Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi

Mwanafunzi Isra Hilal Mwadini akifuatiwa na mwenzake Tamima Abass Sheha wakipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wakati wa hafla ya Maulidi ya Jumuiya ya Chuo cha Samael Academy.Kulia ya Balozi Seif ni Rais wa Sameil Academy Sheikh Nassir Bin Said.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizindua rasmi Bara bara ya pili ya Amani hadi Mtoni baada ya kukamilika awamu ya mwisho ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Akiwa na Balozi mdogo wa India nchini Tanzania wakiangalia maonyesho yaliofanya na Msanii kutoka India, Bi Navi Madhav hapo Ngome Kongwe

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Dk. Khalid S. Mohamed

akizungumza na Wadau wa Maendeleo wa Mfuko wa TASAF, walipofika Ofisini kwake kuzungumzia maendeleo ya Mfuko wa TASAF III,na kutembelea Mradi wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini (PSSN) katika Jimbo la Muyuni Wilaya ya Kusini Unguja katika Kijiji cha Muyuni B

Wazir wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakifurahia jambo wakati wa semina ya siku moja kuhusu matokeo makubwa na ya haraka katika kuleta mageuzi ya kiuchumi na kuleta maendeleo nchini iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein

Wednesday, 29 April 2015

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanbzibar Balozi Seif akijibu maswali aliyoulizwa na Wanahabari wa Shirika la Magazeti ya Serikali la Zanzibar leo






















Makamu wa Pili wa Rais wa Zanbzibar Balozi Seif akijibu maswali aliyoulizwa na Wanahabari wa Shirika la Magazeti ya Serikali la Zanzibar leo Hafsa Golo aliyepo Kati 
 kati na Tatu Makame wa kwanza kushoto. Picha Hassan Issa - OMPR                

Sunday, 19 April 2015

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akiwa na mwenyeji wake Meneja wa Kafaruu Beach Resort Spa Bwana Zakaria Juma wakiangalia baadhi ya majengo yaliyoteketea kwa moto juzi alfajiri.

 Baadhi ya Majengo ya Haoteli ya Karafuu Beach Resort Spa ya Michamvi yaliyoungua kwa moto usiku wa kuamkia juzi na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha. Picha Hassan Issa –OMPR – ZNZ.

 Baadhi ya Majengo ya Haoteli ya Karafuu Beach Resort Spa ya Michamvi yaliyoungua kwa moto usiku wa kuamkia juzi na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha. Picha Hassan Issa –OMPR – ZNZ.

 Baadhi ya Majengo ya Haoteli ya Karafuu Beach Resort Spa ya Michamvi yaliyoungua kwa moto usiku wa kuamkia juzi na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha. Picha Hassan Issa –OMPR – ZNZ.

 Bwawa la Hoteli ya Karafuu Beacha Resort Spa likionekana kuathirika na moto ulioikumba Hoteli hiyo juzi alfajiri. Picha Hassan Issa –OMPR – ZNZ.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akiwa na mwenyeji wake Meneja wa Kafaruu Beach Resort Spa Bwana Zakaria Juma wakiangalia baadhi ya majengo yaliyoteketea kwa moto juzi alfajiri. Picha Hassan Issa –OMPR – ZNZ.






















Maneja wa Hoteli ya Karafuu Beach Resort Bwana Zakaria  Juma akimkaguza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif katika maeneo yaliyoathirika na moto kwenye Hoteli yake iliyopo katika Kijiji cha Michamvi Wilaya ya Kati. Picha Hassan Issa –OMPR – ZNZ.

  Press Release:-

Uongozi wa Hoteli ya Kimataifa ya Karafuu Beach Resort Spa ya Michamvi Wilaya ya Kati umeipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na wananchi wa Kijiji cha Michamvi Wilaya ya kati kwa juhudi walizochukuwa katika kusaidia kuuzima moto mkubwa  uliotokea juzi mnamo saa 10.00 za alfajiri.
Meneja wa Hoteli hiyo Bwana Zakaria Juma alitoa pongezi hizo mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefika Hotelini hapo kuangalia athari ya moto huo kwa lengo la kutoa Pole pamoja  na kuufariji Uongozi na Wafanyakazi wa Hoteli hiyo.
Bwana Zakaria Juma alisema licha ya baadhi ya vitu na vifaa vya Hoteli hiyo kuathiriwa na moto huo lakini juhudi na uungwana ulioonyeshwa na Serikali pamoja na Wananchi ambao ulipelekea kutopotea kwa kitu chochote kilichobakia kwenye kizaa zaa hicho umeleta faraja kwao pamoja na wageni waliokuwemo kwenye Hoteli hiyo.
Meneja huyo wa Karafuu Beach Resort Spa alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba moto huo ambao hadi sasa haujatambulika chanzo chake pamoja na hasara iliyopatikana umeteketeza vyumba 35, Ghala, Duka, Sehemu ya Mapokezi na Mkahawa  wa  Hoteli hiyo.
Alisema vyumba 70 kati ya 135 vya hoteli hiyo vimesalimika baada ya juhudi zilizochukuliwa kwa pamoja kati ya  Wananchi na Wafanyakazi wa Hoteli hiyo kwa kujaribu kuzunguushia mabati eneo la kusini la Hoteli hiyo.
“ Hoteli yetu imejigawa katika maeneo mawili ya vumba na huduma zote. Lipo lile tunaloliita Masai ambalo ndio lililoteketea kwa moto na jengine lililosalimika ni lile liitwalo Bondeni “. Alifafanua Bwana Zakaria Juma.
Alifahamisha kwamba Uongozi wa Juu wa Hoteli hiyo umefikiria kuandaa mpango maalum wa kufanya matengenezo mapya ya  eneo lililoathirika na kuendelea kutoa huduma kama kawaida ifikapo mwezi wa saba mwaka huu.
Bwana Zakaria Juma  alisisitiza kwamba huduma za kupokea wageni zinaendelea kama kawaida katika eneo la Bondeni ambalo halikuathirika na moto huo.
Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwapa pole na kuwafariji wafanyakazi na Uongozi wa Hoteli hiyo aliwataka kuwa wastahamilivu katika kipindi hichi kigumu ambacho kimeleta usumbufu kwa wageni wao.
Balozi Seif ameupongeza Uongozi wa Karafuu Beach Resort Spa kwa umakini wake wa kuuwekea Bima mradi wao jambo ambalo litasaidia kupunguza machungu kutokana na hasara hiyo.
Hata Hivyo Balozi Seif alitahadharisha kwamba ipo haja kwa Uongozi huo kufikiria namna ya ya kubadilisha matumizi ya makuti katika uwezekaji wa majengo ya Hoteli hiyo ambayo ni hatari wakati linapotokea janga la moto.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwahakikishia wawekezaji wa miradi yote ya Kiuchumi na maendeleo kwamba itakuwa pamoja katika kuisaidia wakati inapopata matatizo .

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akionya kwamba wananchi wanalazimika kujenga utamaduni wa kuthamini kazi za wabunifu na wasanii

Gwiji la Taarab asilia enzi zilee Msanii Khamis Juma akiwa miongoni mwa  wabunifu na wasanii maalum  wanne mwaka huu akikonga nyoyo za washiriki wa hafla ya ugawaji wa Mirabaha kwa wabunifu na wasanii Zanzibar zilizofanyika katika Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Zanzibar.  Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
 Mwenyekiti wa Kamati ya ugawaji Mirabaha ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Mh. Salim Nassor Ali –Jazeera akimkabidhi ngao mchangiaji bora wa kusaidia sherehe hizo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Mahadhi Juma Maalim. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Mh. Salim Nassor – Jazeera akimkabidhi ngao msaidizi wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Ustaadhi Suleiman Haji Suleiman akipokea kwa niaba ya Mhe. Balozi Seif ambae Ofisi yake imegharamia sherehe hizo. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  aliyepo kati kati akimkabidhi ngao Msanii Khamis Juma baada ya kufuzu kuwa miongoni mwa wabunifu na wasanii wanne maalum katika sherehe za ugawaji wa Mirabaha Zanzibar. Wa kwanza kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Mheshimiwa Aboubakar Khamis Bakari. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.


 Al - Anisa Mwapombe Hiari tetere wa nyimbo za Taarabu aliyevuma ndani ya mwambao wa Afrika katika miaka ile akifurahia zawadi ya ngao na fedha taslim alizokabidhiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  baada ya kuwa miongoni mwa wabunifu na wasanii wanne maalum katika sherehe za ugawaji wa Mirabaha Zanzibar.  Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.

 Msanii wa Kizazi kipya Baby Jay akipokea zawadi kutoka kwa Balozi Seif kwenye sherehe ya ugawaji wa Mirabaha hapo Salama Bwawani Mjini Zanzibar. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Berry Black Kijana wa  Muziki wa Kizazi kipya akichekelea na kufurahia zawadi aliyokabidhiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwenye sherehe ya ugawaji wa Mirabaha hapo Salama Bwawani Mjini Zanzibar. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.






















Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi   wa Kamati ya ugawaji Mirabaha pamoja na washindi mbali mbali wa tuzo za wabunifu na wasanii bora kwa mwaka huu mara baada ya kukamilika jkwa sherehe hizo hapo Ukumbi wa Salama  Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar. Kushoto ya Balozi Seif ni Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Mh. Aboubakar Khamis,Msanii Khamis Juma, Msanii Mwapombe Hiari na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Mahmoud Thabit Kombo.
Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Said Ali M,barouk, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mh. Abdullah Mwinyi, Mjumbe wa Kamati ya Ugawaji Mirabaha Mh. WEanu Hafidh Ameir pamoja na Mchangiaji bora wa mashindano hayo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Mh. Mahadh Juma Maalim. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.

 Press Release:-

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alionya kwamba wananchi wanalazimika kujenga utamaduni wa kuthamini kazi za wabunifu na wasanii kwa kuona fahari kuzilipia bila ya shuruti pale wanapozitumia jambo ambalo ni uungwana na kinyume chake inahesabika kuwa ni wizi.
Alisema Serikali kupitia Ofisi ya Hakimiliki, Bodi ya Hakimiliki na Jumuiya ya Hakimiliki  Zanzibar { COSOZA } itaendelea kusimamia kazi za wabunifu na wasanii ili kuona kuwa maslahi, nguvu na jasho lao halipotei bure kutokana na ulaghai unaoendelea kufanywa na  watu wanaozipora kazi zao.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa onyo hilo wakati wa hafla ya ugawaji wa Mirabaha kwa Wabunifu na wasanii Zanzibar zilizofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Salama Bwawani Mjini Zanzibar.
Alisema Serikali itaendelea kuchukuwa hatua za kisheria za kuwadhibiti wezi hao wasiojali jasho la wenzao, lakini kazi hiyo inaweza kufanikiwa  kwa ufanisi zaidi endapo wabunifu na wasanii wenyewe  watatoa ushirikiano  kwa taasisi zinazosimamia maslahi yao katika kudhibiti wizi wa kazi zao.
“ Tushirikiane katika kuwasaka, kuwabaini na kuwaripoti katika vyombo vinavyohusika wale wote watakaobainika wanatumia kazi zenu kinyume na sheria na taratibu zilizowekwa “. Alisema Balozi Seif.
Alifahamisha kwamba Serikali haipendi kuwabughudhi wananchi wake katika biashara hata kidogo lakini hulazimika  kuchukuwa hatua  za kisheria mara moja pale ambapo uvunjaji wa sheria unapobainika ili haki ipatikane  kutokana na sheria inavyochukuwa  mkondo wake.
Makamu wa Pili wa  Rais wa Zanzibar aliwazindua wabunifu na wasanii kuwa wanapoingia kwenye mikataba pamoja  na watumiaji wa kazi zao wahakikishe kwamba makubaliano yao yanakuwa halali yanayozingatia misingi ya hakimiliki katika biashara zao.
Balozi Seif aliwataka wabunifu na wasanii wale na tahadhari  wakati wa kuweka saini Mikataba, wanakuwa na makubaliano na maelewano ya kweli ili kuwepuka mizozo baina yao na wale wanaotiliana nao saini mikataba hiyo.
Balozi Seif aliwasihi wamiliki wa vituo vya utangazaji kuheshimu haki  na kazi za wabunifu na wasanii wakielewa kwamba vituo vyao vinategemea kwa kiasi kikubwa kazi hizo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameishukuru na kuipongeza Ofisi ya Msajili wa Hakimiliki kwa kusimamia vyema ukusanyaji na ugawaji wa Mirabaha na kuitaka iendelee na utaratibu huo kwa kila mwaka.
Balozi Seif aliiomba Ofisi hiyo kuandaa mpango maalum kwa wabunifu wa michoro mbali mbali zikiwemo picha za ramani ili wafaidike moja kwa moja na mirabaha kwa makusanyo badala ya utaratibu wa sasa wa makubaliano ya mbunifu na mhitaji wa kazi husika.
Amewapongeza wabunifu na wasanii wote wa Zanzibar waliopo na wale waliotangulia mbele ya haki kwa kazi zao mbali mbali ambazo zimeitangaza  na kuijengea sifa Zanzibar katika medani ya Kimataifa.
Alisema kazi za wabunifu na wasanii hao zimechangia kuelimisha, kuburudisha, kuhamasisha na kuhifadhi utamaduni wa Taifa hili pamoja na kutoa ajira kwa wananchi walio wengi hasa kundi kubwa la Vijana na hatimae kuchangia uchumi wa Taifa.
“ Hatimiliki ukijumlisha na ubunifu na sanaa jawabu unalopata ni ajira pamoja na ukuaji wa uchumi  wa Taifa “. Alisema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Balozi Seif alisema kutokana na umuhimu wa wabunifu na wasanii, Jumuiya ya Kimataifa iliweka misingi mikuu na muhimu ya kufuatwa na nchi zote wanachama katika kusimamia ulinzi, hadhi, haki na maslahi yao  mkataba ambao unasimamiwa na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maslahi ya wabunifu na wasanii { World Intellectual Property Organisation – WIPO }.
Alisema Tanzania iliridhia mkataba huo wa Berne mwaka 1886 wakati Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikaridhia mkataba huo kwa kupitishwa sheria nambari 14 ya mwaka 2003 yenye kusimamia masuala ya Hakimiliki.
“ Sheria hiyo ndio iliyounda Ofisi inayosimamia masuala ya Hakimiliki, Bodi ya Hakimiliki na Jumuiya ya Hakimiliki maarufu COSOZA “. Alisema Balozi Seif.
Akitoa Taarifa  Msimamizi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Hakimiliki Zanzibar Bibi Mtumwa Khatibu Kheir alisema huo ni mgao wa pili wa Mirabaha kwa wabunifu  na wasanii wapatao elfu 1124 wa  zanzibar.
Bibi Mtumwa alisema Ofisi ya Hakimiliki imefanya kazi kubwa na nzuri kwa kushirikiana na kamisheni ya Utalii pamoja na Mamlaka ya Uwekezaji vitega uchumi Zanzibar { ZIPA  } katika kuziunganisha kwa wateja kazi za wabunifu na wasanii.
Hata hivyo Msimamizi na Afisa Mtendaji Mkuu huyo wa Ofisi ya Hakimiliki alitanabahisha kwamba wabunifu na wasanii wasiosajiliwa kamwe hawataweza kufaidika na mgao wa Mirabaha inayotolewa.
Bibi Mtumwa Khatibu Ameir aliwataja wabunifu na wasanii wanne waliokuwa mfano mwaka huu kuwa ni pamoja na Bwana Khamis Juma, Bibi Mwapombe Hiari, Bwana Mwalimu Ali Mwalimu na Marehemu Seif salim.
Mapema akimkaribisha Mgeni rasmi Balozi Seif, Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Mh. Aboubakar Khamis  Bakar  alisema vipaji walivyokuwa navyo wabunifu na wasanii wa  Zanzibar ni vyema vikaenziwa na kuheshimiwa kwa faida ya Taifa kwa jumla.
Waziri Aboubakar alisema Zanzibar imepata umaarufu mkubwa Duniani kutokana na ongezeko la  vipaji vya wabunifu na wasanii wake wanaoonekana kuwa kivutio kwa wageni na watalii mbali mbali wanafuatilia kazi za wabunifu na wasanii hao.
Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar aliwashukuru wachangiaji kutoka Taasisi mbali mbali za Umma na zile binafsi wakiwemo pia watu maarufu kwa uamuzi wao wa kusaidia kufanikisha kazi hiyo muhimu kwa taifa.






Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimpongeza Mwanamichezo Maarufu wa Zanzibar Moh’d Raza kwa jitihada zake za kuunga mkono sekta ya Michezo hapa Nchini.


 Mwanamichezo Maarufu Nchini ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Moh’d Raza Hassanali aliyesimama akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kabla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa Timu ya Soka ya Ofisi ya Makamu wa Pili. Wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Dr. Khalid Salum Moh’d,  wa mwanzo  kushoto ni  Mjumbe wa Kamati ya Ufundi ya Timu ya Ofisi ya Makamu wa Pili Tajo Hassan na Mwenyekiti wa Timu Haroub Gharib Bilal.

 Mwanamichezo Maarufu Moh’d Raza akimkabidhi seti ya Jezi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
 Balozi Seif akiziwashilisha Jezi kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  mara baada ya kukabilidhiwa na Mwanamichezo Maarufu Nchini Moh’d Raza.





















Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Dr. Khalid Salum Moh’d akipokea  soksi na mipira kutoka kwa Balozi Seif iliyotolewa na Moh’d Raza kwa ajili ya Tmu ya Soka ya Wizara yake. 

 Press  Release:-

Mwanamichezo Maarufu Nchini ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Moh’d Raza Hassanali alisema Kampuni yake ya Hassan and Son’s  inakusudia kuanzisha mpango maalum wa kuzisaidia timu za Maskuli Unguja na Pemba ili ile ari na vugu vugu la michezo lirejee kama zamani.
Raza alisema hayo wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi Seti za jezi, soksi na mipira Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa ajili ya Timu ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Hafla hiyo fupi iliyofanyika Ofisini kwa Balozi Seif Vuga Mjini Zanzibar pia ilihudhuriwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Dr. Khalid Salum Moh’d pamoja  na  Viongozi wa Timu ya Wizara hiyo.
Raza alisema wakati umefika kwa washirika wa michezo Nchini kuunga mkono mpango huo wa kurejesha mashindano ya mara kwa mara katika maskuli ya Zanzibar kwa lengo la kuwaandaa vijana kuwa na timu imara zitakazokuwa na uwezo wa Kimataifa.
Akipokea msaada huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alimpongeza Mwanamichezo huyo Maarufu wa Zanzibar Moh’d Raza kwa jitihada zake za kuunga mkono sekta ya Michezo hapa Nchini.
Alisema kitendo cha Mwanamichezo huyo ni miongoni mwa uzalendo aliouonyesha ambao unastahiki kuigwa na washirika pamoja na wanamichezo wengine.
Balozi Seif alisema juhudi za Mwanamichezo huyo zilipelekea kuteuliwa kuwa mshauri wa Rais anayesimamia michezo pamoja na kuwa Mwenyekiti wa Saidia Zanzibar Ishinde { SAZI } katika awamu zilizopita.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alifahamisha kwamba lengo la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambalo limo ndani ya Ilani ya chama cha Mapinduzi ni kukuza  michezo hapa Nchini.
Alishauri Taasisi zinazosimamia michezo Nchini  kwa kushirikiana na Ofisi yake ziandae utaratibu wa kuanzisha Ligi Maalum za Mawizara ya Serikali na tayari Mwanamichezo Moh’d Raza ameonyesha nia shauku ya kuzisaidia Timu hizo kwa kuzipatia vifaa endapo ligi hiyo itaasisiwa rasmi.



 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akihudhuria Mkutano wa pamoja kati ya Uongozi wa Kampuni inayohusika na masuala ya Teknolojia ya Kisasa ya mawasiliano ya Baharini { SRT } na watendaji wa sekta ya Habarini hapo Zanzibar Ocean View.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kati Kati akishindikizwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Said Mohd Dimwa Kulia yake mara baada ya kuhudhuria Mkutano wa pamoja  kati ya Uongozi wa Kampuni inayohusika na masuala ya Teknolojia ya Kisasa ya mawasiliano ya Baharini  { SRT } na watendaji wa sekta ya Habarini hapo Zanzibar Ocean View. Picha Hassan Issa - OMPR – ZNZ.
Afisa Mkuu wa Mradi wa Teknolojia ya Kisasa ya mawasiliano ya Baharini  wa Kampuni ya { SRT } kutoka Nchini Uingereza  Bwana Simon Tucker akielezea umuhimu wa kifaa cha mawasiliano kinachotumika katika vyombo vya usafiri Majini kwenye Mkutano wa pamoja na watendaji wa Sekta ya Baharini hapa Zanzibar.
Picha Hassan Issa - OMPR – ZNZ.





















Balozi Seif akizungumza na Wanahabari   mara baada ya kuhudhuria Mkutano wa pamoja kati ya Uongozi wa Kampuni inayohusika na masuala ya Teknolojia ya Kisasa ya mawasiliano ya Baharini  { SRT } ya Nchini Uingereza na  watendaji wa Taasisi zinazohusika na sekta hiyo hapo Zanzibar. Picha Hassan Issa - OMPR – ZNZ.

 
Press Release:-

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Zanzibar ikiwa ni sehemu ya Dunia hii  inahitaji kuendelea kuwa salama na tulivu kutokana na mazingira yake yaliyozunguukwa na Bahari pembe zote.
Alisema mfumo wa kisasa wa mawasiliano unaotumika katika mataifa mbali mbali Duniani uliolenga zaidi katika maeneo ya bahari  yenye kutoa utajiri mkubwa kwa   asilimia 90% ya Uchumi wa Dunia unafaa kutumika ili kuondoa shaka katika udhibiti wa uvamizi wa vitendo vya kiharamia.
Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akizungumza na Wanahabari wa Vyombo mbali mbali hapa Nchini mara baada ya kuhudhuria Mkutano wa pamoja kati ya Uongozi wa Kampuni inayohusika na masuala ya Teknolojia ya Kisasa ya mawasiliano ya Baharini  { SRT } ya Nchini Uingereza na  watendaji wa Taasisi zinazohusika na sekta hiyo hapo Zanzibar Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar.
Alisema yapo matukio kadhaa ya uvamizi wa vyombo vya Baharini yaliyowahi kuibuka  na kuripotiwa katika ukanda wa Pembe ya Afrika ambayo yalikuwa yakitekelezwa na maharamia kutokana na udhaifu wa mawasiliano uliokuwepo wakati huo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliridhika na kukubaliana na Mfumo wa kisasa waTeknolojia ya mawasiliano ya Baharini  unaotumiwa na Kampuni ya          { SRT } ya Nchini Uingereza katika Mataifa mbali mbali Duniani ambao umesaidia kupunguza wimbi la uharamia katika maeneo ya Baharini.
Akiwasilisha mada ya mfumo wa utendaji kazi wa Kampuni hiyo kwenye  Mkutano huo Afisa Mkuu wa Mradi wa Teknolojia ya Kisasa ya mawasiliano ya Baharini  wa { SRT }  Bwana Simon Tucker alisema  kifaa maalum cha Mawasiliano huwekwa kwenye chombo cha Baharini ambacho husaidia kutoa taarifa za mawasiliano.
Bw. Simon alisema chombo hicho kidogo kinachoweza kuwekwa kwenye boti au hata meli za uvuvi na abiria kinauwezo wa kusafirisha mawimbi ya mawasiliano kwa zidi ya meli 40.
Alisema mradi huo maalum wa mawasiliano ulioanzishwa mwaka 2008 tayari umekuwa ukitoa huduma katika Mataifa mbali mbali ulimwenguni ikiwemo Marekani, India na Ungereza yenyewe.
“  Asilimia 70% ya eneo lote la Dunia limezunguukwa na maji na kulifanya kuwa tegemezi kwa uchumi ulimwenguni kwa zaidi ya asilimia 90% kutokana na rasilmali ya mazao ya baharini kama samaki pamoja na usafirishaji wa mizigo pamoja na abiria “. Alifafanua Bwana Simon Tucker.
Mapema  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Maharini Zanzibar { ZMA } Nd. Abdi Omar alisema Uongozi na watendaji wa Mamlaka hiyo wanajitahidi kumarisha huduma za mawasiliano baharini ili kuijengea mazingira bora sekta hiyo iendelee kutoa huduma kwa ufanisi.
Nd. Abdi alisema hatua hiyo imezingatiwa kutokana na mabadiliko ya Dunia ya Teknolojia yaliyoibua matukio ya kiharamia ambayo yameleta hasara kubwa ya kupotea kwa mali na hata maisha ya watu katika ukanda wa Pembe ya Afrika.
“ Mkutano wetu wa hivi karibu kati yetu ZMA wenzetu wa SUMATRA  ambapo tulishirikisha watendaji wa taasisi za ulinzi wa majini na na polisi bara na Zanzibar ulilenga katika kutafuta mbinu za kujiweka tayari kukabiliana na changamoto yoyote itayojitokeza katika eneo letu “. Alisema Mkurugenzi Abdi.
Mkutano huo mfupi ulihudhuriwa na watendaji kutoka mamlaka ya usafiri wa baharini,  Mamlaka ya Uwekezaji vitege uchumi Zanzibar { ZIPA }, Mamlaka ya Mapato Tanzania { TRA }, Kodi ya Mapato Zanzibar { ZRB }, Wizara ya Fedha, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Ardhi pamoja na Tume ya Mipango.

Tuesday, 14 April 2015

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi msaada wa Vipaza sauti Amiri wa Jumuiya ya Sherehe za Siku Kuu ya Iddi Matemwe

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi msaada wa Vipaza sauti Amiri  wa Jumuiya ya Sherehe za Siku Kuu ya Iddi Matemwe Ustaadhi Kundi Choum Haji kutekeleza ahadi aliyoip[a Jumuiya hiyo wakati wa sherehe za siku kuu ya Iddi el Hajj iliyopita. Picha na Hassan Issa – OPMR – ZNZ.

Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman  Iddi akimkabidhi  mchango wa Shilingi 400,000/-  kwa kila kikundi miongoni mwa  vikundi 14 vya Ushirika wa Akina Mama vilivyomo ndani ya  Wilaya ya Kaskazini “ A “. Picha na Hassan Issa – OPMR – ZNZ.

 Balozi Seif akikabidhi Seti moja ya Jezi na Mipira kwa kila Timu ya Soka miongoni mwa timu nne zilizomo ndani ya Jimbo la Matemwe. Picha na Hassan Issa – OPMR – ZNZ.

 Balozi Seif akiangalia hodhi linalojengwa kwa ajili ya kuhifadhia maji kwenye Msikiti Mkuu wa Kijiji cha Mvuleni Kidoti Jimbo la Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Picha na Hassan Issa – OPMR – ZNZ.






















Balozi Seif akiuagiza Uongozi wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Kijiji cha Mvuleni kufanya Tathmini ya uenzi wa Vyoo ili uwahi kufunguliwa katika muda muwafaka uliopangwa. Picha na Hassan Issa – OPMR – ZNZ.

  Press Release:-

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewakumbusha Wananchi hasa akina Mama Nchini kuwaunga mkono Viongozi wenye muelekeo wa kuwasimamia vyema katika harakati zao za Maendeleo, kiuchumi na ustawi wa Jamii.
Alisema takwimu ya idadi ya watu  Nchini inaoonyesha wazi kwamba Wanawake ndio wenye uwezo wa kutumia kura zao katika kuchaguwa Viongozi watakaowafaa kwenye maeneo yao kutokana na wingi wao.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa kumbusho hilo wakati akikabidhi Vipaza Sauti kwa ajili ya Jumuiya ya Kuhifadhi Quran pamoja na Sherehe za Siku Kuu ya Kiislamu  ya Kijiji cha Matemwe Wilaya ya Kaskazini “A”  Mkoa wa Kaskazini Unguja akitekeleza ahadi aliyoitowa wakati wa Siku Kuu ya Mfunguo Tatu uliopita akiwa mgeni rasmi.
Hafla  hiyo iliambatana pia na Balozi Seif kukabidhi seti za Jezi na Mipira kwa Timu Nne wa Jimbo la Matemwe ambapo Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi akakabidhi fedha taslim kwa baadhi ya vikundi 14 vya Ushirika vya Akina Mama wa Wilaya ya Kaskazini “A” vifaa vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 7,860,000/-.
Balozi Seif alisema huu ni mwaka muhimu kwa Taifa la Tanzania ambapo Wananchi wanapaswa kuwa makini katika kufanya uamuzi  muafaka wa kura ya maoni pamoja na uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba.
Alisema uwamuzi wa Wananchi hao  endapo hautazingatia hatma yao ijayo ya miaka mitano kwa kuchaguwa viongozi makini na imara wasijetafuta visingizio vya lawama kwa  viongozi watakaowaweka madarakani.
Mapema Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akitekeleza ahadi  yake ya  kuviwezesha  Baadhi ya Vikundi vya Ushirika vya akina Mama wa  Wilaya ya Kaskazini “A “ alisisitiza umoja na mshikamano miongoni mwa Wananchi wa Wilaya hiyo.
Mama Asha alisema mshikamano huo ndio njia pekee itakayowawezesha wananchi hao kuendelea na shughuli zao za kujitafutia riziki katika hali ya amani na utulivu.
Alitanabahisha kwamba yapo Mataifa kadhaa duniani yakiwemo yale ya Bara la Afrika ambayo baadhi ya wananchi wake walijaribu kuichezea amani na hivi sasa tayari wameshatumbukia katika dimbwi la vurugu zilizozaa maafa  yaliyoacha  makovu yatayoendelea kukumbukwa milele na Mataifa hayo.
Baadhi ya Vikundi  vipatavyo 14 vya ushirika wa akina Mama wa Wilaya ya Kaskazini  “ A “  vilikabidhiwa fedha taslim shilingi Laki nne kila kimoja ambavyo ni Lamoyoni hulioni, Apewaye hupokea, Atowaye Allah pamoja na Riziki Haiwanwi.
Vyengine ni Hatujali Kitu, Tumia Jasho lako, Tushukuru Mungu, Haraka Sio Mwendo, Kheir Liwe, Tumia Jasho Lako,Wema Si Maneno, Wema wa Maskini hauna sifa, Mtaji wa Maskini pamoja na Mwanzo Mgumu.
Timu wa Mpira wa miguu zilizokabidhiwa seti za Jezi na Mipira ni pamoja na Kikobweni United, Mabundi Sports Club, Kilima Juu Sports Club pamoja na Chimbuko Sports Club.
Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipata fursa ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Kijiji cha Mvuleni Kidoti Jimbo la Nungwi.
Balozi Seif ambae aliridhika na hatua iliyofikiwa ya ujenzi huo aliuagiza Uongozi wa Msikiti huo kufanya tathmini ya makisio ya ujenzi wa vyoo vya Msikiti huo ili kukamilisha kazi yote.
Ufunguzi Rasmi wa Msikiti huo wa Ijumaa wa Mvuleni Kidoti unatarajiwa kufanywa hivi karibuni na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Braza la Mapinduzi Al – Hajj Dr. Ali Mohammed Shein.




Monday, 13 April 2015

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiongea na Wafanyakazi wa shamba la Mipira Kichwele

Mmoja wa Wafanyakazi wa shamba la Mipira Kichwele akiwasilisha malalamiko yao mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hayupo pichani wakidai kutolipwa mishahara yao kati ya miezi mitatu hadi Minane.
Mwakilishi wa Kampuni ya Agro Tec ambae pia ni Makamu Mwenyekiti wa Bidi ya Uongozi wa Kampuni hiyo Bwana Soud Moh’d Achili akitoa ufafanuzi mbele ya Balozi Seif kuhusu shutuma zilizotolewa  na Wafanykazi wa shamba la Mipira Kichwele dhidi ya Kampuni yake.





















Balozi Seif akiwaahidi Wafanyakazi wa shamba la Mipira Kichwele hatua zitakazochukuliwa na Serikali juu ya matatizo yao likiwemo la kulipwa haki zao.

   Press Release:-

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imewahakikishia wafanyakazi wa shamba la Mipira Kichwele kwamba itafanya jitihada na mbinu zote katika kuona wanalipwa mishahara yao  kati ya miezi mitatu hadi Minane wanayoidai Kampuni iliyowekeza Mradi huo ya Agro Tec kwa kipindi kirefu sasa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alitoa kauli hiyo baada ya kupokea malalamiko kadhaa yaliyowasilishwa kwake na Wafanyazi hao wakiushutumu Uongozi wa Kampuni hiyo kuwadhalilisha pamoja na  kutopewa haki zao kadhaa Mkutano uliofanyika katika kituo cha Mradi huo kiliopo pembezoni mwa Wilaya za Kaskazini “B”.
Balozi Seif alisema kwamba Kampuni ya Agro Tec haikuwa makini kujipanga katika uendeshaji mradi huo tokea kukabidhiwa kwake jambo ambalo haina tija Serikali Kuu pamoja na Wafanyakazi wenyewe.
Alisema katika kuondosha utata huo wa muda mrefu ni jambo la msingi kwa Kampuni hiyo kufanya utaratibu wa kulipa haki zinazodaiwa na Wafanyakazi hao ikiwemo zile ya mafao ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii { ZSSF } pamoja na  Fedha za likizo.
Balozi Seif alifahamisha kwamba Serikali Kuu kwa kushirikiana na Taasisi zinazosimamia uwekezaji, ukusanyaji wa Mapato, usimamiaji haki za Wafanyakazi na Mfuko wa hifadhi ya Jamii zitafanya uchunguzi wa kina ili kuona uwezo wa Kampuni hii kama unakidhi kuendelea  kuwekeza mradi huu.
“ Sisi kama Serikali kwa kushirikiana na taasisi zote husika tutauchunguza mradi huu  utendaji wake tokea Kampuni ya Agro Tec ilipokabidhiwa na hatutakuwa na muhali kuifutia kibali  Kampuni hiyo endapo haitatekeleza masharti na makubaliano yaliyowekwa ikiwemo haki za Wafanyakazi “. Alisema Balozi Seif.
“ Nakuhakikishieni wafanyakazi nyote wa shamba la Mipira kwamba haki zenu zote zitapatikana kwa mujibu wa taratibu tulizokubaliana na muwekezaji huyu hata kama kuuzwa mali zake na kufidia madeni anayodaiwa “. Alisisitiza Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwashukuru wafanyakazi hao wa shamba la Mipira lwa Kichwele kwa ustahamalivu wao wa muda mrefu ambao kwa kiasi kikubwa umesaidia kuepusha shari kati yao na Uongozi wa Kampuni n iliyowekeza mradi huo.
Mapema wakitoa malalamiko yao wafanyakazi hao wa shamba la Mipira la Kichwele walimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Bodi iliyopo hivi sasa ya  Kampuni hiyo ya Agro Tec haina maslahi kwao.
Walisema mgogoro  kati yao na Uongozi wa Kampuni hiyo ulioanza tokea mwaka 2013 umesababisha maisha yao kuwa mashakani na kukosa matumaini ya kuendesha maisha yao kupitia mradi huo.
Naye Kamishna wa Kazi Zanzibar Nd.Kubingwa Simba alisema kwamba Muwekezaji ye yote hapa Nchini hawezi kufunga mradi wake mpaka ahakikishe analipa madeni na stahiki zote kwa washirika wake.
Nd. Simba alisema kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa katika masuala ya uwekezaji Mahkama ndio yenye haki na uwezo wa kutoa maamuzi endapo muwekezaji huyo atakwenda kinyume na mkataba aliyofunga.
Kwa Upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Mali Asili Zanzibar Dr. Ased Bakar Ased alisema umri wa uzalishaji wa miti ya mirira ya kichwele na iliyoko Kisiwani Pemba iliyooteshwa mwaka 1977 umepindukia uzalishaji Kiuchumi.
Dr. Ased alisema mashamba ya mipira yameshapoteza muelekeo kutokana na bei ya bidhaa hiyo katika soko la Kimataifa imeshuka kutoka Dola za Kimarekani elfu 2,500 hadi elfu 1200 kwa Tani Moja.
“ Hakuna dalili ya bei ya bidhaa ya mpira kuongezeka kwa vile ushindani wa zao  la mpira kwa sasa haupo tena “. Alifafanua Dr. Ased Bakar Ased.
 Hivi sasa wapo Wafanyakazi 14 kati ya 160 wa shamba la mipira la Kichwele wanaoendelea na kazi kwenye mradi huo uliopewa muekezaji  kuuendesha tokea mwaka 2003.
Yapo madeni kadhaa yanayodaiwa Kampuni ya Agro Tec kutoka kwa wafanyakazi hao ambayo ni Shilingi Milioni 34,411,267 Deni la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar { ZSSF } Shlingi Milioni 3,637,000/-  deni la wagemaji Utomvu na  shilingi 21,000,000/- wafanyakazi wa Viwandani.
Mengine ni shilingi Milioni 34,027,750 wasimamizi wa wafanyakazi Mashambani, shilingi Milioni 8,400,000/- wafanyakazi Ofisini, Milioni 42,000,000/- wafanyakazi wa mipira Kisiwani Pemba na shilingi Milioni 166,000,965/- deni la likizo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi leo akiwa Mgeni rasmi katika kuwaunga mkono Vijana wa Kikundi cha Sarakasi cha Bungi Muembe Kiwete Wilaya ya Kati

Kikundi cha Sarakasi cha We are Stong Acrobatic Show cha Bungi Muembe Kiwete kikitoa Burdani wakati wa sherehe za Kutimia mwaka mmoja toke kikundi hicho kupata usajili rasmi ambapo Mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seifn Ali Iddi. Picha Hassan Issa – OMPR
Kikundi cha Sarakasi cha Muungoni Wilaya ya Kusini Kikifanya vitu vyake katika sherehe za Kutimia mwaka mmoja wa Kikundi cha Sarakasi cha We are Stong Acrobatic Show cha Bungi Muembe Kiwete. Picha Hassan Issa – OMPR
Vijana wa Kikundi cha Sarakasi cha Bihole Bungi wakitoa saluti kwa Mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwenye sherehe za Kutimia mwaka mmoja wa Kikundi cha Sarakasi cha We are Stong Acrobatic Show cha Bungi Muembe Kiwete. Picha Hassan Issa – OMPR
Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Kikundi cha sarakasi cha Muungoni Wilaya ya Kusini baada ya kumalizika kwa sherehe za kikundi cha sarakati cha Bungi muembe Kiwete. Picha Hassan Issa – OMPR
Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Kikundi cha sarakasi cha We are Stong Acrobatic Show cha Bungi Muembe Kiwete mara baada ya kumalizika kwa sherehe za kikundi hicho hapo uwanja wa michezo Bungi. Picha Hassan Issa – OMPR

















Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Kikundi cha Sarakasi cha Bihole Bungi mara tuu baara ya kumalizika kwa  sherehe za kikundi cha sarakati cha Bungi muembe Kiwete. Picha Hassan Issa – OMPR

Press Release:-  {Michezo }
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi leo alikuwa Mgeni rasmi katika kuwaunga mkono Vijana wa Kikundi cha  Sarakasi cha Bungi Muembe Kiwete Wilaya ya Kati kwenye sherehe yao ya kutimia mwaka Mmoja tokea kusajiliwa rasmi.
Sherehe ya Kikundi hicho kiitwacho We are Strong Acrobatic Show ilifanyika katika uwanja wa michezo wa Bungi na kushirikisha pia baadhi ya Vikundi vya sarakasi vya Mkoa wa Kusini Unguja.
Balozi Seif akiwa na baadhi ya Viongozi wa Wilaya ya Kati pamoja na Wananchi wa maeneo jirani ya Kijiji hicho walishuhudia burdani safi iliyoanikiza kwenye uwanja huo na kujumuisha Vikundi vya Sarakasi vya Muongoni, Bihole Bungi pamoja na wenyeji hao  We are Strong Acrobatic Show.
Akizungumza na wanamichezo hao Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliwakumbusha Wanamichezo   hao kuwa makini katika kuimarisha hali ya amani iliyopo kwa lengo la kuendelea kuwa  na fursa nzuri ya kufanya mazoezi  kwa utulivu.
Alisema Vijana wa Sarakasi wanahitaji kuungwa mkono na washirika wa michezo pamoja na Serikali Kuu, na hili litawezekana iwapo hali ya amani itaendelea kudumishwa na kila mwananchi wa Taifa hili.
Balozi Seif aliwapongeza Vijana wa Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja kwa jitihada wanazochukuwa za kuimarisha michezo   ambayo kwa hivi sasa imekuwa sehemu ya ajira hasa kwa vijana.
Katika kuunga mkono vijana hao wa Sarakasi Balozi Seif aliahidi kutafuta fursa za kuwapatia vifaa vya Michezo yao pamoja na nafasi za Taaluma nje ya Nchi kwa kuimarisha ujuzi walionao.
Mapema akisoma Risala Katibu wa CCM wa Tawi la Bungi Safia Ali Vuai alisema Kikundi hicho  cha sarakasi ambacho kiko chini ya Tawi hilo kilianzishwa mwaka 2011 kikiwa na  Vijana 30 ambapo kwa sasa wameongezeka na kufikia 50.
Safia alisema licha ya baadhi ya changamoto zinazokikumba kikundi hicho ikiwemo ukosefu wa kiwanja cha mazoezi na vifaa lakini kimepata mafanikio makubwa ya ongezeko la wanafunzi wa sarakasi pamoja kuunda urafiki na baadhi ya vikundi vya fani hiyo Zanzibar na Dara es salaam.
Balozi Seif pia aliahidi kuvipatia vikundi hivyo mchango wa fedha taslim kutokana na juhudi zao wanazochukuwa za kuhamasisha katika mikutano na shughuli za Chama cha Mapinduzi.


Mhe. Balozi Seif Ali Iddi alitoa nasaha hizo wakati akiyafunga Mafunzo ya Miezi Mitatu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Zanzibar { TEKNOHAMA

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mkuu wa Mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Zanzibar Nd. Abdullah Othman Ali wakati wa hafla ya kuyafunga mafunzo hayo hapo Skuli ya Sekondari Donge Mkoa wa Kaskazini Unguja. Kati kati yao ni Mbunge wa Jimbo la Donge Mheshimiwa Sadifa Juma Khamis, na nyuma ya Balozi Seif ni Mratibu wa Mradi unaoondesha mafunzo hayo Nd.Abdi Hamid Abeid. Picha Hassan Issa – OMPR
Mkuu wa Mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Zanzibar Nd. Abdullah Othman Ali akimpatia maelezo Balozi Seif wakati alipotembelea Darasa la mafunzo hayo hapo Skuli ya Sekondari Donge. Picha Hassan Issa – OMPR













Baadhi ya Wanafuzi wa Darasa la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Zanzibar wakishuhudiwa na Balozi Seif wakiendelea kufanya mazoezi ya vitendo katika kukabiliana na matatizo madogo madogo yanayojichomoza wakati wa matumizi wa kompyuta zao. Picha Hassan Issa – OMPR




















Mmoja wa Wanafunzi wa Darasa la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Zanzibar akiperuzi kuangalia nini kimejiri duniani kupitia mtandao wa Internet  akishuhudiwa na Balozi Seif. Picha Hassan Issa – OMPR


















Baadhi ya Wananchi na Wanafunzi wakisikiliza Hotuba ya Mgeni rasmi  Balozi Seif hayupo pichani wakati akiyafunga mafunzo ya miezi mitatu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Zanzibar hapo Skuli ya Sekondari Donge. Picha Hassan Issa – OMPR















Balozi Seif akimkabidhi Cheti Mwenyekiti wa  Jumuiya Kupambana na changamoto na kuwaendeleza Vijana Zanzibar Bibi Umukulthum kwa kusaidia uendeshaji wa mafunzo ya Teknolijia ya Habari na Mawasiliano. Kati kati yao ni Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva na Utingo Zanzibar Maalim Khamis Mussa, na kushoto ya Balozi Seif ni Mratibu wa Mradi wa Mafunzo ya Teknolijia ya Habari na Mawasiliano Abdi Hamid Abeid na Mkuu wa Mafunzo hayo Nd. Abdulla Othman Ali. Picha Hassan Issa – OMPR





















Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Jimbo la Donge, walimu na wanafunzi wa mafunzo ya Teknolijia ya Habari na Mawasiliano yaliyokuwa yakifanyika katika skuli ya Sekondari ya Donge. Kushoto ya Balozi Seif ni Mwakilishi  wa Jimbo la Donge ambae pia ni Waziri wa Elimu Mh. Ali Juma Shamuhuna, Mratibu wa Mradi wa Mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Abdi Hamid Abeid na Mwenyekiti wa Jumuiya ya ZAFAYCO Bibi Umukulthum. Kulia ya Balozi Seif ni Mbunge wa Jimbo la Donge Mh. Sadifa Juma Khamis, Mkuu wa Mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Zanzibar Nd. Abdullah Othman Ali pamoja na Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva na Utingo Zanzibar Maalim Khamis Mussa. Picha Hassan Issa – OMPR

  Press Release:-
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewaasa Vijana wanaojifunza Taaluma ya Mitandao ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kuwa makini katika matumizi bora ya mfumo huo mpya ili kulinda mila na Tamaduni zao za asili.
Alisema si vyema kuthubutu kufanya matumizi maovu way mfumo huo akijua kwamba yatawashawishi kujiingiza katika matendo yatakayowapelekea kuwa na maamuzi ya kufanya vitendo vilivyo nje ya utamaduni wao.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa nasaha hizo wakati akiyafunga Mafunzo ya Miezi Mitatu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Zanzibar { TEKNOHAMA }  yaliyoendeshwa  kwa pamoja kati ya Umoja wa Madereva na Utingo Zanzibar { UMUZA } na Jumuiya ya kupambana na changamoto na kuwaendeleza Vijana Zanzibar                { ZAFAYCO  } hapo katika Majengo ya  Skuli ya Sekondari Donge Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Alisema Dunia imekuwa na Mabadiliko makubwa ya Teknolojia ya Kisasa ya   Mawasiliano  inayokwenda kwa haraka  kiasi kwamba  Jamii za Kimataifa popote pale zilipo hupata fursa za  kuwasiliana, kushirikiana na hata kupashana taarifa kupitia mfumo huo.
Hata hivyo Balozi Seif alifahamisha kwamba upo upotoshaji wa makusudi unaoendelea kufanywa na baadhi ya Watu ikiwemo pia mitandao ya Kijamii katika matumizi  mabaya ya Mitandao hiyo  jambo ambalo vijana hao wanapaswa kujiepusha nalo.
Alisema Jamii imekuwa ikishuhudia kashfa na matusi yaliyosheheni kwenye baadhi ya Mitandao hiyo tabia ambayo inadhalilisha watu wanaokusidia kuwachafulia wakiwa hawana hatia na pia kwenda kinyume na Haki za Kibinadamu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameipongeza Jumuiya ya kupambana na changamoto na kuwaendeleza Vijana Zanzibar  { ZAFAYCO } pamoja na  Umoja wa Madereva na Utingo Zanzibar  { UMUZA } kwa jitihada zao za kuwanoa vijana katika masuala yanayowagusa moja kwa moja.
Alisema kazi zinazoendeshwa na Taasisi hizo za Kiraia zimekuwa zikiisaidia Serikali Kuu katika azma yake ya kuwapatia taaluma  hasa ile inayokwenda na wakati wa sasa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Wananchi wake katika maeneo  mbali mbali Nchini Mjini na Vijini.        
Balozi Seif alifahamisha kwamba Serikali katika kuziunga Mkono  Taasisi hizo za Kiraia  itajitahidi katika kuona inaunga mkono kazi za Taasisi hizo kwa watendaji na wakufunzi wake kuwawezesha kutoa mafunzo kama hayo kwa Vijana wa Kisiwa cha Pemba.
Katika kuunga mkono jitihada za Jumuiya ya kupambana na changamoto na kuwaendeleza Vijana Zanzibar pamoja na Umoja wa Madereva na Utingo Zanzibar amehidi kuchangia nguvu katika upatikanaji wa Mashine ya Projector pamoja na ile ya Fotokopi ili kuwarahisishia watendaji wa Taasisi hizo kuendesha vyema mradi wao wa mafunzo kwa Vijana.
Akisoma Risala Mkuu wa Mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Nd. Abdullah Othman Ali alisema zaidi ya vijana 368 wa Wilaya Tano za Unguja tayari wameshaptiwa mafunzo hayo yanayochukuwa muda wa miezi mitatu.
Nd. Abdullah alisema kwa kuelewa matatizo na changamoto zinazowakabili vijana katika maeneo mbali mbali Nchini Taasisi hizo zimebuni mradi huo  kwa kuwakusanya pamoja vijana ili kuwapatia mafunzo yanayowawezesha kujiepuisha na makundi maovu.
Hata hivyo Nd. Abdullah alitaja baadhi ya changamoto zinazojichomoza katika mafunzo hayo akizitaja kuwa ni pamoja na muitiko mdogo wa washiriki wa mafunzo hayo hasa katika sehemu za Vijijini pamoja na uhaba wa vifaa vya kujifunzia kama Kompyuta.
Naye Mratibu wa Mradi wa mafunzo hayo wa Jumuiya ya kupambana na changamoto na kuwaendeleza Vijana Zanzibar  { ZAFAYCO } Nd. Abdi Hamid Abeid alisema Jamii inaweza kupunguza uchafuzi wa mazingira endapo itakijika katika katumizi zaidi ya Kompyuta.
Alisema Wanafunzi wa Skuli za Sekondari na Vyuo Vikuu hivi sasa wamekuwa wakitumia kumbu kumbu za vitabu na baadhi ya maandisi na machapisho kupitia mtandao huo badala ya mfumo wa zamani wa kutumia vitabu vilivyokuwa vikitengenezwa kwa karatasi zinazotokana na kukatwa kwa miti.
Mratibu Abdi Hamid alifafanua kwamba upo mfano hai wa matangazo ya matokeo ya mtihani wa Darasa la Saba mwaka huu yaliyochapishwa katika mtandao wa Kompyuta mfumo ambao umeisaidia Serikali Kuu kuwepuka kutoka matangazo ya Redio ambayo yangegharimu mamilioni ya Fedha.
Alieleza kwamba Jamii lazima ikubali kwamba Kompyuta ni rafiki mzuri kwa mtumiaji ambapo  hali hii iko wazi kutokana na mfumo wa watumiaji wa simu za mkono hivi sasa kupata huduma za vocha kwa njia ya kurusha.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif katika ufungaji wa mafunzo hayo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano alikabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo hayo pamoja na Skuli zilizotoa wanafunzi hao.