Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
akisalimiana na Madaktari wa Cuba wanaomaliza muda wao wa utumishi hapa
Zanzibar ambao aliwaandali chakula cha Jioni nyumbani kwake Mazizini nje kidogo
ya Mji wa Zanzibar. Picha Hassan Issa –
OMPR – ZNZ.
Balozi Seif akisalimiana na Mkuu wa Mafunzo wa Madaktari Wazalendo wa Zanzibar waliopata taaluma chini ya Madaktari Mabingwa wa Cuba Dr. Daisy Batlle kabla ya chakula cha jioni alichowaandalia Madaktari mabingwa wa Cuba. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
BaloziSeif akibadilishana mawazo na Kiongozi wa Madaktari wa Cuba Profesa Ulpiano hapo nyumbani kwake Mazizini nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Kiongozi wa Madaktari Mabingwa wa Cuba Profesa Ulpiano wa kwaza kutoka kulia akiwa pamoja na Mwenyeji wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakipata mlo kwenye hafla fupi waliyoandaliwa Madaktari hao. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Baadhi ya Madaktari Mabingwa wa Cuba wanaomaliza muda wao wa kazi hapa Zanzibar wakipata mlo wa jioni nyumbani kwake Balozi Seif Ali Iddi hapo Mazizini.Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Balozi Seif akimzawadia Kasha Kiongozi wa Madaktari wa Cuba Profesa Ulpiano mara baada yam lo wa jioni kama ishara ya kumbukumbu ya uwepo wao hapa Zanzibar. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Mkuu wa Mafunzo wa Madaktari Wazalendo wa Zanzibar waliopata Taaluma chini ya Madaktari Mabingwa wa Cuba Dr. Daisy Batlle akipokea zawadi kutoka kwa Balozi Seif. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Balozi Seif Ali Iddi kati kati ya waliokaa kwenye viti akiwa katika picha ya pamoja na Madaktari Mabingwa wa Cuba wanaomaliza muda wao wa kutoa huduma za Afya hapa Zanzibar. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.

Press Release:-
Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar imeipongeza Serikali ya Cuba kwa juhudi inayoendelea
kuchukuwa katika kuunga mkono harakati za maendeleo ya Kijamii ya Zanzibar hasa
katika Sekta ya huduma za Afya.
Pongezi hizo
zimetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika
hafla Maalum ya chakula cha Jioni aliyowaandalia Madaktari Mabingwa wa Cuba
wanaotoa huduma za Afya pamoja na kutoa mafunzo kwa Madaktari wazalendo wa
Zanzibar.
Hafla hiyo
iliyofanyika katika Makazi ya Balozi Seif yaliyopo Mazizini nje kidogo ya Mji
wa Zanzibar imetayarishwa ili kuwaaga rasmi Madaktari hao baada ya kukamilisha
muda wao wa kutoa huduma za Afya wa miaka miwili ambapo wanatarajiwa kurejea
nyumbani Cuba Mwezi Septemba Mwaka huu.
Balozi Seif
alisema kwamba huduma za afya zilizokuwa zikitolewa na Madaktari Mabingwa hao
wa Cuba zimeweza kuleta faraja kubwa kwa Wananchi walio wengi hapa Zanzibar.
Alieleza
kuwa yapo mafanikio makubwa yaliyopatikana kutokana na uimarishwaji wa mfumo wa
huduma za afya uliopekelea kuongezeka kwa Madaktari wazalendo Nchini kasi
ambayo imekwenda sambamba na ile azma ya Serikali ya kulenga kuwa na huduma za
Afya katika maeneo yasiyozidi kilomita Tano.
Balozi Seif
alisisitiza kwamba bado Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inahitaji kuongeza
nguvu zaidi katika Sekta hiyo muhimu kwa ustawi wa Jamii ili kufikia kiwango
bora cha utoaji wa huduma za afya kilichowekwa na shirika la Afya Duniani { WHO
}.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliwatakia maisha ya furaha na
upendo Madaktari hao wa Jamuhuri ya Cuba wakati watakaporejea Nyumbani kwao
mnamo Mwezi Septemba mwaka huu wa 2015.
Katika hafla
hiyo fupi ya chakula cha jioni Balozi Seif aliwazawadia Madaktari hao Makasha
Maalum kama ishara ya ukumbusho wao wakati walipokuwepo hapa Zanzibar wakitoa
huduma za Afya pamoja na kutoa mafunzo kwa Madaktari Wazalendo.
Akitoa
shukrani kwa niaba wenzake Kiongozi wa Madaktari hao Profesa Ulpiano alisema
wakati wa utumishi wao hapa Zanzibar walilazimika kufanya kazi kwa juhudi,
bidii na maarifa kutokana na ukarimu walioupokea kutoka kwa Wananchi wa
Zanzibar.
Profesa
Ulpiano alisema kwamba Madaktari hao wa Cuba wataendelea kukumbuka maisha ya
Zanzibar ambayo yaliwapa fursa ya kujihisi kwamba wanaishi katika maisha ya
kifamilia kama wapo Nyumbani kwao Cuba.
Zanzibar
imekuwa na uhusiano wa muda mrefu na Nchi za Jamuhuri ya Cuba pamoja na Jamuhuri ya Watu wa
China ambapo Mataifa hayo mawili yamekuwa yakiendeleza ushirikiano huo na
Zanzibar kwa kusaidia kitaaluma huduma za Afya hapa Zanzibar tokea miaka ya 60
mara baada ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964.