Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Ujumbe wa Viongozi wawili wa Taasisi ya Kimataifa ya ushauri wa Uhandisi wa Ujenzi kutoka Nchini Misri ukiongozwa na Makamu Mwenyekiti wake Mhandishi Amr Alouba hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. (Picha na Hassan Issa wa -OMPR - ZNZ)
Makamu
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya ushauri wa Uhandisi wa Ujenzi kutoka
Nchini Misri Mhandisi Amr Alouba akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi baada ya kutembelea baadhi ya maeneo ya uwekezaji
vitega uchumi hapa Zanzibar.( Picha na Hassan Issa wa OMPR ZNZ)
Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amekutana kwa mazungumzo na Ujumbe wa Wataalamu
wa Ujenzi, Miundo mbinu pamoja na usanifu Miji ya Kisasa wa Taasisi ya Ushauri
wa Uhandisi { ECG } Kutoka Nchini Misri.
Ujumbe huo unaoongozwa na
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi hiyo Mhandisi Amr Alouba
upo Nchini kuangalia maeneo ambayo unaweza kushirikiana na Zanzibar
katika Sekta ya Uwekezaji.
Katika mazungumzo yao
yaliyofanyika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
Vuga Mjini Zanzibar Kiongozi wa Ujumbe huo Mhandisi Amr Aloub
alisemaTaasisi hiyo imeamua kuelekeza nguvu zake ndani ya ukanda wa Afrika
Mashariki ili kusaidia miundombinu ya kuinua uchumi wa Mataifa hayo.
Mhandisi Amr alifahamisha
kwamba Taasisi yake yenye kushughulikia ujenzi wa viwanja vya ndege, miji ya
kisasa, vituo vya Kimataifa vya pamoja na usarifu wa majengo ya kibiashara
imeshaamua kushirikiana na Zanzibar katika sekta hizo muhimu kwa uchumi wa
Taifa.
Bwana Amr Alouba na Ujumbe
wake ambae tayari ameshatembea maeneo Huru yaliyotengwa na Serikali pamoja na
Mtaa uliotengwa Kibiashara wa Gulioni,kuelekea Kariakoo hadi Michezani { High
Street } alisema Zanzibar imebarikiwa kuwa na maeneo mazuri kiuwekezaji jambo
ambalo Kampuni yake imeridhina nayo.
Naye Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliupongeza Ujumbe huo kwa uwamuzi wake
wa kutaka kuwekeza vitega uchumi vyake kwa kushirikiana na Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
Balozi Seif alisema
Zanzibar hivi sasa inahitaji kuimarisha uchumi wake kupitia sekta ya Viwanda,
Uvuvi pamoja na maeneo mengine jambo ambalo Kampuni hiyo inaweza kuwa mshirika
mkuu katika uimarishaji wa sekta hizo.
Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar aliueleza Ujumbe huo kwamba uanzishwaji wa viwanda vya kusindika
samaki pamoja na utalii ulenga kusaidia kuongeza kasi ya uzalishaji uchumi
sambamba na upatikanaji wa ajira kwa vijana.
Taasisi hiyo ya ushauri ya
Uhandisi kutoka Nchini Misri Tayari imeshajenga Vituo Sita vya Kimataifa vya
Kibiashara katika Nchi mbali mbali kama vile Qatar, Kuweit na wenyeji Misri,
Sudan, Kenya pamoja na Tanzania Bara.
Mhandisi Amr Aloub amekuwa
mshauri muelekezi aliyesimamia kujengwa kwa Kijiji cha Kibiashara cha
Kimataifa kilichopo katika Mtaa wa Kadizani kwenye Mji wa Cairo
Nchini Misri.