Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiangalia nyumba iliyoporomoka dari na
kujeruhi wakazi wake watatu hapo Mtaa wa Ukutani Mjini Zanzibar. Kulia ya
Balozi Seif ni Mmiliki wa Nyumba Hiyo Bwana Mzee Abdulla Juma.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Balozi Seif akiwaagiza watu wanaoishi ndani ya nyumba iliyoporomoka dari Mtaa wa Ukutani kuhama ili kunusuru maisha yao kutokana na uchakavu wa nyumba hiyo.
Balozi Seif akiwa pamoja na Mmiliki wa nyumba iliyoporomoka Dari eneo la Ukutani Bwana Mzee Abdulla Juma na Mkuu wa Wilaya ya Mjini Kanali Mstaafu Abdi Mahmoud Mzee wakiangalia hali halisi ya mazingira ya nyumba hiyo. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Balozi Seif akiwaagiza watu wanaoishi ndani ya nyumba iliyoporomoka dari Mtaa wa Ukutani kuhama ili kunusuru maisha yao kutokana na uchakavu wa nyumba hiyo.
Aliyepo
mwanzo kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mjini Kanali Mstaafu Abdi Mahmoud Mzee. Picha na
Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Balozi Seif akiwa pamoja na Mmiliki wa nyumba iliyoporomoka Dari eneo la Ukutani Bwana Mzee Abdulla Juma na Mkuu wa Wilaya ya Mjini Kanali Mstaafu Abdi Mahmoud Mzee wakiangalia hali halisi ya mazingira ya nyumba hiyo. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Press Release:-
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewaagiza wananchi wanaoishi kwenye
nyumba mbovu na zile zilizochakaa ndani
ya Mji Mkongwe wa Zanzibar wafanye utaratibu
wa kuhama kwenye nyumba hizo mapema iwezekanavyo ili kunusuru maisha yao.
Alisema
Serikali kamwe haitakuywa tayari kuachia wananchi wake wanaendelea kuishi katika mazingira ya hatari
wakati njia za kuepuka hatari hizo zipo na wala hazina gharama yoyote.
Balozi Seif
Ali Iddi alitoa agizo hilo alipofanya ziara fupi ya kukagua Nyumba ya Bwana
Mzee Abdulla Juma ambayo iliporomoka dari sehemu ya sebule na kujeruhi wakaazi
watatu wa nyumba hiyo iliyopo Mtaa wa Ukutani Mjini Zanzibar.
Watu
waliojeruhiwa ni wadogo wa Mmiliki wa Nyumba Hiyo Bwana Haroun Abdulla Juma na
Fahim Abdulla Juma waliolazwa Hospitali kuu ya Mnazi Mmoja kwa matibabu pamoja
na Peter Monga aliyetibiwa na kuruhusiwa kurejea nyumbani.
Balozi Seif aliutaka uongozi wa Mamlaka ya Mji
Mkongwe wa Zanzibar kuendelea kuzifanyia uhakiki nyumba zote zilizomo ndani ya
mji mkongwe na hatua zichukuliwe mara moja na taasisi zinazohusika katika kuwahamisha
wakaazi wanaoishi kwenye nyumba zisizostahiki kuishi watu.
Mapema
Mmiliki wa Nyumba hiyo Bwana Mzee Abdulla Juma alimueleza Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar kwamba mkasa huo umetokea majira ya saa 11.00 za asubuhi wkati
dari ya nyumba hiyo sehemu ya sebule ilipoporomoka.
Bwana Mzee
alisema wakaazi wa nyumba hiyo kwa kushirikiana na majirani walilazimika
kuuvunja mlango mkuu wa nyumba hiyo ili kumnusuru Mtoto wa mdogo wake
aliyelazwa Hospitali Kuu ya Mnazi mmoja baada ya kuvunjika mguu.
Naye Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mji Mkongwe wa Zanzibar Nd. Mussa Awesu Bakari alisema watendaji wa
Mamlaka hiyo kwa kushirikiana na wataalamu wa Taasisi za majengo na ujenzi
tayari wameshafanya uhakiki wa Nyumba 75 zilizomo ndani ya Mji Mkongwe .
Nd. Mussa
alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba zoezi hilo linaendelea kwa lengo la kubaini
nyumba zisizofaa kutumiwa kwa makazi ya kawaida ya binaadamu.