Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi

Mwanafunzi Isra Hilal Mwadini akifuatiwa na mwenzake Tamima Abass Sheha wakipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wakati wa hafla ya Maulidi ya Jumuiya ya Chuo cha Samael Academy.Kulia ya Balozi Seif ni Rais wa Sameil Academy Sheikh Nassir Bin Said.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizindua rasmi Bara bara ya pili ya Amani hadi Mtoni baada ya kukamilika awamu ya mwisho ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Akiwa na Balozi mdogo wa India nchini Tanzania wakiangalia maonyesho yaliofanya na Msanii kutoka India, Bi Navi Madhav hapo Ngome Kongwe

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Dk. Khalid S. Mohamed

akizungumza na Wadau wa Maendeleo wa Mfuko wa TASAF, walipofika Ofisini kwake kuzungumzia maendeleo ya Mfuko wa TASAF III,na kutembelea Mradi wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini (PSSN) katika Jimbo la Muyuni Wilaya ya Kusini Unguja katika Kijiji cha Muyuni B

Wazir wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakifurahia jambo wakati wa semina ya siku moja kuhusu matokeo makubwa na ya haraka katika kuleta mageuzi ya kiuchumi na kuleta maendeleo nchini iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein

Sunday, 28 June 2015

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiifungua Semina ya Siku moja juu ya mwenendo wa sarafu ya Tanzania dhidi ya Dola ya Kimarekani kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Hapo Ukumbi wa Baraza hilo Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiifungua Semina ya Siku moja juu ya mwenendo wa sarafu ya Tanzania dhidi ya Dola ya Kimarekani kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Hapo Ukumbi wa Baraza hilo Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Picha na Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bwana Juma Hassan Reli akitoa ufafanuzi kabla ya kuanza kwa semina ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar juu ya mwenendo wa sarafu ya Tanzania dhidi ya Dola ya Kimarekani. Picha na Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Mkurugenzi wa Sera za Kiuchumi na Utafiti wa Benki Kuu ya Tanzania Dr. Masawe Joseph akitoa Mada kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi juu ya mwenendo wa sarafu ya Tanzania. Picha na Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mh. Pandu Ameir Kificho  wa pili kutoka kushoto akichangia pamoja na kuliza maswali kwenye semina ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar juu ya mwenendo wa sarafu ya Tanzania dhidi ya Dola ya Kimarekani. Picha na Hassan Issa – OMPR – ZNZ.





















Baadhi ya Watendaji wa Benki Kuu ya Tanzania { BOT } pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia michango na maswali mbali mbali yaliyokuwa yakiulizwa na  baadhi ya Wajumbe hao kwenye kwenye semina hiyo. Picha na Hassan Issa – OMPR – ZNZ.

Press Release:-

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Kimarekani huathirika mara kwa mara kutokana na Taifa kutegemea kuagiza bidhaa zaidi kutoka nje badala ya bidhaa hizo kuzalishwa na makampuni ya hapa nchini
Alisema nyingi ya biadhaa zinazoingizwa Nchini huagizwa kwa fedha za kigeni, hususan Dola za Kimarekani na kuuzwa kwa fedha za Kitanzania jambo ambalo hushajiisha uingizaji zaidi wa bidhaa na huduma kutoka nje.
Balozi Seif Ali Iddid alisema hayo wakati akiifungua Semina ya siku moja ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi juu ya mwenendo wa Sarafu ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani iliyofanyika katika Ukumbi wa juu wa Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Alisema athari ya kuteremka kwa thamani ya sarafu ya Shilingi ya Tanzania hasa katika kipindi cha hivi karibuni imekuwa kubwa zaidi kuliko  faida yake na kupelekea kuzuka kwa malalamiko kwa Wananchi waliowengi hasa wafanyabiashara kutokana na kubadilika sana kiwango cha sarafu hiyo dhidi ya Dola.
Balozi Seif alieleza kwamba kiwango cha ubadilishaji wa fedha kimekuwa ni mojawapo ya kubebea mfuko wa bei nchini ikishuhudiwa kupanda kwa bei za bidhaa zikiwemo zile  zinazotengenezwa hapa nchini ikitwaja sababu kubwa ni mwenendo wa thamani ya shilingi dhidi ya dola.
“ Hivi karibuni tumeshuhudia kupanda kwa bei za bidhaa, zikikwemo zinazotengenezwa na kuzalishwa humu humu nchini sababu inayotajwakuwa  ni mwenendo wa thamani ya shilingi dhidi ya Dola ya Kimarekani “. Alisema Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alishauri kwamba ili kukabiliana na changamoto hiyo ya kuyumba kwa Thamani ya Shilingi ya Kitanzania umefika wakati kwa Wafanyabiashara na wawekezaji wa sekta ya Viwanda wajitahidi kuongeza uzalishaji kwa kutumia rasilmali za ndani ili kudhibiti mfumko huo.
Mapema Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bwana Juma Hassan Reli alisema Fedha za Kigeni ziliadimika Nchini Tanzania katika miaka ya 80 kutokana na udhibiti wa fedha hizo kusimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania chini ya Sheria ya kudhibiti fedha za kigeni ya mwaka 1965.
Bwana Juma Reli alisema hali hiyo ilifungua mianya ya rushwa hasa kwa wale waliopewa dhamana ya kusimamia upatikanaji wa fedha za kigeni  kwa bei rasmi ambayo katika miaka ya kati ya 1967 - 1984 Dola moja ya Kimarekani ilibadilishwa kati ya shilingi 7.14 hadi shilingi 8.13 za Kitanzania.
Alisema mfumo huo pia ulichochea utoroshwaji wa mitaji kupelekwa nje ya nchi kwani Watanzani walio wengi wakipata fedha za kigeni kwa kutumia  njia mbali mbali walishawishika kuzitunza fedha hizo katika Mabenki ya nje ya nchi ili kukwepa sheria.    
Ili kuondokana na changamoto hizo Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania alieleza kwamba Serikali ilifanya mageuzi kupitia sheria ya fedha za Kigeni iliyopitishwa na Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1992 ambayo inamruhusu mtu yeyote kumiliki kiasi chochote cha fedha za kigeni au dhahabu ghafi hapa Nchini.
Alisema Wananchi hivi sasa wana haki ya kununua na kuuza fedha za kigeni kwenye maduka ya kubadilishia fedha pamoja na kuwa na akaunti ya fedha hizo katika mabenki ya Biashara, jukumu la Benki Kuu likibakia kuhakikisha kuwa soko la fedha linaanzishwa na kuendeshwa kwa nguvu za soko.
Bwana Reli alifafanua wazi kwamba soko liliopo sasa la fedha za kigeni linaendelea kukua  ambapo ndio msingi mkuu wa kuweka thamani ya shilingi ya Tanzania  baada ya kuanzishwa na Benki Kuu ya Tanzania mwaka 1994.
Akitoa Mada kwenye Semina juu ya mwenendo wa Sarafu ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani Mkurugenzi wa Sera za Kiuchumi na Utafiti wa Benki Kuu ya Tanzania Dr. Masawe Joseph alisema sarafu ya Fedha ya Tanzania  imeachwa kwenye soko  ili kuiwezesha iende sambamba na masoko mengine ya Sarafu Ulimwenguni.
Dr. Masawe alisema mwenendo wa Shilingi ya Tanzania imeshuka thamani na kuufanya mfumko wa Bei Nchini kufikia asilimia 5.4% ikilinganishwa na Mataifa mengine Duniani zikiwemo baadhi ya Nchi za Bara la Afrika ambazo mfumko wao uko chini ya asilimia 3%.
Mkurugenzi wa Sera za Kiuchumi na Utafiti wa Benki Kuu ya Tanzania            alifafanua kwamba upungufu wa mapato yanayotokana na bidhaa ya dhahabu na bidhaa nyengine asilia umefidiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na kuongezeka kwa bidhaa za viwanda zinazozalishwa na kusafirishwa nje ya Nchi.
Alisema fidia hiyo imeifanya sekta ya Viwanda kukua na kukusanya mapato ya zaidi ya Dola za Kimarekani Elfu Moja kwa sasa kutoka Dola Mia Nane mwaka uliopita ikitanguliwa na Sekta ya Utalii ambayo kwa sasa inashikilia nambari Moja katika kuchangia pato la Taifa.
“ Lazima tuangalie hiyo shilingi ilipo kwa wakati husika ni mahala pake pazuri bila ya kuathiri pande zote zinazohusika kati ya wakusanyaji, wauzaji na watumiaji “. Alifafanua Mkurugenzi huyo wa Sera za Kiuchumi na Utafiti wa Benki Kuu ya Tanzania.
Dr. Masawe alieleza kwamba ni vyema ukawepo uwiano baina ya kushuka na kupanda kwa sarafu ya shilingi kwa vile pande zote husika zina hasara na kunufaika pia,  lakini cha kuzingatia zaidi ni udhibiti makini wa mambo hayo ya kupanda na kushuka.
Wakichangia mada ya mwenendo wa thamani ya shilingi ya Tanzania iliyotolewa na Mkurugenzi wa Sera za Kiuchumi na Utafiti wa Benki Kuu ya Tanzania Dr. Masawe Joseph, baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi  walisema uchumi wa Zanzibar unastahiki kuangaliwa kwa makini kulingana na mazingira yake ili kujieusha na matatizo yanayotokana na kushuka kwa sarafu ya Tanzania.
Wajumbe hao walisema mazingira ya Zanzibar yanategemea uchumi wa bidhaa chache ikilinganishwa na ule wa Tanzania Bara kiasi kwamba maisha ya wananchi walio wengi  Visiwani yanategemea Kilimo ambacho bado hakijawa na nguvu za kuwafanya wawe na uwezo wa kusafirisha kwa lengo la kupata uchumi imara.
Waliushauri Uongozi wa Benki Kuu ya Tanzania kuyaangalia mashirikia na Taasisi za Kiuchumi Nchini katika kuziwezesha wakati inapotokea hali au mazingira ya kuporomoka kwa sarafu ya shilingi ya Tanzania kwenye soko la Dunia.
Walifahamisha kwamba yao mashirika na Taasisi zisizopungua 90 Tanzania Bara ambazo ziliwahi kupewa nguvu ya uwezeshaji na Benki Kuu ya Tanzania katika kujiendesha wakati wa kuporomoka kwa soko la Sarafu Ulimwenguni miaka michache iliyoita.
Walieleza kwamba uimarishaji wa Mashirika na Taasisi za ndani ya Nchi utaongeza ufanisi sambamba na kuwapunguzia ukali wa maisha wafanyakazi wa Taasisi za umma na hata binafsi ambao ndani ya miezi mitatu iliyopita wameshindwa kukidhi mahitaji yao kutokana na kushuka kwa thamani ya shilingi.
Wawakilishi hao wameishauri Benki Kuu ya Tanzania kuangalia mazingira ya matumizi ya fedha ya kigeni  kama Yuan ya Jamuhuri ya Watu wa china kutokana na wafanyabiasha wengi wa Tanzania kwa zaidi ya asilimia 75% kuendesha biashara zao katika soko la China.


 





Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na baadhi ya wateja na walikwa katika futari ya pamoja iliyoandaliwa na Benki ya NMB Tawi la Zanzibar

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza mara baada ya futari ya pamoja iliyoandaliwa na Benki ya NMB Tawi la Zanzibar iliyofanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar. Picha na Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Baadhi ya wateja na walikwa futari ya pamoja iliyoandaliwa na Benki ya NMB Tawi la Zanzibar ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi. Picha na Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Baadhi ya wateja na walikwa futari ya pamoja iliyoandaliwa na Benki ya NMB Tawi la Zanzibar ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi. Picha na Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Zanzibar Bwana Abdulla Duchi akitoa neon la shukrani kwa wateja na wananchi walioalikwa na Uongozi wa Benki hiyo katika futari ya pamoja hapo Zanzibar Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar. Picha na Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Meneja Mkuu wa Idara inayoshughulikia fedha ya NMB Bwana Waziri Banabas akielezea mikakati ya Benki hiyo mara baada ya futari ya pamoja iliyoandaliwa na Benki hiyo Tawi la Zanzibar hapo Kilimani. Picha na Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Meneja Mkuu wa Idara inayoshughulikia fedha ya NMB Bwana Waziri Banabas akielezea mikakati ya Benki hiyo mara baada ya futari ya pamoja iliyoandaliwa na Benki hiyo Tawi la Zanzibar hapo Kilimani. Picha na Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Balozi Seif aliyepo kati kati kwa waliokaa vitini akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Benki ya NMB Makao Makuu Dar es salaa na Tawi la Zanzibar. Picha na Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Balozi Seif akibadilishana mawazo na baadhi ya Viongozi wa Benki ya NMB Pamoja na Wananchi walioshiriki futari ya pamoja iliyoandaliwa na Benki hiyo Tawi la Zanzibar.Picha na Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
 Balozi Seif akiagana na Baadhi ya Viongozi wa Benki ya NMB hapo Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani mara baada ya kukamilika kwa futari ya pamoja. Picha na Hassan Issa – OMPR – ZNZ.





















Balozi Seif akiagana na Baadhi ya Viongozi wa Benki ya NMB hapo Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani mara baada ya kukamilika kwa futari ya pamoja. Picha na Hassan Issa – OMPR – ZNZ.

   Press Release:-

Benki ya kuhudumia wateja wadogo wadogo Tanzania { NMB } imeahidi kuendelea kutoa huduma za Kijamii katika maeneo mbali mbali Nchini Tanzania ili lengo la kuanzishwa kwake liweze kufikiwa kwa ufanisi.
Meneja Mkuu wa Idara inayoshughulikia masuala ya fedha ya Benki Hiyo Bwana Waziri Banabas alitoa ahadi hiyo wakati Uongozi wa Benki hiyo Tawi la Zanzibar ulipowaandalia futari ya pamoja baadhi ya wateja wake, Viongozi wa Taasisi tofauti Nchini pamoja na Wananchi.
Futari hiyo ya pamoja iliyoandaliwa ndani ya kumi la kwanza la rehema la Mwezi Mtukufu wa ramadhani imefanyika mara baada ya sala  Magharibi kwa washiriki hao iliyofanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar.
Meneja Mkuu huyo wa Idara inayoshughulikia masuala ya fedha ya Benki ya NMB Bwana Waziri Banabas alisema faida ya fedha zinazokusanywa na Benki hiyo kwa mujibu wa taratibu iliyojipangia hutolewa katika kusaidia sekta za afya pamoja na  elimu.
Bwana Banabas alifahamisha kwamba kutokana na kukua kwa uchumi wa Zanzibar na wananchi wake  kuhitaji huduma za Kibenki Uongozi wa NMB una mpango wa  kuongeza Matawi pamoja na ATM ili kukidhi mahitaji ya wananchi hao.
Alisema Benki ya NMB Hivi sasa ina jumla ya Matawi 17 katika maeneo mbali mbali nchini Tanzania ambapo mawili kati ya hayo yapo kwa upande wa Zanzibar kiwango ambacho kinastahiki kuongezwa.
Akigusia changamoto za uhaba wa vifaa vya maabara katika Maskuli mengi hapa Zanzibar Meneja Mkuu huyo wa Idara inayoshughulikia masuala ya fedha ya Benki ya NMB Bwana Waziri Banabas alisema Uongozi wake utazingatia kwa kina tatizo hilo.
Alielezea matumaini yake kuona kwamba Benki ya NMB italipa kiapaumbele suala hilo kwa nia ya kulitafutia mbinu na ufumbuzi wa kudumu kwa lengo la kuwaondoshea usumbufu wa changamoto zinazowakabili wanafunzi wa Zanzibar.
Bwana Waziri Banabas amewapongeza Wananchi na wateja wote Nchini Tanzania waliosaidia kuifanya Benki ya NMB kuwa ya kwanza Tanzania kwa kukusanya shilingi Bilioni 156 mwaka uliopita.
Akitoa shukrani kwa niaba ya washiriki wa futari hiyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliupongeza Uongozi wa Benki ya NMB Kwa kujipangia utaratibu wa kusaidia huduma za kijamii licha ya jukumu lao la kukusanya mapato.
Balozi Seif alisema Benki ya NMB imeanzishwa maalum ili kuwapa nguvu Wananchi wa kipato cha chini kuapata mikopo ya kuwawezesha kiuchumi ili waendeshe maisha yao ya kila siku kwa matumaini makubwa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwataka Wananchi wote kuitumia Benki hiyo ya NMB katika shughuli zao za ujasiri amali ambazo ndio njia pekee itakayowakomboa kutokana na ukali wa maisha.
Alisema NMB  yeye binafsi imemuwezesha kujenga mapenzi na upendo kwa Wananchi wa Jimbo lake la Kitope mara tuu baada ya kuchaguliwa kuwa Mbunge wao wa Jimbo hilo Mwaka 2005 kwa kupata mkopo mkubwa aliouelekeza katika kuanzisha miradi ya maendeleo ya Wananchi Jimboni humo.
Uongozi wa Benki ya NMB tayari umeshafutarisha Wateja na Viongozi wa Kisiwa cha Pemba na kuahidi kuendeleza utamaduni huo kila mwaka ili kuwapa fursa wateja wake kukaa pamoja na kubadilishana mawazo na fikra zitakazosaidia kuongeza ufanisi wa Benki hiyo.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiufunga Mkutano wa 20 wa Baraza la Wawakilishi kwenye ukumbi wa Baraza hilo hapo Mbweni uliokuwa ukijadili Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2015/2016.

Baadhi ya Wajumbe wa Barazala Wawakilishi Zanzibar wakifuatilia Hotuba na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif hayupo pichani wakati akiufunga Mkutano wa 20 wa Baraza la Wawakilishi  kwenye ukumbi wa Braza hilo hapo Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Balozi Seif Ali Iddi akiufunga Mkutano wa 20 wa Baraza la Wawakilishi  kwenye ukumbi wa Braza hilo hapo Mbweni uliokuwa ukijadili Bajeti nya Serikali kwa mwaka 2015/2016.  Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
 Balozi Seif Ali Iddi akiufunga Mkutano wa 20 wa Baraza la Wawakilishi  kwenye ukumbi wa Braza hilo hapo Mbweni uliokuwa ukijadili Bajeti nya Serikali kwa mwaka 2015/2016.  Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Waziri wa Ncho Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed Aboud Mohammed  akitoa shukrani kwa nmiaba ya Mawaziri wenzake kwenye hitimisho la Mkutano wa 20 wa Baraza la Wawakilishi  Zanzibar.  Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Mwakilishi wa Viti Maalum Wanawake CCM Mh. Panya  Ali Abdulla akitoa shukrani kwa niaba ya Wawakilishi wenzake { Back Banchers } wakati wa hitimisho la Mkutano wa 20 wa Baraza la Wawakilishi  Zanzibar.  Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.






















Mtangazaji wa Shrika la Utangazaji Zanzibar Khamis Fakih Moh’d akipata ufafanuzi kutoka kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif mara baada ya kuufunga Mkutano wa 20 wa Baraza la Wawakilishi  mapema asubuhi.  Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.

Press Release:-

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema wakati harakati za uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 zimeanza kwa vyama vya siasa kutafuta wagombea wa nafasi mbali mbali za uongozi Viongozi pamoja na wananchi wanaweza kuchaguana bila ya kutukanana,kugombana nakuepuka kuhamasishana katika kufanya vurugu zinazoweza kuvuruga zoaezi zima la uchaguzi huo.
Alisema mafanikio yaliyopatikana kwa muda mrefu yanategemea kudumu kwa hali ya amani na utulivu kwa vile kila mwana jamii na mwananchi ana haki na wajibu wa kusimamia maendeleo hayo.
Akiufunga Mkutano wa 20 wa Baraza la Wawakilishi uliokuwa ukijadili Bajeti ya Serikali ya mwaka 2015/2016 katika ukumbi wa Baraza hilo Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar Balozi Seif alielezea matumaini yake kwamba  wananchi wataendelea kuiamini na kuiunga mkono Serikali yao inayoongozwa na Rais kutoka CCM.
Alitanabahisha kwamba Serikali itahakikisha ulinzi na usalama unaimarika na haitokuwa tayari kumvumilia mtu au kikundi chochote kitakachovunja sheria  na kuihatarisha amani na utulivu wa nchi.
Balozi Seif Ali Iddi alionya kwamba watu wasifikirie hata siku moja kwamba vikundi vinavyojitayarisha au kutayarishwa  na wachochezi kufanya vitendo vya kuhatarisha amani ya nchi vinaikomoa Serikali, bali vielewe kwamba vinajikomoa vyenyewe.
Akizungumza bila ya uwepo wa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka Chama cha Wananachi { CUF } ndani ya kikao hicho Balozi Seif aliwaeleza wananchi kwamba yapo mafanikio makubwa yaliyopatikana  ndani ya Kipindi cha Kwanza cha Awamu ya Saba katika Sekta mbali mbali ikiwemo Afya, Elimu, Utalii, Maji, Miundombinu na Mawasiliano,Sekta za Uzalishaji viwandani, kilimo, mifugo na uvuvi.
 Alisema mafanikio hayo ya kupigiwa mfano yametokana na utekelezaji sahihi wa Ilani ya CCM ya mwaka 2010 – 2015  chini ya usimamizi wa  Rais wa Zanzibar ambae pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar  Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein ambapo hakuna shaka  kwa mafanikio hayo   Wananchi walio wengi watamrejesha tena kuiongoza Zanzibar iliyoamua kuwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  yenye mfumo wa Umoja wa Kitaifa.
Balozi Seif alisema katika kipindi cha miaka mitano (2010 – 2015), Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetoa fidia ya jumla ya Shs. 7,129,591,148 za kuendeleza kilimo, kwa ajili ya ununuzi wa mbolea, madawa, mbegu na kutoa huduma za matrekta kwa wakulima.
Alisema hadi kufikia asilimia 5.6 mwaka 2014 hali inayotokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa ndani  unaotokana na juhudi zilizochukuliwa na Serikali katika kuwapatia ruzuku za pembejeo wakulima hapa Nchini. 
Balozi Seif alieleza kwamba Kilimo bado kinaendelea kuwa muhimili Mkuu wa Uchumi wa Taifa kwa kutoa ajira kwa wananchi walio wengi na ndio maana Serikali ikalazimika kutekeleza mipango na miradi mbali mbali ya kilimo.
Akigusia sekta ya utalii inayoendelea kuimarika na kuwa tegemeo la kuongeza pato la Taifa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  alisema idadi ya watalii walioingia Nchini imeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka na kufikia watalii Laki 274,619 mwaka 215.
Alisema ongezeko hilo linatokana na kuimarika kwa miundombinu  ya utalii pamoja na hali ya kudumisha amani na amewahakikishia watalii usalama wao kwa kipindi chote ambnacho watakuweo hapa Nchini.
Alifahamisha kwamba katika kuimarisha zaidi sekta ya Utalii Serikali imeamua kuibadilisha mandhari ya Hoteli ya Bwawani ambayo ina Historia kubwa baada ya kuatikana kwa mwekezaji ambae yuko tayari kuibadilisha hali hiyo.
Balozi Seif alisema Mazungumzo baina ya Serikali ya Mainduzi ya Zanzibar na Mwekezaji aliyechaguliwa kuendesha mradi huo yamefikia hatua nzuri na kinachobakia kwa sasa ni Serikali kumkabidhi mradi huo mwekezji husika na kufungaq naye mkataba.
Kuhusu Sekta ya miundombinu  ya mawasiliano ya Bara bara Mtendaji Mkuu huyo wa Serikali alisema Serikali imejenga bara bara mpya kwa kiwango cha lami zenye urefu wa kilomita mia 243.85 na Bara bara nyengine zenye urefu wa kilomita 39.3 zimejengwa kwa kiwango cha kifusi na zile zenye urefu wa Kilomita 656 zimefanyiwa matengenezo mbali mbali.
Alisema miundombinu hiyo kwa kiasi kikubwa itasaidia  kuimarisha uchumi wa Taifa na kutoa wito kwa wananchi pamoja na watumiaji wa bara bara hizo kuzitunza kwa faida yao na vizazi vijavyo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaasa wale watu wenye tabia ya kuzichoma bara bara hizo kwa makusudi kutokana na ushabiki wa kisiasa ni vyema wakaacha tabia hiyo yenye kuigharimu fedha nyingi Serikali Kuu katika kuzitengeneza upya.
Balozi Seif aliwashukuru na kuwapongeza Wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi kwa michango,mapendekezo na ushauri walioutoa wakati wa kuzijadili Hotuba za Bajeti zilizowasilishwa kwenye Baraza hilo la WEawakilishi Zanzibar.
Alisema katika Mikutano yote ya Baraza la Wawakilishi, Mkutano wa mwaka huu ulikuwa wa kupigiwa mfano kwa kupitishwa bajeti zote kwa urahisi na bila ya pingamizi zozote.
Balozi Seif alieleza kwamba upitishwaji wa Bajeti hizo ulikuwa rahisi kutokana na sababu ya kutumia mfumo mpya wa Bajeti uitwao Program Based Bujet { PBB } uliosaidia kupunguza vikwazo kutoka kwa Wajumbe wakati wa Kamati.
Baraza hilo la Wawakilishi la Nane tokea kuasisiwa kwake hadi sasa limeshafanya jumla ya Mikutano 20 katyika Mikutano ambayo jumla ya maswali ya msingi 1,630 na yale ya nyongeza elfu 3,277 yameulizwa kwa Serikali na kujibiwa.
Baraza hilo pia limefanikiwa kujadili na kupitisha miswada ya sheria ipatayo 63 na hatimae kutungwa kwa sheria kutokana na miswada hiyo pamoja na kuidhinisha Bajeti ya Serikali na Mawizara mara Tano hadi kipindi hichi Bajeti ambazo zimesaidia kufanikisha kupatikana kwa maendeleo makubwa hapa Nchini.



Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balizi Seif Ali Iddi akiwaasa Wazee Nchini kuwadhibiti watoto wao kutojiingiza katika makundi yanayoandaliwa na baadhi ya watu

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Vijana na wazee wa Fujoni Nyumba ya Ndege alipokwenda kutekeleza ahadi yake ya kusaidia ujenzi wa uwanja wa michezo wa Fujoni Boys { Hibury }. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Balozi Seif akimkabidhi fedha Taslim Shilingi Milioni 4,000,000/- Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kaskazini “ B “ Nd. Hilika Ibrahim kwa ajili ya matengenezo ya uwanja wa michezo wa Timu ya Soka ya Fujoni Boys. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.






















Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akiwapongeza wananchi wa Fujoni kwa umakini wao wa kutetea na kulinda sera za Chama Tawala kinachoonbgoza Dola Tanzania. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.



                                            Press Release:-

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balizi Seif Ali Iddi amewaasa Wazee Nchini kuwadhibiti watoto wao kutojiingiza katika makundi yanayoandaliwa na baadhi ya watu wakiwemo wanasiasa kufanya vurugu zinazoashirika kutaka kuvuruga amani ya Nchi.
Akaonya kwamba asijetokea mzazi atakayetaka kuilaumu Serikali wakati vyombo vyake vya dola  vitakavyotekeleza majukumu yake katika kuwadhibiti watu watakaobainika kusababisha vurugu ndani ya kipindi hichi kinachoelekea kwenye uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba.
Balozi Seif Ali Iddi  ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Kitope alitoa wosia huo wakati akikabidhi mchango wa shilingi Milioni 4,000,000/- akitekeleza ahadi aliyotoa  tarehe 4 June mwaka huu kusaidia matengenezo ya uwanja wa michezo wa Timu ya soka ya Fujoni Boys { HIBURY } hafla iliyofanyika katika Maskani ya Nia Njema Nyumba ya Ndege Fujoni.
Balozi Seif alisema Serikali ina taarifa kwamba wapo watu na baadhi ya wanasiasa waliojiandaa kifedha kuwashawishi vijana kujiingiza katika makundi na kufanya vurugu ndani ya zoezi la uandikishaji wa vitambulisho vya kupiga kura pamoja na uchaguzi wa mwezi Oktoba.
Aliwatahadharisha Wazazi pamoja na Vijana kwamba Serikali kupitia vyombo vyake vya Dola iko makini na tayari imeshajiandaa kukabiliana na vurugu ama njama yoyote itakayoandaliwa ya kutaka kujaribu kutia doa zoezi hilo la uandikishaji wapiga kura pamoja na uchaguzi Mkuu.
Alifahamisha kwamba inasikitisha kuona mtego huo unaoandaliwa na kuwahusisha zaidi Vijana mara zote unafanywa na watu wanaokuwa mbali na matatizo yanayowakumba vijana hao baada ya kuhusika na vurugu hizo.
“ Wazee lazima wajizatiti katika kuhakikisha wanawanusuru watoto wao na mtego unaoandaliwa na watu wenye nia na muelekeo wa maslahi yao binafsi “. Alisema Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alieleza kwamba wapo Watu na baadhi ya makundi yasiyoitakia kheir nchi hii ambao tayari wameshaanza kuonyesha dalili za kuleta  Vurugu.
Balozi Seif aliwahakikishia Wananchi wote Nchini kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Ile ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania zitajitahidi kuona amani na utulivu wa Nchi unaendelea kudumu katika muda wote.
Akigusia kitendo cha Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Chama cha Wananchi { CUF } kutoka kwenye Kikao cha Baraza la Wawakilishi kilichokuwa kikiendelea kwenye Baraza hilo Mbweni  hapo juzi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema uamuzi wao haukuzingatia upeo wa Demokrasia ya mfumo wa vyama vingi wa Siasa uliopo hapa Nchini.
Balozi Seif akiwa Mtendaji Mkuu wa Serikali alielezea masikitiko yake kutokana na uwamuzi wa Wajumbe hao wa Upande wa Upinzani uliokuwa na nia ya kutaka kuvuruga mfumo mzima wa muenendo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar unaofuata Mfumo wa Umoja wa Kitaifa.
Alisema ususiaji wa Wajumbe hao katika Vikao vya Baraza hilo lililokuwa likijadili na kutaka kupitisha matumizi ya Serikali yalikuwa na lengo la kutaka kuzuia matumizi halisi ya fedha kwa Taasisi za Umma za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar jambo ambalo lingevuruga mfumo mzima wa uendeshaji wa Serikali.
“ Licha ya misaada ya baadhi ya wahisani lakini fedha nyingi zinazotumika kwenye uchaguzi wetu zinatoka katika mfuko Mkuu wa Serikali. Sasa mbinu za Wajumbe hao kukimbia kupitisha makadirio ya matumizi kwa Wizara inayosimamia fedha zinaashiria kutaka kuharibika kwa uchaguzi Mkuu “. Alifafanua Balozi Seif.
Mapema Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi alisema Viongozi na wanachama wa vyama vya Upinzani ni vyema wakazingatia umuhimu wa kuwa na uvumilivu wa kisiasa ndani ya mfumo wa vyama vingi  vya siasa hapa Nchini.
Mama Asha alisema yapo mambo na baadhi ya matukio yenye kuleta kero na hata usumbufu kwa Viongozi na Wanachama wa Chama cha Tawala cha CCM  lakini wana CCM hao wanalazimika kukubali kuvumilia kwa lengo la kudumisha amani na upendo miongoni mwa jamii.
Amewapongeza Wananchi wa Fujoni kwa msimamo wao madhubuti wa kulinda na kutetea sera za Chama Tawala cha Mapinduzi zilizopata ridhaa za wananchi walio wengi  kwenye uchaguzi wa mwaka 2010 na kupata fursa ya kuongoza Dola.


Thursday, 25 June 2015

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Muasisi wa Chama cha ASP na muanzilishi wa Chama cha Mapinduzi Mzee Kombo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Muasisi wa Chama cha ASP na muanzilishi wa Chama cha Mapinduzi Mzee Kombo  Mzee Kombo wakati alipokwenda nyumbani kwake Miembeni kumjulia hali. Picha Hassan Issa OMPR – ZNZ.



















Muasisi wa Chama cha ASP na muanzilishi wa Chama cha Mapinduzi Mzee Kombo  Mzee Kombo akimpatia maelezo Balozi Seif juu ya maendeleo ya Afya yake iliyopata mtihani wa maradhi hivi karibuni. Picha Hassan Issa OMPR – ZNZ.

Sunday, 21 June 2015

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikagua Kituo cha mradi huo { Comanding Post } kiliopo Malindi Mjini Zanzibar na kujionea Teknolojia mpya itakayotumika katika kuziongoza Kamera hizo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipata maelezo kutoka kwa Katibu wa Kamati ya Wataalamu ya usimamizi wa Mradi wa CCTV Camera Nd. Jabir Haji Abdulla juu ya mfumo wa utendaji kazi wa mradi wa Camera za kurikodi matukio mbali mbali ndani ya Mji Mkongwe wa Zanzibar. Kulia ya Balozi Sei ni Balozi Mdogo wa Jamuhuri ya Watu wa China aliyepo Zanzibar Bwana Xie Yun Liang. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Katibu wa Kamati ya Wataalamu ya usimamizi wa Mradi wa CCTV Camera Nd. Jabir Haji Abdulla akionyesha picha mbali mbali zinazonaswa na kurikodiwa katika maeneo mbali mbali ya Mji Mkongwe. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Katibu wa Kamati ya Wataalamu ya usimamizi wa Mradi wa CCTV Camera Nd. Jabir Haji Abdulla akionyesha picha mbali mbali zinazonaswa na kurikodiwa katika maeneo mbali mbali ya Mji Mkongwe. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Mounekano wa Picha  tofauti zinazochukuliwa na kunaswa katika kituo cha kuongozea Camera za CCTV Malindi Mjini Zanzibar. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.


















Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akifurahia mfumo wa Camera za CCTV unavyofanya kazi ambao amesema utasaidia kupunguza au kuondosha kabisa matukio ya uhalifu na uzembe katika bara bara za Mji Mkongwe wa Zanzibar. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.

 Press Release:-

Zanzibar inatarajia kuimarika zaidi kiulinzi na kiusalama sambamba na kuongeza mapato yake kupitia sekta ya utalii baada ya kukamilika kwa mradi muhimu wa Kamera za  kurikodi matukio mbali mbali ya kila siku { CCTV CAMERA } zinazofungwa katika eneo la Mji Mkongwe wa Zanzibar.
Mradi huo muhimu wa Camera uliofadhiliwa na Kampuni ya Kimataifa ya Mtandao wa Mawasiliano ya Kisasa ya ZTE yenye Makao Makuu yake Nchini  Jamuhuri ya Watu wa China umekuja Zanzibar kufuatia ziara ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyoifanya Nchini China mwisho mwa mwaka uliopita.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipata fursa ya kukagua Kituo cha mradi huo { Comanding Post } kiliopo Malindi Mjini Zanzibar na kujionea Teknolojia mpya itakayotumika katika kuziongoza Kamera hizo.
Katibu wa Kamati ya Wataalamu ya usimamizi wa Mradi wa CCTV Camera Nd. Jabir Haji Abdulla alimueleza Balozi Seif kwamba mradi huo unatarajiwa kuwa na Carema 300 lakini zitakazofungwa kwa sasa ni Kamera 150 ambapo hadi sasa Kumi tayari zimeshafungwa.
Nd. Jabir alisema Kituo hicho  kitakachokuwa chini ya uangalizi  wa Idara zote za ulinzi Nchini  likiwemo Jeshi la Polisi, usalama wa Taifa, KMKM hivi sasa tayari kina uwezo kamili wa kurikodi matukio mbali mbali yanayotokea katika eneo la Mji Mkongwe.
Katibu huyo wa Kamati ya Wataalamu ya usimamizi wa mradi huo alieleza kwamba Kamera za mradi huo zenye uwezo wa kuvuta tukio kwa zaidi ya mita 150 zitasaidia kurikodi matukio mbali mbali kama ujambazi, makosa ya bara barani yanayofanywa na madereva wazembe pamoja na kuongoza misafara ya viongozi wakuu.
Alifahamisha kwamba katika kuimarisha hali ya usalama ndani ya Mji wa Zanzibar  upo mradi mwengine  unaotarajiwa kusimamiwa na Kampuni ya Zest utakaohusisha maeneo ya Bagharesa, Mlandege pamoja na Majengo ya Nyumba za Maendeleo Michezani.
“ Kamera hizi zenye uwezo wa kuzunguuka pembe zote { 360% }  zina uwezo wa kuvuta tukio lolote kwa zaidi ya Mita 150 na kuwa na vigezo vya kuufanya mji salama “. Alifafanua Katibu huyo wa Kamati ya Wataalamu ya Usimamizi wa CCTV.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliipongeza Kampuni ya ZTE kwa jitihada ilizochukuwa za kutekeleza kwa vitendo ahadi iliyompa  kuanzisha mradi huo wakati wa ziara yake Nchini China.
Balozi Seif alisema Serikali ilipaswa kuwa na mradi huu muhimu kwa muda mrefu uliopita hasa ikilinganishwa na matukio mbali mbali yaliyowahi kutokea hapa nchini likiwemo la hujuma dhidi ya wageni wanaotembelea katika maeneo ya Utalii.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alielezea matumaini yake kwamba mradi huo kwa kiasi kikubwa utakapokamilika utasaidia kupunguza matukio tofauti ya uhalifu, ujambazi pamoja na ajali za kizembe zinazotokea bada barani.
Mradi  wa Kamera za  kurikodi matukio mbali mbali ya kila siku { CCTV CAMERA } ndani ya Mji wa Zanzibar umeripotiwa kuwa wa mwanzo kuwekwa ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki.

 


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wazee na Viongozi wa Shehia za Muyuni “A “ na Muyuni “B” katika kikao cha kujadili matatizo yaliyojitokeza baina ya Wananchi dhidi ya viongozi wao wa shehia hizo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Wazee na Viongozi wa Muyuni “A “ na Muyuni “ B “ kabla ya kuzungumza nao kujadili tatizo la migogoro ya Ardhi. Picha Hassan Issa– OMPR – ZNZ.
Baadhi ya Viongozi wa Shehia za Muyuni “A “ na Muyuni “ B “ wakimsikiliza Balozi Seif hayupo pichani wakati wa kujadili changamoto zinazowakabili za migogo ya Ardhi { Hifadhi ya Misitu } ndani ya Shehia hizo. Wa kwanza kutoka kushoto ni Afisa Tawala wa Wilaya ya Kusini Bi Kibibi Mwinyi Hassan. Picha Hassan Issa– OMPR – ZNZ.






















Balozi Seif akizungumza na Wazee na Viongozi wa Muyuni “A “ na Muyuni “ B “ baada ya kupokea changamoto zinazowakabili za migogoro ya ardhi. Kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkopa wa Kusini Unguja Dr. Idriss  Hijja na Kushoto yake ni Mwenyekiti wa Kikao hicho Diwani Mstaafu wa Muyuni Bwana Abdulla  Hija Abdulla. Picha Hassan Issa– OMPR – ZNZ.

Press Release:-

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haipendelei kuona Wananchi katika baadhi ya shehia wanalumbana na kufikia hatua ya kuhitilafiana katika mambo ambayo wakiamua kukaa pamoja katika kuyajadili kwa njia ya vikao  yanaweza kurekebishika bila ya kutumika nguvu za Serikali Kuu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Wazee na Viongozi wa Shehia za Muyuni “A “ na Muyuni “B” katika kikao cha kujadili matatizo yaliyojitokeza baina ya Wananchi dhidi ya viongozi wao wa shehia hizo.
Balozi Seif Ali Iddi alisema tabia ya baadhi ya wananchi hasa Vijana kutumia njia ya mkato katika maamuzi yao ya  kurejesha Kadi za uanachama ni udhaifu unaofa kuepukwa kwa vile hauwezi ukatoa suluhu ya tatizo linalolalamikiwa na Wananchi hao.
Alisema maisha ya amani na utulivu ndio yanayotegemewa  na Serikali Kuu kuendelea kushamiri ndani ya Shehia hapa nchini ambazo zinawajibika kufanya kazi kwa umakini.
Balozi Seif alieleza kuwa  Sheha wa Shehia yoyote ile hapa Zanzibar ni mtumishi wa Serikali kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar asiyepaswa kuhusika na vitendo vinavyoashiria vurugu ndani ya eneo lake.
Mapema  Diwani Mstaafu wa Wadi ya Muyuni Bwana Abdulla Hijja Abdulla ambae ndie mwenyekiti wa Kikao hicho alielezea matatizo mengi yanayowasumbuwa Wananchi hao wa Muyuni  “ A “ na Muyuni “ B “ hasa lile la hifadhi ya msitu ambalo waliamuwa kuianzisha kwa hatma yao ya baadaye.
Bwana Abdulla alisema uchelewaji wa kuchukuliwa hatua  za kisheria katika ngazi za Shehia, Wilaya na Mkoa dhidi ya  watu waliomua kuvamia hifadhi hiyo ndilo tatizo kuu lililoibua mtafaruk kati ya Wananchi hao wa Uongozi wa Shehia hizo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kusini Nd. Khamis Jabir Makame alisema alilazimika kulitembelea eneo la Mgogoro wa Ardhi katika eneo la Hifadhi ya Muyuni  muda mfupi uliopita ili kujionea hali halisi ya kile kinacholalamikiwa.
Nd. Jabir alikieleza kikao hicho kwamba akiwa pamoja na Viongozi wenzake wa Wilaya alibaini kuwepo kwa miti ya kudumu iliyooteshwa kwa muda mrefu katika eneo hilo pamoja na Miti ya matunda ambayo tayari imeaanza kuzaa.



Friday, 19 June 2015

Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi akitoa wosia wakati wa kuwapokea Vijana Sita wa Kijiji cha Fujoni walioamua kuacha kutumia Dawa za kulevya

Mbunge wa Jimbo la Kitope ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akisalimiana na mmoja kati ya Vijana sita walioamua kuachana na matumizi ya Dawa za Kulevya katika Kijiji cha Fujano hapo katika Viunga vya vya Skuli ya Fujoni.
Kati kati yao ni Mwakilishi wa Umoja wa kusaidia mapambano dhidi ya matumizi ya Dawa za kulevya na Pombe Tanzania Bwana  Abdulrahman Mohammed Abdulla. Mwakilishi wa Umoja wa kusaidia mapambano dhidi ya matumizi ya Dawa za kulevya na Pombe Tanzania Bwana  Abdulrahman Mohammed Abdulla akielezea mikakati ya taasisi yake katika mapambano dhidi ya Dawa za kulevya hapa Nchini.
Balozi Seif akizungumza na baadhi ya Wananchi mara ya kukabidhiwa Vijana Sita walioamua kuachana na matumizi ya Dawa za kulevya waliokuwa wakipata mafunzo kwenye Kituo cha Mombasa nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Kushoto ya Balozi Seif ni Sheha wa Shehia ya Fujoni Bwana Said Mgeni Bakari na wa kwanza kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kaskazini “ B “ Nd. Hilika Khamis na Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kitope Mama Asha Suleiman Iddi.


Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi shilingi Milioni 5,000,000/- Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Zanzibar { ZAWA } Dr. Mustafa Gharu aliyevaa T. Shirt ya Buluu hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kwa ajili ya uendelezaji wa ujenzi wa kibanda cha maji katika kijiji cha Kinduni.
 
 Press release:-

Wazazi wameaswa kuwa tayari kuwapokea Vijana au watoto wao walioamua kuacha matumizi ya dawa za kulevya ili kuwalinda na vishawishi vinavyoweza kutoa nafasi ya kuwarejesha tena kwenye matumizi ya Dawa hizo pamoja pombe haramu.
Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi ametoa wosia huo wakati wa kuwapokea Vijana Sita wa Kijiji cha Fujoni walioamua kuacha kutumia Dawa za kulevya na kupata mafunzo watakayoyatumia kuwasomesha wenzao kuachana na Dawa hizo hapo katika Skuli ya Fujoni Wilaya ya Kaskazini “ B “.
Balozi Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema wapo Wazazi na Familia  Nchini ambao bado wanaendelea  na tabia ya kuwatenga Vijana wao walioathirika na Dawa za kulevya kwa kuchelea kufanyiwa matendo ya maudhi kama wizi.
Alisema tabia hiyo inafaa kuachwa kwa vile kama haikutafutiwa ufumbuzi  inaweza kuzalisha zaidi Vijana wanaotumbukia katika matumizi ya Dawa za kulevya na hatimae kuwa na kundi kubwa la  walevi ndani ya Jamii ambao ni nguvu kazi ya Taifa.
Balozi Seif alionyesha furaha yake kutokana na ujasiri  mkubwa ulioonyeshwa na vijana hao wa kuamuwa kuacha matumizi ya Dawa za kulevya na kujitolea kuwa mfano kwa wenzao wenye tabia hiyo.
Aliwaomba Vijana hao kuwa na hadhari ya kutokubali kudanganywa na baadhi ya watu hasa wanasiasa ya kushawishiwa kujiingiza matika matendo maovu kama uvunjifu wa Amani.
Balozi Seif alisema katika kipindi hichi cha Taifa kukaribia katika uchaguzi Mkuu Vijana wana wajibu wa kupima kwanza chochote wanachoambiwa kabla ya kufikia uamuzi wa kuchukuwa hatua.
Katika kukabiliana na changamoto hizo Balozi Seif alifahamisha kwamba akili za kuambiwa lazima vijana hao pamoja  na Wananchi wote wanapaswa kuzichanganya  na zao ili kupata maamuzi muwafaka.
Akiunga mkono maamuzi ya Vijana pamoja na wazee wa Kijiji cha Fujoni katika juhudi za kukaa pamoja na kutafuta mbinu za kukabiliana na matatizo ya matumizi ya Dawa za kulevywa Kijijini hapo Balozi Seif aliahidi kuwapatia Boti ya Uvuvi na vifaa vyake ili iwasaidie katika shughuli zao za kujiongezea ajira.
Balozi Seif alieleza kwamba Mapato ya Boti hiyo pia wanaweza kuanzia jengo la Ofisi yao kwa hatua ya ujenzi wa msingi na yeye atakuwa tayari kuongeza nguvu katika kuwapatia vifaa ikiwemo matofali kwa ajili ya kuendeleza jengo lao.
Akitoa Taarifa fupi  Mwakilishi wa Umoja wa kusaidia mapambano dhidi ya matumizi ya Dawa za kulevya na Pombe Tanzania Bwana  Abdulrahman Mohammed Abdulla alisema Taasisi yao iliyoasisiwa mwaka 2009 tayari imeshafungua vituo Vinne vya kutoa mafunzo kwa vijana walioamua kucha dawa za kulevya Bara na Zanzibar.
Bw. Abdulrahman alisema vijana kati ya 56 na 65 wameshapatiwa mafunzo kwenye vituo hivyo ambapo zaidi ya asilimia 35% ya Vijana waliopita kwenye vituo hivyo wamerejea katika hali za kawaida na kufanya matumizi ya udungaji wa sindao kupungua pia.
Alifahamisha kwamba mafunzo hayo hulengwa zaidi katika kuwapatia Vijana hao ushauri nasaha unaojumuisha uwepo kwa baadhi ya wazazi kwenye vituo hivyo, tiba pamoja na huduma za michezo.
Mwakilishi huyo wa Umoja wa kusaidia mapambano dhidi ya matumizi ya Dawa za kulevya na Pombe Tanzania alifahamisha kwamba zipo baadhi ya changomoto zinazokwamisha utekelezaji na malengo ya taasisi hiyo.
Alitaja baadhi changamoto hizo kuwa ni pamoja na ukosefu wa huduma rafiki katika Vituo vya Afya jambo ambalo huwakatisha tamaa Vijana walioamua kuacha matumizi ya Dawa za kulevya na kurejea tena baada ya kukosa usimamizi mzuri.
Mapema Sheha wa Shehia ya Fujoni Bwana Said Mgeni Bakari alisema Wananchi wa Kijiji cha Fujoni waliadhimia kusimamia mapambano dhidi ya matumizi ya Dawa za kulevya ndani ya Kijiji hicho.
Sheha Said alisema dhamira hiyo ndiyo iliyoibua kuanzishwa kwa Kikundi shirikishi na Polisi jamii kwa lengo la kukabiliana na wimbi la vitendo hivyo vya matumizi pamoja na uuzaji wa Dawa za kulevya na Pombe  ndani ya Kijiji hicho.
Alifahamisha kwamba licha ya juhudi zilizochukuliwa na Wananchi hao lakini bado lipo tatizo la ukosefu wa vifaa vya kufanyia kazi pamoja na Ofisi kwa Kikundi hicho cha Polisi Jamii na ulinzi shirikishi Fujoni.
Vijana hao Sita wa Kijiji cha Fujoni walioamua kuachana na matumizi ya Dawa za Kulevya walipatiwa mafunzo ya Miezi sita katika Nyumba ya kurekebishia Tabia kwa watu walioamua kuacha Matumizi ya Dawa za Kulevya ya Mombasa nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Wakati huo huo Mbunge huyo wa Jimbo la Kitope Balozi Seif ameukabidhi Uongozi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar { ZAWA } shilingi Milioni 5,000,000/-  kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Kibanda cha Maji katika Kijiji cha Kinduni.
Ujenzi wa Kibanda hicho una lengo la kuimarisha miundo mbinu ya upatikanaji wa huduma za Maji safi na Salama ndani ya Kijiji hicho chenye changamaoto ya upatikanaji wa huduma hiyo muhimu.
Balozi Seif aliushukuru Uongozi mzima wa Mamlaka ya Maji Zanzibar kwa hujudi uliochukuwa wa kushirikiana na ule wa Jimbo la Kitope katika kuwaondoshea usumbufu wa huduma ya maji safi na salama wananchi wa jimbo hilo.
Alisema juhudi hizo kwa kiasi kikubwa zimechangia kutatua changamoto za upatikanaji wa huduma ya maji katika Vijiji vingi vilivyomo ndani ya Jimbo la Kitope.
Akipokea fedha hizo  kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa  Kibanda cha Maji Kinduni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Zanzibar { ZAWA } Dr. Mustafa Garu alisema miradi mingi ya Maji iliyoanzishwa na Mamlaka hiyo inatekelezwa ili kuwaondoshea  usumbufu wa huduma ya Maji Wananchi walio wengi Nchini.
Dr. Garu aliutaja mradi wa Maji uliopata Mkopo kupitia Benki ya Maendeleo ya Afrika uko tayari kufanya kazi na utakuwa ukihudumia kwenye maeneo mengi ya Mji wa Zanzibar.
Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Mamlaka ya Maji Zanzibar aliwahakikishia Wananchi kwamba Mamlaka hiyo itafanya juhudi ya kuwapatia huduma za maji wananchi wakaondelea kuwa na uhaba wa huduma hiyo katika kipindi kinachoingia cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Alisema ule mpango wa kusambaza huduma za maji  Mjini na Baadhi ya Vijiji vyenye upungufu wa huduma hiyo kwa kutumia Magari maalum ya kusambazia maji utaendelea kutekelezwa ili kuwapa fursa Wananchi kupata muda wa kufanya mambo mengine ya Kimaisha.

























Tuesday, 16 June 2015

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akiwaaga Madaktari Mabingwa wa China 21 waliomaliza muda wao wa kutoa huduma za Afya Zanzibar na kuwakaribisha wapya 21 walioingia Zanzibar mwishoni mwa wiki iliyopita kushika nafasi hizo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwakaribisha Madaktari Mabingwa ya Jamuhuri ya Watu wa China waliowasili Zanzibar wiki iliyopita kushina nafasi ya wenzao waliomaliza muda wao wa miaka miwili. Picha na Hassan Issa – OMPR
Mke wa Mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi na Mke wa Balozi Mdogo wa China hapa Zanzibar Bibi Xie Yun wakipata mlo katika tafrija walioandaliwa Madaktari mabingwa wa China waliomaliza muda na wale wapya hapo Mazizini nje kidogo ya mji wa Zanzibar. Picha na Hassan Issa – OMPR
Balozi Seif Ali Iddi wa pili kutoka kushoto akiambatana na Balozi Mdogo wa China hapa Zanzibar Bwana Xie Yun Liang kwenye chakula alichowaandalia Madaktari mabingwa wa china waliomaliza muda wao na wapya hapo nyumbani kwake Mazizini.
Picha na Hassan Issa – OMPR
Baadhi ya Madaktari Mabingwa wa China waliomaliza muda wao wa kazi hapa Zanzibar wakipata mlo kwenye tafrija walioandaliwa rasmi na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif. Picha na Hassan Issa – OMPR
Balozi Seif akimzawadia Dr.Xia Jun  aliyemaliza muda wake wa kufanya kazi hapa Zanzibar kwenye tafrija maalum aliyowaandalia  nyumbani kwake Mazizini kuwaaga rasmi. Kati kati yao ni Kiongozi wa Madaktari Mabingwa waliomaliza muda wao wa kufanya kazi Zanzibar Dr. Liu Yaping. Picha na Hassan Issa – OMPR

Balozi Seif na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi wakiwa katika picha ya pamoja na Madaktari bingwa wa China mara baada ya kula nao chakula cha pamoja nyumbani kwake Mazizini. Picha na Hassan Issa – OMPR
Baadhi ya Madaktari mabingwa wa China waliohudhuria tafrija iliyoandaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wakionyesha furaha katika picha ya pamoja. Picha na Hassan Issa – OMPR
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Moh’d Aboud Moh’d akimpongeza Kiongozi wa Madaktari Mabiungwa wa China waliomaliza muda wao Dr. Liu Yaping kwa kuisimamia vyema Timu yake. Picha na Hassan Issa – OMPR
Balozi Seif na Mkewe Mama Asha wakiwa katika picha ya pamoja na Madaktari Mabingwa wa China wale waliomaliza muda wao wa kutoa huduma ya afya na wale wapya bada ya kula nao chakula cha pamoja. Kushoto ya Balozi Seif ni Kiongozi wa Madaktari wapya wa China Dr. Xu Zhuo Qun, Waziri wa Afya Mh. Rashid Sef, Waziri wa Nchini Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Moh’d Aboud Moh’d, Naibu Waziri wa Afya Mh. Mahmoud Thabit Kombo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dr. Saleh Moh’d Jidawi Kulia ya Balozi Seif ni Balozi Mdogo wa China hapa Zanzibar Bwana Xie Yun Liang, Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi, Mke wa Balozi Mdogo wa China Mama Xie Liang, Kiongozi wa Timu ya Madaktari Mabingwa waliomaliza muda wao Dr. Liu Yaping na Mtapta wa kutafsiri lugha Bibi Liu Hualian. Picha na Hassan Issa – OMPR




















Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Rashid Seif akitoa shukrani kwa Madaktari Mabingwa wa China waliopmaliza muda wao wa kutoa huduma za afya Zanzibar kwenye tafrija iliyoandaliwa na Balozi Seif Mazizini. Picha na Hassan Issa – OMPR

   Press Release
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeipongeza Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China kwa msimamo wake wa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kusaidia Taalamu na uwezeshaji katika sekta mbali mbali za maendeleo na Kiuchumi Nchini.
Pongezi hizo zimetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  wakati akiwaaga Madaktari Mabingwa wa  China 21 waliomaliza muda wao wa kutoa huduma za Afya Zanzibar na kuwakaribisha wapya 21 walioingia Zanzibar mwishoni mwa wiki iliyopita kushika nafasi hizo.
Maagano  na makaribisho hayo ambayo yaliambatana na chakula cha mchana alichowaandalia Madaktari Mabingwa hao wa Kichina yamefanyika nyumbani kwake Mazizini nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Balozi Seif alisema Jamuhuri ya Watu wa china imekuwa mshirika mkubwa wa maendeleo wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla mara baada ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 ambapo nchi hiyo ilianza kuleta timu ya Madaktari bingwa wa afya kufanya kazi Zanzibar kuanzia mwaka 1965.
Alisema timu za madaktari hao wa China zimekuwa zikifanya kazi kubwa za kutoa huduma za afya licha ya baadhi ya wakati kufanyakazi katika mazingira magumu jambo ambalo limeleta faraja na upendo kwa wananchi wanaopata fursa ya kuhudumiwa na Madaktari hao.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  aliwaeleza Madaktari hao  Mabingwa wa China walioambatana na Balozi wao Mdogo hapa Zanzibar Bwana Xie Yun Liang kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeipa kipaumbele sekta ya afya kutokana na umuhimu wake wa kulinda na kustawisha afya za  Wananchi wake.
Alisema kipaumbele hicho ni pamoja na kuimarisha miundo mbinu katika ujenzi wa vituo vya afya sambamba na vile vinavyoanzishwa  na Wananchi wenyewe vinavyokadiriwa kupatikana katika umbali usiozidi Kilomita Tano.
Naye Balozi Mdogo wa Jamuhuri ya Watu wa China Bwana Xie Yun Liang aliihakikishia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwamba Nchi hiyo itaendelea kusaidia maendeleo ya Zanzibar katika lengo lake la kuimarisha uhusiano wa kihistoria  uliopo wa muda mrefu kati ya pande hizo mbili uliodumu kwa zaidi ya miaka Hamsini sasa.
Balozi Xie alisema mkazo pamoja na mipango itaendelea kuimarishwa katika kuona China inazidisha nguvu zake za misaada katika Sekta za Afya, Elimu pamoja na miundombinu ya huduma za maji, kilimo na mawasiliano.
Mapema Kiongozi wa Madaktari  wa China waliomaliza muda wao wa kazi wa miaka miwili Zanzibar Dr. Liu Yaping kwa niaba ya wenzake alisema wanajivunia ushirikiano mkubwa walioupata kutoka kwa wenyeji wao ambao umewajengea nguvu za kufanya kazi kwa ari.
Dr. Liu Yaping alifahamisha kwamba kazi ya afya inahitaji uvumilivu mkubwa unaoibua upendo mkubwa na kusaidia kuleta ushirikiano kati ya Daktari na Mgonjwa na hatimae kuzaa udugu kati ya wahusika hao wawili.
Kiongozi huyo wa Madaktari Bingwa wa China waliomaliza muda wao ameushukuru Uongozi wa Wizara ya Afya Zanzibar  kwa msaada mkubwa ulioipa Timu yake katika muda wao wote  wa miaka miwili waliokuwepo  hapa Zanzibar.
Timu  Mpya ya Madaktari Bingwa 21 kutoka Jamuhuri ya Watu wa China inayoongozwa na Dr. Xu Zhuo Qun itakuwepo Zanzibar kutoa huduma za Afya ambapo miongoni mwao Madaktari 12 watafanya kazi Unguja na 9 Kisiwani Pemba.