Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi
msaada wa Vipaza sauti Amiri wa Jumuiya
ya Sherehe za Siku Kuu ya Iddi Matemwe Ustaadhi Kundi Choum Haji kutekeleza
ahadi aliyoip[a Jumuiya hiyo wakati wa sherehe za siku kuu ya Iddi el Hajj
iliyopita. Picha na Hassan Issa –
OPMR – ZNZ.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akimkabidhi mchango wa Shilingi 400,000/- kwa kila kikundi miongoni mwa vikundi 14 vya Ushirika wa Akina Mama vilivyomo ndani ya Wilaya ya Kaskazini “ A “. Picha na Hassan Issa – OPMR – ZNZ.
Balozi Seif akikabidhi Seti moja ya Jezi na Mipira kwa kila Timu ya Soka miongoni mwa timu nne zilizomo ndani ya Jimbo la Matemwe. Picha na Hassan Issa – OPMR – ZNZ.
Balozi Seif akiangalia hodhi linalojengwa kwa ajili ya kuhifadhia maji kwenye Msikiti Mkuu wa Kijiji cha Mvuleni Kidoti Jimbo la Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Picha na Hassan Issa – OPMR – ZNZ.
Balozi Seif akiuagiza Uongozi wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Kijiji cha Mvuleni kufanya Tathmini ya uenzi wa Vyoo ili uwahi kufunguliwa katika muda muwafaka uliopangwa. Picha na Hassan Issa – OPMR – ZNZ.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akimkabidhi mchango wa Shilingi 400,000/- kwa kila kikundi miongoni mwa vikundi 14 vya Ushirika wa Akina Mama vilivyomo ndani ya Wilaya ya Kaskazini “ A “. Picha na Hassan Issa – OPMR – ZNZ.
Balozi Seif akikabidhi Seti moja ya Jezi na Mipira kwa kila Timu ya Soka miongoni mwa timu nne zilizomo ndani ya Jimbo la Matemwe. Picha na Hassan Issa – OPMR – ZNZ.
Balozi Seif akiangalia hodhi linalojengwa kwa ajili ya kuhifadhia maji kwenye Msikiti Mkuu wa Kijiji cha Mvuleni Kidoti Jimbo la Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Picha na Hassan Issa – OPMR – ZNZ.
Balozi Seif akiuagiza Uongozi wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Kijiji cha Mvuleni kufanya Tathmini ya uenzi wa Vyoo ili uwahi kufunguliwa katika muda muwafaka uliopangwa. Picha na Hassan Issa – OPMR – ZNZ.
Press Release:-
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
Ali Iddi amewakumbusha Wananchi hasa akina Mama Nchini kuwaunga mkono Viongozi
wenye muelekeo wa kuwasimamia vyema katika harakati zao za Maendeleo, kiuchumi
na ustawi wa Jamii.
Alisema
takwimu ya idadi ya watu Nchini
inaoonyesha wazi kwamba Wanawake ndio wenye uwezo wa kutumia kura zao katika
kuchaguwa Viongozi watakaowafaa kwenye maeneo yao kutokana na wingi wao.
Balozi Seif
Ali Iddi alitoa kumbusho hilo wakati akikabidhi Vipaza Sauti kwa ajili ya
Jumuiya ya Kuhifadhi Quran pamoja na Sherehe za Siku Kuu ya Kiislamu ya Kijiji cha Matemwe Wilaya ya Kaskazini
“A” Mkoa wa Kaskazini Unguja akitekeleza
ahadi aliyoitowa wakati wa Siku Kuu ya Mfunguo Tatu uliopita akiwa mgeni rasmi.
Hafla hiyo iliambatana pia na Balozi Seif kukabidhi
seti za Jezi na Mipira kwa Timu Nne wa Jimbo la Matemwe ambapo Mkewe Mama Asha
Suleiman Iddi akakabidhi fedha taslim kwa baadhi ya vikundi 14 vya Ushirika vya
Akina Mama wa Wilaya ya Kaskazini “A” vifaa vyote vikiwa na thamani ya shilingi
Milioni 7,860,000/-.
Balozi Seif
alisema huu ni mwaka muhimu kwa Taifa la Tanzania ambapo Wananchi wanapaswa
kuwa makini katika kufanya uamuzi
muafaka wa kura ya maoni pamoja na uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba.
Alisema
uwamuzi wa Wananchi hao endapo
hautazingatia hatma yao ijayo ya miaka mitano kwa kuchaguwa viongozi makini na
imara wasijetafuta visingizio vya lawama kwa
viongozi watakaowaweka madarakani.
Mapema Mke
wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akitekeleza
ahadi yake ya kuviwezesha
Baadhi ya Vikundi vya Ushirika vya akina Mama wa Wilaya ya Kaskazini “A “ alisisitiza umoja na
mshikamano miongoni mwa Wananchi wa Wilaya hiyo.
Mama Asha
alisema mshikamano huo ndio njia pekee itakayowawezesha wananchi hao kuendelea
na shughuli zao za kujitafutia riziki katika hali ya amani na utulivu.
Alitanabahisha
kwamba yapo Mataifa kadhaa duniani yakiwemo yale ya Bara la Afrika ambayo
baadhi ya wananchi wake walijaribu kuichezea amani na hivi sasa tayari
wameshatumbukia katika dimbwi la vurugu zilizozaa maafa yaliyoacha
makovu yatayoendelea kukumbukwa milele na Mataifa hayo.
Baadhi ya
Vikundi vipatavyo 14 vya ushirika wa
akina Mama wa Wilaya ya Kaskazini “ A “ vilikabidhiwa fedha taslim shilingi Laki nne
kila kimoja ambavyo ni Lamoyoni hulioni, Apewaye hupokea, Atowaye Allah pamoja
na Riziki Haiwanwi.
Vyengine ni
Hatujali Kitu, Tumia Jasho lako, Tushukuru Mungu, Haraka Sio Mwendo, Kheir
Liwe, Tumia Jasho Lako,Wema Si Maneno, Wema wa Maskini hauna sifa, Mtaji wa
Maskini pamoja na Mwanzo Mgumu.
Timu wa
Mpira wa miguu zilizokabidhiwa seti za Jezi na Mipira ni pamoja na Kikobweni
United, Mabundi Sports Club, Kilima Juu Sports Club pamoja na Chimbuko Sports
Club.
Wakati huo
huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipata fursa ya
kukagua maendeleo ya ujenzi wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Kijiji cha Mvuleni
Kidoti Jimbo la Nungwi.
Balozi Seif
ambae aliridhika na hatua iliyofikiwa ya ujenzi huo aliuagiza Uongozi wa
Msikiti huo kufanya tathmini ya makisio ya ujenzi wa vyoo vya Msikiti huo ili
kukamilisha kazi yote.
Ufunguzi
Rasmi wa Msikiti huo wa Ijumaa wa Mvuleni Kidoti unatarajiwa kufanywa hivi
karibuni na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Braza la Mapinduzi Al – Hajj Dr.
Ali Mohammed Shein.