Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi

Mwanafunzi Isra Hilal Mwadini akifuatiwa na mwenzake Tamima Abass Sheha wakipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wakati wa hafla ya Maulidi ya Jumuiya ya Chuo cha Samael Academy.Kulia ya Balozi Seif ni Rais wa Sameil Academy Sheikh Nassir Bin Said.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizindua rasmi Bara bara ya pili ya Amani hadi Mtoni baada ya kukamilika awamu ya mwisho ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Akiwa na Balozi mdogo wa India nchini Tanzania wakiangalia maonyesho yaliofanya na Msanii kutoka India, Bi Navi Madhav hapo Ngome Kongwe

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Dk. Khalid S. Mohamed

akizungumza na Wadau wa Maendeleo wa Mfuko wa TASAF, walipofika Ofisini kwake kuzungumzia maendeleo ya Mfuko wa TASAF III,na kutembelea Mradi wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini (PSSN) katika Jimbo la Muyuni Wilaya ya Kusini Unguja katika Kijiji cha Muyuni B

Wazir wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakifurahia jambo wakati wa semina ya siku moja kuhusu matokeo makubwa na ya haraka katika kuleta mageuzi ya kiuchumi na kuleta maendeleo nchini iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein

Wednesday, 27 August 2014

Kampuni ya Mitandao ya simu za Mkononi ya Tigo imejitolea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar


 Makamu wa Rais wa Kampuni ya Tigo yenye makao Makuu yake Nchini Sweeden Bwana Arthur Basting akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake Jengo la Msekwa ndani ya Viunga vya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma.
  Makamu wa Rais wa Kampuni ya Tigo Bwana Arthur Basting akimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif nia ya Kampuni hiyo ya kutaka kushirikiana na SMZ Katika miradi ya mitandao ya mawasiliano.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Kampuni ya Tigo aliokutana nao kwenye ofisi yake iliyop[o jengo la Msekwa ndani ya Bunge la Jamuhuri ya Muungano Mjini Dodoma.

press release
Kampuni ya Mitandao ya simu za Mkononi ya Tigo imejitolea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye sekta ya uwekezaji katika masuala ya mitandao ya mawasiliano sambamba na kusaidia huduma za Kijamii kwa wananchi wa Visiwa vya Unguja na Pemba.
Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo yenye Makao Makuu yake Mjini Stokholmes Nchini Sweeden Bwana Arthur Basting alieleza hayo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake katika Jengo la Msekwa ndani ya Viunga vya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma.
Bwana Arthur Basting ambae anasimamia Kampuni Tigo Barani Afrika alisema Uongozi wa Taasisi hiyo imejikita kutoa ushirikiano huo ikizingatia zaidi umuhimu wa mawasiliano ya Teknolojia yaliopo hivi sasa Ulimwenguni kote.
Bwana Arthur alisema Uongozi wa Kampuni ya Tigo unafurahia kuona kwamba Teknolojia ya Mawasiliano kupitia simu za Mikononi hivi sasa imeenea na kupokelewa vyema na wananchi wa Bara la Afrika.
Alisema kutokana na hatua hiyo Uongozi wa Taasisi hiyo umefikiria kuongeza kuhuduma zake mara dufu ndani ya Bara la Afrika ili kuona sekta ya  mawasiliano inaendelea kutoa huduma katika masuala ya kijamii na uchumi.
Bwana Arthur alifahamisha kwamba  mfumo ulioanzishwa na Kampuni hiyo wa huduma za kusafirisha fedha kupitia mtandao wa Simu za Kiganjani umeleta faraja kwa watu mbali mbali ukionyesha mafanikio makubwa ya kupunguka kwa unyang’anyi na wizi wa fedha baina ya watu au hata taasisi.
Naye Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya Tigo Hapa Tanzania Bibi Sylvia Balwire alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwamba Kampuni hiyo tayari imeanza mipango maalum ya kusaidia huduma za Kijamii katika maeneo mbali mbali hapa Nchini.
Bibi Sylvia alisema Wataalamu wa Tigo hivi sasa wako katika hatua za mwisho kukamilisha mipango ya kusaidia uendelezaji wa mradi wa kilimo cha Mwani Kisiwani Pemba.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliuomba Uongozi wa Kampuni ya Tigo kushirikiana na Kampuni ya Zantel katika kuona huduma za mitandao ya mawasiliano inazidi kuimarika.
Balozi Seif aliueleza Ujumbe wa Kampuni hiyo kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itakuwa tayari wakati wowote kutoa ushirikiano wa karibu ili kuongeza nguvu zitakazoiwezesha Kampuni hiyo kutekeleza malengo iliyojipangia.
Hata hivyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliusharui Uongozi huo kuongeza nguvu zake zaidi katika kusaidia miradi ya Kijamii ambayo bado inaonekana haijawa na nguvu za kujiendesha yenyewe.
 “ Hadi wakati huu tunaozungumza zipo skuli zetu nyingi hazijawa na vikalio, huduma za maabara na Maktaba, hata vifaa katika vituo vyetu vya Afya. Uwepo wenu kama wawekezaji unaweza pia kuyaangalia maeneo hayo muhimu kwa ustawi wa Jamii yetu “. Alisema Balozi Seif.
Balozi Seif alitoa mifano ya miradi hiyo ambayo inaweza kuongezewa nguvu na Kampuni hiyo ya Tigo kuwa ni pamoja na huduma za afya, Kilimo pamoja na Elimu.

Tuesday, 26 August 2014

Rais Kikwete Atembelea Chuo Kikuu cha Mzumbe, Morogoro.




 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua jengo la mihadhara la Chuo Kikuu cha Mzumbe Morogoro akisaidiwa na uongozi wa chuo hicho alipotembelea hapo na kuzindua ukumbi wa huo jengo la wahadhiri chuoni hapo

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi ya picha yake ya kuchorwa wakati alipotembelea Chuo Kikuu cha mzumbe ambapo walihutubia wanafunzi, wahadhiri na wananchi katika chuo hicho baada ya kuzindua ukumbi wa mihadhara na jengo la wahadhiri chuoni hapo

Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Morogoro wakiweka kumbumbuku ujio wa Rais Kikwete alipotembelea hapo na kuzindua ukumbi wa huo jengo la wahadhiri chuoni hapo 

Meza kuu ikifurahia jambo wakati Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa Mvomero Mhe Amos Makalla akipohutubia wanafunzi, wahadhiri na wananchi katika chuo hicho wakati Rais Kikwete alipotembelea na kuzindua ukumbi wa mihadhara na jengo la wahadhiri chuoni hapo 

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea risala toka kwa Rais wa Serikali ya Wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Mzumbe Mhe Boniface Maiga wakati Rais Kikwete alipotembelea na kuzindua ukumbi wa mihadhara na jengo la wahadhiri chuoni hapo

 Rais wa Serikali ya Wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Mzumbe Mhe Boniface Maiga akisoma risala wakati Rais Kikwete alipotembelea na kuzindua ukumbi wa mihadhara na jengo la wahadhiri chuoni hapo


:Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa serikali ya wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Mzumbe mjini Morogoro baada ya kuwahutubia chuoni hapo 
 Umati wa wanafunzi, wahadhiri na wananchi wakimsikiliza Rais Kikwete akiwahutubia alipotembelea hapo na kuzindua ukumbi wa huo jengo la wahadhiri chuoni hapo(Picha na Ikulu)

Monday, 25 August 2014

Dk Shein awaapisha mawaziri na wakuu wa mikoa Ikulu leo

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Dk.Sira Ubwa  Mamboya kuwa Waziri wa Kilimo na Maliasili katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar kabla Dk.Sira alikuwa Naibu Waziri wa Afya.{Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Juma Duni Haji  kuwa Waziri wa  Miundombinu na Mawasiliano katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar kabla alikuwa  Waziri wa Afya.{Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Rashid   Seif Suleiman kuwa Waziri wa Afya,awali alikuwa Waziri wa   Miundombinu na Mawasiliano hafla ya kiapo imefanyika katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo.{Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Mahmoud Thabit Kombo  kuwa Naibu Waziri wa Afya,  hafla ya kiapo imefanyika katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo.{Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Meja mstaafu Juma Kassim Tindwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja,katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar kabla alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba,(Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw.Omar Khamis Othman kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini  Pemba katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo ,  (Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Mwanajuma Majid Abdulla kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo ,kabla alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Pemba, (Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]



 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw.Ayoub Mohamed Mahmoud kuwa Mkuu wa Wilaya Magharibi  leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,awali alikua Afisa Tawala katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini magharibi Unguja, (Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bibi Hanuna Masoud Ibrahim kuwa Mkuu wa Wilaya ya  Chake chake Pemba leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar, (Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]

Friday, 22 August 2014

Balozi Seif akutana na Uongozi wa Wanafunzi wa Wanaosoma Korea.


Uongozi wa Jumuiya Watanzania wanaosoma Nchini Korea ya Kusini { KOIKA } ukiongozwa na Rais wake Nd. Steven Katemba ukijitambulisha rasmi kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Nyumbani kwake Mazizini Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar mara baada ya kucgauliwa rasmi mwezi Mei Mwaka huu.Nyuma ya Ndugu Steven ni Makamu wa Rais wa Jumuiya hiyo kwa upande wa Zanzibar NduguBukheit Juma.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kati kati akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Jumuiya ya Watanzania wanaosoma Nchini Korea ya Kusini { KOIKA } uliofika nyumbani kwake kujitambulisha rasmi baada ya kushika wadhifa huo.Kushoito ya Balozi Seif ni Rais wa Jumuiya hiyo ya KOIKA Nd. Steven Katemba na Makamu wa Rais wake Nd. Bukheit Juma.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.


Jumuiya ya Wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma Nchini Korea ya Kusini { KOIKA } imejipanga kuwa kiunganishi kizuri cha wanataaluma wa Korea ya Kusini na wale wa Kitanzania kwa lengo la kudumisha uhusiano uliopo kati ya nchi mbili hizo.

Rais wa KOIKA  aliyekuwa kinara wa Ujumbe wa Viongozi Wanne wa Jumuiya  hiyo Ndugu Steven Katemba alieleza hayo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Nyumbani kwake Mazizini Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Nd. Steven na ujumbe wake ambao wapo Nchini Tanzania kujitambulisha rasmi baada ya kuchaguliwa kwao kushika dhamana hiyo ya Uongozi wa Jumuiya mnamo Mwezi Mei mwaka huu alisema zipo fursa nyingi za kimasomo na uhusiano Nchini Korea Kusini ambazo Vijana wa Kitanzania wanaweza kuzichangamkia.

Alieleza kwamba Korea ya Kusini iliyopo Bara la Asia ni miongoni mwa Nchi chache za Bara hilo ziliyopiga hatua kubwa za maendeleo na kiuchumi kiasi kwamba Tanzania inaweza kujifunza kupitia maendeleo hayo.

Alisema Jumuiya yao mbali ya kuanzishwa kwa lengo la kusaidiana kupambana na matatizo yanayowakabili katika mafunzo yao lakini pia imejipanga kushiriki katika shughuli za Kijamii hapa Tanzania.

Rais huyo wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma Nchini Korea ya Kusini alifahamisha kwamba wanachama wa jumuiya hiyo tayari wameshajipanga kufanya kazi za Kijamii hivi karfibuni katika Nyumba za Wazee ziliopo Mtaa wa Sebleni Mjini Zanzibar.


Alisema kazi hizo zitakuwa ni pamoja na kufanya usafi utakaoambatana na kubadilishana mawazo na wazee hao  ambao tayari wameshatumia muda wao mwingi wa maisha katika Kujenga Taifa la Tanzania.
Akitoa Shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliipongeza Jumuiya hiyo ya Wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma Nchini Korea Kusini kwa uamuzi wao wa kuunda Jumuiya itakayowasaidia kukabiliana na changa moto zozote zitakazojitokeza mbele yao.

Balozi Seif alisema kitendo cha vijana hao kuamua kujishirikisha katika shughuli za Kijamii kinaweza kuamsha ari na chachu kwa vijana wengine nchini na hata wale wanaosoma mataifa wengine kuunda vikundi kama hivyo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliueleza Uongozi wa Jumuiya hiyo ya Koika kwamba uhusiano uliopo kati ya Korea ya Kusini na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ni mkubwa na Vijana hao wana haki na wajibu wa kusaidia kuudumisha uhusiano huo muhimu kwa ustawi wa pande zote mbili.

Zaidi ya Wanafunzi mia Tisa na Kumi wa Kitanzania wanasoma Nchini Korea ya Kusini ambao kati ya hao Mia Moja na Mbili wanatoka Visiwani Zanzibar.

Rais Kikwete aweka jiwe la msingi na kufungua Kituo cha Afya Kibaoni Morogoro.Vijijini.



  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria kufungua kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mama Salma Kikwete pamoja na Wabunge Mhe Abdul Mketeme (kushoto) na Mhe Getrude Rwakatale (kulia) wakifunua pazia kwa pamoja kuashiria kufungua kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea akikagua wodi mpya ya  kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa maeneo mbali mbali ya kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini baada ya kukifungua
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wazazi baada ya kufungua kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini
 Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa  kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini, baada ya kukifungua kituo hicho cha Afya kutowa huduma kwa Wananchi wa kijiji hicho.(Picha na Ikulu)

Thursday, 21 August 2014

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amekutana kwa mazungumzo na Ujumbe wa Wataalamu wa Ujenzi, Miundo mbinu pamoja na usanifu Miji ya Kisasa wa Taasisi ya Ushauri wa Uhandisi { ECG } Kutoka Nchini Misri.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Ujumbe wa Viongozi wawili wa Taasisi ya Kimataifa ya ushauri wa Uhandisi wa Ujenzi kutoka Nchini Misri ukiongozwa na Makamu Mwenyekiti wake Mhandishi Amr Alouba hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. (Picha na Hassan Issa wa -OMPR - ZNZ)


























Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya ushauri wa Uhandisi wa Ujenzi kutoka Nchini Misri Mhandisi Amr Alouba akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi baada ya kutembelea baadhi ya maeneo ya uwekezaji vitega uchumi hapa Zanzibar.( Picha na Hassan Issa wa OMPR ZNZ)



Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amekutana kwa mazungumzo na Ujumbe wa Wataalamu wa Ujenzi, Miundo mbinu pamoja na usanifu Miji ya Kisasa wa Taasisi ya Ushauri wa Uhandisi { ECG } Kutoka Nchini Misri.
Ujumbe huo unaoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi hiyo Mhandisi Amr Alouba upo Nchini  kuangalia maeneo ambayo unaweza kushirikiana na Zanzibar katika Sekta ya Uwekezaji.
Katika mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisi ya  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Vuga Mjini Zanzibar  Kiongozi wa Ujumbe huo Mhandisi Amr Aloub alisemaTaasisi hiyo imeamua kuelekeza nguvu zake ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki ili kusaidia miundombinu ya kuinua uchumi wa Mataifa hayo.
Mhandisi Amr alifahamisha kwamba Taasisi yake yenye kushughulikia ujenzi wa viwanja vya ndege, miji ya kisasa, vituo vya Kimataifa vya pamoja na usarifu wa majengo ya kibiashara imeshaamua kushirikiana na Zanzibar katika sekta hizo muhimu kwa uchumi wa Taifa.
Bwana Amr Alouba na Ujumbe wake ambae tayari ameshatembea maeneo Huru yaliyotengwa na Serikali pamoja na Mtaa uliotengwa Kibiashara wa Gulioni,kuelekea Kariakoo hadi Michezani { High Street } alisema Zanzibar imebarikiwa kuwa na maeneo mazuri kiuwekezaji jambo ambalo Kampuni yake imeridhina nayo.
Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliupongeza Ujumbe huo kwa uwamuzi wake wa kutaka kuwekeza vitega uchumi vyake kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Balozi Seif alisema Zanzibar hivi sasa inahitaji kuimarisha uchumi wake kupitia sekta ya Viwanda, Uvuvi pamoja na maeneo mengine jambo ambalo Kampuni hiyo inaweza kuwa mshirika mkuu katika uimarishaji wa sekta hizo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliueleza Ujumbe huo kwamba uanzishwaji wa viwanda vya kusindika samaki pamoja na utalii ulenga kusaidia kuongeza kasi ya uzalishaji uchumi sambamba na upatikanaji wa ajira kwa vijana.
Taasisi hiyo ya ushauri ya Uhandisi kutoka Nchini Misri Tayari imeshajenga Vituo Sita vya Kimataifa vya Kibiashara katika Nchi mbali mbali kama vile Qatar, Kuweit na wenyeji Misri, Sudan, Kenya pamoja na Tanzania Bara.
Mhandisi Amr Aloub amekuwa mshauri muelekezi aliyesimamia kujengwa kwa Kijiji cha Kibiashara cha Kimataifa  kilichopo katika Mtaa wa Kadizani  kwenye Mji wa Cairo Nchini Misri.