Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa pamoja na watendaji wa wodi ya
wagonjwa wa Kifua Kikuu alipofanya ziara ya ghafla katika Hospoitali Kuu ya
Mnazi mmoja kuangalia hali ya usafi wa vyoo kwenye Wodi hiyo. Kulia ya
Balozi Seif ni Mhandisi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Yahya Makame Ameir. Picha Hassan Issa –
OMPR – ZNZ.
Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa pamoja na watendaji wa wodi ya
wagonjwa wa Kifua Kikuu alipofanya ziara ya ghafla katika Hospoitali Kuu ya
Mnazi mmoja kuangalia hali ya usafi wa vyoo kwenye Wodi hiyo. Picha Hassan Issa –
OMPR – ZNZ.
Balozi Seif akiangalia hasara ilizozikumba baadhi ya nyumba
zilizoathirika kwa upepo katika Jimbo la Kwamtipura Mjini Zanzibar. Kulia ya Balozi
Seif ni Sheha wa Shehia ya Kwamtipura Bwana Machano Salum Khamis, Mwakilishi wa
Jimbo la Kwamtipura Mh. Hamza Hassan Haji
na kushoto yake ni Mbunge wa Jimbo hilo Mh. Kheir Khamis. Picha Hassan Issa –
OMPR – ZNZ.
Balozi Seif alionyesha masikitiko yake wakati akiiangalia moja ya
nyumba zilizopatwa na maafa ya upepo iliyopo pembezoni mwa skuli ya Msingi ya
Kwamtipura. Picha Hassan Issa –
OMPR – ZNZ.Balozi Seif akiwafariji baadhi ya wananchi wa Jimbo la Kwamtipura ambao Nyumba zao zimepata maafa ya Upepo mkali uliovuma juzi na jana mchana. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Balozi Seif akimkabidhi vyakula na baadhi ya Vifaa Sheha wa Shehia ya Kwamtipura Bwana Machano Salum Khamis kwa ajili ya kuwafariji wananachi waliopatwa na janga na maafa ya upepo Kwamtipura. Kulia ya Balozi Seif ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Press Release:-
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewaagiza watendaji wa Hospitali Kuu ya Mnazi mmoja kuacha
tabia ya kuyafumbia macho matatizo yanayoibuka katika utendaji wao wa kazi na badala yake waiarifu Serikali
Kuu ili hatua za dharura zichukuliwe katika kuyakabili matatizo hayo.
Alisema
kuendelea kuyaacha matatizo hayo yasambae mbali ya kuchafua mazingira lakini pia yanaweza
kusababisha maambukizi ya maradhi na kuwaongezea wagonjwa mtafaruku unaoweza
kuepukika.
Balozi Seif
Ali Iddi alitoa agizo hilo alipofanya ziara ya ghafla kuangalia hali ya usafi sehemu
ya vyoo vya wodi ya wagonjwa wa Kifua
Kikuu katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar.
Ziara hiyo
ya Balozi Seif imekuja kufuatia Taarifa
za Shirika la Utangazi Zanzibar {
ZBC } zilizoelezea hali isiyoridhisha katika sehemu hizo ambayo ilileta
mtafaruku kwa Wagonjwa walioazwa kwenye wodi hiyo.
Balozi Seif
alisema yeye kama Kiongozi Mkuu wa shughuli
za Serikali atakuwa tayari wakati wowote kutoa msaada au ushauri wake katika kutanzua matatizo
ambayo Viongozi wa Taasisi hiyo
wameshindwa kuchukuwa hatua.
Alisema
Wagonjwa pamoja na wananchi wamekuwa
wakilalamikia kero, changamoto na
hata matatizo yanayowakabili katika kupata huduma za afya kwenye Hospitali ya Mnazi Mmmoja ambayo yamekuwa
yakisababishwa na baadhi ya watendaji wazembe.
“ Msifikie
pahala mkawa na tabia ya kuvilaumu
vyombo vya Habari kwa kuwapasha Habari Wananchi juu ya uzembe mnaoendelea kuufanya katika
maeneo yenu ya Kazi “. Alionya Balozi Seif.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar alielezea kwamba Vyombo vya Habari vitaendelea kuwa na
haki na wajibu wa kutoa Taarifa kwa umma
matukio ya uzembe unaofanywa na baadhi ya watendaji hao.
Wakati huo
huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alifanya ziara ya
kuwafariji wananchi wa Jimbo la Kwamtipura ambao nyumba zao zimeathirika kwa
upepo mkali uliovuma ghafla juzi na jana mchana.
Balozi Seif
ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Maafa Zanzibar alipata wasaa wa
kuziangalia Nyumba sita za wananchi hao ambazo baadhi yake zimeezuka kabisa
mapaa yake.
Sheha wa Shehia ya Kwamtipura Bwana Machano Salum
Khamis { Mbonga } alimueleza Makamu wa ili wa Rais Kwamba upepo huo uliovuma
juzi na jana mchana umeezua baadhi ya mapaa nyumba sita ambazo nyengine
zimepata athari na kuta zake.
Sheha
Machano alisema uongozi wa Shehia ulikutana na waathirika hao kuanza kufanya tathmini
ya hasara ya nyumba zilizopatwa na maafa hayo na kuchukuwa hatua za
dharura za uhifadhi wa familia hizo.
Naye
Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipuira Mh. Hamza Hassan Juma alisema Uongozi wa
Kamati ya Jimbo la Kwamtipura , wananchi na familia zilizopatwa na maafa hayo
zilishirikiana pamoja katika kujaribu kurejesha hali ya kawaida ya mazingira ya
nyumba hizo.
Mh. Hamza
alisema hatua hiyo iliyochukuliwa ya
dharura kwa pamoja imeweza kuleta faraja kwa familia hizo kurejea katika mazingira ya
hali ya kawaida.
Akizungumza
na familia za waathirika wa maafa hayo ya upepo katika skuli ya Maandalizi ya
Kwamtipura Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif aliwataka Wananchi
hao mkuwa na subira katika kipindi hichi cha maafa.
Balozi Seif
aliyeambatana na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi na kugawa sadaka kidogo kwa
familia za maafa hayo alisema ameshtuka mara baada ya kusikia tukio hilo
lililoleta hasara kubwa kwa familia hizo.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar amewashukuru
Wananchi na watu wenye uwezo kwa moyo wao waliouonyesha katika kujaribu kusaidia familia hizo wakati
wa tukio hilo.
Alisema
linapotokeza tatizo miongoni kwa mmoja kati ya jamii ni vizuri tatizo hilo
likawa na watu wote katika kulitafutia ufumbuzi wa pamoja na si vyema kwa
baadhi ya watu kufurahia majanga yanayowapata wenzao kwa sababu tu za itikadi
za kisiasa.