Wasanii wa Kikundi cha Tausi Kilicho chini ya Gwiji la
Sanaa Nchini Bibi Maryam Hamdan kikitoa burdani ya Maulidi ya Homu kwenye
uzinduzi wa Tamasha la 18 la Filam la Nchi za Jahazi Zanzibar { ZIFF } hapo Hoteli ya Double Tree
By Hilton Shangani Mjini Zanzibar.
Picha na Hassan Issa – OMPR
Picha na Hassan Issa – OMPR
Wasanii wa Kikundi cha Tausi Kilicho chini ya Gwiji la
Sanaa Nchini Bibi Maryam Hamdan kikitoa burdani ya Maulidi ya Homu kwenye
uzinduzi wa Tamasha la 18 la Filam la Nchi za Jahazi Zanzibar { ZIFF } hapo Hoteli ya Double Tree
By Hilton Shangani Mjini Zanzibar. Picha na Hassan Issa –
OMPR
Mkurugenzi wa Tamasha la Filam la Nchi za Jahazi Zanzibar { ZIFF } Profesa Martin Mhando akitoa
neneo la makaribisho kwenye uzinduzi wa Tamasha hilo hapo shangani.
Picha na Hassan Issa – OMPR
Picha na Hassan Issa – OMPR
Meneja wa Taasisi ya Kimataifa inayosimamia kukuza vipaji vya wasanii
katika ukanda wa Afrika Mashariki { ZUKU } Bibi Maud Roger akiahidi taasisi
yake kuendelea kusaidia vipaji vya vijana katika utengenezaji wa filam zilizo
bora Nchini. Picha na Hassan Issa –
OMPR
Baadhi ya washirika wa Tamasha la Filam la Nchi za Jahazi Zanzibar { ZIFF } waliohudhuria uzinduzi wake
kutimia miaka 18 tokea kuasisiwa kwa Tamasha hilo hapa Nchini. Picha na Hassan Issa –
OMPR
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wa Pili kutoka Kushoto akiwa mgeni rasmi kwa
Niaba ya Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohammed Shein akijumuika pamoja na baadhi ya
viongozi kwenye uzinduzi wa Tamasha la 18 la Filam la Nchi za Jahazi Zanzibar
hapo Double Tree By Hilton Shangani Mjini Zanzibar. Kulia ya
Balozi Seif ni Waziri wa Habari, Utamduni, Utalii na Michezo Mh. Said Ali
Mbarouk, kushoto ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF Mh. Mahmoud Thabit
Kombo na msanii wa filam ya sarafina kutoka Nchini Afrika Kusini Laleta Kumalo. Picha na Hassan Issa –
OMPR
Mwenyekiti wa Bodi ya Tamasha la Filam la Nchi za Jahazi Zanzibar { ZIFF } Mahmoud Thabit Kombo akitoa
neno la kumkaribisha mgeni rasmi kulizindua Tamasha hilo hapo Double Tree By
Hilton Shangani. Picha na Hassan Issa –
OMPR
Msanii Mkongwe wa nyimbo kutoka Johannesburg Nchini Afrika Kusini Doroth Masuka akipongeza juhudi
zinazochukuliwa na Serikali pamoja na
washirika wake katika kuimarisha vipaji vya wasanii hapa Nchini. Picha na Hassan Issa –
OMPR
Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
Viongozi na washirika wa Tamasha la
Filam la Kimataifa la Nchi za Jahazi mara baada ya kulizindua Tamasha hilo kwa
niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein. Picha na Hassan Issa –
OMPR
Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
Viongozi na washirika wa Tamasha la
Filam la Kimataifa la Nchi za Jahazi mara baada ya kulizindua Tamasha hilo kwa
niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein. Kulia ya
Balozi sdEIF NI Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh, Said Ali
Mbarouk na Meneja wa Taasisi ya Kimataifa inayosimamia kukuza vipaji vya
wasanii katika ukanda wa Afrika Mashariki { ZUKU } Bibi Maud Roger. Kushoto ya
Balozi Seif ni Mwenyekiti wa Bodi ya Tamasha la Filam la Nchi za Jahazi Zanzibar { ZIFF } Mahmoud Thabit Kombo pamoja
na Msanii Maarufu Duniani aliyeigiza filam Maarufu ya Mchezo wa sarafina kutoka
Nchini Afrika Kusini Bibi Laleta Kumalo. Picha na Hassan Issa –
OMPR
Press Release:-
Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuunga mkono
juhudi zinazochukuliwa na Uongizi wa Tamasha la Kimataifa la Filam la Nchi
za Jahazi Zanzibar { ZIFF } katika azma
yake ya kuijengea nguvu tasnia ya Filam Nchini inayoonekana kusaidia ukuaji wa
uchumi kupitia sekta ya Utalii.
Kauli hiyo
imetolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dr.
Ali Mohammed Shein katika Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati
akilizindua Tamasha la 18 la Kimataifa la Filam la Nchi za Jahazi
Zanzibar { ZIFF } hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Double Tree By
Hilton Shangani Mjini Zanzibar.
Dr.
Shein alisema kwamba Tamasha la Nchi za
jahazi limekuwa na mchango mkubwa katika kuitangaza Zanzibar Kimataifa hali
ambayo imetoa ushawishi kwa wageni na watalii wengi kuamua kuvitembelea Visiwa
vya Zanzibar kujionea mazingira na rasilmali zilizopo.
Alisema kupitia
Tasnia ya filam zinazotayarishwa na wasanii mbali mbali kwa kushirikiana na
wadau wa Fani hiyo chini ya Wataalamu wa Ziff wageni na watalii mbali mbali
Duniani wamekuwa wakivutiwa na fukwe pamoja na Utamaduni uliojaa ukarimu wa Watu wa Visiwa vya
Zanzibar.
Rais wa
Zanzibar aliushauri Uongozi wa Tamasha la Kimataifa la Filam la Nchi za Jahazi
Zanzibar { ZIFF } kuendelea kufanya juhudi zaidi za kuwashawishi wasanii wa
Kimataifa kuzitumia Fukwe na Tamaduni za Zanzibar katika kutengeneza Filam mbali
mbali kwa lengo la kuitangaza zaidi Zanzibar Kimataifa.
“
Zanzibar ni Visiwa vya maumbile ya
Utamaduni ya Ukarimu pamoja na fukwe za kuvutia mambo ambayo yakitangazwa vyema
wasanii wa Kimataifa wanaweza kushawishika kuyatumia katika kutengeneza Filamu zao
“. Alifafanua Dr. Shein.
Alifahamisha
kwamba Tamasha la Kimataifa la Filam la Nchi za Jahazi, Tamasha la Iddi,
Tamasha la Mzanzibari pamoja na Sherehe
za Mwaka Kogwa zinazofanyika Makunduchi ni Mambo muhimu yanayopaswa kuimarishwa
katika kukuza na kusimamia Utamaduni na Historia ya Zanzibar na Watu wake.
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amewapongeza Wasanii wa Maigizo
pamoja na Filam Nchini kutokana na kazi
kubwa wanayoendelea kuifanya ya kuelimisha Jamii sambamba na kuwapatia Burdani.
Alisema
mbali ya Tasnia hiyo kutoa ajira pana kwa kundi kubwa hasa Vijana Nchini lakini
pia imepanua soko la filam za nyumbani na kuleta unafuu kwa kila mtu kumudu
kununua na kuangalia kazi za wasanii wa hapa Nchini hali iliyopelekea kufikia
asilimi 80% ya filamu za Kiswahili zinazoangaliwa tofauti na miaka iliyopita
nyuma.
Mapema
Meneja wa Taasisi ya Kimataifa inayosimamia kukuza vipaji vya wasanii katika
ukanda wa Afrika Mashariki { ZUKU } Bibi Maud Roger aliahidi kwamba Taasisi
yake itaendelea kukuza vipaji vya wasanii kwa lengo la kufikia kiwango
kinachokubalika Kimataifa.
Bibi Roger
alisema hatua hiyo muhimu itaweza kuwajengea uwezo wa kiajira badala ya
kusubiri kutegemea zile za Serikali ambazo kwa sasa upo upungufu mkubwa hata
katika Mataifa yaliyoendelea.
Meneja wa
Taasisi hiyo ya Zuku alifahamisha kwamba mpango maalum umeandaliwa na Uongozi
wa Taasisi hiyo baina ya miaka sita na kumi kwa kuwadhamini Vijana wapatao Kumi
wanaopata Mafunzo ya msingi kuweza kutengeneza Filam zitazokubalika Kimataifa.
Wakitoa
salamu zao kwenye uzinduzi wa Tamasha hilo la 18 la Kimataifa la Filam la Nchi
za Jahazi Msanii Gwiji Duniani kutoka
Nchini Afrika Kusini Laleta Kumalo aliyeigiza filam Maarufu ya sarafina pamoja na
Msanii Mkongwe wa Nchi Hiyo Doroth Masuka wameelezea faraja yao kutokana na
Serikali kupitia taasisi za kijamii zilivyojikita katika kusaidia vijana kwenye
fani ya sanaa.
Akimkaribisha
mgeni rasmi katika uzinduzi wa Tamasha la 18 la Ziff Mwenyekiti wa Bondi ya
Tamasha hilo Mahmoud Thabit Kombo alisema Ziff itaendelea kushirikiana na wadau
wote wa ndani na nje ya nchi katika kuona Taasisi hiyo muhimu inazidi
kuimarika.
Mahmoud
Thabit Kombo alisema uimarikaji huo utawapa nguvu na ari Vijana walioamua
kujiajiri kupitia Tasnia ya Filam inayoonekana kupata umaarufu siku hadi siku
hapa Duniani.
Uzinduzi wa
Tamasha hilo la 18 la Kimataifa la Filam la Nchi za Jahazi Zanzibar { ZIFF } limekwenda sambamba na siku yake
lililoasisiwa rasmi Tarehe 18 Julai Mwaka 1997 likitimiza umri wa miaka 18
sasa.