Wednesday, 20 August 2014

Ufunguzi wa Michezo ya Majeshi ya Afrika Mashariki Uwanja wa Amaan Zanzibar


.Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa na Mawaziri wa Ulinzi wa Nchi zao na Majenerali wa Majeshi wa Nchi washiriki wa michuzo ya majeshi Tanzania.
Bendera za Nchi Washiriki katika Michezo ya Majeshi ya 8 yaliofunguliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akimuwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein.  
Wasanii wa Bendi ya Muziki ya Jeshi la Wananchi Tanzania wakitowa burudani katika uwanja wa Amaan wakati wa ufunguzi wa Michezo ya Majeshi Tanzania yaliofanyika katika uwanja 
Wananchi wakifuatlia ufunguzi wa Michezo ya Majeshi wa Nchi za Afrika Mashariki katika viwanja wa Amaan Zanzibar.
Wanamichezo wa Michezo ya Majeshi wakishangilia wakati wa Ufunguzi wa michezo hiyo iliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar BaloziSeif Ali Iddi, akipokelewa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange alipowasili katika viwanja vya Amaan kumuwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wac Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,akipokea Bwaride la Vikosi vya Ulinzi washiriki wa Michuano ya 8 ya Michezo ya Majeshi ya Afrika Mashariki yaliofanyika katika uwanja wa Amaan Zanzibar. 

Wakuu wa Majeshi kutoka Nchi washiriki wa Michezo ya Majeshi ya Afrika Mashariki wakipokea heshima ya Wanamichezo waliokuwa wakipita mbele ya Mgeni rasmin wa ufunguzi wa michezo hiyo.












Wanajeshi na Wananchi wakiwa katika uwanja wa Amaan wakihudhuria ufunguzi wa michezo ya 8 ya Majeshi wa Afrika Mashari yaliofanyika katika uwanja wa Amaan Zanzibar.
Mawaziri wa Ulinzi wa Nchi za Afrika Mashiriki wakihudhuria michezo ya 8 ya Majeshi yaliofunguliwa leo katika viwanja vya Amaan Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akiwahutubia Wanamichezo wa Michezo ya Majeshi wa Nchi za Afrika Mashariki, akimuwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, ufunguzi huo umefanyika katika viwanja vya Amaan Zanzibar.  

Waziri wa Ulinzi Tanzania Mhe. Hussein Mwinyi akihutubia na kutowa Salami kwa Washiriki wa Michezo ya Majeshi wakati wa Ufunguzi wake uliofanyika leo katika uwanja wa Amaan Zanzibar.

Mkuu wa Mjeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange,mwenyeji wa Michezo ya Majeshi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Michezo ya Majesho wa Nchi za Afrika Mashiriki yaliofunguliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif AliIddi, akimuwakilisha Rais wa Zanzibar Dkt. Shein. 
Wanafunzi wa Skuli ya Bilal Muslim wakiwa katika viwanja vya Amaan wakishuhudia Ufunguzi wa michezo ya Majeshi Tanzania.

Wanajeshi wakicheza Ngoma na kutowa burudani wakati wa sherehe za ufunguzi wa michezo ya Majeshi Tanzania.