Gwiji la Taarab asilia enzi zilee Msanii Khamis Juma akiwa
miongoni mwa wabunifu na wasanii
maalum wanne mwaka huu akikonga nyoyo za
washiriki wa hafla ya ugawaji wa Mirabaha kwa wabunifu na wasanii Zanzibar
zilizofanyika katika Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Zanzibar. Picha Hassan Issa –
OMPR – ZNZ.
Mwenyekiti wa Kamati ya ugawaji Mirabaha ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Mh. Salim Nassor Ali –Jazeera akimkabidhi ngao mchangiaji bora wa kusaidia sherehe hizo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Mahadhi Juma Maalim. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Mh. Salim Nassor – Jazeera akimkabidhi ngao msaidizi wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Ustaadhi Suleiman Haji Suleiman akipokea kwa niaba ya Mhe. Balozi Seif ambae Ofisi yake imegharamia sherehe hizo. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Al - Anisa Mwapombe Hiari tetere wa nyimbo za Taarabu aliyevuma ndani ya mwambao wa Afrika katika miaka ile akifurahia zawadi ya ngao na fedha taslim alizokabidhiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif baada ya kuwa miongoni mwa wabunifu na wasanii wanne maalum katika sherehe za ugawaji wa Mirabaha Zanzibar. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Msanii wa Kizazi kipya Baby Jay akipokea zawadi kutoka kwa Balozi
Seif kwenye sherehe ya ugawaji wa Mirabaha hapo Salama Bwawani Mjini Zanzibar. Picha Hassan Issa –
OMPR – ZNZ.
Berry Black Kijana wa Muziki wa Kizazi kipya akichekelea na kufurahia zawadi aliyokabidhiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwenye sherehe ya ugawaji wa Mirabaha hapo Salama Bwawani Mjini Zanzibar. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Mwenyekiti wa Kamati ya ugawaji Mirabaha ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Mh. Salim Nassor Ali –Jazeera akimkabidhi ngao mchangiaji bora wa kusaidia sherehe hizo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Mahadhi Juma Maalim. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Mh. Salim Nassor – Jazeera akimkabidhi ngao msaidizi wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Ustaadhi Suleiman Haji Suleiman akipokea kwa niaba ya Mhe. Balozi Seif ambae Ofisi yake imegharamia sherehe hizo. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliyepo kati kati akimkabidhi ngao Msanii
Khamis Juma baada ya kufuzu kuwa miongoni mwa wabunifu na wasanii wanne maalum
katika sherehe za ugawaji wa Mirabaha Zanzibar. Wa kwanza
kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Mheshimiwa Aboubakar Khamis
Bakari. Picha Hassan Issa –
OMPR – ZNZ.
Al - Anisa Mwapombe Hiari tetere wa nyimbo za Taarabu aliyevuma ndani ya mwambao wa Afrika katika miaka ile akifurahia zawadi ya ngao na fedha taslim alizokabidhiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif baada ya kuwa miongoni mwa wabunifu na wasanii wanne maalum katika sherehe za ugawaji wa Mirabaha Zanzibar. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Berry Black Kijana wa Muziki wa Kizazi kipya akichekelea na kufurahia zawadi aliyokabidhiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwenye sherehe ya ugawaji wa Mirabaha hapo Salama Bwawani Mjini Zanzibar. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Balozi Seif akiwa katika
picha ya pamoja na Viongozi wa Kamati
ya ugawaji Mirabaha pamoja na washindi mbali mbali wa tuzo za wabunifu na
wasanii bora kwa mwaka huu mara baada ya kukamilika jkwa sherehe hizo hapo
Ukumbi wa Salama Hoteli ya Bwawani Mjini
Zanzibar. Kushoto ya
Balozi Seif ni Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Mh. Aboubakar Khamis,Msanii
Khamis Juma, Msanii Mwapombe Hiari na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Mahmoud
Thabit Kombo.
Kulia ya
Balozi Seif ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Said Ali
M,barouk, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mh. Abdullah Mwinyi, Mjumbe wa Kamati
ya Ugawaji Mirabaha Mh. WEanu Hafidh Ameir pamoja na Mchangiaji bora wa
mashindano hayo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Kimataifa wa
Tanzania Mh. Mahadh Juma Maalim. Picha Hassan Issa –
OMPR – ZNZ.
Press Release:-
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alionya kwamba wananchi
wanalazimika kujenga utamaduni wa kuthamini kazi za wabunifu na wasanii kwa
kuona fahari kuzilipia bila ya shuruti pale wanapozitumia jambo ambalo ni
uungwana na kinyume chake inahesabika kuwa ni wizi.
Alisema
Serikali kupitia Ofisi ya Hakimiliki, Bodi ya Hakimiliki na Jumuiya ya
Hakimiliki Zanzibar { COSOZA }
itaendelea kusimamia kazi za wabunifu na wasanii ili kuona kuwa maslahi, nguvu
na jasho lao halipotei bure kutokana na ulaghai unaoendelea kufanywa na watu wanaozipora kazi zao.
Balozi Seif
Ali Iddi alitoa onyo hilo wakati wa hafla ya ugawaji wa Mirabaha kwa Wabunifu
na wasanii Zanzibar zilizofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Salama Bwawani
Mjini Zanzibar.
Alisema
Serikali itaendelea kuchukuwa hatua za kisheria za kuwadhibiti wezi hao
wasiojali jasho la wenzao, lakini kazi hiyo inaweza kufanikiwa kwa ufanisi zaidi endapo wabunifu na wasanii
wenyewe watatoa ushirikiano kwa taasisi zinazosimamia maslahi yao katika
kudhibiti wizi wa kazi zao.
“
Tushirikiane katika kuwasaka, kuwabaini na kuwaripoti katika vyombo
vinavyohusika wale wote watakaobainika wanatumia kazi zenu kinyume na sheria na
taratibu zilizowekwa “. Alisema Balozi Seif.
Alifahamisha
kwamba Serikali haipendi kuwabughudhi wananchi wake katika biashara hata kidogo
lakini hulazimika kuchukuwa hatua za kisheria mara moja pale ambapo uvunjaji wa
sheria unapobainika ili haki ipatikane
kutokana na sheria inavyochukuwa mkondo wake.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar aliwazindua
wabunifu na wasanii kuwa wanapoingia kwenye mikataba pamoja na watumiaji wa kazi zao wahakikishe kwamba
makubaliano yao yanakuwa halali yanayozingatia misingi ya hakimiliki katika
biashara zao.
Balozi Seif aliwataka
wabunifu na wasanii wale na tahadhari wakati
wa kuweka saini Mikataba, wanakuwa na makubaliano na maelewano ya kweli ili
kuwepuka mizozo baina yao na wale wanaotiliana nao saini mikataba hiyo.
Balozi Seif
aliwasihi wamiliki wa vituo vya utangazaji kuheshimu haki na kazi za wabunifu na wasanii wakielewa
kwamba vituo vyao vinategemea kwa kiasi kikubwa kazi hizo.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar ameishukuru na kuipongeza Ofisi ya Msajili wa
Hakimiliki kwa kusimamia vyema ukusanyaji na ugawaji wa Mirabaha na kuitaka
iendelee na utaratibu huo kwa kila mwaka.
Balozi Seif
aliiomba Ofisi hiyo kuandaa mpango maalum kwa wabunifu wa michoro mbali mbali
zikiwemo picha za ramani ili wafaidike moja kwa moja na mirabaha kwa makusanyo badala
ya utaratibu wa sasa wa makubaliano ya mbunifu na mhitaji wa kazi husika.
Amewapongeza
wabunifu na wasanii wote wa Zanzibar waliopo na wale waliotangulia mbele ya
haki kwa kazi zao mbali mbali ambazo zimeitangaza na kuijengea sifa Zanzibar katika medani ya
Kimataifa.
Alisema kazi
za wabunifu na wasanii hao zimechangia kuelimisha, kuburudisha, kuhamasisha na
kuhifadhi utamaduni wa Taifa hili pamoja na kutoa ajira kwa wananchi walio wengi
hasa kundi kubwa la Vijana na hatimae kuchangia uchumi wa Taifa.
“ Hatimiliki
ukijumlisha na ubunifu na sanaa jawabu unalopata ni ajira pamoja na ukuaji wa
uchumi wa Taifa “. Alisema Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar.
Balozi Seif alisema
kutokana na umuhimu wa wabunifu na wasanii, Jumuiya ya Kimataifa iliweka
misingi mikuu na muhimu ya kufuatwa na nchi zote wanachama katika kusimamia
ulinzi, hadhi, haki na maslahi yao mkataba ambao unasimamiwa na shirika la Umoja
wa Mataifa linaloshughulikia maslahi ya wabunifu na wasanii { World
Intellectual Property Organisation – WIPO }.
Alisema
Tanzania iliridhia mkataba huo wa Berne mwaka 1886 wakati Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar ikaridhia mkataba huo kwa kupitishwa sheria nambari 14 ya mwaka
2003 yenye kusimamia masuala ya Hakimiliki.
“ Sheria
hiyo ndio iliyounda Ofisi inayosimamia masuala ya Hakimiliki, Bodi ya
Hakimiliki na Jumuiya ya Hakimiliki maarufu COSOZA “. Alisema Balozi Seif.
Akitoa
Taarifa Msimamizi na Afisa Mtendaji Mkuu
wa Ofisi ya Hakimiliki Zanzibar Bibi Mtumwa Khatibu Kheir alisema huo ni mgao
wa pili wa Mirabaha kwa wabunifu na
wasanii wapatao elfu 1124 wa zanzibar.
Bibi Mtumwa
alisema Ofisi ya Hakimiliki imefanya kazi kubwa na nzuri kwa kushirikiana na
kamisheni ya Utalii pamoja na Mamlaka ya Uwekezaji vitega uchumi Zanzibar {
ZIPA } katika kuziunganisha kwa wateja
kazi za wabunifu na wasanii.
Hata hivyo
Msimamizi na Afisa Mtendaji Mkuu huyo wa Ofisi ya Hakimiliki alitanabahisha
kwamba wabunifu na wasanii wasiosajiliwa kamwe hawataweza kufaidika na mgao wa
Mirabaha inayotolewa.
Bibi Mtumwa
Khatibu Ameir aliwataja wabunifu na wasanii wanne waliokuwa mfano mwaka huu
kuwa ni pamoja na Bwana Khamis Juma, Bibi Mwapombe Hiari, Bwana Mwalimu Ali
Mwalimu na Marehemu Seif salim.
Mapema
akimkaribisha Mgeni rasmi Balozi Seif, Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Mh.
Aboubakar Khamis Bakar alisema vipaji walivyokuwa navyo wabunifu na
wasanii wa Zanzibar ni vyema vikaenziwa
na kuheshimiwa kwa faida ya Taifa kwa jumla.
Waziri
Aboubakar alisema Zanzibar imepata umaarufu mkubwa Duniani kutokana na ongezeko
la vipaji vya wabunifu na wasanii wake wanaoonekana
kuwa kivutio kwa wageni na watalii mbali mbali wanafuatilia kazi za wabunifu na
wasanii hao.
Waziri wa
Katiba na Sheria Zanzibar aliwashukuru wachangiaji kutoka Taasisi mbali mbali
za Umma na zile binafsi wakiwemo pia watu maarufu kwa uamuzi wao wa kusaidia kufanikisha
kazi hiyo muhimu kwa taifa.