Wanaushirika wa Jitihada Njema wa Bandarini Zanzibar wakiserebuka
na ngoma ya Utamaduni ya Kibati wakati
wa uzinduzi wa Ushirika wao katika
ukumbi wa Salama Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar. Picha Hassan Issa -
OMPR
Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Bandari waliojumuika pamoja na wanaushirika wa Jitihada Njema wakati wa hafla ya zinduzi wa Ushirika huo Salama Bwawani Mjini Zanzibar. Picha Hassan Issa - OMPR
Baadhi ya wanaushirika wa Jaitihada Njema wa Bandarini Malindi wakifuatia Hotoba ya uzinduzi wa ushirika wao iliyotolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif hayupo pichani kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein. Picha Hassan Issa - OMPR
Balozi Seif Ali Iddi aliyepo kati kati waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na Oongozi wa Shirika la Bandari, Bodi ya Shirika pamoja na Ushirika wa Jitihada Njema mara baada ya kuuzindua rasmi ushirika huo hapo katika ukumbi wa Salama Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar. Picha Hassan Issa - OMPR
Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Bandari waliojumuika pamoja na wanaushirika wa Jitihada Njema wakati wa hafla ya zinduzi wa Ushirika huo Salama Bwawani Mjini Zanzibar. Picha Hassan Issa - OMPR
Baadhi ya wanaushirika wa Jaitihada Njema wa Bandarini Malindi wakifuatia Hotoba ya uzinduzi wa ushirika wao iliyotolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif hayupo pichani kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein. Picha Hassan Issa - OMPR
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizindua rasmi Ushirika
wa Jitihada Njema wa Bandarini Malindi kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali
Mohammed Shein. Kulia ya
Balozi ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Bandari Zanzibar Nd. Salim Senga
Salmin na Kushoto yake ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa
Jamii, Vijana , Wanawake na Watoto Nd. Ali Khamis. Picha Hassan Issa -
OMPR
Balozi Seif Ali Iddi aliyepo kati kati waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na Oongozi wa Shirika la Bandari, Bodi ya Shirika pamoja na Ushirika wa Jitihada Njema mara baada ya kuuzindua rasmi ushirika huo hapo katika ukumbi wa Salama Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar. Picha Hassan Issa - OMPR
Press Release:-
Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar imewahakikishia wananchi kwamba itaendelea kuchukuwa
hatua madhubuti katika kuviimarisha vyama vya ushirika kwa kuendelea kuvifanyia
ukaguzi, kuwapatia mafunzo wanachama wa vyama hivyo pamoja na kutoa mikopo
yenye masharti nafuu ili kuviongezea mtaji.
Kauli hiyo
imetolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali
Mohemmed Shein wakati wa hafla fupi ya kuuzindua Ushirika wa Jitihada njema wa
Bandarini Malindi Mjini Zanzibar.
Rais wa
Zanzibar Dr. Shein ambae Hotuba yake ilisomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali inatambua umuhimu wa
mchango wa vyama vya ushirika katika kutoa ajira, kuimarisha uchumi na kukuza
Demokrasi Nchini.
Alisema
hatua kadhaa zimeshachukuliwa katika kuimarisha sekta hiyo sambamba na
kukamilika kwa sera ya maendeleo ya Ushirika Zanzibar ya mwaka 2014 ambapo hivi
sasa inafanyiwa mapitio sheria nambari 4 ya mwaka 1986.
Alifahamisha
kwamba utaratibu wa kuvisajili vyama vya ushirikia nchini unaendelea kwa lengo
la kuviimarisha, kuvitambua na kuhakikisha vyama vya vyote vya ushirika
vinafanya kazi zake kisheria.
“ Serikali
tayari imeshasajili vyama vya ushirika mia 749 vya uzalishaji malio na utoaji
huduma. Kiwango hicho kinafanya idadi ya vyama vilivyosajiliwa kufikia elfu
2,493 Zanzibar wakati saccos 16 zimeshasajiliwa na kufanya idadi ya jumla
kufikia 203 “. Alisema Dr. Shein.
Rais wa
Zanzibar alieleza kwamba vyama vya ushirika nchini vimefanikiwa kutengeneza
mtaji unaofikia shilingi Bilioni 3.5 ambao umeweza kutoa mikopo zaidi ya
shilingi Bilioni Saba katika kipindi cha mwaka 2012 hadi 2015.
Alisema
katika tathmini iliyofanywa kwa vyama 88
vya ushirika imebainika kwamba zaidi ya wanachama elfu 6,835 wamepata fursa ya
kujiajiri wenyewe kupitia sekta ya ushirika.
Alisema ni
jambo la faraja kuona kwamba katika kipindi kirefu sekta ya ushirika imeanza
kuwavutia wasomi waliomaliza vyuo vya elimu ya juu ambapo jumla ya vyama vinne
vya ushirika vya wasomi vyenye vijana 72 vinavyojishughulisha na utoaji wa
huduma za mafunzo na shughuli za kilimo vimesajiliwa.
Dr. Shein
alieleza kwamba hayo nji mafanikio makubwa katika utekelezaji wa azma ya
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha maendeleo ya Sekta ya
ushirika kwa mujibu wa Mkuza Awamu ya Pili na Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi
ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2010 --2015.
Rais wa
Zanzibar aliupongeza Ushirikia wa Jitihada Njema wa Bandarini Zanzibar kwa
mafanikio uliopata ndani ya kipindi cha mwaka mmoja tokea kuanzishwa kwake na
kuongeza idadi ya wanachama iliyofikia 200.
Alisema
uamuzi wa kuanzishwa kwa ushirika wa Jitihada Njema mwaka 2014 ni wa busara
katika kukabiliana na tatizo la ajira hapa nchini pamoja na kwenda
sambamba na lengo la Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar inayowataka
Wananchi kuanzisha vikundi vya ushirika kwa ajili ya kujiimarisha kiuchumi na
kupambana na umaskini.
Alieleza
faraja yake kwa kuona ushirika huo unaweza kulipa mishahara na maposho
wanachama wake bila ya kutetereka, kumudu kuwalipia wanachama wake katika Mfuko
wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar { ZSSF } pamoja na kuwawekea uhakika wa kupata
huduma za afya wakati wanapozihitaji.
Dr. Shein
alitoa rai kwa wanaushirika hao wa Jitihada Njema Bandarini Zanzibar kuzingatia
nidhamu ya kazi, uaminifu na uadilifu katika kuzishughulikia mali za watu zenye
thamani kubwa.
Alisema
lengo la Serikali Kuu ni kuona kuwa muda wa kuhudumia wafanyabiashara
wanaotumia Bandari ya Zanzibar unakuwa mchache ili kuwavutia wateja pamoja na
wageni wanaotumia Bandari hiyo.
Alieleza
kuwa Zanzibar ina Histori ndefu ya shughuli za Bandari kwa kutoa huduma kwa
vyombo mbali mbali vya usafiri wa Bandari vinavyochukuwa mizigo na abiria
katika ukanda wa mwambao wa Afrika Mashariki.
Alisema
umaarufu wa Bandari ya Zanzibar uliongezeka zaidi katika Karne ya 19 kupitia
Bandari ya zamani ya Malindi iliyokuwa ikihudumia majahazi na vyombo vyengine
vidogo vidogo vya usafiri wa Baharini.
Rais Shein
alieleza kuwa shughuli za Bandari ziliimarika zaidi kutokana na kukua kwa
muingiliano wa Zanzibar na Mataifa mengine uliosababisha kukuwa kwa biashara na
kulazimika kujengwa kwa Bandari ya Malindi mwaka 1924 ambayo iliweza
kuzihudumia meli ndogo ndogo na Matishali.
Alisema
ukuaji wa bishara ndani ya Bandari ya Malindi iliifanya Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar kuanzisha Shirika la Bandari kwa sheria nambari 1 ya Mwaka 1997.
Alieleza
kwamba shirika la Bandari ni Mtoto wa lililokuwa shirika la ukapuaji nna
uteremshaji wa mizigo Bandarini la Zanzibar Wharfage lililoanzishwa Mwezi
August Mwaka 1972 likiwa shirika pekee la Serikali na kufanyakazi kwa
kipindi cha miaka 33.
“ Nimefurahi
kusikia kwamba waanzilishi wa ushirika wa Jitiohada Njema Bandarini mmetokana
na shirika la Bandari na kwa hivyo mna uzoefu wa maeneo
Rais wa
Zanzibar aliwaahidi wanachama wa ushirika wa Jitihada Njema kwamba Serikali
itashirikiana nao katika kuona changamoto zinazowakabili zinatafutiwa ufumbuzi
ili wapate mafanikio zaidi.
Akisoma
Risala ya wana ushirika wa Jitihada Njema
Bandarini Mmoja wa Wanaushirika huo Bwana Ali Mohammed alisema Vibarua
wa shirika la Bandari walifikia uamuzi wa kuanzisha ushirika huo kwa nia ya
kuwa na nguvu za pamoja katika utekelezaji wa majukumu yao na kukabiliana na
changamoto zinazowakabili.
Bwana Ali
Mohammed alisema ushirika huo ulioanza na wanachama 100 umekusudia kufanya kazi
zake kwa stara tofauti na baadhi ya watu wanavyozifikiria kazi zao ukilenga
kushawishi kupunguza wimbi kubwa la ukosefu wa ajira liliopo kwa vijana hapa
nchini.
Mwanaushirika huyo
wa ushirika wa Jitihada njema Bandarini alifahamisha kwamba zipo
changamoto zinazoukabili ushirika huo akizitaja kuwa ni pamoja na ofisi bora na
ya uhakika itakayoweza kukidhi mahitaji ya wanaushirika hao.
Katika kuimarisha
malengo ya ushirika huo na kujiendesha kimaisha Bwana Ali Mohammed aliiomba
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Uongozi wa Shirika { ZSSF } ili uwakubalie kuendesha shughuli za
usafi katika kiwanja wa Watoto Kariakoo pamojan na Mnara wa Michenzani mara
utakapoanza kutoa huduma.
Akimkaribisha
Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi
wa Jamii, Vijana Wanawake na Watoto Nd.Ali Khamis alisema ipo miongozo zaidi ya 15
iliyotayarishwa na Wizara ambayo itajenga mwenendo wa mfumo wa uendeshaji bora
wa vyama vya ushirika.
Nd.Ali
Khamis alisema hatua hiyo inalenga
kuimarisha nguvu za vikundi vya ushirika ambavyo ndio kimbilio la wananchi
walio wengi Nchini katika kujiimarisha kiuchumi na kuongeza mapato yao.
Alifahamisha
kwamba Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana , Wanawake na Watoto
italifanyia kazi suala la mafunzo kwa wanaushirika wa Jitihada Njema Bandarini
ili wafikie hatua ya kufanya kazi zao kitaalamu na ufanisi wenye uhakika.
Naibu Katibu
Mkuu huyo wa Wizara ya Uwezeshaji alitoa pongezi Maalum kwa wanaushirika hao wa
Jitihada njema kwa mafanikio makubwa wayiyoyapata ndani ya miezi 15 tokeaa
ulipoundwa na kuonyesha mfano mzuri wa kuigwa na vikundi vyengine vya ushirika
hapa Nchini.
“ Ushirika
haupendezi hata kidogo kuona wanachama wake wanajenga tabia na mfumo wa mambo
yao kuomba wafanyiwe na Serikli. Nyinyi
wana Jitihada Njema mmeonyesha mfano baada ya kuomba mpatiwe Sehemu ya kujenga
Ofisi wakati wenzenu huomba wapatiwe Ofisi “. Alifafanua Nd.Ali
Ushirika wa
Jitihada Njema Bandarini Zanzibar unajishughulisha na kazi wa utoaji wa huduma
za Makontena Bandarini pamoja na kufanya usafi wa mazingira katika eneo lote la
Bandari ya Zanzibar iliyopo Malindi Mjini Zanzibar.
Akitoa
shukrani kwa Niaba ya Bodi ya Shirika la
Bandari pamoja na Uongozi wa Ushirika wa Jitihada Njema na Wanaushirika wenzake
Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mzee Omar Haji alisema Uongozi huo hautamvumilia
Mfanyakazi yeyote atakayeanzisha siasa ndani ya Bandari.
Mzee Omar
alisema Bandari ni eneo maalum la kuhudumia watu likisimamiwa na watendaji wenye
itikadi, makabila na jinsia tofauti kiasi kwamba kuruhusu masuala hayo ni
kuvuruga mfumo mzima wa utendaji wa eneo hilo.
“ Siasa
zinae sehemu na maeneo yake maalum. Hivyo kamwe hatutamruhusu mtendaji au
mfanyakazi ye yote kuingia ndani ya Bandari akaanza kutuhubiria Siasa ambazo
baadaye zinaweza kuleta chuki na uhasama “. Alisema Makamu Mwenyekiti huyo wa
Bodi ya Shirika la Bandari Zanzibar.