Baadhi ya Majengo ya Haoteli ya Karafuu Beach
Resort Spa ya Michamvi yaliyoungua kwa moto usiku wa kuamkia juzi na
kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha. Picha Hassan Issa
–OMPR – ZNZ.
Baadhi ya Majengo ya Haoteli ya Karafuu Beach
Resort Spa ya Michamvi yaliyoungua kwa moto usiku wa kuamkia juzi na
kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha. Picha Hassan Issa
–OMPR – ZNZ.
Baadhi ya Majengo ya Haoteli ya Karafuu Beach
Resort Spa ya Michamvi yaliyoungua kwa moto usiku wa kuamkia juzi na
kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha. Picha Hassan Issa
–OMPR – ZNZ.
Bwawa la Hoteli ya Karafuu Beacha Resort Spa likionekana
kuathirika na moto ulioikumba Hoteli hiyo juzi alfajiri. Picha Hassan Issa
–OMPR – ZNZ.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akiwa na mwenyeji wake Meneja wa
Kafaruu Beach Resort Spa Bwana Zakaria Juma wakiangalia baadhi ya majengo
yaliyoteketea kwa moto juzi alfajiri. Picha Hassan Issa
–OMPR – ZNZ.
Maneja wa Hoteli ya Karafuu Beach Resort Bwana Zakaria Juma akimkaguza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif katika maeneo yaliyoathirika na moto kwenye Hoteli yake iliyopo katika Kijiji cha Michamvi Wilaya ya Kati. Picha Hassan Issa –OMPR – ZNZ.
Maneja wa Hoteli ya Karafuu Beach Resort Bwana Zakaria Juma akimkaguza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif katika maeneo yaliyoathirika na moto kwenye Hoteli yake iliyopo katika Kijiji cha Michamvi Wilaya ya Kati. Picha Hassan Issa –OMPR – ZNZ.
Press Release:-
Uongozi wa
Hoteli ya Kimataifa ya Karafuu Beach Resort Spa ya Michamvi Wilaya ya Kati umeipongeza
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na wananchi wa Kijiji cha Michamvi Wilaya
ya kati kwa juhudi walizochukuwa katika kusaidia kuuzima moto mkubwa uliotokea juzi mnamo saa 10.00 za alfajiri.
Meneja wa
Hoteli hiyo Bwana Zakaria Juma alitoa pongezi hizo mbele ya Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefika Hotelini hapo kuangalia athari
ya moto huo kwa lengo la kutoa Pole pamoja
na kuufariji Uongozi na Wafanyakazi wa Hoteli hiyo.
Bwana
Zakaria Juma alisema licha ya baadhi ya vitu na vifaa vya Hoteli hiyo
kuathiriwa na moto huo lakini juhudi na uungwana ulioonyeshwa na Serikali pamoja
na Wananchi ambao ulipelekea kutopotea kwa kitu chochote kilichobakia kwenye
kizaa zaa hicho umeleta faraja kwao pamoja na wageni waliokuwemo kwenye Hoteli
hiyo.
Meneja huyo
wa Karafuu Beach Resort Spa alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
kwamba moto huo ambao hadi sasa haujatambulika chanzo chake pamoja na hasara
iliyopatikana umeteketeza vyumba 35, Ghala, Duka, Sehemu ya Mapokezi na Mkahawa
wa Hoteli hiyo.
Alisema vyumba
70 kati ya 135 vya hoteli hiyo vimesalimika baada ya juhudi zilizochukuliwa kwa
pamoja kati ya Wananchi na Wafanyakazi
wa Hoteli hiyo kwa kujaribu kuzunguushia mabati eneo la kusini la Hoteli hiyo.
“ Hoteli
yetu imejigawa katika maeneo mawili ya vumba na huduma zote. Lipo lile
tunaloliita Masai ambalo ndio lililoteketea kwa moto na jengine lililosalimika
ni lile liitwalo Bondeni “. Alifafanua Bwana Zakaria Juma.
Alifahamisha
kwamba Uongozi wa Juu wa Hoteli hiyo umefikiria kuandaa mpango maalum wa
kufanya matengenezo mapya ya eneo
lililoathirika na kuendelea kutoa huduma kama kawaida ifikapo mwezi wa saba
mwaka huu.
Bwana
Zakaria Juma alisisitiza kwamba huduma
za kupokea wageni zinaendelea kama kawaida katika eneo la Bondeni ambalo
halikuathirika na moto huo.
Naye Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwapa pole na kuwafariji
wafanyakazi na Uongozi wa Hoteli hiyo aliwataka kuwa wastahamilivu katika
kipindi hichi kigumu ambacho kimeleta usumbufu kwa wageni wao.
Balozi Seif ameupongeza
Uongozi wa Karafuu Beach Resort Spa kwa umakini wake wa kuuwekea Bima mradi wao
jambo ambalo litasaidia kupunguza machungu kutokana na hasara hiyo.
Hata Hivyo
Balozi Seif alitahadharisha kwamba ipo haja kwa Uongozi huo kufikiria namna ya
ya kubadilisha matumizi ya makuti katika uwezekaji wa majengo ya Hoteli hiyo
ambayo ni hatari wakati linapotokea janga la moto.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar aliwahakikishia wawekezaji wa miradi yote ya Kiuchumi
na maendeleo kwamba itakuwa pamoja katika kuisaidia wakati inapopata matatizo .