Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi

Mwanafunzi Isra Hilal Mwadini akifuatiwa na mwenzake Tamima Abass Sheha wakipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wakati wa hafla ya Maulidi ya Jumuiya ya Chuo cha Samael Academy.Kulia ya Balozi Seif ni Rais wa Sameil Academy Sheikh Nassir Bin Said.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizindua rasmi Bara bara ya pili ya Amani hadi Mtoni baada ya kukamilika awamu ya mwisho ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Akiwa na Balozi mdogo wa India nchini Tanzania wakiangalia maonyesho yaliofanya na Msanii kutoka India, Bi Navi Madhav hapo Ngome Kongwe

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Dk. Khalid S. Mohamed

akizungumza na Wadau wa Maendeleo wa Mfuko wa TASAF, walipofika Ofisini kwake kuzungumzia maendeleo ya Mfuko wa TASAF III,na kutembelea Mradi wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini (PSSN) katika Jimbo la Muyuni Wilaya ya Kusini Unguja katika Kijiji cha Muyuni B

Wazir wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakifurahia jambo wakati wa semina ya siku moja kuhusu matokeo makubwa na ya haraka katika kuleta mageuzi ya kiuchumi na kuleta maendeleo nchini iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein

Sunday, 18 January 2015

Balozi Seif Ahudhuria Maulidi ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW)

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwahutubia na kutoa nasaha zake kwa Waumini wa Dini ya Kiislam waliohudhuria  maulid ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad yalioandaliwa na Taasisi ya Samael Academy yaliofanyika katika Msikiti wa Gombani Chakechake Kisiwani Pemba.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwahutubia na kutoa nasaha zake kwa Waumini wa Dini ya Kiislam waliohudhuria  maulid ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad yalioandaliwa na Taasisi ya Samael Academy yaliofanyika katika Msikiti wa Gombani Chakechake Kisiwani Pemba.
 Kiongozi wa Taasisi ya Samael Academy sheikh Said Nassor Abdalla, akisoma risala ya Taasisi hiyo, wakati wa sherehe za Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW)yalioadhimishwa katika msikiti mkuu wa Gombani kisiwani PembaPemba, 
 Baadhi wa waumini wa dini ya kiislamu waliohudhuria maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika katika msikiti wa Gombani Chake Chake Pemba, ambayo yameandaliwa na taasisi ya Samael Academy na kuhutubiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe: Baloz Seif Ali Idd,

Rais wa Jumuiya ya Samael Academy Sheikh Nassir Bin Said akitoa salamu kwenye hafla ya maulidi ya Kuzaliwa Mtume Muhammad { SAW } yaliyofanyika Masjid Rahman Gombani chake chake Pemba.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiteta na Rais wa Jumuiya ya Samel Academy Sheikh Nassir Bin Said wakati wa hafla ya Maulidi ya uzawa wa Mtume Muhammad { SAW } hapo Gombani chake chake Pemba.
Afisa Mdhamini Wizara ya Katiba na Sheria Pemba Sheikh Omar Khamis  aisifu Samael Academy kwa uamuzi wake wa kusaidia jamii Kisiwani Pemba.
 Mwanafunzi Isra Hilal Mwadini akifuatiwa na mwenzake Tamima Abass Sheha wakipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wakati wa hafla ya Maulidi ya Jumuiya ya Chuo cha Samael Academy.Kulia ya Balozi Seif ni Rais wa Sameil Academy Sheikh  Nassir Bin Said.
Mwanafunzi Chum Hijjaakifuatiwa na Awat Abdulla wa Samel Academy wakipokea zawadi kutoka kwa Balozi Seif baada ya kuhitimu mafunzo yao.

Na Othman Khamis. OMPR.
Jamii ya Kiislamu Nchini inapaswa kufuata vilivyo mafundisho sahihi aliyokuwa akiyasimamia  Kiongozi wa Dini ya Kiislamu Mtume Muhammad { SAW } ili  Jamii hiyo ipate fursa nzuri ya kuishi katika maisha ya furaha na ustaarabu wa maendeleo makubwa ndani ya Dunia hii.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo katika hafla ya maulidi ya uzawa wa Mtume Muhammad { SAW } yaliyoandaliwa na Chuo cha Samail Academy na kufanyika katika Msikiti Rahman uliopo Gombani Mjini Chake chake Kisiwani nPemba.

Balozi Seif alisema kigezo chema alichokuwanacho Kiongozi huyo wa waislamu kilijikita zaidi katika kusimamia vyema suala la kudumisha amani katika Dunia, kuleta umoja baina ya waislamu, kujikubalisha kuishi na mayatima sambamba na watu wa rika zote bila ya ubaguzi.

Aliupongeza Uongozi wa Chuo cha Samail Academy kwa juhudi zao walizozichukuwa na hatua waliyoifikia katika kuijenga jamii kitaaluma na maadili yanayokubalika.

Balozi Seif  alitoa wito kwa vijana kujishughulisha zaidi katika kutafuta elimu kwani ndio nyenzo pekee inayomfanya mwenye nayo anapoitumia vizuri hupata maendeleo makubwa.


Hata hivyo alionya kwamba wapo baadhi ya watu wamekuwa wakiitumia vibaya elimu waliyobarikiwa kwa kupotosha wenzao wasiokuwa nayo ili kufikia malengo yao binafsi.

“ Kuna  Watu huitumia elimu kuwageuza wenzao kuwa ngazi ya kupandia kuyafikia malengo yao binafsi. Mwenyezi muungu hayataki mambo hayo. Tutumie elimu  kwa kuelimisha wengine “. Alisisitiza Balozi Seif.

Alisema mafanikio makubwa kitaaluma na kijamii yatapatikana endapo jamii itajikubalisha kujituma  katika misingi ya  uaminifu licha ya changamoto za kimaisha  zinazowazunguuka katika maeneo yao.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akiridhia kukubali kuwa mlezi wa chuo hicho cha Samael Academy aliahidi kuzishughulikia changamoto zinazowakabili  Walimu na Wanafunzi hao kwa kutoa mchango wake kadri hali itakavyoruhusu.

Akisoma Risala Mudiri wa Samaeil Academy Sheikh Said Abdulla Nassor alisema Taasisi hiyo iliyoasisiwa mwaka 2012 na kusajiliwa rasmi Mwaka 2014 inajishughulisha na masuala ya kijamii katika maeneo mbali mbali hapa nchini.

Mudir Said alisema Samael Academy imejikita katika kusaidia jamii katika uchimbaji wa visima, kuunganisha Madrasa kuwa na nguvu za pamoja, kuwakusanya watoto yatima kwa kuwajengea mazingira bora ya kielimu na maisha yao ya baadae pamoja na kuanzisha mafunzo kwa walimu wanaotoa hotuba misikitini.

Alisema yao mafanikio makubwa tokea kuanzishwa kwa taasisi hiyo  mwaka 2012 akizitaja kuwa ni pamoja na kuzikusanya na kuzisajili madrasa zipatazo 95 zenye wanafunzi elfu 10,995, kusajili mayatima 712 pamoja na kuzitembelea madrasa kwa kuangalia changamoto zinazozikabili.

Mudiri huyo wa Samael Academy Sheikh Said Abdulla Nassor alifahamisha kwamba moja kati ya jambo lililopewa kipaumbele na taasisi hiyo ni kuwaendeleza wanafunzi na vijana waliofanikiwa kumaliza kuhifadhi juzuu 30 za Quran tukufu.

Hata hivyo Sheikh Said Abdulla Nassor alielezea changamoto zinazoikabili Taasisi hiyo akizitaja kuwa ni pamoja na vikwazo kwa baadhi ya watendaji wa taasisi za umma wanavyovitoa kwa Taasisi hiyo pamoja na usumbufu wa vifaa vya msaada vinavyotolewa wanafadhili wakati wa kutolewa bandarini.

Akitoa salamu zake Rais wa Samael Academy Sheikh Nassir Bin Said alisema Uongozi wa Jumuiya ya Taassi hiyo unafarajika na muitikio mkubwa wa wazazi na walezi waliooonyesha katika kuipokea taasisi hiyo yenye mnasaba na mazingira yao.

Sheikh Nassir alisema juhudi zitaendelea kuchukuliwa na Uongozi huo ili kuona malengo yaliyokusudiwa ya kusaidia jamii kukabiliana na mazingira yanayowazunguuuka yanafanikiwa vyema na kustawisha jamii zao.

Akimkaribisha mgeni rasmi katika hafla hiyo ya Maulidi ya uzawa wa Mtume Muhammad { SAW } Afisa mdhamini Wizara ya Katiba na Sheria Pemba Bwana Omar Khamis alisema Samel Academy tayari imeshaonyesha nia sahihi ya kutaka kusaidia jamii hapa nchini.

Sheikh Omar alisema Taasisi hiyo iko mbioni kujenga misikiti mikubwa mitatu Kisiwani Pemba,maandalizi ya ujenzi wa chuo Kikuu cha Kiislamu Chamanangwe pamoja na ujenzi wa chuo cha Amali Chake chake Pemba.

Alisema uanzishwaji wa chuo hicho cha amali umelenga kuwajengea mazingira mazuri wanafunzi watakaopata taaluma kwenye taasisi hiyo ambapo maandalizi yameanza katika kuhakikisha kwamba wanafunzo hao wanapata ajira ndani na nje ya Nchi.

Alifafanua kwamba Nchi za Saudi Arabia na Iraq ambazo zimeamuwa kujitolea kusaidia harakati za ujenzi wa chuo hicho cha amali Kisiwani Pemba zimekubali kuwapokea baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho  wamalizapo mafunzo kwa kuwapatia fursa za ajira katika Mataifa hayo.

Friday, 16 January 2015

Balozi Seif Achangia saruji mifuko 200 kwa Ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya Donge Unguja.

Balozi Seif akimkabidhi mifuko ya saruji 200 Mlezi wa Jumuiya ya Maendeleo Donge Nd. Moh’d Abdulla Khamis akitekeleza ahadi yake hapo skuli ya Sekondari Donge Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na Uongozi wa Jumuiya ya Maendeleo Donge pamoja na Wananchi wa Kijiji hicho kwenye hafla kukabidhi mifuko 200 ya Saruji akitekeleza ahadi aliyotoa mwezi mmoja uliopita.kushoto ya Balozi ni Mbunge wa Jimbo la Donge Mh. Sadifa Juma Khamis na kulia yake ni Mlezi wa Jumuiya ya Maendeleo Donge Nd. Moh’d Abdulla Khamis na Mke wa Balozi Seif Mama Asha Suleiman Iddi.
 Mbunge wa Jimbo la Donge Mh. Sadifa Juma Khamis akitoa mchango wa papo kwa papo wa shilingi Milioni 1,000,000/-.Mchango huo ni kuongeza nguvu za upigaji plasta wa madarasa ya Skuli ya Sekondari ya Donge kwenye hafla ya makabidhiano ya saruji iliyotolewa  na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
 Baadhi ya Wzee na Viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo Donge  wakimsikiliza Balozi Seif hayupo pichani wakati wa hafla ya kukabidhi saruji kwa uendelezaji wa skuli ya sekondari ya Donge.(Picha na Hassan Issa OMPR)

     
Na Othman Khamis 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewaasa Vijana kuzitumia fursa  nzuri zinazoandaliwa na wazazi wao katika kuwajengea  miundombinu na mazingira bora ya kupata elimu ambayo ndio mzingi pekee utakaowapa manufaa  katika hatma yao ya baadaye.

Alisema elimu ndio rasilmali muhimu kwa vijana katika wakati huu wa mabadilio yanayokwenda na wakati wa  sayansi na teknolojia ulimwenguni kote.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa wasia huo wakati akikabidhi mifuko 200 ya Saruji kwa ajili ya uendelezaji wa ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya Donge akitekeleza ahadi aliyoitoa mwezi uliopita wakati akiuzindua Uongozi wa Jumuiya ya Maendeleo Donge.

Akiahidi kuchangia tena shilingi Milioni 2,000,000/- kuunga mkono uendelezaji wa  Jengo hilo katika kazi za upigaji plasta Balozi Seif aliwataka wanafunzi kuacha mchezo na badala yake wapende masomo yao na kuwaheshimu walimu wao ili kupata maendeleo yenye mafanikio.   

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  alisema ameamua kutekeleza ahadi hiyo katika kipindi kifupi  kwa kuthamini umuhimu wa elimu pamoja na kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na  wazazi katika kuekeza kwenye sekta ya taaluma.


Balozi Seif alifahamisha kwamba karne ya sasa imebadilisha mfumo mzima wa elimu ambao kwa njia ye yote mwanafunzi analazimika kufanya jitihada za zaiada katika kutafuta elimu itakayomuwezesha kujijengea mazingira bora ya ajira wakati amalizapo masomo.

“ Karne ya sasa imebadilika kutokana na Darasa la 12 kukosa thamani kwa zaidi ya miaka 20 ambayo inamlazimu kijana kusoma elimu ya ziada  kama anahitaji kuwa na ajira nzuri  “. Alisema Balozi Seif.

Aliwakumbusha vijana kuangalia mambo yatakayowafaa katika maisha yao ya baadaye badala ya kuamua kufuatilia upuuzi unaopenda kuenezwa na watu wajiojikubalisha kupigania ubinafsi.

Balozi Seif alisema wakati umefika kwa jamii kuwatenga watu wanaopita mitaani kushawishi vijana kuwachukia viongozi wao waliojikubalisha kuwaletea maendeo kwenye maeneo yao.

“ Hawa Watu wanaopita pita na kushawishi vijana kuwachukia viongozi wao wanaowasaidia katika harakati zao za kimaendeleo wanafaa kutengwa na Jamii “. Alisema Balozi Seif.

Aliwakumbusha Wazazi na Walezi wa Kijiji cha Donge kuendelea kushirikiana, kupendana pamoja na kushikamana ili kupata nguvu za pamoja katika kujiletea maendeleo yao na vizazi vyao vya baadae.

Mapema Mlezi wa Jumuiya ya Maendeleo Donge Bwana Moh’d Abdulla Khamis amesema wananchi wa Jimbo la Donge wameelezea faraja yao kutokana na kauli ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ya kutekeleza ahadi yake katika muda mfupi.

Bwana Moh’d Abdulla alisema ahadi ya Balozi Seif ndani ya kipindi cha mwezi mmoja uliopita ameifanya kama Kiongozi anayekereketwa na maendeleo yanayaopatikana katika sekta ya elimu.

“ Si wepesi kwa Viongozi  wengi hapa nchini kuahidi au kutenda jambo la kutaka kusaidia jamii na kulitekeleza kwa muda mfupi “. Alisema Mlezi huyo wa Jumiya ya Maendeleo ya Donge.

Alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Donge Mh. Sadifa Juma Khamis   kwa wepesi wa maamuzi yake katika kusaidia harakati za Wananchi hasa katika sekta muhimu ya Elimu.

Akitoa shukrani kwa niaba ya Wana jumuiya ya Maendeleo Donge pamoja na Wananchi wa Jimbo hilo Mzee Moh’d Rafii alimtaja Balozi Seif kama mfano wa Kiongozi anayetekeleza  agizo la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete la kuwataka viongozi kufuatilia kero za Wananchi badala ya kukaa maofisini.

Katika makabidhiano hayo ya saruji kwa ajili ya upigaji plasta madarasa ya skuli ya Sekondari ya Donge Mbunge wa Jimbo hilo Mh. Sadifa Juma Khamis alikabidhi mchango wa shilingi Milioni 1,000,000/-  papo hapo kusaidia kazi hiyo.

Mh. Sadifa ambaye tayari ameshakabidhi matofali  Elfu 10,000 kutekeleza ahadi aliyoitoa kwenye Skuli hiyo pia akaahidi kuchangia shilingi Milioni tano zitakazoongeza nguvu za kazi hiyo ya upigaji plasta kwenye skuli hiyo.

Thursday, 15 January 2015

Balozi Seif Akabidhi Mabomba ya Maji Safi kwa Wananchi wa Kijiji cha Kirombero Unguja


Mbunge wa Jimbo la Kitope ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi Mabomba ya kusambazia maji safi Diwani ya Wadi ya Upenja Bibi Asha Abdulla Mussa kwa ya Kijiji cha kilombero Mkoa wa Kaskazini Unguja.Kati kati yao ni Mke wa Balozi Seif Mama Asha Suleiman Iddi.
Mabomba ya kusambazia maji safi katika Kijiji cha Kilombero yenye gharama ya shilingi Milioni 17,000,000/- yaliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kitopo Balozi Seif Ali Iddi.
Mbunge wa Jimbo la Kitope ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Balozi Seif Ali Iddi akishiriki katika kazi ya uchimbaji mtaro kwa ajili ya ulazaji wa mabomba  kwa ajili ya huduma za kusambazia maji safi katika Kijiji cha Kilombero.(Picha na Hassan Issa – OPMR)

Na.Othman Khamis.OMPR.
Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi alisema licha ya juhudi zinazochukuliwa na viongozi katika kuchangia nguvu za kukabiliana na matatizo mbali mbali yanayowakabili wananchi katika maeneo yao lakini bado jukumu hilo litaendelea kubakia mikononi mwa  wananchi  wenyewe.

Alisema Viongozi na hata Serikali Kuu huhamasika  na kushawishika zaidi kusaidia hata uwezeshaji na hata vifaa  kwenye miradi ya Jamii baada ya kuona nguvu za Wananchi zimeanza au kuiendelezwa katika kujikomboa  na umaskini au kujitafutia maendeleo yao.

Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema hayo wakati akikabidhi mabomba 250 ya kusambazia huduma za maji safi na salama kwa ajili ya Wananchi wa Kijiji cha Kilombero hapo katika  kituo cha Kilimo Kilombero Wilaya ya Kaskazini “ B “ Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Mabomba hayo yaliyogharimu jumla ya shilingi Milioni 17,000,000/- nusu ya gharama ya fedha hizo imetokana na mfuko wa Jimbo { CDF } na nusu iliyobakia imetolewa na Mbunge huyo wa Jimbo la Kitope.

Balozi Seif pia alishiriki kazi ya uchimbaji mtaro wa ulazaji wa bomba hizo unaoanzia kwenye kisima kilichochimbwa kwa ajili ya mradi huo wa usambazaji maji ambacho kimeshakalimika uliokwenda sambamba na upatikanaji wa huduma za umeme katika kisima hicho.

Aliwapongeza wananchi wa Kijiji cha Kilombero kwa kazi kubwa wanayoendelea kuifanya ya kujiondoshea matatizo yanayowakabili ikiwemo kushiriki katika kazi za usambazaji wa huduma za maji safi.

Balozi Seif alisema huduma za upatikanaji wa maji safi ni zao hivyo lazima wahakikishe wanashiriki kwa nguvu zao zote katika kukabiliana na changamoto kama hizo za jamii.

Aliwaeleza wananchi hao wa Kijiji cha Kilombero kwamba jitihada zitaendelea kuchukuliwa  na Uongozi wa Jimbo hilo za kusambazwa huduma za maji safi na salama katika mitaa ya kijiji hicho mara baada ya Bomba za maji hayo kufikishwa katika eneo la Skuli ya Kilombero kutoka kwenye kisima hicho.

“ Suala la tataizo la huduma za maji safi ndani ya kijiji cha Kilombero litaendelea kubakia katika historia  siku chache zijazo “. Alisema Mbunge huyo wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi.

Aliendelea kuwaasa wananchi hasa vijana kujiepusha na tabia ya kushawishiwa na baadhi ya Watu wakiwemo wanasiasa katika kujiingiza kwenye uchochezi unaozaa balaa na matatizo.

Balozi Seif alisema ni vyema kwa wananchi hao wakalazimika kuelewa athari ya uchochezi unaofanywa na wanasiasa  hao ambao mara nyingi unalenga kuwanufaisha wao binafsi.

Mapema Diwani wa Wadi ya Upenja Bibi Asha Abdulla Mussa  akipokea  mchango wa mabomba hayo ya usambazaji maji safi katika Kijiji cha Kilombero alimpongeza Mbunge huyo wa Jimbo la Kitope kwa moyo wake wa kusaidia kuondosha matatizo yanayowakabili wananchi wa Jimbo lake.

Diwani Asha alimuomba Mbunge huyo kuendelea na juhudi hizo  ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikileta faraja kwao Viongozi wa wadi na Matawi yaliyomo ndani ya  Jimbo hilo pamoja na wananchi wote.

Akitoa shukrani kwa niaba ya Wananchi wa Kijiji cha Kilombero  Msimamizi wa Kamati ya mradi wa Maji ya Kijiji hicho Bwana Moh’d Haji Faki alimuhakikishia mbunge huyo wa Jimbo la Kitope kwamba Wananchi wa Kijiji hicho wako tayari muda wowote kushiriki katika kazi za maendeleo wakati watapotakiwa kufanya hivyo.

Bwana Moh’d alisema mradi huo wa usambazaji huduma za maji safi katika Kijiji hicho ni miongoni mwa kazi hizo ambazo wataendelea kushirikiana katika kuzitekeleza kwa faida yao na ustawi wa vizazi vyao.

Zaidi ya shilingi Milioni 20,000,000/- zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi zimetumika katika ujenzi  wa Kisima cha Maji ya Kilombero kwa lengo la kuwaondoshea usumbufu wa miaka mingi wa huduma za upatikanaji wa maji safi na salama wananchi wa Kijiji hicho.

Tuesday, 13 January 2015

PBZ Yakabidhi Fulana kwa Ajili ya Sherehe za Miaka 51 ya Mapinduzi


Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Ndg, Haji Ame, akitowa shukrani kwa Uongozi wa Benki ya Watu wa Zanzibar kwa kukabidhi Fulana mia tano kwa ajili ya sherehe za miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar, makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi hiyo Vuga Zanzibar.
Kaimu Mkurugenzi Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ndg Seif Suleiman, akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi fulana 500 kwa ajili ya sare ya kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar, yatakayoadhimishwa 12,Jan 2015 katika viwanja vya Amaan Zanzibar.
Kaimu Mkurugenzi Masoko wa PBZ,Ndg. Seif Suleiman, akionesha moja ya fulana zilizotolewa na PBZ, kwa ajili ya kusherehekea sherehe za kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika viwanja vya Amaan Zanzibar.  
Kaimu Mkurugenzi Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Ndg Seif Suleiman, akimkabidhi moja ya fulana 500 zilizotolewa na PBZ kwa Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi Ndg Haji Ame, makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Vuga. 
Kaimu Mkurugenzi Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Ndg Seif Suleiman, akimkabidhi moja ya fulana 500 zilizotolewa na PBZ kwa Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi Ndg Haji Ame, makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Vuga. 
Kaimu Mkurugenzi Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Ndg Seif Suleiman, akimkabidhi moja ya fulana 500 zilizotolewa na PBZ kwa Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi Ndg Haji Ame, makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Vuga. 

Monday, 12 January 2015

Mwenyekiti wa Kamati ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiambatana na baadhi ya Viongozi wa Kamati 10 zilizopewa jukumu la kusimamia maandalizi ya sherehe za Miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 Makamanda  shupavu Wanawake wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania  { JWTZ } wakionyesha umahiri wao katika kulichapa gwaride wakijiandaa na Kilele cha maadhimisho ya kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar hapo Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar.  Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

 Mwenyekiti wa Kamati ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa Balozi Seif akiwa pamoja na Viongozi wa Kitaifa na Makamanda wa Vikosi vya ulinzi wakiangalia hatua za matayarisho ya mwisho ya Gwaride litakalopamba kilele cha maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar hapo Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.



 Vijana wa Muziki wa Kikazi Kipya Zanzibar wakiimba wimbo maalum utakaoburudisha  kwenye sherehe za maadhimisho ya Kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12 Uwanja wa Amani.  Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
























Mwenyekiti wa Kamati ya Sherehe na maadhimisho ya Kitaifa Balozi Seif akizungumza na wajumbe wa Kamati hiyo walipokuwa wakitathmini matayarisho ya kwisho ya kilele cha sherehe za Mapinduzi zinazofikia ukingoni Januari 12 2015 uwanjani Aamani.  Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

   Press Release:-

Matayarisho ya mwisho kwa ajili ya kilele cha maadhimisho ya kusherehekea kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 yamefikia hatua ya mafanikio makubwa  katika kukamilika kwake.

Maadhimisho hayo yaliyoanza Tarehe  Pili Januari 2015 kwa usafi wa mazingira, uzinduzi pamoja na  uwekaji wa mawe ya msingi ya miradi mbali mbali ya Taasisi za Umma na zile binafsi yakiwemo mashindano ya michezo na burdani tofauti yanafikia kilele chake Januari 12 siku ambayo wakwezi na Wakulima walijikomboa kutoka katika makucha ya wakoloni.

Vikosi vya ulinzi na usalama vya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na vile vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar vilikamilisha matayarisho ya mwisho ya Gwaride  rasmi hapo Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar linalotarajiwa kupamba maadhimisho hayo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiambatana na baadhi ya Viongozi wa Kamati 10 zilizopewa jukumu la kusimamia maandalizi ya sherehe hizo walishuhudia gwaride la vikosi hivyo vinavyoonekana kuwiva katika kiwango kilichokusudiwa.

Vikosi vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania { JWTZ }, Polisi, Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo { KMKM }, Mafunzo,Jeshi la Kujenga Uchimi { JKU }, Kikosi cha Zimamoto na Uokozi na Valantia vilionekana kuupamba uwanja wa amani kwenye matayarisho hayo vikiwa tayari kwa ajili ya Kilele cha maadhimisho hayo.

Gwaride hilo lililoongozwa na Luteni Kanali Moh’d Khamis Adam liliambatanisha pia na matayarisho mengine ya mwisho ya ngoma za utaduni pamoja na muziki wa Kizazi kipya watakaopata fursa ya kutoa burdani kwenye kilele cha maadhimisho hayo ya kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa katika Ukumbi wa Watu mashuhuri { VIP } uliopo Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar mara baada ya kuangalia  matayarisho hayo Mwenyekiti wa Kamati hiyo Balozi Seif aliyapongeza majeshi yote kwa hatua yaliyochukuwa ya kushiriki vyema kwenye maandalizi ya sherehe hizo.

Balozi Seif alisema juhudi zilizoonyeshwa na wapiganaji hao katika kulichapa gwaride  zimeonyesha wazi umahiri wao katika kutekeleza vyema majukumu wanayopangia na Taifa.

“ Nimeridhika na maandlizi yote yaliyochukuliwa  na  Kamati  zote zilizoshiriki kikamilifu katika matukio mbali mbali tokea sherehe zetu zilipoanza Mapema mwezi huu. Mambo mazuri sana licha ya kasoro ndogo ndogo zilizojitokeza ambazo uwezo wa kuzikamilisha upo “. Alisema Balozi Seif.

Mapema Katibu wa Kamati ya Sherehe na Maadshimisho ya Kitaifa  Dr. Khalid Salum Moh’d alisema Kamati imeandaa utaratibu kwa Wananchi watakaokosa kuingia ndani ya Uwanja  wa Amani kuziona sherehe hizo kupitia TV maalum zitakazowekwa upande wa jukwa la mashariki  { Maarufu jukwaa la Urusi }.

Dr. Khalid alisema TV hizo zimeandaliwa kwa lengo la kupunguza msongamano mkubwa unaoweza kutokea endapo wananchi watajitokeza kwa wingi kuhudhuria sherehe hizo za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia miaka 51.

Wageni wa Kimataifa wapatao 120  miongoni mwao  wakiwemo Mabalozi  80 wa Nchi za Nje waliopo Tanzania wamethibitisha kuhudhuria sherehe hizo, waandishi wa Habari 160 wataripoti  matukio ya sherehe hizo wakati vituo vya TV Vinne na Redio 6 vinatarajiwa kutangaza moja kwa moja sherehe hiyo.




Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifungua tamasha la Pili la Biashara la mwaka 2015 la maadhimisho ya kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar linalofanyika katika uwanja wa michezo wa Maisara Mjini Zanzibar.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akilifungua Tamasha la Pili la Biashara Zanzibar linalofanyika katika uwanja wa michezo wa Maisara Mjini Zanzibar. Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Mh. Nasso Ahmed Mazrui na kushoto yake ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Baisra Tanzania { Tantrade } Bibi Jackline na Naibu Waziri wa Biashara Zanzibar Mh. Thuwaiba Kisasi. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
 Kikundi cha Sarakasi cha Young Brother Acrobatic kutoka Kijiji cha Muyuni kikifanya vitu vyake wakati wa hafla ya ufunguzi wa Tamasha la Biashara Zanzibar Hapo Maisara Suleiman. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
 Ofisa Kutoka Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bibi Robi Bwire akimpatia maelezo Balozi Seif wakati akikagua mabanda ya maonyesho kwenye Tamasha la Biashara.  Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
 Balozi Seif akifurahia bidhaa zinazouzwa na Kampuni ya Pakiza General Traders kwe nye Tamasha la Pili la Biashara Zanzibar.  Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.























Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Baisra Tanzania { Tantrade } Bibi Jackline na Waziri wa Biashara Zannzibar Mh. Mazrui wakifurahia bidhaa za Miti shamba kwenye banda la Maonyesho la Uganda.  Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.


 Press Release:-

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametoa wito kwa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar  kuanzisha eneo maalum kwa maonyesho ya biashara kwa lengo la kutanua zaidi uhusiano wa kibiashara kati ya Zanzibar na Mataifa mengine Duniani.

Alisema maonyesho ya Kibiashara siyo tu yanavutia na kushawishi wawekezaji lakini pia huongeza ushirikiano karibu baina ya wafanyabiashara wenyewe kwa wenyewe .
Balozi Seif alitoa wito huo wakati akilifungua tamasha la Pili la Biashara la mwaka 2015 la maadhimisho ya kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar linalofanyika katika uwanja wa mishezo wa Maisara Mjini Zanzibar.

Alisema lengo kuu la Tamasha la biashara Zanzibar  ni kushajiisha ukuaji wa biashara kwa azma ya kuirejeshea Zanzibar hadhi yake ya kuwa kituo cha biashara katika mwambao wa Afrika Mashariki kwa karne kadhaa zilizopita.

Balozi Seif alifahamisha kwamba uwepo wa matamasha kama haya Zanzibar hutoa fursa kwa wageni kujipangia muda wa kutembelea Zanzibar kwa mapumziko pamoja na kujipatia mahitaji yao ya bidhaa tofauti zinazozalishwa ndani na hata kwa zile Taasisi za nje zinazoshiriki maonyesho hayo.

Alisema wafanyabiashara  pamoja na wajasiri amali wanapaswa kuitumia vyema fursa hiyo adhimu ya tamasha la biashara ili wakuze biashara zao kwa vile ni moja kati ya sekta muhimu ya kukuza uchumi na kutoa ajira kwa wananchi walio wengi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema Serikali itaendelea kushirikiana na wafanyabiashara wa pande zote mbili za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Afrika Mashariki katika kuhakikisha sekta ya biashara inazidi kukua  sambamba na matamasha ya biashara ili kuongeza idadi ya wageni.

Balozi Seif  alisisitiza umuhimu wa matamasha kama haya ya biashara kujumuishwa pia maonyesho ya utamaduni wa Mzanzibari kama kazi za sanaa ya mkononi, vyakula vya mwambao wa pwani ya Afrika Mashariki na Muziki ambao unaonekana kutoweka katika Historia kutokana na mabadiliko ya utandawazi.

Aliwaomba wafanyabiashara kuziepuka bidhaa zilizo chini ya kiwango kwani kufanya hivyo kutamfanya mnunuzi wa bidhaa zao kupoteza fedha bure pamoja na kuharibiwa mipango yake.

Balozi Seif alieleza kwamba Serikali imeanzisha Taasisi inayosimamia viwango kwa lengo la kukuza ubora wa bidhaa zinazozalishwa pamoja na zile zinazoagiziwa nje ya nchi masuala ambayo yanakwenda sambamba na mikakati ya kuwasaidia wjasiri amali wa Zanzibar katika kufikia viwango vinavyokubalika katika masoko ya Kimataifa.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameipongeza Wizara ya Biashara Zanzibar kwa kushirikiana na mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania { Tantrade } pamoja na Jumuiya ya Wafanyabiashara Zanzibar kwa wazo lao la pamoja la kuanzisha na kuendeleza Tamasha la Biashara hapa Zanzibar.

“ Na hili ni tamasha la Pili huku tukisherehekea miaka 51 ya Mapinduzi ya Januari mwaka 1964 lengo likiwa kushajiisha ukuaji wa biashara kwa azma ya kuirejeshea Zanzibar hadhi yake ya kuwa kituio cha Biashara Mwambao wa Afrika Mashariki “. Alisema Balozi Seif.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliipongeza Mamlaka ya Maendeleo ya Baisra Tanzania { Tanzania Trade Development Authority – Trade } kwa uamuzi  wake wa kuisaidia Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar katika taaluma ya Maonyesho na matamasha ya Baishara.

Balozi Seif aliitaka Mamlaka hiyo kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika sekta hiyo ili ifikie hatua ya kujiendesha yenyewe katika sekta hiyo muhimu ya Uchumi wa Taifa.
Aliwashukuru washiriki wa wa tamasha hili la Biashara Zanzibar kutoka ndani na nje ya Nchi, Taasisi za Umma na zile Binafsi, Mapampuni  kwa kushiriki kwenye tamasha la mwaka huu na kuwaomba washiriki kwenye matamasha yanayokuwa yanaandaliwa hapa Zanzibar.

Mapema Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Mh. Nassor Ahmed Mazrui alisema ukuaji wa sekta ya B iashara hapa Nchini umeongeza mapato ya nchi sambamba na huduma za fedha.

Waziri Mazrui alisema Tamasha la Biashara la Mwaka huu limeshirikisha zaidi ya Makampuni 160 katika ya 200 yaliyoomba kushiriki katika  Tamasha hili kutoka Tanzania Bara na wenyeji  Zanzibar yakiwemo Makapumi mawili ya Kigeni.
Alifahamisha kwamba mbali ya bidhaa mbali mbali zitakazouzwa na kuonyeshwa kwenye Tamasha hilo la bishara lakini pia huduma za Michezo ya Watoto itakuwepo ili kuwapa fursa watoto watakaotembelea Tamasha hilo kupata burdani.

Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko aliwapongeza washiriki wa Tamasha  la kwanza la mwaka J ana lililofanikiwa vyema kutokana na kukusanya mapato zaidi hya shilingi Milioni 220,630,150/- kutokana na bishara za papo kwa papo.

Alisema Tamasha la mwaka pia lilipokea maombi ya wateja kutoka makampuni na watu binafsi kwa ajili ya kupata huduma zenye gharama ya zaidi ya shilingi Milioni 90,000,00o/-.
Tamasha la Pili la Biashara la mwaka 2015 la maadhimisho ya kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar limeanza Tarehe 7 Januari mwaka huu wa 2015 na kuendelea hadi Tarahe 13 Mwezi huu.





Kilele cha miaka 51 ya Mapinduzi uwanja wa Amaan



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, akisalimiana na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein, wakati wa sherehe za miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar kwenye uwanja wa Aman, leo Jumatatu Januari 12, 2015
JK na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange
JK, akisabahiananna Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, a.k.a "Mzee Rukhsa"
JK akisalimiana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad
JK akisaliamiana na REais Mstaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Benjamin Mkapa, "Mzee wa uwazi na Ukweli"
JK akisalimiana na Mama Fatma Karume, mjane wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Abeid Aman Karume