Monday, 12 January 2015

Balozi Seif awaandalia chakula cha mchana vijana wa Chipukizi


 Vijana Cipukizi wa UVCCM wakipata mlo kwenye tafrija iliyoandaliwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif Ali Iddi akitekeleza ahadi aliyowapa Vijana hao.
 Balozi Seif akijumuika pamoja na Vijana Chipukizi pamoja na baadhi ya Viongozi wa  UVCCM kwenye chakula cha mchana aliyowaandaliwa baada yakzi ngumu waliyoifanya Vijana hao ya kushiriki matembezi ya   kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar mwaka jana.

 Makamu Mkuu wa Chipukizi wa UVCCM Zanzibar PiliHassan Suluhu akimpongeza Balozi Seif kwa kutimiza ahadi yake aliyoitowa kwao mwaka uliopita ya kula nao pamoja katika chakula cha mchana.
 Baadhi ya Vijana Chipukizi wa UVCCM wakimsikiliza Balozi Seif hayupo pichani wakati akiwapongeza kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kulitumikia Taifa hili wakiwa na umri mdogo.

Balozi Seif akizungumza na Vijana Chipukizi wa UVCCM Mara baada ya kula nao chakula cha mchana hapo kwenye ukumbi wa UVCCM Maisara Mjini Zanzibar.