Boti
ya Uvuvi iliyogharamiwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa CCM Balozi
Seif kwa Vijana wa Maskani ya Tuheshimiane Makangale iliyotengenezwa
huko Mtambwe iko tayari kwa shughuli za Uvuvi. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Fundi Mkuu wa Boti iliyotengenezwa kwa vijana wa Tuheshimiane Makangale Bwana Masoud Juma Masoud akimkabidhi rasmi Boti hiyo Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif baada ya kukamilisha ujenzi wake hapo katika Kijiji cha Mtambwe. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Fundi Mkuu wa Boti iliyotengenezwa kwa vijana wa Tuheshimiane Makangale Bwana Masoud Juma Masoud akimkabidhi rasmi Boti hiyo Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif baada ya kukamilisha ujenzi wake hapo katika Kijiji cha Mtambwe. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Balozi
Seif akimkabidhi rasmi Sheha wa Shehia ya Makangale Kaskazini Bwana
Moh’d Juma Ali Boti ya Uvuvi kwa Vijana wa Makangale akitekeleza ahadi
aliyowapa vijnana hao wakati wa ziara yake Kijijini hapo. Nyuma ya Balozi Seif aliyevaa kitenge cha Bendera ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mh. Omar Khamis Othman. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Press Release:-
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi Balozi
Seif Ali Iddi alitahadharisha kwamba si vyema kwa watu au vikundi
vyenye uwezo wa kutoa ajira kuwanyanyasa wananchi wenzao katika miradi yao ya kiuchumi kwa sababu za itikadi ya Kisiasa.
Alisema
tabia hiyo mbaya inayoashiria kuleta ubaguzi, uhasama na na hatimae
kuzaa chuki miongoni mwa jamii inakwenda kinyume na Ubinaadamu na
maamrisho ya Mwenyezi Muungu.
Balozi
Seif Ali Iddi ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alitoa
tahadhari hiyo wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Boti ya Uvuvi na
Mashine yake kwa Vijana wa Maskani ya Tuheshimiane Mnarani katika
Kijiji cha Makangale ambao walifukuzwa katika shughuli za ajira ya
uvuvi baada ya kukamua kwa hiari yao kukihama chama cha Wananchi {CUF }
na kujiunga na Chama cha Mapinduzi { CCM }.
Boti
na mashine hiyo vyenye thamani ya shilingi za Kitanzania Milioni Nane,
Laki Nne na Hamsini Elfu { 8,450,000/- } amevitoa kwa vijana hao
kufuatia ahadi aliyowapa miezi michache iliyopita wakati wa ziara yake
Kisiwani Pemba.
“ Leo nina furaha na shauku kubwa katika kukamilisha ahadi
niliyoitoa wakati wa ziara yangu ya Mkoa wa Kaskazini Pemba kwenye
Kijiji cha Makangale wakati nilipokutana na vijana hao wakanieleza
changamoto zinazowakabili baada ya kuamua kuiacha CUF “. Alisema Balozi
Seif.
Alisema
anashangaa kuona baadhi ya watu ndani ya Visiwa vya Unguja na Pemba
bado wameamua kuendeleza vitendo vya chuki, uhasama na uadui dhidi ya
wenzao kwa sababu tu za itikadi za kisiasa na kidini.
Alisema
Zanzibar iliamua kuondosha uhasama na chuki miongoni mwa wananchi wake
kwa kuunda Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye mfumo wa Umoja wa
Kitaifa kwa lengo la kurejesha umoja upendo na mshikamano ulioasisiwa na
vizazi vya karne zilivyopita.
Mjumbe
huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi
Balozi Seif aliwaomba wananchi Nchini kote kuendeleza Umoja, upendo na
mshikamano ili Taifa hili lizidi kupiga hatua kubwa ya Maendeleo.
Balozi
Seif aliwakumbusha wananchi wa kisiwa cha Pemba kuendelea kuunga mkono
Katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba na kuipigia kura ya
ndio wakati ukifika.
Alisema
Kero nyingi zilizokuwa zikilalamikiwa na wananchi wa Zanzibar tayari
zimepatiwa ufumbuzi ndani ya Katiba inayopendekezwa. Hivyo cha Msingi ni
kukahiukisha kwamba Katiba hiyo inafanikiwa ili ile kiu ya Wananchi hao
iweze kumalizika.
Aliwaeleza
wananchi hao kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Chini ya Chama
cha Mapinduzi itaendelea kuwatumikia Wananchi wote bila ya ubaguzi kwa
vile imeshaamua kuiendesha katika mfumo wa Umoja wa Kitaifa.
Aliwatahadharisha
wananchi hao kuwa makini na baadhi ya watu walioamua kuwapotosha
Wananchi juu ya Katiba iliyopendekezwa ambayo imegusa na kukidhi
mahitaji ya wananchi na makundi yote yaliyopo hapa nchini.
Akisoma
Risala ya Vijana hao wa Makangale Mjumbe wa Umoja wa Vijana wa CCM wa
Kijiji cha Makangale Nd. Mwinyi Mwewe Mwinyi kwa niaba ya wenzake
alimuhakikishia Balozi Seif kwa wataitunza Boti hiyo ili iwaongezee
kipato n a kuendesha maisha yao ya kila siku.
Mwinyi
Mwewe alisema Vijana hao wamefarijika kutokana na Sera za Chama cha
Mapinduzi Kutekelezeka vyema na kumpongeza Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif kwa kutekeleza ahadi
aliyowapa katika kipindi kifupi.
Alisema
huo ni uungwana unaofaa kuigwa na viongozi wengine ndani ya Chama
pamoja na Serikali katika kuwatumikia wananchi wanaowaongoza hasa
kujaribu kusaidia kero na changamoto zinazowakabili.
Nd.Mwinyi
Mwewe kwa niaba ya wenzake wameahidi kulipa ihisani kwa Chama cha
Mapinduzi kwa kuitetea Katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba
pale wakati utakapowadia.
Mapema
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mh. Omar Khamis Othman alisema kwamba
msaada wa Boti hiyo ya Uvuvi kwa Vijana wa Makangale itawaondoshea udhia
na mashaka walaiyokuwa wakiyapata.
Mh.
Omar kitendo cha Balozi Seif mbali ya kuleta faraja kwa vijana hao
lakini pia kimeisaidia Serikali ya Mkoa huo katika harakati zake za
kuwaunganisha vijana pamoja na kuwajengea mazingira ya ajira.