Baadhi ya Wajumbne wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia Hotub a ya Balozi Seif hayupo pichani wakati akiifunga semina ya uchamguzi wa Bajeti na masuala yua Uchumi. Picha na Issa Hassan - OMPR – ZNZ
Waziri wa Fedha ZanzibarMh. Omar Yussuf kulia na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Mh. Nassor Ahmed Mazrui wakiwa makini kufutailia Hotuba ya Balozi Seif kwenye Semina yao. Picha na Issa Hassan - OMPR – ZNZ
Baadhi ya Watendaji Wakuu wa Serikali ambao wameshiriki Semina ya uchambuzi wa Bajeti na masuala ya Uchumi hapo Z. Ocean Hoteli Chuwini Wilaya ya Magharibi “ A “. Picha na Issa Hassan - OMPR – ZNZ
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mh. Pandu Ameir Kificho Kulia na Waziri wa Nchi Ikulu na Utawala Bora Dr. Mwinyihaji Makame wakikamilisha Semina hayo ya uchambuzi wa Bajeti na masuala ya Uchumi. Picha na Issa Hassan - OMPR – ZNZ.
Press Release:-
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema yapo matumaini makubwa ya kukua kwa Uchumi wa
Zanzibar kukua ambako kutategemea pia
Uchaguzi Mkuu wa Mwezi wa Oktoba mwaka huu kama utakwenda kwa amani na utulivu.
Alisema
Serikali kwa upande wake itahakikisha Tume ya Uchaguzi Zanzibar inaendesha
Uchaguzi wenye uwazi, huru na haki kwa wagombea wote watakaobahatika kushiriki
kwenye uchaguzi huo.
Balozi Seif
Ali Iddi akiwa kiongozi wa shughuli za Serikali alisema hayo wakati akiifunga
Semina ya siku Nne ya Wajumbe wa Bawaza la Wawakilishi pamoja na watendaji
Wakuu wa Serikali juu ya uchambuzi wa Bajeti na Masuala ya Uchumi iliyokuwa
ikifanyika katika ukumbi wa Z Ocean Hoteli Chuwini Wilaya ya Magharibi “A”.
Alisema
Uchaguzi ulio salama na haki utakuwa kichocheo kikubwa kitakachotoa
fursa ya kusaidia kukua kwa uchumi wa Taifa sambamba na kuhamasiha wawekezaji
wengi zaidi kumiminika nchini kwa lengo la kuwekeza miradi yao ya Kiuchumi.
Balozi Seif
aliwanasihi wanasiasa ni vyema wakajiepusha na kauli za kuchochea vurugu, huku
akiwataka wananchi kutokubali kuchochewa kuanzisha fujo wakati Waandishi wa
Habari wakawajibika ipasavyo kutekeleza majukumu yao kwa jamii katika misingi
ya uadilifu.
“Sifikiri
kabisa
kwamba kutakuwepo au kuja kwa
muwekezaji kutaka kuanzisha miradi ya kiuchumi wakati atashuhudia
pamoja na kuona utulivu wa amani unakosekana kutokana na fitna na
baadhi ya watu “. Alisema
Balozi Seif.
Akizungumzia
umuhimu wa kutunza Mazingira Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar alitahadharisha kwamba Jamii ikiendelea kuchafua
mazingira ielewe kwamba Mvua zitapungua na hatimae kuathiri Sekta ya kilimo kwa kiasi kikubwa.
Alifahamisha
kwamba utunzaji wa mazingira kwa kila Taasisi au Mtu ni jambo la lazima
kutokana na Wananchi walio wengi Zanzibar wanbategemea Kilimo katika kuendesha
maisha yao.
Balozi Seif
alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na
Taasisi tofauti wakiwemo washirika wa
Maendeleo itaendelea kudhibiti uchafuzi wa mazingira kwa kasi zaidi ikiwemo
kutunza vianzio vya Maji.
Kuhusu
Bajeti inayozingatia matokeo { PBB } ambao ni mfumo mpya utakaotumika katika
majadiliano ya Baraza la Wawakilishi kwenye Bajeti ya mwaka huu Balozi Seif alisema
mfumo huu utawasaidia Wananchi kuelewa kwa uwazi Bajeti ya Serikali yao na
imeleta matokeo gani kwao.
Alisema
Mfumo huu mpya ambao utawapa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuendelea
kujifunza unasaidia kujenga uwazi katika suala zima la matumizi ya Serikali
jambo ambalo ni muhimu katika jitihada za kukuza uchumi wa Wananchi.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar aliotoa wito kwa Wizara ya Fedha kuendeleza jitihada
zake za kuelimisha watendaji wa Taasisi
za Serikali ili Mpango wa Bajeti
inayozingatia matokeo { PBB } ufahamike vizuri zaidi.
“Mpango wa
Bajeti inayozingatia matokeo { PBB } itatusaidia kuelewa walengwa wa program ni
nani, program itatoa huduma gani “. Alifafanua Mtendaji Mkuu huyo wa Shughuli
za Serikali.
Mapema
Mshauri wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Bwana Mussa alisema mfumo mpya wa
Bajeti { Bajet Office } tayari umeshaanzishwa na Mabunge mengi Ulimwenguni
yakiwemo pia baadhi ya Mabunge ya
Afrika.
Bwana Mussa
alisema Baraza la Wawakilishi Zanzibar limeanza na maandalizi ya kutumia mfumo huu mpya tokea mwaka 2012 kwa hatua za
awali ambao utekelezaji wake unaweka wazi matumizi ya Serikali.
Akiwasilisha
majumuisho ya wanasemina Ndugu Hamad alisema Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi
pamoja na watendaji wakuu wa Serikali walipendekeza uwepo wa ubunifu katika
uimarishaji wa vianzio vya mapato ya ndani.
Nd. Hamadi
alisema mageuzi Katika uwajibikaji lazima uanzie kwa viongozi na baadaye kuteremka kwa wananchi sambamba na changamoto
mbali mbali zinazokwaza utekelezaji wa Mpango wa Kupunguza Umaskini Zanzibar {
MKUZA } ziondolewe.
Aidha
alieleza kuwa washiriki wa Semina hiyo wakapendekeza pia kuwepo kwa Bajeti
inayozingatia jinsia ijielekeze katika kutatua changamoto za Wanawake, Watoto
pamoja na Makundi Mengine.
Semina
hiyo
ya siku Nne ya kujifunza Mpango wa Bajeti inayozingatia matokeo {
PBB } pamoja na mambo mengine imejadili mada mbali mbali zikiwemo hali
ya
Uchumi, Idadi ya watu na Maendeleo, Uwazi na Uwajibikaji pamoja na
Wajibu wa
Baraza la Wawakilishi wa kusimamia Bajeti.