Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani hapa Zanzibar Dr.
Andermichael Ghirmay akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibnar Balozi
Seif hapo Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dr. Saleh Mohammed Jidawi. Picha Hassan Issa
–OPMR –ZNZ.
Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani hapa Zanzibar Dr. Andermichael Ghirmay akimuelezea Balozi Seif Mikakati ya WHO iliyoweka katika kuisaidia Zanzibar.
Picha Hassan Issa –OPMR –ZNZ.
Press Release:-
Mwakilishi
wa Shirika la Afya Duniani Hapa Zanzibar Dr. Andemichael Ghirmay ameishauri Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
kujiweka tayari kukabiliana na miripuko ya maradhi yoyote
yanayoweza kutokea visiwani ili kulinda
ustawi wa Wananchi na wageni wanaoingia
Nchini..
Alisema
Zanzibar imekuwa kituo kikubwa kinachopokea watu wengi kutoka nchi mbali mbali Duniani
kufuatia kuimarika kwa Sekta ya Utalii kiasi kwamba tahadhari ya huduma za afya
kwa wananchi pamoja na wageni wanaoingia nchini ni vyema ikazingatiwa kwa umakini.
Dr.
Andemichael Ghirmay alitoa ushauri huo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi huko Ofisini kwa Balozi iliyopo
ndani ya Jengo la Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Alisema
juhudi za pamoja kati ya Serikali, watendaji wa Sekta ya Afya kwa kushirikiana
na Taasisi na mashirika ya maendeleo ya Kitaifa na Kimataifa lazima zichukuliwe
katika kudhibiti maradhi hasa yale ya miripuko ambayo mengi kati yao huchipuka
kutokana na maingiliano ya wasafari za Kimataifa.
Mwakilishi
huyo wa Shirika la Afya Duniani hapa Zanzibar Dr Andemichael ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
kupitia Wizara ya Afya kwa utayari wake ilipojiandaa kukabiliana na maradhi ya
Ebola endapo yangetokea nchini ambayo yaliwahi kuenea Magharibi mwa Nchi za Bara la Afrika katika
miezi ya hivi karibuni.
Dr.
Andemichael Ghirmay alisema katika kuimarisha huduma za Afya kwa Nchi
wanachama Shirika hilo la Afya Duniani
litaendelea kutoa msukumo zaidi wa kitaalamu kwa Zanzibar katika mapambano dhidi ya maradhi
mbali mbali yanayowasumbua wananchi.
Alieleza
kwamba Shirika hilo katika mipango yake sita iliyojipangia ya kutoa elimu,
Ushauri na kusaidia Utafiti kwa Nchi wanachama
Zanzibar imo katika mchakato wa kuendelea kuungwa mkono na shirika hilo katika kupambana na maradhi mbali
mbali sambamba na kusaidia Utafiti katika maradhi hayo.
Mwakilishi
huyo wa shirika la Afya Duniani Dr. Andemichael Ghirmay amepongeza ushirikiano
anaoendelea kuushuhudia uliopo kati ya Wananchi, Wafanyabiashara pamoja na
Viongozi wao wa Majimbo katika ujenzi wa Vituo vya Afya katika Majimbo yao.
“ Mimi kama
Mtaalamu wa Sekta ya Afya nimefarajika sana kuona mshikamano uliopo kati ya
Wabunge na Wawakilishi kwa kushirikiana na wafanyabiashara pamoja na wananchi
wao katika ujenzi wa vituo vya huduma za Afya katika Majimbo yao“. Alisema Dr. Andemichael
Ghirmay.
Akitoa
shukrani zake kwa mchango mkubwa
unaotolewa na Shirika la Afya Duniani { WHO } hapa Zanzibar Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi alisema Zanzibar imepiga hatua kubwa katika sekta ya Afya kufuatia
kuungwa mkono na Shirika hilo.
Balozi Seif
alisema zipo huduma nyingi za afya zinazoendelea kutolewa katika Hospitali
mbali mbali kubwa sambamba na vituo vya Afya vya Wilaya na Vijiji ambazo msingi wake mkubwa unatokana na shirika
hilo.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar aliliomba Shirika la Afya Duniani kupitia Mwakilishi
wake huyo hapa Zanzibar liendelee kuisaidia Zanzibar kiuwezeshaji, vifaa pamoja
na Taaluma ili ifikie lengo lake la kutoa huduma za afya kwa wananchi
waliowengi Mjini na Vijijini.
Alisema Sera
ya Serikali kupitia Wizara ya Afya ni
kuona wananchi wote ndani ya Visiwa vya Unguja na Pemba wanaendelea kupata huduma za afya si zaidi ya
umbali wa kilomita tano kwenye makazi wanayoishi.
Mapema
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dr. Saleh Mohamed Jidawi alisema
kwamba Uongozi wa Shirika la Afya
Duniani umekuwa karibu mno na Wizara ya Afya Zanzibar.
Dr. Jidawi
alisema Shirika hilo ni kiungo kikubwa kinachoendelea kuisaidia Zanzibar
katika mapambano yake dhidi ya udhibiti
wa maambukizi ya vizuri wa Ukimwi, chanjo kwa akina Mama Wajawazito na Watoto pamoja na kukabiliana na
maradhi ya kichocho.
“ Wizara ya Afya
tumefanikiwa vyema katika kupambana na udhibiti wa maradhi ya Kichocho na
maambukizi ya kuenea kwa virusi vya ukimwi hapa nchini kutokana na kuungwa
mkono na wenzetu wa WHO “. Alisema Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Afya Zanzibar.
Alisema
mchango wa Utafiti na utaalamu wa Shirika shirika hilo katika mapambano dhidi
ya maradhi ya Malaria umeiwezesha Zanzibar kudhitibi maradhi ya Malaria chini
ya Asilimia 0.6%.