Balozi Mdogo Mpya wa India Hapa Zanzibar Bwana Satendar Kumar akisalimiana na Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Picha Hassan Issa–
OMPR – ZNZ.
Balozi Mdogo Mpya wa India Hapa Zanzibar Bwana Satendar Kumar akijitambulisha rasmi kwa
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi. Picha Hassan Issa–
OMPR – ZNZ.
Balozi Seif akibadilishana mawazo na Balozi Mdogo Mpya wa India Hapa Zanzibar Bwana Satendar Kumar Ofisini kwake Mtaa wa Vuga Mjini Zanzibar. Picha Hassan Issa– OMPR – ZNZ.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akipokea zawadi kutoka kwa Balozi Mdogo Mpya wa India Hapa Zanzibar Bwana Satendar Kumar. Picha Hassan Issa– OMPR – ZNZ.
Balozi Seif akibadilishana mawazo na Balozi Mdogo Mpya wa India Hapa Zanzibar Bwana Satendar Kumar Ofisini kwake Mtaa wa Vuga Mjini Zanzibar. Picha Hassan Issa– OMPR – ZNZ.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akipokea zawadi kutoka kwa Balozi Mdogo Mpya wa India Hapa Zanzibar Bwana Satendar Kumar. Picha Hassan Issa– OMPR – ZNZ.
Press Release:-
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
ameyashauri Makampuni na Taasisi za uwekezaji kutoka Nchini India kuwekeza miradi yao
katika Visiwa vya Unguja na Pemba ili
kuitikia wito wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wa kukaribisha
wawekezaji mbali mbali kuwekeza hapa
Nchini .
Alisema
India bado ina nafasi pana kwa Makampuni yake kuwekeza miradi yao ya
Kiuchumi hasa katika Sekta ya Viwanda kama ilivyowahi kutumia fursa hiyo hapa
Zanzibar katika miaka ya 80.
Akizungumza
na Balozi Mdogo Mpya wa India hapa
Zanzibar Bwana Satendar Kumar hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema
kwamba Sekta ya Viwanda ni eneo muhimu
katika kukuza uchumi na kupunguza Umaskini.
Alisema Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa na malengo la kuimarisha sekta hiyo kwa azma
ya kulisaidia kundi kubwa la Vijana
wasio na ajira ambalo limekuwa likiongezeka kila mwaka baada ya kumaliza masomo
yao.
“ Ipo haja
kwa wawekezaji wa Sekta ya Viwanda kutoka Nchini India kurejea tena Zanzibar
kuwekeza miradi yao ya viwanda ili kusaidia uchumi wa Taifa pamoja na kupnguza
wimbi la vijana wasio na ajira “. Alisema Balozi Seif.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar aliipongeza India kwa jitihada zake za kusaidia
Maendeleo ya Wananchi ikiwa nchi ya kwanza iliyojikubalisha kuiunga mkono Zanzibar katika ujenzi wa
Viwanda vidogo vidogo.
Akizungumzia
miradi mengine ya Kiuchumi na Maendeleo ya Kijamii Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif aliiomba Serikali ya India kupitia Balozi wake Mdogo huyo kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika
harakati za Maendeleo kwenye sekta hizo.
Balozi Seif alitolea mfano Sekta za Elimu,
Teknolojia ya Mawasiliano ya Habari na Mawasiliano pamoja na kilimo ni miradi
ambayo inafaa kupewa msukumo na India katika kuisaidia Zanzibar Kitaaluma.
Alisema
Zanzibar inakusudia kuimarisha Kilimo cha mpunga kwa lengo la kupunguza
uagizaji wa bidhaa ya mchele nje ya Nchi ambayo ni chakula kikuu kinachotumia
fedha nyingi za kigeni.
Balozi Seif
alifahamisha kwamba mpango huo utasaidia uzalishaji wa mpunga kwa kiwango
inachokadiriwa kufikia Asilimia 50% ambapo mahitaji ya mchele kwa sasa ni
asilimia 80% inayoagizwa kutoka nje ya
Nchi.
Mapema
Balozi Mdogo Mpya wa India hapa Zanzibar Bwana Satendar Kumar alimueleza Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwamba uhusiano wa Kidiplomasia kati ya
India na Tanzania ikiwemo Zanzibar utaendelea kuimarishwa siku hadi siku.
Balozi
Satendar alisema uhusiano huo umejengwa katika mpango Maalum wa Maendeleo wa
India – Afrika uliojikita kwa Wataalamu
wa Nchi hiyo kusaidia taaluma katika sekta za afya, elimu, miradi ya Kazi za amali
pamoja na Teknolojia ya Mawasiliano na Habari.
Alifahamisha
kwamba mpango huo utajenga nguvu za ajira kwa Vijana wanaomaliza masomo yao ya
Sekondari na vyuo vikuu ambao kwa sasa wanashindwa kuendesha maisha yao
kutokana na ukosefu wa ajira ya kukidhi mahitaji yao ya maisha.