Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwakaribisha
Madaktari Mabingwa ya Jamuhuri ya Watu wa China waliowasili Zanzibar wiki
iliyopita kushina nafasi ya wenzao waliomaliza muda wao wa miaka miwili. Picha na Hassan Issa –
OMPR
Mke wa Mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi
na Mke wa Balozi Mdogo wa China hapa Zanzibar Bibi Xie Yun wakipata mlo katika
tafrija walioandaliwa Madaktari mabingwa wa China waliomaliza muda na wale
wapya hapo Mazizini nje kidogo ya mji wa Zanzibar. Picha na Hassan Issa –
OMPR
Balozi Seif Ali Iddi wa pili kutoka kushoto akiambatana na Balozi Mdogo wa
China hapa Zanzibar Bwana Xie Yun Liang kwenye chakula alichowaandalia
Madaktari mabingwa wa china waliomaliza muda wao na wapya hapo nyumbani kwake
Mazizini.
Picha na Hassan Issa – OMPR
Picha na Hassan Issa – OMPR
Baadhi ya Madaktari Mabingwa wa China waliomaliza muda wao wa kazi
hapa Zanzibar wakipata mlo kwenye tafrija walioandaliwa rasmi na Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif. Picha na Hassan Issa –
OMPR
Balozi Seif akimzawadia Dr.Xia Jun
aliyemaliza muda wake wa kufanya kazi hapa Zanzibar kwenye tafrija
maalum aliyowaandalia nyumbani kwake
Mazizini kuwaaga rasmi. Kati kati
yao ni Kiongozi wa Madaktari Mabingwa waliomaliza muda wao wa kufanya kazi
Zanzibar Dr. Liu Yaping. Picha na Hassan Issa –
OMPR
Balozi Seif na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi wakiwa katika picha ya pamoja na Madaktari bingwa wa China mara baada ya kula nao chakula cha pamoja nyumbani kwake Mazizini. Picha na Hassan Issa – OMPR
Baadhi ya Madaktari mabingwa wa China waliohudhuria tafrija iliyoandaliwa
na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wakionyesha furaha katika
picha ya pamoja. Picha na Hassan Issa –
OMPR
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Moh’d
Aboud Moh’d akimpongeza Kiongozi wa Madaktari Mabiungwa wa China waliomaliza
muda wao Dr. Liu Yaping kwa kuisimamia vyema Timu yake. Picha na Hassan Issa –
OMPR
Balozi Seif na Mkewe Mama Asha wakiwa katika picha ya pamoja na Madaktari
Mabingwa wa China wale waliomaliza muda wao wa kutoa huduma ya afya na wale
wapya bada ya kula nao chakula cha pamoja. Kushoto ya
Balozi Seif ni Kiongozi wa Madaktari wapya wa China Dr. Xu Zhuo Qun, Waziri wa
Afya Mh. Rashid Sef, Waziri wa Nchini Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Mh. Moh’d Aboud Moh’d, Naibu Waziri wa Afya Mh. Mahmoud Thabit Kombo
na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dr. Saleh Moh’d Jidawi Kulia ya
Balozi Seif ni Balozi Mdogo wa China hapa Zanzibar Bwana Xie Yun Liang, Mke wa
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi, Mke wa Balozi Mdogo
wa China Mama Xie Liang, Kiongozi wa Timu ya Madaktari Mabingwa waliomaliza
muda wao Dr. Liu Yaping na Mtapta wa kutafsiri lugha Bibi Liu Hualian. Picha na Hassan Issa –
OMPR
Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Rashid Seif akitoa shukrani kwa Madaktari
Mabingwa wa China waliopmaliza muda wao wa kutoa huduma za afya Zanzibar kwenye
tafrija iliyoandaliwa na Balozi Seif Mazizini. Picha na Hassan Issa –
OMPR
Press Release
Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar imeipongeza Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China kwa
msimamo wake wa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kusaidia Taalamu na uwezeshaji
katika sekta mbali mbali za maendeleo na Kiuchumi Nchini.
Pongezi
hizo
zimetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
wakati akiwaaga Madaktari Mabingwa wa China 21 waliomaliza muda wao wa
kutoa huduma
za Afya Zanzibar na kuwakaribisha wapya 21 walioingia Zanzibar mwishoni
mwa
wiki iliyopita kushika nafasi hizo.
Maagano na makaribisho hayo ambayo yaliambatana na
chakula cha mchana alichowaandalia Madaktari Mabingwa hao wa Kichina
yamefanyika nyumbani kwake Mazizini nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Balozi Seif
alisema Jamuhuri ya Watu wa china imekuwa mshirika mkubwa wa maendeleo wa Zanzibar
na Tanzania kwa ujumla mara baada ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 ambapo
nchi hiyo ilianza kuleta timu ya Madaktari bingwa wa afya kufanya kazi Zanzibar
kuanzia mwaka 1965.
Alisema timu
za madaktari hao wa China zimekuwa zikifanya kazi kubwa za kutoa huduma za afya
licha ya baadhi ya wakati kufanyakazi katika mazingira magumu jambo ambalo
limeleta faraja na upendo kwa wananchi wanaopata fursa ya kuhudumiwa na
Madaktari hao.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaeleza
Madaktari hao Mabingwa wa China walioambatana
na Balozi wao Mdogo hapa Zanzibar Bwana Xie Yun Liang kwamba Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar imeipa kipaumbele sekta ya afya kutokana na umuhimu wake
wa kulinda na kustawisha afya za Wananchi wake.
Alisema
kipaumbele hicho ni pamoja na kuimarisha miundo mbinu katika ujenzi wa vituo
vya afya sambamba na vile vinavyoanzishwa na Wananchi wenyewe vinavyokadiriwa kupatikana
katika umbali usiozidi Kilomita Tano.
Naye Balozi
Mdogo wa Jamuhuri ya Watu wa China Bwana Xie Yun Liang aliihakikishia Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar kwamba Nchi hiyo itaendelea kusaidia maendeleo ya
Zanzibar katika lengo lake la kuimarisha uhusiano wa kihistoria uliopo wa muda mrefu kati ya pande hizo mbili
uliodumu kwa zaidi ya miaka Hamsini sasa.
Balozi Xie
alisema mkazo pamoja na mipango itaendelea kuimarishwa katika kuona China
inazidisha nguvu zake za misaada katika Sekta za Afya, Elimu pamoja na
miundombinu ya huduma za maji, kilimo na mawasiliano.
Mapema
Kiongozi wa Madaktari wa China
waliomaliza muda wao wa kazi wa miaka miwili Zanzibar Dr. Liu Yaping kwa niaba
ya wenzake alisema wanajivunia ushirikiano mkubwa walioupata kutoka kwa wenyeji
wao ambao umewajengea nguvu za kufanya kazi kwa ari.
Dr. Liu
Yaping alifahamisha kwamba kazi ya afya inahitaji uvumilivu mkubwa unaoibua
upendo mkubwa na kusaidia kuleta ushirikiano kati ya Daktari na Mgonjwa na
hatimae kuzaa udugu kati ya wahusika hao wawili.
Kiongozi
huyo wa Madaktari Bingwa wa China waliomaliza muda wao ameushukuru Uongozi wa
Wizara ya Afya Zanzibar kwa msaada
mkubwa ulioipa Timu yake katika muda wao wote
wa miaka miwili waliokuwepo hapa
Zanzibar.
Timu Mpya ya Madaktari Bingwa 21 kutoka Jamuhuri
ya Watu wa China inayoongozwa na Dr. Xu Zhuo Qun itakuwepo Zanzibar kutoa
huduma za Afya ambapo miongoni mwao Madaktari 12 watafanya kazi Unguja na 9
Kisiwani Pemba.