Balozi Wa Jamuhuri ya Ireland Nchini Tanzania Balozi Fionnuala
Gilsenan aliyefuatana na ujumbe wa Nchi yake uliofanya ziara hapa Zanzibar akisalimiana na Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi nje ya Ofisi yake Vuga Mjini Zanzibar. Kati kati
yao ni Waziri wa Nchi Maendeleo ya Biashara na Ushirikaino wa Ireland Bwana
Sean Sherlock. Picha Hassan Issa –
OMPR – ZNZ.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifanya
mazungumzo na ujumbe wa Jamuhuri ya Ireland ukiongozwa na Waziri wa Nchi
Maendeleo ya Biashara na Ushirikaino wa Ireland Bwana Sean Sherlock. Picha Hassan Issa –
OMPR – ZNZ.
Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya Pamoja na Waziri wa Nchi Maendeleo ya Biashara na Ushirikaino wa Ireland Bwana Sean Sherlock kulia yake baada ya kumaliza mazungumzo yao. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Balozi Seif Kati Kati akiw na Mgeni wake Waziri wa Nchi Maendeleo ya Biashara na Ushirikaino wa Ireland Bwana Sean kulia yake pamoja na Waziri wa Kilimo na Mali Asili Zanzibar Dr. Sira Ubwa Mwamboya wakibadilishana mawazo mara baada ya mazungumzo yao. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya Pamoja na Waziri wa Nchi Maendeleo ya Biashara na Ushirikaino wa Ireland Bwana Sean Sherlock kulia yake baada ya kumaliza mazungumzo yao. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Balozi Seif Kati Kati akiw na Mgeni wake Waziri wa Nchi Maendeleo ya Biashara na Ushirikaino wa Ireland Bwana Sean kulia yake pamoja na Waziri wa Kilimo na Mali Asili Zanzibar Dr. Sira Ubwa Mwamboya wakibadilishana mawazo mara baada ya mazungumzo yao. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Press Release:-
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametoa wito kwa
Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Jamuhuri ya Ireland kuitumia fursa ya
uwekezaji iliyopo Zanzibar na Tanzania kwa ujumla katika kuwekeza miradi yao ya
Kiuchumi na maendeleo.
Alisema
uwekezaji wa washirika hao wa maendeleo nchini Tanzania utaongeza nguvu katika
kuimairisha uhusiano wa Kidiplomasia uliopo kati ya Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania na Ireland.
Akizungumza
na Ujumbe wa Jamuhuri ya Ireland ukiongozwa na Waziri wa Nchi Maendeleo ya
Biashara na Ushirikaino wa Ireland Bwana Sean Sherlock hapo Ofisini kwake Vuga
Mjini Zanzibar Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema Zanzibar
na Tanzania bado zina mazingira mazuri na rasilmali zinazoweza kutumika katika
uwekezaji.
Balozi Seif
aliwahakikishia wawekezaji wa Ireland kwamba licha ya kwamba Taifa la Tanzania
linakabiliwa na kura ya Maoni pamoja na Uchaguzi Mkuu mwaka huu lakini litaendelea
kubakia katika hali ya amani na utulivu.
“ Tunawatoa
hofu wa Irish watakaoamua kuja kuwekeza miradi yao ya kibiashara kwa kusaidia
uchumi ya Nchi wasiwe na wasi wasi wowote kwani Tanzania itaendelea kubakia
kuwa kisiwa cha amani Duniani “. Alisema Balozi Seif.
Naye Waziri
wa Nchi Maendeleo ya Biashara na Ushirikiano wa Ireland Bwana Sean Sherlock
alimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwamba uhusiano
kati ya Ireland na Tanzania utaendelea kuimarishwa Kwa ustawi wa Wananchi wa
pande zote mbili.
Bwana Sean
Sherlock`alisema uhusiano huo utaelekezwa zaidi katika kuona wataalamu wa sekta
mbali mbali za Maendeleo wa Ireland hasa katika sekta ya Kilimo na utalii
wanaongeza nguvu zao za kitaalamu kwa kusaidia wataalamu wazalendo.
Waziri wa
Nchi Maendeleo ya Biashara na Ushirikaino wa Ireland Bwana Sean Sherlock
alisisitiza kwamba Nchi yake itajitahidi kuunga mkono juhudi za Zanzibar na
Tanzania kwa ujumla katika kusaidia kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya
tabia nchi zinazoonekana kuiikumba Dunia hivi sasa.
Mapema
Waziri wa Kilimo na Mali Asili Zanzibar Dr. Sira Ubwa Mwamboya aliueleza Ujumbe
huo wa Ireland kwamba uimarishaji wa
miundo mbinu katika Sekta ya Kilimo ni jambo la msingi lililopewa kipaumbele na
Wizara hiyo.
Dr. Sira
alisema hatua hiyo ya Serikali kupitia Wizara husika ya Kilimo imekuja kufuatia
Wananchi walio wengi ndani ya Visiwa vya Zanzibar ambao wanafikia zaidi ya asilimia 80%
wanaendesha maisha yao kwa kutegemea sekta mama ya kilimo.
Alifahamisha
kwamba Wizara ya Kilimo na Mali Asili Zanzibar inaendelea ya juhudi za
kukabiliana na mabadiliko ya Tabia Nchi ikitumia wataalamu wake kwa kushirikiana
na washirika wa Maendeleo ndani na nje ya Nchi.
Naye Katibu
Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar Bibi Amina Khamis alisema Dira ya
Maendeleo ya Zanzibar imeundwa maalum na Serikali kuu kwa lengo la kusaidia
mipango ya Maendeleo katika kuimarisha Kiuchumi.
Bibi Amina
alisema Mpango wa kupunguza umaskini Zanzibar MKUZA umetoa fursa pana zaidi
katika sekta za Kilimo na Utalii ambazo zimeonyesha muelekeo wa mzuri wa
kupunguza wimbi la ukosefu wa ajira unaowakumba zaidi Vijana wanaomaliza masomo
yao ya sekondari.