati ya Mapokezi ya Ujio wa Rais wa Msumbiji Bwana Philipe Nyusi hapo katika jengo la watu mashuhuri { VIP } Kongwe katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar. Picha na Hassan Issa OMPR – ZNZ.
Bwa Philipe Jacinto akiwa katika harakati za kampeni wakati wa uchaguzi Mkuu wa Msumbiji ambapo aliinuka kidedea na kuliongoza Taifa hilo katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Picha na Hassan Issa OMPR – ZNZ.
Wanachama wa Chama cha Frelimo wakati wa Kampeni za Uchaguzi Nchini Msumbiji na hatimae chama hicho kufanikiwa kuongoza Dola. Picha na Hassan Issa OMPR – ZNZ.
Press
Release:-
Matayarisho kwa ajili ya ujio wa Rais wa Jamuhuri ya
Msumbiji Bwana Philipe Jacinto Nyusi anayefanya ziara rasmi ya Kiserikali
Nchini Tanzania yamekamilika kwa upande
wa hapa Zanzibar.
Bw. Nyusi anaiongoza
Jamuhuri ya Msumbiji katika kipindi cha Miaka Mitano baada ya kuingia
Madarakani kwenye Uchaguzi Mkuu wa Nchi
hiyo wa Tarehe 15 Oktoba mwaka 2014 Kupitia chama Tawala cha Frelimo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi akiwa pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa alipata fursa ya kukagua
matayarisho hayo yaliyoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania { JWTZ }
pamoja na vikundi vya burdani.
Matayarisho ya mapokezi hayo yamefanyika katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amaan Karume ambapo Nyimbo za Taifa za
Msumbiji na wa Zanzibar ziliiimbwa zikiambatana na mizinga
21 ya majaribio kupigwa kuashiria kukamilika kwa maandalizi hayo.
Bwana Philipe Nyusi anayetarajiwa kupokelewa rasmi
na mwenyeji wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Braza la Mapinduzi Dr. Ali
Mohammed Shein mchana wa Jumatatu ya Tarehe 18 Mei mwaka huu atapata fursa ya
kupokea saluti na kukagua gwaride rasmi lililotayarishwa kwa heshima yake.
Katika mapokezi hayo Dr. Shein anatarajiwa pia kuambatana
na Viongozi mbali mbali wa Serikali, Kisiasa, wananchi pamoja na Raia wa
Msumbiji wanaoishi hapa Zanzibar .
Bwana Philipe Jacinto Nyusi aliyezaliwa Tarehe 9 Febuari mwaka 1959 katika Kijiji cha Namai kwenye Jimbo la Cabo
Delgado ndani ya Wilaya ya Mueda Nchini Msumbiji akitokea katika familia ya
wazazi waliopigania uhuru wa Taifa hilo kutoka kwa Wareno ana stashahada ya
Uhandisi ya chuo Kikuu cha Manchester Nchini
Uingereza .
Kiongozi
huyo wa Msumbiji Bwana Nyusi kabla ya kuwa Waziri wa Ulinzi wa Msumbiji kuanzia
Tarehe 27 Machi mwaka 2008 hadi 2014 aliwahi pia kuwa Mhadhiri katika Kampus
ya Nampula ya chuo Kikuu cha Pedagogica.
Kiongozi
huyo wa Jamuhuri ya Msumbiji Bwana Philipe
Jacinto Nyusi anakamata wadhifa huo akiwa Rais wa Nne Tokea Taifa hilo
kutoka mikononi mwa Ureno akitanguliwa na Kiongozi wa kwanza wa Ukombozi
Rais Samora Machel, Bw. Joaquim Chisano
pamoja na Bwana Armando Guebuza.
Bwana Nyusi
mwenye umri wa miaka 56 akiwa
ni Rais wa 4 kuchaguliwa Kidemokrasi Nchini Msumbiji wazazi wake walimvusha
kupitia Mto Ruvuma na kuingia Nchini Tanzania kupata elimu yake ya awali
katika Skuli ya Msingi ya Frelimo
Tunduru Nchini Tanzania.
Alifanikiwa kuendelea na masomo yake ya Sekondari kwa
kujiunga na Skuli ya Frelimo ya Mariri iliyopo Cabo Delgado na baadaye
Sekondari ya Samora Mashel Mjini Beira.
Mwaka 1973 Bwana Philipe Nyusi
aijiunga na Chama cha Frelimo akiwa na umri wa Miaka 14 na kujiingiza katika
masuala ya kisiasa na baadaye kupata mafunzo ya kijeshi katika Kambi ya mafunzo ya Nachingwea Nchini
Tanzania.
Akiwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya
Ukombozi wa Frelimo Bwana Philipe Nyusi alipata mafunzo ya Uongozi katika
Mataifa ya India, Afrika Kusini, Swaziland na Marekani.
Mwaka 1990 Bwana Philipe Nyusi
alikamilisha mafunzo yake ya Shahada ya
kwanza ya Uhandisi katika chuo kikuu cha
Ufundi cha Brno iliyokuwa Czechoslovakia. Pia alipara stashahada ya Uongozi
katika Chuo Kikuu cha Manchester Nchini
Uingereza.
Kwenye Utumishi wa Umma Bwana Nyusi
aliwahi kufanya kazi katika Mamlaka ya Bandari na Reli ambapo utendaji wake
ulimuwezesha kuchaguliwa kuwa Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka hiyo baadaye kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Mamlaka
hiyo.
Mnamo
Tarehe 1 Machi 2014 Kamati Kuu ya Taifa ya Chama cha Frelimo ilimchaguwa Bwana
Philipe Nyusi kuwa mgombea wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa Nchi hiyo
baada ya kupata asilimia 68% ya kura dhidi ya mgombea mwenzake wa chama hicho
Bibi Luisa Diogo aliyepata asilimia 31%.
Hiyo
ilikuwa raundi ya pili ya kumtafuta Kinara wa Frelimo atakayeipeperusha Bendera
ya Chama hicho kwenye uchaguzi Mkuu wa
Vyama vingi Nchini Msumbiji wa 2014 baada ya ile ya kwanza aliyopata asilimia 46% chini ya kiwango
kinachokubalika kwa mujibu wa Katiba ya Nchi hiyo cha asilimia 50%.
Bwana
Philipe Jacinto Nyusi alifanikiwa
kueperusha Bendera ya Chama cha Frelimo baada ya kushinda Uchaguzi Mkuu wa
Tarehe 15 Oktoba mwaka 2014 kwa kupata
Kura Milioni 2,778,497 sawa na asilimia 57.03%.
Aliwashinda
Wapinzani wake Bwana Afonso Dhlakama wa Chama che Renamo aliyepata kura Milioni
1,783,382 sawa na asilimia 36.61%
akishika msindi wa Pili na Bwana Dayiz
Simango wa Chama cha MDM aliyepata Kura Laki 309,925 sawa na asilimia 6.36%.
Kiongozi
huyo wa Jamuhuri ya Msumbiji Bwana Philipe
Jacinto Nyusi anakamata wadhifa huo akiwa Rais wa Nne Tokea Taifa hilo
kutoka mikononi mwa Ureno akitanguliwa na Kiongozi wa kwanza wa Ukombozi
Rais Samora Machel, Bw. Joaquim Chisano pamoja
na Bwana Armando Guebuza.