Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
akisalimiana na Wasanii 11 wa Kizazi kipya wanaoendesha Tamasha la Uzalendo
Tanzania kabla yha klulizindua rasmi kwenye uwanja wa amani Mjini Zanzibar. Picha Hassan Issa – OMPR
– ZNZ.
Balozi Seif akitoa hotuba ya kulizindua Tamasha la Uzalendo Tanzania kwenye uwanja wa Amani lililoshuhudia na mamia ya wapenda burden hapa Zanzibar. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Msanii wa Kizazi Kipya Miki wa Pili akitoa shukrani kwa Serikali zote mbili Nchini Tanzania kuunga mkono kazi za wasanii zilizokuwa hazitambuliwi katika kipindi cha miaka kumi iliyopita. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Mashabiki wa Burdani ndani ya Viunga vya Mji wa Zanzibar wakiserebuka kwenye Tamasha la Uzalendo Tanzania lililofanyika katika Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar.
Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Umati wa mashabiki wa Burdani wakishuhudia waimbaji mbali mbali wa Kizazi Kipya wakifanya vitu vyao katika Jukwaa maalum lililojengwa pembezoni mwa Uwanja wa amani kwenye Tamasha la Uzalendo Tanzania. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.

Press Release:-
Kundi
la wasanii kumi na moja wa kizazi
kipya Ndani ya Tanzania leo limeuvamia
uwanja wa michezo Amani kufanya Tamasha la Pili la Uzalendo Tanzania la Mwaka
2015.
Tamasha hilo
lililoasisiwa Mwaka Jana Mjini Dodoma na
Rais wa Jamuhuri ya Muungano w Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete lina lengo la
kueneza ujumbe wa kudumisha amani na Umoja Miongoni mwa Watanzania wote.
Mamia ya
Vijana na wapenda burdani walionekana kumiminika katika uwanja huo wa amani kushuhudia
waimbaji maarufu wa Kikazi kipya wakifanya vitu vyao jambo ambalo liliwafanya
wengi wa mashuhuda hao kuwacha viti vyao na kuanza kuserebuka.
Balozi Seif
Ali Iddi alisema kwamba wasanii Nchini Tanzania wana dhamana kubwa katika
kuhakikisha Taifa linaendelea kuwa na amani na utulivu kupitia fani yao ya sanaa.
Akilizindua
Tamasha la Pili la Uzalendo Tanzania la Mwaka 2015 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
alisema wasanii ndio kioo cha jamii kinachoweza kutumika katika kufikisha
ujumbe na hata masuala ya maendeleo ya Kijamii.
Alisema
mchango wa wasanii katika jukumu kubwa linalolikabili taifa ndani ya mwaka huu
wa 2015 kwenye kura ya maoni sambamba na uchaguzi Mkuu wa Mwezi wa Oktoba ni
muhimui sana.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaomba wasanii hao kuhakikisha kwamba suala la
Amani linakuwa ndio dira itakayowapa
mwanga wa kuendeleza shughuli zao za sanaa popote pale Nchini Tanzania.
Alisema
Zanzibar na Tanzania kwa ujumla ni kisiwa cha amani Duniani. Hivyo juhudi za
pamoja kati ya wasanii na wananchi zinahitajika ili kuona lulu hiyo ya amani
Nchini Tanzania inaendelea kudumu.
Mapema
Mjumbe wa Kamati ya Tamasha hilo Nd. Shaib Ibrahim Mohammed alisema kwamba hilo
ni tamasha la kwanza kufanyika hapa Zanzibar likiwa na ujumbe wa kuendelea
kusisitiza umuhimu wa kudumisha amani, Umoja na Upendo miongoni mwa Jamii hapa Tanzania.
Akitoa
shukrani mwa niaba ya Kundi hilo Msanii Miki wa Pili alizishukuru na
kuzipongeza Serikali zote mbili Nchini Tanzania kwa kufahamu umuhimu na mchango
wa Wasanii.
Miki alisema
fani ya sanaa ndani ya ardhi ya Tanzania ilikuwa ikitambuliwa kama kazi ya
kihuni katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.
Alisema
Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba wana haki ya kupongezwa kwa kujenga historia
ya kudumu iliyoainisha umuhimu wa kutambiliwa kwa kazi za wasanii na kupelekea
kuingizwa ndani ya Katiba inayopendekezwa.