Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akiongozana na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Mhe.Bihindi Hamad, kwenda kukagua timu za JKU na Mtibwa wakati wa mchezo wao wa Nusu Fainal ya Kombe la Mapinduzi, uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar timu ya Mtibwa imeshinda kwa peneti 4-3.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akisalimiana na wachezaji wa timu ya Mtibwa kabla ya kuaza mchezo wao wa Nusu Fainmali ya Kombe la Mapinduzi uliofanyika uwanja wa Amaan.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akisalimiana na wachezaji wa timu ya JKU kabla ya kuaza mchezo wao wa Nusu Fainmali ya Kombe la Mapinduzi uliofanyika uwanja wa Amaan.
Kikosi cha timu ya JKU kilichotowa upinzani kwa timu ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa Amaan katika mchezo wao wa nusu fainal ya Kombe la Mapinduzi.
Kikosi cha timu ya Mtibwa Sugar kilichofanikiwa kuingia Fainal ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuitoa timu ya JKU katika mchezo wao wa Nusu Fainal uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.
Mchezaji wa timu ya JKU na wa Mtibwa wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa Nusu Fainal uliofanyika uwanja wa Amaan, Timu ya Mtibwa imeshinda kwa penenti 4-3.
Golikipa wa timu ya Mtibwa Said Mohammed akiokoa moja ya hatari golini kwake huku mshambuliaji wa timu ya JKU Mbarouk Chande akikimbilia mpira huo.
Mshambuliaji wa timu ya Mtibwa Mzamiru Yassin, akimpita beki wa timu ya JKU Suleiman Omry.
Mchezaji wa timu ya JKU na wa Mtibwa wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa kutafuta nafasi ya kucheza Fainal ya Kombe la Mapinduzi mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan, timu ya mtibwa imeshinda mchezo huo na itacheza Fainal na timu ya Simba baada ya kufanikiwa kuifunga timu ya Polisi bao 1--0, katika nusu fainali yao iliofanyika usiku.
Golikipa wa timu ya Mtibwa Said Mohammed akiokoa moja ya hatari golini kwake huku mshambuliaji wa timu ya JKU Amour Janja akiwa tayari kuleta madhara, timu ya Mtibwa imeshinda kwa penenti 4--3
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akiwa na Viongozi wengine wa Serekali na ZFA wakifuatilia mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi Kati ya Mtibwa na JKU uliofanyika uwanja wa Amaan.
Mshambuliaji wa timu ya Mtibwa Sugar Ame Ali akimpita beki wa timu ya JKU Khamis Abdallah, wakiwa katika mchezo wao wa Nusu Fainali kugombea kuzeza Fainali ya Kombe la Mapinduzi.
Mchezaji wa timu ya JKUna Mtibwa wakiwania mpira
Wachezaji wa timu ya Mtibwa wakishangilia ushindi wao dhidi ya timu ya JKU baada ya kushinda kwa njia ya penenti 4--3