Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi Seti za
Jezi na Mipira Mmoja wa Viongozi wa timu 60 zilizomo ndani ya Jimbo la Kitope
hapo Kijiji cha Kipandoni Upenja Wilaya ya Kaskazini “B”.Aliyepo kati
kati yao ni Mke wa Balozi Seif Mama Asha Suleiman Iddi. Picha Hassan Issa –
OMPR
Baadhi ya Timu za Mitaa zilizomo ndani ya Jimbo la Kitope zilizopata vifaa
vya Michezo vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo hilo Balozi Seif Ali Iddi. Picha Hassan Issa –
OMPRKocha na Kepteni wa Timu ya Soka ya Kipandoni Star Jeilan Omar Jeilan akipokea mchango wa shilingi 500,000/- kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi kwa ajili ya kununulia Posi na Nyafu kwa ajili ya Kwinja chao cha michezo. Picha Hassan Issa – OMPR
Press Release:-
Mbunge wa
Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi leo amekabidhi vifaa vya michezo kwa Timu 60 za Mpira wa soka zilizomo ndani ya
Jimbo hilo ili kusaidia nguvu na chachu ya kuimarisha Michezo katika Jimbo la
Kitope.
Vifaa hivyo
ambavyo ni seti za Jezi na Mipira vyenye Thamani ya shilingi Milioni Nane, Laki
Nne na Hamsini Elfu { 8,450,000/- }
vimekabidhiwa kwa timu hizo hapo Kipandoni Wadi ya Upenja Wilaya ya
Kaskazini “B”.
Balozi Seif
akiambatana na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi pamoja na baadhi ya Viongozi wa
Wadi ya Upenja na Jimbo la Kitope akikabidhi Seti za Jezi na Mipira kwa Timu za
Jimbo hilo zinazoshiriki Ligi ya Kanda ya Unguja,Daraja la Pili na daraja la
Tatu.
Na pia
akakabidhi mipira kwa 36 ya Mitaani pamoja na timu mbili za watoto wadogo
wa Kijiji cha Kipandoni na kuahidi
kuonyesha nia ya kusaidia kuwatengenezea Kiwanja watakachokichaguwa ili kiwe na
hadhi ya michezo ya Kitaifa ndani ya
Wilaya ya Kaskazini “B”.
Akizungumza
na Wanamichezo hao Mbunge huyo wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi aliwataka Vijana hao kujiepusha na makundi ya
baadhi ya watu wanaojaribu kuwashawishi wajiingize katika mambo yaliyo nje ya
Sekta ya Michezo.
Balozi Seif
alisema ni vyema kwa vijana hao wakaendelea kuwaamini Viongozi waliokubali
kuwatumikia katika mambo na harakati zao za kila siku hasa zile za michezo
ambazo kwa sasa husaidia kutoa ajira.
Aliwataka
wanamichezo hao kupitia Viongozi wao waangalie utaratibu wa kutafuta kiwanja kitakachowekewa
miundo mbinu ambayo baadaye kitakidhi mahitaji ya kuchezewa Ligi yenye hadhi ya
Kitaifa.
Mapema Mke
wa Mbunge huyo wa Jimbo la Kitope Mama Asha Suleiman Iddi alisema katika kuunga
mkono juhudi za wanamichezo hao alisema ni vyema kwa wanasoka hao wanzishe
utaratibu wa kuanza kuchangia hata kwa kiwango kidogo ili kuwapa nguvu Viongozi
na wafadhili wanaoonyesha nia ya kuwasaidia.
Mama Asha
alisema Viongozi wa Jimbo hilo watashawishika na kuongeza nguvu zao kwa Timu
ambazo tayari zimeshajikubalisha
kujisaidia zenyewe zikisubiri nguvu za ziada.
Mapema
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar Wilaya ya Kaskazini “ B” Tongoa
Moh’d Hassan alisema Wilaya hiyo bado inakabiliwa na changamoto kubwa ya
ukosefu wa Kiwanja cha soka chenye hadhi inayokubalika kwa michezo mikubwa.