Baadhi ya Wanawake walioshiriki kwenye Kongamano la Wanawake na
Uongozi katika Katiba inayopendekezwa lililoandaliwa na Taasisi ya
Mwanaharakati Siti Binti Saad lililofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Grand
Palace Malindi Mjini Zanzibar.
Picha Hassan Issa - OMPR – ZNZ.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akilifunguwa Kongamano la Wanawake na Uongozi katika Katiba inayopendekezwa lililofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Grand Palace Malindi Mjini Zanzibar. Picha Hassan Issa - OMPR – ZNZ.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mh. Abdulla Mwinyi akitoa nena la shukrani kwa Mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya kulifungua Kongamano la Wanawake na Uongozi. Picha Hassan Issa - OMPR – ZNZ.
Mtangazaji wa Zamani wa Kituo cha Matangazo ya Televisheni Zanzibar Karume House Bibi Neema Mussa Maisara akiipitia Katiba iliyopendekezwa kwenye Kongamano la Wanawake na Uongozi hapo Grand Palace Malingi Mjini Zanzibar. Kulia yake ni msanii maarufu Zanzibar Bi Tele, Naibu Katibu Mkuu wa Wazazi Zanzibar Bibi Salama Aboud Talib na Makamu mwenyekiti Mstaafu wa UWT Zanzibar Bibi Mvita Mussa Kibendera.Picha Hassan Issa - OMPR – ZNZ.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad wa kwanza kulia Bibi Nasra Moh’d Hilal akiwa pamoja na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi kulia yake wakiipitia Katiba iliyopendekezwa kwenye Kongamano la Wanawake na Uongozi hapo Grand Palace Malindi. Picha Hassan Issa - OMPR – ZNZ.

Press Release:-
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif li Iddi amewanasihi akina mama Nchini kwamba mwaka huu ni wa kupata kile
wanachokihitaji kwa karne nyingi zilizopita katika kuongeza kasi ya ushiriki
wao kwenye uchaguzi Mkuu ujao unaojenga
mazingira yao katika mamlaka ya maamuzi ya Taifa hili.
Alisema
wakipoteza fursa hii mwaka huu inaweza kuwachukuwa miaka mingi ijayo kupatikana
kwake kwa vile wasiopenda maendeleo ya Wanawake bado wapo ndani ya Taifa hili.
Balozi Seif
Ali Iddi alieleza hayo wakati akilifungua Kongamano la Mwanamke na Uongozi
katika Katiba inayopendekezwa lililoandaliwa na Taasisi ya Mwanaharakati Siti
Binti Saad lililofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Grand Palace Kinu cha Taa
Malindi Mjini Zanzibar.
Alisema mara
nyingi wanaume kwa kupendelea kuendeleza mfumo dume wako mstawi wa mbele
kupinga wanawake kupata haki zao kama inavyoshuhudiwa hivi sasa hapa nchini
katika kipindi hichi cha mpito kuelekea kwenye kura ya maoni.
Balozi Seif
lifahamisha kwamba ipomiofano inayoonyesha wazi kwamba wana harakati na
wanamageuzi katika maeneo mbali mbali Duniani imewachukuwa takriban miaka zaidi
ya 100 ya kupata haki wanawake katika kupiga kura kama wanaume.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar alieleza kuwa Utafiti katika fani ya Uongozi
inaonyesha kwamba taasisi zenye Uongozi ulio sawa kijinsia hufanya vyema ikilinganishwa na zile
zinazoendeshwa na kutawaliwa na mfumo dume.
Alisema
Taifa ya Tanzania imeliona tatizo hili na tayari imejaribu kulitafutia ufumbuzi
kwa kupendekeza Katiba Mpya inayotoa nafasi kwa akina mama kushiriki sawia na
wanaume katika vyombo vya maamuzi kama Bunge.
“ Bila shaka
tyunaamini Bunge la Hamsini kwa Hamsini litakuwa na ufanisi zaidi kuliko bunge
la sasa hivi. Hali kama hiyo tunaamini itakuwepo pia kwenye vyombo vyengine vya
kupitisha maamuzi kama Baraza la Mawaziri na Kadhalika “. Alifafanua Balozi
Seif.
Alisema
kitwakimu idadi ya Wanawake hapa Nchini bado ni kubwa kwa asilimia 51% ikilinganishwa na wanaume. Hivyo uwezekano wa
kupita kirahisi Katiba iliyopendekezwa ni kiubwa zaidi iwapo akina mama hao
watajitokeza kwa wingi kuipigia kura ya ndio.
Balozi Seif
alisisitiza kwamba Katiba iliyopendekezwa endapo itafanikiwa kupita itasaidia
kufungua milango mingi ya fursa za Uongozi kwa akina mama walio wengi hapa
Nchini.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar aliwataka wanawake Nchini kujipanga vizuri katika
kushika nafasi mbali mbali za uongozi wa Taifa hili lakini cha msingi kwao hilo
litafanikiwa endapo wataamua kujitokeza kuomba nafasio hizo.
Alisema kama
ilivyokuwa muhimu kujitokeza kwao kuomba kuchaguliwa lakini muhimu pia kuchagua
wagombea wanaowapenda ambao watajikita
zaidi katika kukubali kuwatumikia.
“ Mkikosea
mwaka huu kumchagua kiongozi asiyefaa, ina maana kwamba mtakuwa mmekosea kwa
kipindi cha miaka mitano ijayo “. Alitahadharisha Balozi Seif.
Balozi Seif
aliitanabahisha jamii kwamba kuibeza Katiba iliyopendekezwa ni sawa na kubeza
juhudi za wanawake walizochukuwa miaka mingi iliyopita katika kudai haki zao na
hatimae kufanikiwa kuziingiza katika sheria mama ya nchi ambayo ni Katiba iliyopendekezwa.
Aliwashauri
akina mama kuwapuuza akina Baba hao hata
kama wanatoka katika vyama wanavyovipenda au Taasisi za Kidini au zile za
kiraia wanazozifuata na badala yake watumie busara alizozichukuwa Mwanaharakati
Siti Binti Saad.
Alisema jibu
sahihi la kebehi na jeuriza zinazoendelea kutolewa na baadhi ya akiba Baba ni
kwa akina mama hao kutumia busara kwa kuipigia kura ya ndio Katiba
inayopendekezwa.
Balozi Seif alieleza
kuwa kwa mujibu wa Ibara ya 57 ya Katiba inayopendekezwa zipo haki kadhaa za
wanawake zitakazosaidia kuondoa baadhi
ya mfumo dume iliokuwa ukiwakandamiza kwa miaka kadhaa iliyopita.
Alizitaja
baadhi ya haki hizo kwa mujibu wa ibara hiyo y 57 kuwa ni pamoja na
kuheshimiwa, kuthaminiwa na kutambuliwa utu wa mwanamke, kulindwa dhidi ya
ubaguzi, udhalilishwaji, dhulma, unyanyasaji, ukatili wa kijinsia na mila
potovu.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar aliipongeza Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti
Saad kwa juhudi zake ilizochukuwa katika kuandaa kongamano hilo la Mwanamke na
Uongozi katika Katiba inayopendekezwa.
Balozi
Seif alisema si rahisi kwa Taasisi
change kama hiyo kufanya mambo makubwa kama hayo lakini imeonyesha pamoja na uchanga
huo imeweza kufanya masuala mazito ya
kupigiwa mfano.
Mapema
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwanaharakati Siti Binti Saada Bibi Nasra Moh’d Hilal
aliwatanabahisha akina mama wenzake kwamba huu ni wakati mzuri kwao kuitumia
nafasi iliyokuwemo ndani ya Katiba iliyopendekezwa katika kujiimarisha
kiuongozi.
Bibi Nasra
alisema njia pekee katika kuhakikisha wana wake hao wanaitumia fursa hiyo ni
kujitokeza kwa wingi kushiriki katika kupiga kura ya maoni sambamba na ushiriki
wa uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu.