Mmoja wa Wafanyakazi wa shamba la Mipira Kichwele akiwasilisha
malalamiko yao mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
hayupo pichani wakidai kutolipwa mishahara yao kati ya miezi mitatu hadi
Minane.
Mwakilishi wa Kampuni ya Agro Tec ambae pia ni Makamu Mwenyekiti wa Bidi ya Uongozi wa Kampuni hiyo Bwana Soud Moh’d Achili akitoa ufafanuzi mbele ya Balozi Seif kuhusu shutuma zilizotolewa na Wafanykazi wa shamba la Mipira Kichwele dhidi ya Kampuni yake.
Balozi Seif akiwaahidi Wafanyakazi wa shamba la Mipira Kichwele hatua zitakazochukuliwa na Serikali juu ya matatizo yao likiwemo la kulipwa haki zao.
Mwakilishi wa Kampuni ya Agro Tec ambae pia ni Makamu Mwenyekiti wa Bidi ya Uongozi wa Kampuni hiyo Bwana Soud Moh’d Achili akitoa ufafanuzi mbele ya Balozi Seif kuhusu shutuma zilizotolewa na Wafanykazi wa shamba la Mipira Kichwele dhidi ya Kampuni yake.
Balozi Seif akiwaahidi Wafanyakazi wa shamba la Mipira Kichwele hatua zitakazochukuliwa na Serikali juu ya matatizo yao likiwemo la kulipwa haki zao.
Press Release:-
Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar imewahakikishia wafanyakazi wa shamba la Mipira Kichwele kwamba
itafanya jitihada na mbinu zote katika kuona wanalipwa mishahara yao kati ya miezi mitatu hadi Minane wanayoidai
Kampuni iliyowekeza Mradi huo ya Agro Tec kwa kipindi kirefu sasa.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alitoa kauli hiyo baada ya kupokea
malalamiko kadhaa yaliyowasilishwa kwake na Wafanyazi hao wakiushutumu Uongozi
wa Kampuni hiyo kuwadhalilisha pamoja na
kutopewa haki zao kadhaa Mkutano uliofanyika katika kituo cha Mradi huo kiliopo
pembezoni mwa Wilaya za Kaskazini “B”.
Balozi Seif alisema
kwamba Kampuni ya Agro Tec haikuwa makini kujipanga katika uendeshaji mradi huo
tokea kukabidhiwa kwake jambo ambalo haina tija Serikali Kuu pamoja na
Wafanyakazi wenyewe.
Alisema katika
kuondosha utata huo wa muda mrefu ni jambo la msingi kwa Kampuni hiyo kufanya
utaratibu wa kulipa haki zinazodaiwa na Wafanyakazi hao ikiwemo zile ya mafao
ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii { ZSSF } pamoja na Fedha za likizo.
Balozi Seif
alifahamisha kwamba Serikali Kuu kwa kushirikiana na Taasisi zinazosimamia
uwekezaji, ukusanyaji wa Mapato, usimamiaji haki za Wafanyakazi na Mfuko wa
hifadhi ya Jamii zitafanya uchunguzi wa kina ili kuona uwezo wa Kampuni hii
kama unakidhi kuendelea kuwekeza mradi
huu.
“ Sisi kama
Serikali kwa kushirikiana na taasisi zote husika tutauchunguza mradi huu utendaji wake tokea Kampuni ya Agro Tec
ilipokabidhiwa na hatutakuwa na muhali kuifutia kibali Kampuni hiyo endapo haitatekeleza masharti na
makubaliano yaliyowekwa ikiwemo haki za Wafanyakazi “. Alisema Balozi Seif.
“
Nakuhakikishieni wafanyakazi nyote wa shamba la Mipira kwamba haki zenu zote
zitapatikana kwa mujibu wa taratibu tulizokubaliana na muwekezaji huyu hata
kama kuuzwa mali zake na kufidia madeni anayodaiwa “. Alisisitiza Balozi Seif.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar aliwashukuru wafanyakazi hao wa shamba la Mipira lwa
Kichwele kwa ustahamalivu wao wa muda mrefu ambao kwa kiasi kikubwa umesaidia
kuepusha shari kati yao na Uongozi wa Kampuni n iliyowekeza mradi huo.
Mapema
wakitoa malalamiko yao wafanyakazi hao wa shamba la Mipira la Kichwele
walimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Bodi iliyopo hivi sasa
ya Kampuni hiyo ya Agro Tec haina
maslahi kwao.
Walisema
mgogoro kati yao na Uongozi wa Kampuni
hiyo ulioanza tokea mwaka 2013 umesababisha maisha yao kuwa mashakani na kukosa
matumaini ya kuendesha maisha yao kupitia mradi huo.
Naye
Kamishna wa Kazi Zanzibar Nd.Kubingwa Simba alisema kwamba Muwekezaji ye yote
hapa Nchini hawezi kufunga mradi wake mpaka ahakikishe analipa madeni na
stahiki zote kwa washirika wake.
Nd. Simba
alisema kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa katika masuala ya uwekezaji Mahkama
ndio yenye haki na uwezo wa kutoa maamuzi endapo muwekezaji huyo atakwenda
kinyume na mkataba aliyofunga.
Kwa Upande
wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Mali Asili Zanzibar Dr. Ased Bakar
Ased alisema umri wa uzalishaji wa miti ya mirira ya kichwele na iliyoko Kisiwani
Pemba iliyooteshwa mwaka 1977 umepindukia uzalishaji Kiuchumi.
Dr. Ased
alisema mashamba ya mipira yameshapoteza muelekeo kutokana na bei ya bidhaa
hiyo katika soko la Kimataifa imeshuka kutoka Dola za Kimarekani elfu 2,500
hadi elfu 1200 kwa Tani Moja.
“ Hakuna
dalili ya bei ya bidhaa ya mpira kuongezeka kwa vile ushindani wa zao la mpira kwa sasa haupo tena “. Alifafanua
Dr. Ased Bakar Ased.
Hivi sasa wapo Wafanyakazi 14 kati ya 160 wa
shamba la mipira la Kichwele wanaoendelea na kazi kwenye mradi huo uliopewa
muekezaji kuuendesha tokea mwaka 2003.
Yapo madeni
kadhaa yanayodaiwa Kampuni ya Agro Tec kutoka kwa wafanyakazi hao ambayo ni
Shilingi Milioni 34,411,267 Deni la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar { ZSSF }
Shlingi Milioni 3,637,000/- deni la
wagemaji Utomvu na shilingi 21,000,000/-
wafanyakazi wa Viwandani.
Mengine ni
shilingi Milioni 34,027,750 wasimamizi wa wafanyakazi Mashambani, shilingi
Milioni 8,400,000/- wafanyakazi Ofisini, Milioni 42,000,000/- wafanyakazi wa
mipira Kisiwani Pemba na shilingi Milioni 166,000,965/- deni la likizo.