Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Kuwaenzi Waasisi wa Taifa la Tanzania hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Kulia
ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo Kanal Mstaafu Kabenga Nsa
Kaisi na kushoto ya Balozi na Mke wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Zanzibar
Mama Fatma Karume. Picha na Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Press Release:-
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali alisema kwamba kizazi kipya kinapaswa kuelewa azma ya waasisi wa Taifa la Tanzania Marehemu
Mzee Abeid Aman Karume na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere wakati walipokuwa mstari wa mbele kudai Uhuru na haki za jamii
ya Watu wote.
Alisema watoto waliowengi wa kizazi
kipya bado wanaendelea kuwa njia panda wakikosa kumbu kumbu kadhaa za
Viongozi waasisi ambazo zingewapa fursa na nafasi pana ya kuelewa
malengo sahihi ya waasisi hao.
Balozi
Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya
Udhamini wa Mfuko wa kuwaenzi Waasisi wa Taifa la Tanzania ulioongozwa
na Mwenyeki wake Kanal Mstaafu Kabenga Nsa Kaisi aliokutana nao Ofisini
kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Alisema
yapo mataifa mengi duniani kama Vietnam, Jamuhuri ya Watu wa China na
Korea ya Kaskazini yenye Historia kubwa ya kuenzi kazi na kumbu kumbu za
waasisi wao kitendo ambacho Bodi hiyo itastahiki kuiga mfano huo.
Balozi
Seif alifahamisha kwamba wapo baadhi ya watu wanaoendelea kuzidhihaki
kazi zilizofanywa na waasisi wa Tanzania kiasi kwamba iwapo hakutakuwa
na juhudi za makusudi kizazi kipya kinaweza kupotea na kukosa Historia
yao.
Alitolea
mfano wa Mapinduzi Daima yanayodhihakiwa na baadhi ya watu hao wakikosa
kuelewa dhamiri halisi inayokusudiwa ya kuyaenzi yale yote
yaliyotangazwa mara baada ya Mapinduzi ya Mwaka 1964 ambayo
yatamstawisha Mwananchi wa Taifa hili katika maisha yake yote.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwahakikisha Wajumbe wa Bodi ya Udhamini
wa Mfuko wa Kuwaenzi Waasisi wa Tanzania kwamba Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar itatoa kila aina msaada utakaohitajika na Wajumbe hao ili
kuona malengo waliyojipangia yanafanikiwa vyema.
Aliwashauri
wajumbe wa Bodi hiyo kuwasiliana na wazee wanaoielewa vyema Historia ya
Uhuru wa Tanganyika na Mapinduzi ya Zanzibar ili iendelee kuenziwa na
kizazi kipya.
Alieleza
kwamba Kizazi kipya ni vizuri kikajengewa mazingira bora ya kujifunza
moyo wa kujitolea kupitia waasisi wa Taifa la Tanzania ambalo
linaendelea kuwa chuo kwa baadhi ya Nchi washirika kupata Taaluma ya
Historia yake.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar alielezea faraja yake kutokana na Serikali
ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuona umuhimu wa kupitisha Sheria
ndani ya Bunge 2004 ya kuunda bodi ya Udhamini wa Mfuko wa kuwaenzi
waasisi wa Taifa la Tanzania.
Mapema
Mwenyekiti wa Bodi hiyo Kanal Mstaafu Kabenga Nsa Kaisi alisema jukumu
kubwa la Bodi hiyo ni kukusanya kumbu kumbu za waasisi Taifa la Tanzania
na kuzihifadhi kwa faida ya vizazi vipya.
Kanal
Mstaafu Kabenga alisema bodi tayari imeshaandaa mikakati ya jinsi ya
kupata uwezo wa kifedha zitakazokidhi uanzishwaji wa vituo viwili vya
Kumbu kumbu vitakavyowekwa Tanzania bara na Zanzibar.
Alifahamisha
kwamba Wajumbe wa Bodi hiyo watasimamia kuonba kwamba mchango wa
Viongozi waasisi haufanyiwi dhihaka na kazi kubwa ya wajumbe hao ni
kusimamia taaluma ili Jamii ifahamu azma hya waasisi hao katika
kupigania Uhuru na haki za Mwafrika.
“ Kazi yetu inayofanana na wenzetu inatupa faraja kuona Mtaifa ya Dunia hii yanaendelea kuwaenzi waasisi wa Nchi zao.