Kikundi cha Muziki wa Morden Taarab cha Big Staa chenye mastakimu yake
Ofisi ya Mkoa Mjini Amani kikitoa burdani kwenye tafrija ya kuwapongeza
Viongozi na watendaji wa Taasisi zilizochini ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar baada ya kupita kwa Bajeti ya Wizara hiyo pamoja na kuagana kwa
kukaribia kukamilika kwa kipindi cha miaka mitano. Picha Hassan Issa –
OMPR – ZNZ.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyepo mwanzo kushoto akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Baraza la Wawakilishi inayosimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Serikali Kushoto yake Mh. Hamza Hassan Juma na Mjumbe wa Kamati hiyo Mh. Makame Mshimba Mabrouk kwenye tafrija ya kuwapongeza watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Balozi Seif wa pili kutoka kushoto akijumuika pamoja na Viongozi na watendaji wa Ofisi yake kwenye tafrija aliyowaandalia baada ya kupita kwa Bajeti ya Wizara hiyo katika Kikao cha Baraza la Wawakilishi kinachoendelea. Kushoto ya Balozi Seif ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed Aboud Mohammed, Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Baraza la Wawakilishi inayosimamia Ofisi za Viongozi Mh. Ali Mzee Ali, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh. Hamza Hassan Juma, Mh. Makame Mshimba Mbarouk pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh. Saleh Nassor Juma. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Baadhi ya Watendaji wa Taasisi zilizochini ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakijipatia mlo kwenye tafrija hiyo iliyofanyika katika Makazi ya Balozi Seif yaliyopo Mazizini nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed Aboud Mohammed akizungumza kabla ya kumkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kuzungumza na Viongozi na watendaji wa Ofisi yake. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Balozi Seif akitoa nasaha zake mara baada ya kuwaandalia chakula cha usiku Viongozi na Watenmdaji wa Taasisi zilizochini ya Ofisi yake kufuatia kupitishwa kwa Bajeti ya Wizara hiyo pamoja na kuagana baada ya kufanyakazi pamoja katika kipindi cya miaka mitano iliyopita. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Balozi Seif kati kati akiwa pamoja na wake zake Mama Pili Seif Iddi na Mama Asha Suleiman Iddi wakijumuika pamoja katika kusakata rumba kwenye tafrija ya kuwapongeza watendaji wa Ofisi yake hapo Nyumbani kwake Mazizini nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.

Press Release:-
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Watendaji wa Taasisi za
Serikali wana wajibu wa kutumia vipaji walivyojaaliwa kuwa navyo katika kubuni mbinu
na mikakati watakayohisi kwamba inaweza kutaleta faida na ufanisi katika maeneo
yao ya kazi sambamba na Serikali Kuu kwa
jumla.
Alisema
faida ya ubunifu watakaoutumia watendaji hao utaongeza kasi ya uwajibikaji
endapo wataendelea kushikamana baina yao katika kufanya kazi kwa juhudi,
maarifa na nidhamu kwa kutumia vipaji hivyo.
Balozi Seif
Ali Iddi alisema hayo wakati wa hafla maalum ya chakula cha usiku
alichowaandalia watendaji wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi yake kufuatia
kukamilisha na hatimae kupita kwa Bajeti
ya Wizara hiyo pamoja na kuagana baada ya kufanya kazi pamoja katika kipindi
chote cha miaka mitano tokea mwaka 2010.
Hafla hiyo
ya chakula cha usiku iliyofanyika katika Makaazi ya Balozi Seif Mazizini Nje
kidogo ya Mji wa Zanzibar ilijumuisha pia baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu
ya Baraza la Wawakilishi inayosimamia Ofisi za Viongozi wakuu wa Serikali,
wafanyakazi wa Baraza hilo wakiwemo wawakilishi wa taasisi tofauti za ndani na
nje ya nchi wanaofanya kazi pamoja na watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar.
Balozi Seif
aliwapongeza watendaji wa taasisi zote zilizo chini ya Ofisi yake kwa kufanya
kazi nzuri katika utekelezaji wa majukumu yao likiwemo pia suala la kutengeneza Bajeti na hatimae kupita bila
ya vikwazo katika Kikao cha Bajeti cha Baraza la Wawakilishi kinachoendelea.
Alisema
hatua hiyo imempa moyo na faraja kubwa iliyosababisha ndani ya kipindi cha
miaka mitano cha uwepo wake katika Wizara hiyo kutokwaruzana au kumgomba Mfanyakazi
ye yote kwa vile kila mmoja likuwa akijuwa wajibu wake.
“ Miaka
mitano ya uwepo wangu ndani ya Ofisi hii sijawahi kumgomba Mfanyakazi hata
mmoja ukiachia zile kasoro ndogo ndogo za kibinaadamu zisizoepukika. Hii
inatokana na kila mtendaji kuelewa wajibu wake ipasavyo “. Alisema Balozi Seif.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar ambae ndie Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar aliwaasa Viongozi wa Taasisi hizo pamoja na nyengine za umma kuwa na tahadhari wakati
wanaposimamia haki za watendaji wao na kuepuka fitna na majungu ambazo hatimae
huzaa chuki kati yao na watendaji hao.
Balozi
Seif
alisema wapo baadhi ya viongozi wanaokumbwa na kashfa na matatizo
kutokana na
vitendo wanavyowafanyia watendaji wa ngazi ya chini ambapo hutoa
mwanya kwa wafanyakazi wanaowaongoza kufurahia wakati wanapohamishwa
au kustaafu
kazi.
“ Tumekuwa
tukishuhudia mara kwa mara mikasa inayowakumba baadhi ya Viongozi wa Taasisi
ambapo watendaji wao hufikia maamuzi ya kupika pilau au biriani wanapopata
taarifa kwamba Bosi wao kastaafu au kuhamishwa na kupelekwa katika sehemu nyengine
ya kazi “.Alitahadharisha Balozi Seif.
Aliuwakumbusha
Viongozi hao kwa kushirikiana na watendaji wao kuendelea kupendana ili
inapotokea kukutana tena baada ya kumaliza utumishi wao wakumbatiane kwa
kuonyeshana upendo wao wa dhati.
Mapema
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Dr. Khalid Salum
Mohammed kwa niaba ya Watendaji wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo
amemshukuru na kumpongeza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi kwa kuwaongoza vyema watendaji hao katika utekelezaji wa majukumu yao.
Dr. Khalid
alisema Uongozi huo wa busara wa Balozi
Seif Ali Iddi umesaidia kuleta ufanisi na kuiwezesha Ofisi hiyo inayoratibu
shughuli nzima za Serikali kufikia
malengo iliyojipangia ya zaidi ya asilimia 90% katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Alifahamisha
kwamba Watendaji wa Taasisi zote zinazofanyakazi chini ya Ofisi hiyo wamefarajika na utendaji wa Kiongozi
huyo pamoja na wale waliochini yake ulioonyesha upendo na mshikamano miongoni
mwa wafanyakazi wote.
Dr. Khalid
alisema mshikamano huo wa pamoja kati ya viongozi na watendaji hao ndiyo chachu
ya mafanikio yaliopelekea kuibua wafanyakazi bora wapatao 11 ndani ya Taasisi
zilizo chini ya Ofisi hiyo jambo ambalo linastahiki kupongezwa na kuigwa na
Taasisi nyengine za Umma hapa Nchini.
Naye
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar inayosimamia
Ofisi za Viongozi Wakuu wa Serikali Mh. Hamza Hassan Juma alisema
Utamaduni wa kupongezana ulioanzishwa na
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar baada ya kazi ngumu wanazozifanya unafaa
kuigwa na Taasisi nyengine hasa wakati watendaji wanapopata mafanikio makubwa.
Mh. Hamza
alisema uratibu makini uliokuwa
ukisimmamiwa na watendaji wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar umesaidia kuleta mafanikio makubwa katika utendaji mzima wa
Serikali.
Mwenyekiti
huyo wa Kamati ya Kudumu ya Baraza la Wawakilishi inayosimamia Ofisi za
Viongozi Wakuu wa Serikali ameipongeza Idara ya Maafa Zanzibar chini ya Mkurugenzi
wake kwa juhudi zake za kutoa elimu kwa Umma iliyosaidia kupunguza majanga ya
maafa wakati wa mvua za masika
zilizopita hivi karibuni.
Akimkaribisha
Balozi Balozi Seif kuzungumza na hadhara
hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed
Aboud Mohammed amewashukuru na kuwapongeza Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Baraza la Wawakilishi
inayosimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Serikali kwa kusimamia vyema na
uadilifu utendaji Mzima wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Waziri Aboud
alisema usimamizi wa Kamti hiyo umeiwezesha Ofisi hiyo kuratibu vyema Ilani ya
Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 kwa zaidi ya asilimia 95% chini ya rasilmali
iliyopo ya Taifa ya amani na utulivu inaoendelea kupatikana kutokana na umoja
na mshikamano miongoni mwa Wananchi wote.