Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wa Tatu
kutoka kushoto akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Abiria { Terminal 11 }
katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar wa Abeid Amani Karume akiwa
pamoja na uongozi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar. Picha na Hassan Issa
OMPR – ZNZ.
Msimamizi wa ujenzi wa jengo la Abiria katika uwanja wa ndege wa
Zanzibar upande wa Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar kupitia Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Nd. Yassir De
Costa akimpatiamaelezo Balozi Seif hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa mradi huo. Picha na Hassan Issa
OMPR – ZNZ.
Mshauri wa mradi wa ujenzi wa jengo la abiria { Terminal 11 } kutoka
Kampuni ya ADPI ya Nchini Ufaransa
Mhandisi Guillaume Verna akifafanua hatua zilizochukuliwa katika
utaalamu utaotumika katika ujenzi wa mikonga kwenye jengo hilo jipya la abiria.
Picha na Hassan Issa OMPR – ZNZ.
Eneo litakalotumika kwa huduma mbali mbali ikiwemo maduka na katika jengo
jipya la abiria linaloendelea kujengwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Zanzibar. Picha na Hassan Issa
OMPR – ZNZ.
Eneo la Nje ya jengo la Abiria litakalotumiwa na abiria wanaosafiri na kuingia Nchini kwa kutumia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume uliopo Kiembe Samaki Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Picha na Hassan Issa OMPR – ZNZ.
Picha na Hassan Issa OMPR – ZNZ.
Eneo la Nje ya jengo la Abiria litakalotumiwa na abiria wanaosafiri na kuingia Nchini kwa kutumia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume uliopo Kiembe Samaki Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Picha na Hassan Issa OMPR – ZNZ.
Press Release:-
Harakati za
ujenzi wa Jengo jipya la Abiria wa usafiri wa Anga katika uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Abeid Amani Karume ulipo Kiembe Samaki Nje kidogo ya Mji wa
Zanzibar zimekuwa zikiendelea kama
kawaida kufuatia marekebisho ya ujenzi wa jengo hilo utaozingatia kiwango cha Kimataifa.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipata fursa ya kukagua harakati
za ujenzi huo unaofanywa na wahandisi wa
Kampuni ya Kimataifa ya Beijing Construction Engineering Group { GCEG } ya Nchini Jamuhuri ya Watu wa
China Chini ya Usimamizi uelekezi wa Kampuni ya ADPI ya Nchini Ufaransa.
Msimamizi wa
ujenzi wa Mradi huo kwa upande wa Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar
Nd. Yassir De Costa alimueleza Balozi Seif kwamba ujenzi huo hivi sasa uko
katika hatua za uwezekaji paa na baadaye kuwekwa vioo.
Nd. Costa
alisema Jengo hilo kubwa litakuwa na
lango kuu kwa ajili ya abiria wote wa ndege za kimataifa na Kitaifa ambapo
baadaye watajigawa kwa mujibu wa safari za abiria hao katika huduma za ndani.
Alieleza
kwamba mizigo ya abiria itafanyiwa ukaguzi mbara mbili kabla ya kuingizwa ndani
ya ndege utaratibu ambao utathibitisha usalama wa abiria, mizigo na eneo lote
la uwanja wa ndege.
Msimamizi
huyo wa mradi wa ujenzi wa Jengo la abiria wa Serikali alifahamisha kwamba
abiria wapatao 500 watakuwa wakihudumiwa ndani ya saa moja katika eneo la jengo
hilo la abiria.
Naye mshauri
wa mradi wa ujenzi wa jengo la abiria { Terminal 11 } kutoka Kampuni ya ADPI ya
Nchini Ufaransa Mhandisi Guillaume Verna
alisema kwamba ujenzi wa Mikonga itakayohudumia ndege kubwa katika jengo hilo
imezingatiwa katika kiwango kikubwa.
Mhandisi
Guillaume alisema utafiti wa kina umefanywa katika kuona mikonga itakayopjengwa
haiathiri jengo hilo kwa mujibu wa vipimo vinavyokubalika Kimataifa.
Mapema
Katibu Mkuu Wizara ya Maiundombinu na Mawasiliano Zanzibar Dr. Juma Malik Akio
alisema Serikali ya Jamuhuri ya China ambayo ndio mfadhili wa Ujenzi huo
Kupitia Benki ya Exim imeridhia kuendelea kutekelezwa kwa mradi huo.
Dr. Malik
alisema Wizara ya Miundombinu na Mawasliano kwa kushirikiana na wadau wa Mradi
huo wanaandaa utaratibu wa kumaliza ujenzi huo kwa mujibu wa ushauri wa
Kitaalamu.
Alisema mategemeo ya mradi wa ujenzi huo yalipangwa
kukamilika mwezi Oktoba mwaka huu lakini kutokana na kusita kwa muda ujenzi huo
unatazamiwa kukamilika si zaidi ya mwishoni mwa mwaka huu.
Alieleza
kwamba mategemeo ya mradi wa ujenzi wa
jengo hilo yalipangwa kukamikia mwezi oktoba mwaka huu lakini kutokana na
kusita kwa muda ujenzi huo unatazamiwa kukamilika si zaidi ya mwishoni mwa
mwaka huu.
Akitoa
shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alielezea faraja
yake kutokana na kuendelea kwa ujenzi wa
jengo hilo ambao uko katika hatua
inayoridhisha.
Balozi Seif
aliwapongeza wahandisi wa ujenzi huo pamoja na usimamizi mahiri wa mshauri
muelekezi wa mradi huo hatua ambayo kumalizika kwake kutatoa faraja kwa abiria
wanaotumia uwanja wa ndege wa Zanzibar.
Balozi Seif
alifahamisha kwamba matarajio ya abiria wanaotumia uwanja huo wataondokana
na usumbufu wa kushuka au kufuata ndege
masafa marefu kwa miguu hasa wakati wa mvua.