Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi

Mwanafunzi Isra Hilal Mwadini akifuatiwa na mwenzake Tamima Abass Sheha wakipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wakati wa hafla ya Maulidi ya Jumuiya ya Chuo cha Samael Academy.Kulia ya Balozi Seif ni Rais wa Sameil Academy Sheikh Nassir Bin Said.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizindua rasmi Bara bara ya pili ya Amani hadi Mtoni baada ya kukamilika awamu ya mwisho ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Akiwa na Balozi mdogo wa India nchini Tanzania wakiangalia maonyesho yaliofanya na Msanii kutoka India, Bi Navi Madhav hapo Ngome Kongwe

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Dk. Khalid S. Mohamed

akizungumza na Wadau wa Maendeleo wa Mfuko wa TASAF, walipofika Ofisini kwake kuzungumzia maendeleo ya Mfuko wa TASAF III,na kutembelea Mradi wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini (PSSN) katika Jimbo la Muyuni Wilaya ya Kusini Unguja katika Kijiji cha Muyuni B

Wazir wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakifurahia jambo wakati wa semina ya siku moja kuhusu matokeo makubwa na ya haraka katika kuleta mageuzi ya kiuchumi na kuleta maendeleo nchini iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein

Thursday, 31 July 2014

Sala ya Eid ul Fitr viwanja vya Maisara


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa nne kulia) akijumuika na Waislamu mbali mbali na Viongozi katika Swala ya Eid el Fitri iliyoswaliwa kitaifa katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Zanzibar  leo asubuhi katika kusherehekeka mfunguo wa Mwezi Mtukufu wa  Ramadhan.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]
 Baadhi ya Mashekhe na Viongozi wakijumuika na Waislamu mbali mbali na Viongozi katika Swala ya Eid el Fitri iliyoswaliwa kitaifa katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Zanzibar  leo asubuhi katika kusherehekeka mfunguo wa Mwezi Mtukufu wa  Ramadhan.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.] 
  Baadhi ya waislamu waliomaliza Swala ya Eid el Fitri wakimasikiliza Sheikh Mziwanda  Ng'wali  Ahmed  (hayupo pichani ) alipokuwa akitoa Khutba baada ya swala hiyo ambapo aliwataka waislamu kusherehekea Sikukuu ya Eid kwa upendo na mashirikiano katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Zanzibar  leo asubuhi [Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]
 Sheikh Mziwanda  Ng'wali  Ahmed (aliyesimama) akitoa Khutba baada ya Swala ya  Eid el Fitri mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein na Viongozi mbali mbali wa Kitaifa na Wailslamu waliojumuika kwa pamoja katika viwanja  vya Maisara Suleiman Mjini Zanzibar leo asubuhi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Watoto walioshiriki katika Swala ya Eid el Fitri na kuwatakia Kheri katika kusherehekea Sikukuu hii ya  kumaliza mfungo wa Mwezi Mtukufu wa  Ramadhan.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]

Wednesday, 30 July 2014

Mwenge wa Uhuru wawasili Zanzibar


 Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Getrudi Mpaka akitoa salam za Mkoa huo kabla ya kuukabidhi Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Mjini Magharibi leo july 30.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadiki akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi Khamis, makabidhiano hayo yamefanyika uwanja wa ndege mkongwe Kiembesamaki leo. (Picha na Makame Mshenga- Maelezo Zanzibar).
 Vijana wa Chipukizi wakiimba nyimbo ya Mwenge.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Ikulu na Utawala Bora Dkt. Mwinyihaji Makame akishika mwenge wa Uhuru ulipowasili Zanzibar.
 
Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Hamza Ibrahim kutoka Mjini Magharibi na maaskari wakiukimbiza Mwenge.

 Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi Khamis akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Magharibi Hasan Mussa Takrima kwa ajili ya kuukimbiza katika Wilaya yake
Mkuu wa Wilaya ya Magharibi Hasan Mussa Takrima akikimbiza Mwenge wa Uhuru mara baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini tayari kuanza ziara yake

Baraza la eidul Fitr Salama Hall Bwawani




Baadhi ya Wananchi na Waislamu wasikiliza hotuba iliyotolewa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja,katika kusherehekea Sikukuu yaEid el Fitri, [Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]
Wananchi mbali mbali wakike na wakiume wakiwa katika Ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Zanzibar wakati sherehe za Baraza la EId el Fitri lililohutubiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein katika kusherehekea Sikukuu ya Eid el Fitri baada ya kumalizika kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, [Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake kwa Wananchi na Waislamu katika Baraza la Eid El Fitri lililofanyika leo katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja,[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]
 Baadhi ya Viongozi na wageni mbali waliohudhuria katika sherehe za Baraza la Eid el Fitri wakiangalia na kusikiliza Hotuba iliyotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja,[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]

  Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akiwaongoza wake mbali ,mbali wa Viongozi wa Kitaifa pamoja na wananchi  waliohudhuria katika sherehe za Baraza la Eid el Fitri wakielekea   kupata viburudishaji baada ya kumalizika kwa Hotuba   iliyotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein  katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Mjini Unguja leo. [Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Sheinakisalimiana na wake wa Viongozi (pichani) akipena mkono na Mama Fatma Karume,(kulia) akiwepo na Mama Mwanamwema Shein katika viwanja vya ukumbi wa Salama Hall Bwawani Mjini Zanzibar,(wa pili kushoto) Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]






Maalim Seif akitoa mkono wa Eid El Fitr kwa wadau mbali mbali baada ya kumalizika Baraza la Eid lililofanyika Ukumbi wa Salama, Hoteli ya Bwawani Zanzibar

Sunday, 27 July 2014

Balozi Seif awatembelea Wazee wasiojiweza waliopo katika nyumba za Serikali Welezo na Sebleni

 Baadhi ya Wazee wa nyumba za Serikali za Welezo wakifutilia maelezo ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seifhayupo pichani wakati  alipowatembelea kwenye makazi yao.
 Balozi Seif akigawa zawadi kwa mmoja wa wazee wa Welezo alipowatembelea na kuwafariji wakiwa ndani ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

 Baadhi ya Wazee wa nyumba za Sebleni wakifuatilia hotuba ya Balozi Seif hayupo pichani wakati akijiandaa kuwapatia zawadi kwa ajili ya siku kuu ya Iddi el Fitri.
Balozi Seif akibadilishana mawazo na baadhi ya wazee wa kike wanaotunzwa katika nyumba za Serikali zilizopo Sebleni Mjini Zanzibar.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akitoa zawadi kwa Wazee wa kiume wa Sebleni
Balozi Seif akiagana na wazee wa Sebleni mara baada ya kuwasalimia na kuwapatia zawadi kwa ajili ya kusherehekea vyema siku kuu ya Iddi el Fitri.

Mzee Omar Said wa Nyumba za Sebleni kwa niaba ya wazee wenzake wa Sebleni na Welezo akimshukuru Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar hayupo pichani kwa juhudi zake za kufuatilia changamoto zinazowakabili wazee hao.

Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ
 
Na Othman Khamis Ame, OMPR
 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuwa na wajibu na jukumu kubwa la  kuwatunza na kuwathamini wazee wasiojiweza hivi sasa kutokana na mchango wao mkubwa walioutoa kwa  nchi hii wakati wa kulitumikia Taifa lao.
Alisema mchango wa wazee hao umekuwa ukiendelea kutumiwa na wananchi walio wengi hapa nchini ikiwemo kigezo cha amani na utulivu  kinachotokana na juhudi za wazee hao wakati wa kupigania utu wa mwafrika.
 
Balozi Seif Ali Iddi alieleza hayo wakati wa ziara yake fupi ya kuwasalimia Wazee wanaotunzwa katika Nyumba za Serikali za Welezo na Sebleni na kuwapatia zawadi ya nguo kwa ajili ya kusherehekea vyema siku Kuu ya Iddi El Fitri inayotarajiwa kufanyika mapema wiki ijayo.
 
Alisema wazee wa Taifa hili wametumia muda wao mkubwa wa kujenga mazingira bora ili kizazi chao kiendelee kuishi kwa amani na furaha tofauti na enzi zao zilizokumbwa na mitihani ya kutawaliwa jambo ambalo liliwakosesha uhuru wa kidemokrasia wa kufanya wanalolihitaji katika maisha yao.


“ Sisi kama Viongozi wa Serikali bado tunathamini na kuheshimuj wazee wetu waliotumia muda wao mkubwa wa kulitumikia Taifa letu kazi ambayo kwa sasa tunafaidika nayo “. Alisema Balozi Seif.
 
Akigusia suala la mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliwaahidi Wazee hao wa Welezo na Sebleni kwamba ule utaratibu wake wa kufutari nao pamoja utaendelea kama kawaida penye majaliwa kwa miaka ijayo.
 
Balozi Seif aliwafahamisha wazee hao kwamba mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani wa mwaka huu ilishindikana kufutari nao pamoja kutokana na kutingwa na majukumu mengi  ya kitaifa.
 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapatia zawadi ya madira na mitandio yao wazee wa kike na wale wazee wa kiume wakafaidika na kivazi cha asili cha kiko na fulana zake ili wazitumkie siku ya furaha ya iddi el fitri.
 
Akitoa skurani kwa niaba ya wazee hao wa Welezo na Sebleni Mzee Omar Said alimpongeza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa juhudi zake za kuendelea kufuatilia changamoto zinazowakabili wazee hao.
 
Mzee Omar alisema juhudi hizo zimekuwa zikiwapa faraja wazee hao na kuendelea kujenga imani kwa Serikali ambayo inaelewa mchango wao katika ukombozi wa Visiwa hivi.
 
Mapema Katibu Mkuu Wizara ya Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii, Vijana Wanawake na Watoto Bibi Asha Abdulla alisema Nyumba za Wazee ziliopo Welezo zimekuwa zikihudumia wazee wapatao 42 ambao kati yao wanawake wapo 14 wakati wazee wa Kiume wanafikia 31.
 
Kwa upande wa Sebleni Katibu Mkuu Asha alisema Nyumba hizo zinahudumia wazee 46 ambao kati ya hao wazee wa kike wanafikia 29 na wale wa Kiume wapo idadi ya 17 wakiwa chini ya usimamizi wa Idara ya Ustawi wa Jamii iliyopewa jukumu la kuwahudumia wazee hao.
 
 

Rais Kikwete afutarisha wananchi wa mikoa Mitatu ya Unguja

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  akiwaongoza waumini wa dini ya Kiislamu pamoja na wananchi wa mikoa Mitatu ya Unguja katika futari ya pamoja iliyoandaliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete na kufanyika katika Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Zanzibar.
 Viongozi na wananchi wa Mikoa Mitatu ya Unguja wakijichukulia mlo katika futari ya pamoja iliyoandaliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete hapo Bwawani Mjini Zanzibar.
 Viongozi na wananchi wa Mikoa Mitatu ya Unguja wakijichukulia mlo katika futari ya pamoja iliyoandaliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete hapo Bwawani Mjini Zanzibar.
 Viongozi na wananchi wa Mikoa Mitatu ya Unguja wakijichukulia mlo katika futari ya pamoja iliyoandaliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete hapo Bwawani Mjini Zanzibar.
 Waumini na Wananchi mbali mbali wa Mikoa Mitatu ya Unguja wakiendelea kufutari pamoja wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa Niaba ya Rais wa Muungano Dr. Kikwete.
Waumini na Wananchi mbali mbali wa Mikoa Mitatu ya Unguja wakimsikiliza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa Niaba ya Rais wa Muungano Dr. Kikwete alipokuwa akiwashukuru

 
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na Waumini na Wananchi wa Mikoa Mitatu ya Unguja mara baada ya futari ya pamoja  akimuwakilisha Rais Kikwete aliyeandaa futari hiyo.
Balozi Seif akiagana na Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Mh. Aboubarak Khamis Bakari mara baada ya futari ya pamoja iliyofanyika katika ukumbi wa Salama Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar.Pembeni kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mh. Abdulla Mwinyi ambae ndie Mkuu wa Mkoa mwenyeji wa shughuli hiyo.

Mazrui afungua maonyesho ya Biashara viwanja vya Maisara


 Mwenyekiti wa Mamlaka ya kukuza Biashara Tanzania (TANTRADE) Bi. Thabetha Mwambenja akiteta jambo na Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko wa Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui katika ufunguzi wa maonyesho ya Biashara ya Edi el Fitri yanayofanyika Uwanja wa Maisara Mjini Zanzibar.
 Sehemu ya waalikwa waliofika katika maonyesho ya Biashara ya Edi El Fitri yanayoandaliwa kwa pamoja kati ya TANTRADE na Wizara ya Biashara ya Zanzibar kila mwaka wakimsikiliza mgeni Rasmi katika ufunguzi wa maonyesho hayo.
 Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko wa Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui akikata utepe kufungua maonyesho ya Biashara ya Ed El Fitri katika viwanja vya Maisara, wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa TANTRADE Bi. Sabetha Mwambenja na kati kati ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE Bi. Anna Bulondo.
 Waziri wa Biashara Viwana na Masoko Nassor Ahmed Mazrui akiangalia bidhaa za wajasiriamali kwenye maonyesho ya Biashara ya Edi El Fitri katika kiwanja cha Maisara. 


Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko wa Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui katika picha ya pomoja na viongozi mbali mbali.

Friday, 25 July 2014

Waziri Aboud atembelea maduka Chakechake


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe:Mohammed Aboud Mohammed, akiangalia kiatu cha Kike wakati alipotembelea maduka mbali mbali na kujuwa bei za bidhaa, ndani ya mji wa chake chake katika kuelekea skukuu ya Edd el fitr.
 
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe:Mohammed Aboud Mohammed, akiangalia mtandio wakati alipotembelea wafanya biashara wadogo wadogo waliomo ndani ya mji wa chake chake.
 
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe:Mohammed Aboud Mohammed, akiangalia suruali ya mtoto, wakati alipofanya zaiara ya kuangalia bei za bidhaa madukani, ikiwa ni kuelekea skukuu ya Edd el fitr.
MKUU wa Wilaya ya Chake Chake, Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla akimpatia maelekezo waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar, Mhe:Mohammed Aboud Mohammed mwenye kanzu wakati alipotembelea maduka ya Chake Chake kuangalia bei za bidhaa kuelekea skukuu ya Edd el fitr

Thursday, 24 July 2014

Dk Shein azindua mradi wa SAEMAUL UDONG Cheju


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.ALi Mohamed Shein akipata maelezo kutoka Naibu katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Maliasili Nd,Juma Ali Juma wakati alipotembelea kituo cha kukausha Embe Dodo katika Kijiji cha Cheju kibonde maji leo  kilichojengwa na Shirika la misaada la Koika nchini Korea kupitia    Mradi wa  SAEMAUL UDONG   .[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.ALi Mohamed Shein na Balozi wa Korea Bw.IL Chung (katikati) wakiangalia embe zilizokaushwa zikiwa katika Mpango maalum wa kuhifadhiwa  wakati alipotembelea kituo cha kukausha Embe Dodo katika Kijiji cha Cheju kibonde maji leo kilichojengwa na Shirika la misaada la Koika nchini Korea kupitia Mradi wa  SAEMAUL UDONG   .[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]  
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.ALi Mohamed Shein na Balozi wa Korea Nchini Tanzania Bw.IL Chung (katikati) wakiangalia embe zilizokaushwa zikiwa katika Mpango maalum wa kuhifadhiwa  wakati alipotembelea kituo cha kukausha Embe Dodo katika Kijiji cha Cheju kibonde maji leo  kilichojengwa na Shirika la misaada la Koika nchini Korea kupitia Mradi wa SAEMAUL UDONG   .[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]  
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.ALi Mohamed Shein(katikati) na Balozi wa Korea Nchini Tanzania Bw.IL Chung wakipata maelezo kutoka Naibu katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Maliasili Nd,Juma Ali Juma (kulia) wakati alipotembelea mitambo katika kituo cha kukausha Embe Dodo katika Kijiji cha Cheju kibonde maji leo kilichojengwa na Shirika la misaada la Koika nchini Korea kupitia  Mradi  SAEMAUL UDONG   .[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.ALi Mohamed Shein akibadilishana mawazo na  na Balozi wa Korea Nchini Tanzania Bw.IL Chung mara baada ya kutembelea  kituo cha kukausha Embe Dodo katika Kijiji cha Cheju kibonde maji leo kilichojengwa na Shirika la misaada la Koika nchini Korea kupitia  Mradi  SAEMAUL UDONG   .[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]